TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, February 4, 2015

Serikali yajenga barabara zenye urefu wa kilometa 42 mji wa Dodoma

jeni
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Jenista Mhagama akijibu swali  Mbunge Bungeni.
………………………………………………………………………………..
Na Lorietha Laurence-Maelezo , Dodoma SERIKALI kupitia mradi wa uendelezaji miji (TSCP) imefanikiwa kujenga barabara zenye urefu wa kilometa 42 kwa mji wa Dodoma kwa msaada wa mfuko wa Benki ya Dunia. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Jenista Mhagama ameeleza hayo Bungeni Dodoma, kuwa ujenzi huo wa barabara umehusisha pia ujenzi wa mifumo ya maji ya mvua ,dampo la kisasa kwa kijiji cha Chidaya pamoja na mitambo y usombaji taka.

“Maboresho hayo ya miundombinu kwa mji wa Dodoma, ni kuhakikisha kuwa mji mkuu huu wa Tanzania unakuwa katika madhari mazuri na yenye kukidhi haja za wananchi wake”, alisema Waziri Mhagama. Alizitaja barabara hizo kuwa ni pamoja na maboresho ya barabara ya Mwanza, Barabara ya 6 hadi 11,Barabara za Nkuhungu na Chamwino-chang’ombe zenye jumla ya kilomita 15.7 ambapo ujenzi umekamilika kwa asilimia 100. Aidha aliongeza kuwa jumla ya kilomita 27.12 za barabara za pembezoni mwa mji nazo zilijengwa kwa kiwango cha lami ambazo ni Area A kilomita 5.82, Kikuyu kilomita 5.65,Kisasa kilometa 12.90 na Chamwino kilometa 2,75. Hata hivyo, alisema Benki ya Dunia imeahidi kutoa Dola za Kimarekani milioni 7.66 kwa ajili ya kukamilisha mapungufu yaliyojitokeza katika awamu ya kwanza kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Independence na barabara ya mbeya kuelekea uhindini.

No comments:

Post a Comment