TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, January 31, 2015

Serikali yapewa ushauri na PAC juu ya kuinusuru kampuni ya TTCL

KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imetoa mapendekezo ya kuinusuru Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kutokana na hali mbaya ya kampuni hiyo kifedha kwa sasa ambapo inaendeshwa kwa hasara huku ikiwa na madeni makubwa. PAC imetoa mapendekezo hayo katika taarifa yao kwa bunge ya mwaka juu ya ukaguzi wa hesabu za Serikali kwa mashirika ya umma iliyotolewa Januari 28 mwaka 2015. 
 Kwa mujibu wa taarifa ya PAC hali ya mapato na matumizi ya TTCL kwa mwaka 2012 ilipata hasara ya bilioni 20.883 huku kwa mwaka 2013 ikipata hasara ya bilioni 16.258. PAC ilisema majumuisho ya hasara ya TTCL kupata hasara kwa takribani kwa miaka 10, Kampuni sasa imekuwa na hasara ambayo kwa mwaka 2013 ilifikia bilioni 334.48, jambo ambalo limeiondolea mvuto wa kukopeshwa na taasisi za fedha hata zile zenye nia ya kuikopesha.
 "...Ukosefu wa fedha za kutosha kutekeleza miradi ya Kampuni umekuwa kikwazo kwa TTCL kukabiliana na ushindani wa kibiashara. Kwa kipindi kirefu ufanisi wa TTCL kiuwekezaji na kifedha umeendelea kudorora. Tangu TTCL ibinafsishwe mwaka 2001, hakuna uwekezaji mkubwa uliofanyika na mpango wa kutafuta mkopo kutoka mabenki ya ndani na nje ya nchi unakwamishwa na masharti ya kupata udhamini wa Serikali," ilieleza taarifa hiyo ya PAC. PAC iliongeza kuwa ukiacha madeni yaliopo pia TTCL inadaiwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) jumla ya bilioni 25 hivyo kufanya jumla ya deni kufikia bilioni 101.6. 
Kamati hiyo ya bunge imesema kuna umuhimu wa Serikali kufanya maamuzi ya haraka ya kuikwamua TTCL ili iweze kuendelea kutoa huduma kwenye Sekta ya Mawasiliano ikizingatiwa kuwa ndiyo inayoendesha Mkongo wa Taifa wa mawasiliano. Katika mapendekezo ya PAC ili kuikwamua TTCL imeishauri Serikali kununua hisa asilimia 35 zinazomilikiwa na Bharti Airtel katika TTCL kwa gharama ndogo kwani Bharti Airtel haikutimiza kikamilifu masharti ya mkataba wa mauziano ya hisa hizo hapo awali kwani tangu inunue hisa hizo haijafanya uwekezaji katika Kampuni ya TTCL. 

Friday, January 30, 2015

Tathmini Ya Programu ya IFAD nchini Tanzania yaonyesha Mafanikio Makubwa

Mkurugenzi wa IFAD, Ofisi huru ya Tathmini, Mr Oscar Garcia akitoa ripoti ya tathmini ya programu ya IFAD nchini Tanzania jinsi ilivyoweza kuonyesha mafanikio makubwa wakati wa warsha ya siku moja iliyofanyika Januari 29, 2014 jijini Dar katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwl Nyerere.
 Waziri wa Kilim, Chakula na Ushirika Tanzania Bara, Mh Steven Wassira akisoma hotuba fupi wakati wa warsha ya siku moja iliyolenga kuonyesha mafanikio ya programu ya IFAD nchini Tanzania, warsha iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwl Nyerere Januari 29, 2014 jijini Dar.

TAARIFA (DPD) KATIKA KUZINGATIA SIKU YA KIMATAIFA YA FARAGHA

Mataifa mbalimbali duniani ifikapo tarehe 28 ya kila mwezi wa kwanza wanaadhimisha siku ya kimataifa ya faragha ya taarifa ambapo kunakua na matukio mbali mbali ya kuhamasisha njia rafiki za kuweka salama taarifa za watu hasa wawapo mtandaoni. Taarifa zaidi za siku hii "BONYEZA HAPA"

Siku hii imekua ikitumika vizuri kwa ushirikiano mkubwa ma mashirika binafsi, serikali na vyombo vya habari kukumbusha watumiaji mitandao kuzingatia matumizi salama ya mitandao ili kubakisha taarifa za watumiaji mtandao salama.
Inafahamika, ukuaji wa wa kasi wa Teknolojia umeambatana matumizi yasiokusudiwa wa teknolojia ambapo umekua ukihatarisha sana ufaragha wa watumiaji wa teknolojia hizo. Kwa kuzingatia hili siku ya kimataifa ya faragha ya taarifa imekua ikihimizwa kutumika vizuri kukumbusha watumiaji mtandao yale yanayoweza kuhakikisha taarifa zao zinabaki salama watumiapo mitandao.

FAHARI HUDUMA WAKALA NA SimBanking NI KAMPENI ILIYOZINDULIWA NA BENKI YA CRDB

Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi huo.
BENKI ya CRDB imezindua kampeni maalum ya utumiaji wa huduma zake kupitia simu za mkononi ‘SimBanking’  kupitia kwa mawakala  wa ‘FahariHuduma’.

Akizungumza jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa kampeni hiyo ijulikanayo kama ‘Tuma Pesa na SimBanking Shinda Passo’, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Dk. Charles Kimei alisema lengo la kuanzisha kampeni hiyo ni kuwakumbusha wateja wake na watanzania wote kwa ujumla umuhimu wa kutumia njia hizo mbadala ili kupata huduma kwa urahisi na uharaka.

Alisema kampeni hiyo inatarajiwa kutoa magari kumi na mbili ambapo kila mwezi mshindi mmoja atazawadiwa gari hilo, pamoja na zawadi ya gari la wateja watakaotumia huduma hizo pia wataweza kujishindia zawadi nyingine mbalimbali zikiwemo solar power, tables na simu za kisasa za mkononi.

“Tunataka kuwavutia wateja wetu kuziamini na kuzitumia zaidi huduma hizi kwani ni sawa kabisa na kupata huduma kupitia matawi yetu,”.

Akielezea namna ya kushiriki  na jinsi mshindi atakavyopatikana, Dk. Kimei alisema kuwa shindano hilo ni la wateja wote wa CRDB watumiao huduma hizo na mshindi atakuwa ni yule mwenye miamala mingi zaidi kwa mwezi husika.

Thursday, January 29, 2015

MZEE YUSUPH NA JAHAZI NDANI YA MWANZA NA HII NDIYO RATIBA YAKE

Mpango mzima wa 'Harakati za Valentine ndani ya Villa Park Mwanza, utakao anza rasmi Alhamisi ya tarehe 12/02/2015 ambapo Mfalme Mzee Yusufu na Bendi yake ya Jahazi Mordrn Taarab kuhusika, kiingilio nishilingi 10,000/=

Kisha Jumamosi ya tarehe 14/02/2015 Valentines Day bendi ya Super Kamanyola kutambulisha safu ya waimbaji wake wapya, Kiingilio Sebuleni Tshs 5,000/= na Tshs10,000/= utazama hadi Disco ambako kutakuwa na mpambano wa Ma-Dj NANI MKALI KATI YA DJ TASS (MAGIC FM) V/s DJ EDDY (RFA).
Moja kati ya ma-dancer wa Super Kamanyola anaitwa Cathy Butamu. 

MAENDELEO SASA KUPATIKANA NHC GEITA NA KAGERA

Mkurugenzi Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu akikagua viwanja vya NHC Wilayani Chato vinavyokusudiwa kujengwa nyumba za gharama nafuu ikiwa ni program ya NHC ya kuzifikia Wilaya zote nchini.
Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC BW. Nehemia Kyando Mchechu ukikagua nyumba za makazi za NHC Wilayani Chato alipotembelea Wilaya hiyo jana.

AKCLASSICOSMETICS YAWAANDALIA MAMBO MAKALI KATIKA MWAKA HUU WA 2015

NANI ASIYEWATAMBUA #AKCLASSICOSMETICS WAO NI MWENDO WA VITU VYA UKWEE NA ORIGINAL KABISA??? SASA MALI MPYA IMEINGIA #TEAMNATURALHAIR MPOO? SAFARI HII HAMJASAHAULIKA!!

PIA KUNA HABARI NJEMA KWA WADAU WOTE WANAOSUMBUKA NA MATATIZO MBALI MBALI KUHUSU NGOZI ZAO KAMA VILE KUUNGUA KWA MIKOROGO,WEUSI WA MACHONI(DARK CYCLE),KUSWEAT KULIKOPITILIZA,AKCLASSIC WAMEAMUA KUCHIMBA NA KUJA NA MAJIBU YA MATATIZO YENU TENA MADINI YASIYO NA MADHARA KABISAAA KWA NGOZI YAKO!!

   WALE WALIOTOKA KUJIFUNGUA NA YALE YOTE YATOKANAYO HATUJAWASAHAU PIA KUANZIA CORSETS,NYWELE(T444Z JBCO NA HAIRFINITY,SHEAR MOISTURE),WEUSI WA KWAPA NA SHINGO NA OFCOUZ NA BIDHAA ZA KUPIGA USO NA MWILI MSASA!!
 
  INGIA   www.akclassic.blogspot.com KUONA PICHA ZAIDI NA MAELEZO!!

   TUPIGIE 0753482909/0713468393.
TUPO KINONDONI KWA MANYANYA NA MLIMANI CITY KWA NJE(0PP. TOTAL PETROL STATION)
TUTAKUFIKIA MPAKA MLANGONI!!
KARIBUNI WOTE.

Mr. McDowall amaliza mafunzo ya Siku mbili na Maafisa Mawasiliano

 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano toka Wizara ya Nishati na Madini Bi. Badra Masoud akitoa somo kwa Maafisa Mawasiliano mara baada ya Mafunzo kutoka kwa Mkufunzi toka Uingereza Bw. Simon McDowell leo Mjini Mtwara
 Afisa Mawasiliano wa Ofisi ya Rais Sekretariat ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Kassim Nyaki akitoa somo kwa Maafisa Mawasiliano mara baada ya Mafunzo kutoka kwa Mkufunzi toka Uingereza Bw. Simon McDowell leo Mjini Mtwara

KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA AMALIZA ZIARA YAKE YA SIKU 15 KISIWANI UNGUJA NA PEMBA

 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM,Vuai Ali Vuai kuelekea kukishiriki upandaji wa mboga mboga na kutia mbolea katika shamba la Wajasiliamali lenye ekari nne na nusu la ushirika wa Jambo Group Cooperative Society,lenye jumla ya washirika wapatao 15,katika kijiji cha Wambaa Kwaanzani,wilaya ya Mkoani ,Kusini Pemba.
Kinana amemaliza ziara ya siku 15 katika visiwa vya Unguja na Pemba Zanzibar ambapo amekagua na kushiriki ujenzi katika miradi 40 mikoa 12. 

Katika ziara hiyo,Ndugu Kinana alijionea mafanikio makubwa ya kimaendeleo yaliyofanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Rais Dk. Ali Mohamed Shein, zikiwemo barabara, hospitali, elimu na maji pamoja na kusambazwa umeme karibu kila kona. 

Katika ziara hiyo ,Ndugu Kinana amewataka viongozi wa dini na Serikali kukemea kitendo cha CUF kuwaita wanaohamia CCM makafiri. Naye Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Zanzibar, Vuai Ali Vuai, alimpongeza Ndugu Kinana kwa ziara yake, kwamba imekuwa ya mafanikio makubwa na imewapa somo na moyo wa kuimarisha chama visiwani.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki upandaji wa mboga mboga na kutia mbolea katika shamba la Wajasiliamali lenye ekari nne na nusu la ushirika wa Jambo Group Cooperative Society,lenye jumla ya washirika wapatao 15,katika kijiji cha Wambaa Kwaanzani,wilaya ya Mkoani ,Kusini Pemba.

JIPATIE NAKALA YAKO YA GAZETI LA UWAZI MIZENGWE YA UCHAGUZI KILA IJUMAA

UBALOZI WA TANZANIA NCHINI UFARANSA JIJINI PARIS -RAIS KIKWETE AFUNGUA RASMI MAJENGO .

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua rasmi majengo ya ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa yaliyoko jijini Paris Jumatano jioni Januari 28, 2015. Pamoja naye ni Mama Sallma Kikwete, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe, Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Hamad Msauni na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mhe Mhe Begum Taj.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na wafanyakazi wa ubalozi baada ya kufungua rasmi majengo ya ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa yaliyoko jijini Paris Jumatano jioni Januari 28, 2015. Pamoja naye ni Mama Sallma Kikwete, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe, Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Hamad Msauni na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mhe Mhe Begum Taj.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na balozi wa New Zealand nchimni Uraransa baada ya kufungua rasmi majengo ya ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa yaliyoko jijini Paris Jumatano jioni Januari 28, 2015. Katikati Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa  Mhe Begum Taj. New Zealand ndiyo iliyoiuzia Tanzania majengo hayo ambayo ya ghorofa tano ya ofisi pamoja na jengo lingine la makazi ya balozi na maafisa wa ubalozi.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua na kuweka saini kitabu cha wageni  baada ya kufungua rasmi majengo ya ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa yaliyoko jijini Paris Jumatano jioni Januari 28, 2015. Katikati Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa  Mhe Begum Taj. New Zealand ndiyo iliyoiuzia Tanzania majengo hayo ambayo ya ghorofa tano ya ofisi pamoja na jengo lingine la makazi ya balozi na maafisa wa ubalozi.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akijichanganya na wageni waalikwa ambao ni mabalozi wa nchi mba,limbali za Afrika pamoja na wana Jumuiya ya Watanzania  baada ya kufungua rasmi majengo ya ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa yaliyoko jijini Paris Jumatano jioni Januari 28, 2015. Katikati Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa  Mhe Begum Taj. New Zealand ndiyo iliyoiuzia Tanzania majengo hayo ambayo ya ghorofa tano ya ofisi pamoja na jengo lingine la makazi ya balozi
na maafisa wa ubalozi. PICHA NA IKULU.



WAKUNGA WA JADI WATHAMINIWA NA SERIKALI

Na Abdula Ali   Maelezo-Zanzibar      .
                                     
Naibu waziri wa afya Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo amesema Serikali haiwazarau Wakunga wa Jadi na badala yake imeamua kuwapatia vibali maalumu ambavyo vitawahalalishia ufanyaji wa kazi zao bila ya usumbufu ili kuokoa vifo vya akina mama wajawazito wakati wa kujifungua.

Hayo ameyasema katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Wilaya ya Magharibi Unguja wakati akijibu swali la mwakilishi wa kuteuliwa wa Nafasi Maalumu za Wanawake Mhe. Panya Ali Abdalla.

RAIS KIKWETE NA RAIS WA UFARANSA FRANCOIS HOLLANDE WAKUTANA JIJINI PARIS

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika Ikulu ya Ufaransa
maarufu kama Champs L’Elysee jijini Paris Jumatano jioni Januari 28,
2015 kuonana na mwenyeji wake Rais Francois Hollande.

UBALOZI WA TANZANIA NCHINI UFARANSA WASHEREHEKEA UFUNGUZI WA MAJENGO YAKE

 Balozi Begum Taj akikaribisha wageni
 Sehemu ya Umati
 Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwa na watoto wa wanaJumuiya ya Watanzania

WATANZANIA NCHINI MASCUT - OMAN WAENDELEZA CHANGAMOTO KATIKA MAONESHO YA KIMATAIFA YANAYOENDELEA NCHINI HUMO.

Wageni mbalimbali wakiingia na kutoka Katika Banda la Watanzania kujione bidhaa za Watanzania Wanaoshiriki katika Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa,Ubunifu na Utamaduni yanayoendelea Mascut-Oman. 
Msanii wa kuchora Fred Halla akifanya sanaa yake ya Uchoraji katika Katika Banda la Watanzania.Fred ni mmoja wa Watanzania Wanaoshiriki katika Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa,Ubunifu na Utamaduni yanayoendelea Mascut-Oman. 

ALI KIBA MIONGONI MWA WASANII WATAKAOPANDA JUKWA LA SAUTI ZA BUSARA

 Msanii wa Bongo fleva nchini, Ali Kiba akiimba akapela moja ya nyimbo zake wakati wa mkutano huo na wandishi wa habari (Hawapo pichani), katika mkutano huo juu ya ushiriki wake kwenye tamasha hilo linalotarajia kufanyika Februari 12 hadi 15, Ngome Kongwe, Zanzibar. kushoto kwake, ni Mkurugenzi wa tamasha hilo, Yusuf Mahmoud 'Dj Yusuf, akifuatiwa na Mwenyekiti wa Bodi wa Busara Promotions, Simai Mohammed.
 
=======  ====== ======
Ali Kiba ahidi makubwa Sauti za Busara Februari 12
Ali Kiba atamba kufanya kweli Sauti za Busara mwaka huu
Ali Kiba kupiga shoo ya 'live' Sauti za Busara Feb 12
Na Andrew Chale

Mkali wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ali Kiba ametamba kukonga nyoyo watu mbalimbali watakaojitokeza kwenye tamasha la 12 la Sauti za Busara linalotarajia kufanyika, Februari 12 hadi 15, Ngome Kongwe, Zanzubar.
 Mwenyekiti wa Bodi wa Busara Promotions, wandaaji wa tamasha la Sauti za Busara, Simai Mohammed (katikati) akiongea na wandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati wa mkutano wa wanahabari Jijini Dar es Salaam, juu ya tamasha la 12 la Sauti za Busara, litakalofanyika, Februari 12 hadi 15, mwaka huu, Ngome Kongwe, Zanzibar. Wengine (kushoto) ni Meneja wa tamasha hilo, Journey Ramadhani. na upande wa kulia ni Mkurugenzi wa tamasha hilo, Yusuf Mahmoud 'Dj Yusuf, akifuatiwa na msanii wa bongo fleva nchini, Ali Kiba (kulia).

MKOA WA ARUSHA WAENDELEA KUNUFAIKA NA HUDUMA ZA AIRTEL JIMBO LA MONDULI

Wanafunzi wa shule ya sekondari Nanja wakionyesha vitabu vyao mara baada ya Airtel kukabithi msaada wa vitabu vya sayansi kwa shule hiyo chini ya mpango wake wa Airtel shule yetu.

Wanafunzi na walimu wa shule ya Sekondari Nanja wamepokea msaada wa vitabu kutoka Airtel, Msaada utakaoweza kuchangia katika kutatua tatizo la uhaba wa vitabu shule ni hapo.

Akitoa taarifa ya shule , Mkuu wa shule ya sekondari ya Nanja Bwana Yona luka alisema” shule yetu ina jumla ya wanafunzi 549 na walimu 32, matokeo ya shule ya kidato cha nne yanakuwa kila mwaka ufaulu wa asilimia 71% pamoja na kukua kwa kiwango cha ufaulu bado shule inachangamoto nyingi ikiwemo uhaba wa vitabu na walimu.

Meneja Mauzo wa Airtel Kanda ya Kaskazini Brighthon Majwala akikabithi vitabu kwa Afisa Elimu wa shule za sekondari halimashauri ya Monduli Bwana Shaban Kasim Mgunya kwaajili ya shule ya sekondari Nanja iliyoko Monduli mkoani Arusha. wakishuhudia ni baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Nanja.

UONGOZI BORA KUPEWA TUZO KESHO

Tuzo za bodi yenye uongozi bora katika sekta ya kibenki na bima zijulikanazo kama Best Board Leadership Awards (BBLA) zinatarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam kesho, ambapo taasisi saba zitashiriki katika tuzo hizo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam hapo jana, Mratibu wa tuzo hizo, Bi. Neema Gerald, amezitaja benki zilizothibitisha kushiriki katika tuzo hizo kuwa ni pamoja na Benki ya Posta (TPB), Benki ya Exim na Benki ya CRDB.
“Kwa upande wa makampuni ya bima, watakaoshiriki ni Heritage Insurance, Alliance Insurance Corporation, Alliance Life Assurance na Strategis Insurance (T) Limited,” alisema.
Kwa mujibu wa Bi. Neema, tuzo hizo maalum kwa ajili ya sekta za kibenki na bima ni mpango pekee uliopo unaolenga kutambua mchango wa uongozi bora wa Bodi za Wakurugenzi katika sekta hizo mbili.
“Ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwa makampuni yaliyoonyesha mwamko wa kushiriki. Tuzo hizi zinalenga kutambua mchango mkubwa unaotolewa na kundi la watu waliokabidhiwa dhamana ya kufanya maamuzi kwa niaba ya wanahisa,” alisema.
Kwa mujibu wa mratibu huyo, Tuzo hizi zitatoa fursa ya ufahamu ni kwa jinsi gani bodi bora inaweza kusaidia taasisi kupata mafanikio na kufikia utendaji bora hususani katika eneo walilobobea kiutalaam.
"Tumeona umuhimu wa kutambua na kuthamini mchango unaotolewa na wakurugenzi wa bodi katika taasisi zao. Tunaamini kuwa katika kila mafanikio ya taasisi ya kifedha, nyuma yake kuna bodi ya wakurugenzi imara na makini. Sasa, sifa hizi ambazo wajumbe wa bodi wengi wanakua nazo zinapaswa kutambuliwa na kuthaminiwa, " alisema.
Akizungumzia tuzo hizo, Bw. Laurence Mwangoka, Meneja Mauzo wa Hoteli ya Serena, ambayo ni moja kati ya wadhamini, alisema kuwa tuzo hizo zimeanzishwa wakati muafaka nchini kipindi ambapo sekta za Bima na kibenki zinapitia mabadiliko makubwa katika ukuaji wake.
Mbali na Hoteli ya Serena, wadhamini wengine wa tukio hilo la kipekee ni pamoja na Excel Management and Outsourcing, Fix Agency Ltd, IPP Media,Real PR Solutions, Lilacnshades, Afrimax Strategic Partnerships Limited na Capital Plus International huku wadhamini zaidi wakiaswa kujitokeza.

VIONGOZI TEMEKE WAPONGEZA MAFANIKIO KATIKA SHULE YA KIISLAMU TWAYYAIBAT ISLAMIC SEMINARY

Mkuu wa Wilaya Temeke, Sofia Mjema, kulia akimkabidhi cheti Mr Yakubu kwa kutambua mchango wake kwa maendeleo ya shule ya Twayyibat Islamic Seminary, iliyopo Temeke, jijini Dar es Salaam jana.
Meneja wa Skywadrs Construction, Saeed Pirbaksh Mulla, akipokea cheti cha kutambua mchango wa kampuni yao kwenye shule hiyo. Cheti hicho anakabidhiwa na Mkuu wa Wilaya Temeke, Sofia Mjema, kulia.

Wednesday, January 28, 2015

Ziara ya Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC mikoani

New Picture (4)Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu wakikagua eneo lililotengwa kwa ajili ya NHC kujenga nyumba za gharama nafuukatika Halmashauri ya Wilaya Serengeti-Mugumu. Eneo hili lina ekari 134 na miundombinu ya maji na umeme.
New Picture (5)Afisa Mipango Miji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mugumu Serengeti akimuonyesha Mkurugenzi Mkuu wa NHC ramani ya mpango Miji inayoonyesha eneo la NHC la kujenga nyumba za gharama nafuu.

Dharuba kubwa ya theluji na upepo mkali imeipelekea kusimamisha huduma za umma kaskazini mashariki ya Marekani.

By Abou Shatry Washington DC
 
Zaidi ya watu 60 million wataathirika kutokana na kimbunga kikubwa cha upepo unaoambatana na unyeshaji wa theleji katika eneo la kaskazini mashariki ya Marekani.
A plow truck clears snow off South Church Street, in Hazleton, Pennsylvania on Monday. The area received another three-inches of snow overnight
Lori maalumu la usafishaji likiondoa theluji iliondoka barabara ya South Church Street, katika mji wa Hazleton, Pennsylvania siku ya Jumatatu Jan 26, 2015. Photo via .dailymail.co.uk
Kwa mujibu wa kitengo cha hali ya hewa nchini Marekani, imetaja maeneo ambayo yataathiriwa na dhoruba hiyo, ya kihistoria ambayo itapelekea zaidi ya watu kadhaa kukosa huduma ya umeme, pamoja na huduma za usafiri wa anga na nchi kavu.
 
Imetaja baadhi ya majimbo ambayo yatakumbwa na kimbunga hicho kuwa ni New York, New Jersey, Massachusetts, Connecticut na Rhode Island, ambapo imepelekea viongozi wakuu wa majimbo hayo kutangaza hali ya hatari kwa tukio hilo ambalo litatokea siku ya Jumatatu, Jumanne na Jumatano.
 
Imetabiriwa kiasi cha unyeshaji wa theluji hiyo 36inches katika jimbo la New York 16 hadi 26 inches katika jimbo la Boston, na kiwango kingine kama hicho katika baadhi ya majimbo mengine
 
Zaidi ya safari za ndege 3,800 zimesimamishwa mapema leo Jumaatatu katika viwavya vya ndege vya JFK, LaGuardia na Newark airports, pia huduma za shule kufungwa siku ya jumanne na jumatano katika majimbo hayo.
Chanzo: swahilivilla