TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, January 27, 2015

AKILI ZA KUAMBIWA CHANGANYA NA ZAKO KINANA AWAAMBIA WANA (CUF) WETE PEMBA

 3Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Mh.Mwinyijuma  Hamad Mshauri wa kikundi cha Ushirika Cha ufugaji wa Samaki na Uhifadhi wa Mazingira  Gando Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua na kuhimiza utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 , Kinana akihutubiwa wananchi leo katika Wete mjini amewaambia wananchi kwamba viongozi wa Chama cha CUF wakiwaambia jambo wanatakiwa kuchanganya na akili zao pia ili kutafakari watakayoambiwa badala ya kukubali kila kitu. Ameongeza kwamba Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mh. Maalim Seif Sharif Hamad pamoja na viongozi wenzake wa CUF wapo katika serikali ya umoja wa kitaifa ya SMZ lakini pamoja na hayo wameshindwa kupeleka Maji, Umeme, Barabara, Afya na mambo mengine mengi  huko Pemba.
Lakini  Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein ndiye anayepeleka maendeleo hayo huko Pemba bila kubagua kwamba watakaofaidi ni wafuasi wa CCM au CUF kwakuwa anatekeleza ilani ya chaguzi ya CCM Chama ambacho kiko madarakani , Jambo la msingi ni kupeleka  huduma kwa Wazanzibari wote bila kujali Itikadi zao. Ameongeza kwamba Mbunge wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania anapokea shilingi milioni 25 kila mwezi ikiwa ni Mfuko wa maendeleo wa jimbo na Mwakilishi anapokea shilingi milioni 15 kila mwezi vilevile lakini wanazipeleka wapi? “Waulizeni wapi wanapeleka fedha hizo  badala ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Pemba” 4Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua mabwawa ya kufugia samaki ya kikundi cha  kikundi cha Ushirika Cha ufugaji wa Samaki na Uhifadhi wa Mazingira  Gando Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba
5Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Mh.Mwinyijuma  Hamad Mshauri wa kikundi cha Ushirika Cha ufugaji wa Samaki na Uhifadhi wa Mazingira  Gando Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba na kujionea miti iliyooteshwa katika bustani ya kikundi hicho. 6Vijana wakitengeneza maseredani majiko ya udongo katika kijiji cha Chanjaani shehia ya Ukunjwi katika jimbo la Gando. 7Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akishiriki kupaka rangi majiko yaliyotengenezwa tayari katika kijiji cha Chanjaani Shehia ya Ukunjwi Mkoa wa Kaskazini Pemba. 
 8 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na viongozi aliofuatana nao wakiangalia mafundi wa Tanesco wakati wakiunganisha umeme  katika mradi wa usambazajiwa umeme jimbo la Mtambwe wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba 9Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiunganisha umeme wakati aliposhiriki shughuli ya usambazajiwa umeme jimbo la Mtambwe wilaya ya Wete  Mkoa wa Kaskazini Pemba 10Afisa Uhusiano wa Shirika la Umeme Zanzibar Fakhi Othman Sharif akitoa taarifa kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati alipotembelea na kukagua mradi wa Usambazaji wa umeme jimbo la Mtambwe.  11Mmoja wa wananchi wa jimbo hilo akielezea furaha yake mara baada ya baada ya kuunganishiwa umeme katika kijiji chao. 12Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akishiriki shughuli ya kuunganisha mabomba ya maji katika mradi wa usambazaji maji jimbo la Mtambwe Wete  Mkoa wa Kaskazini Pemba 13Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katikati, Balozi Amani Karume kushoto na Mama Maua Daftari kulia wakishiriki kufukia mambomba ya maji katika mradi huo.  14Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akisikiliza taarifa ya Hamiar Adi Makamu Mwenyekiti  kuhusu ujenzi wa Maskani ya Jakaya Kikwete Sheia ya Chekea Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba ambapo Kinana ameichangia maskani hiyo mabati 50 na mifuko 20 ya saruji. 15Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Ndugu Maua Daftari akizungumza wakati msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ulipotembelea katika tawi la Kigangani jimbo la Ole. 16Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Ndugu Maua Daftari akizungumza katika mkutano wa hadhara mjini Wete Pemba. 17Viongozi mbalimbali wakiwa wamekaa meza kuu wakati wa mkutano huo.  18Mkutano huo ukiendelea. 21Mohamed Abood  Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohamed  Aboud Mohamed akiwahutubia wananchi katika mkutano huo. 22Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Mtemani mjini Wete Kaskazini Pemba. 23Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwapa somo wananchi hao waliohudhuria kwenye mkutano huo.

No comments:

Post a Comment