TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, January 27, 2015

WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU YA KWANZA WA RAIS FATMA ABDULHABIB FEREJI AELEZEA JUU YA UKATAJI WA MITI AINA YA MIKOKO

index
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu ya kwanza wa Rais Fatma Abdulhabib Fereji
…………………………………….
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu ya kwanza wa Rais Fatma Abdulhabib Fereji amesema ukataji wa miti aina ya mikoko husababisha uharibifu mkubwa wa mazingira na kufanya maji ya bahari kuingia katika maeneo ya kilimo na makaazi ya watu.
Hayo ameyaeleza katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani wakati alipokuwa akijibu suala la Mwakilishi Bikame Yussuf Khamis alietaka kujua mpango wa dharura wa Serikali katika kuyanusuru mazingira ya bahari ili kuviokoa visiwa vidogo.
Waziri Fereji amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiyana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatarajia kutekeleza mradi wa kujenga uwezo wa kuhimili athari za mabadiliko ya tabia ya nchi katika maeneo ya ukanda wa pwani ya Tanzania utakaohusisha maeneo ya Bagamoyo , Pangani , Rufiji na Zanzibar.
Amesema eneo la Kisiwapanza ni miongoni mwa maeneo ya Zanzibar yanayotegemewa kuwemo kwenye mradi huu na tayari wataalamu wa mradi huo wamefika Zanzibar kwa ajili ya kuangalia maeneo ya mradi ambayo ni Kisiwapanza , Tumbe na Ukele kwa Pemba na maeneo ya Kilimani na Bwawani kwa Unguja. Hivi sasa wataalamu hao wako katika hatua ya mataarisho na kufahamu upeo wa mradi kwenye maeneo husika ambapo Zanzibar imekadiriwa kupata kiasi cha dola za marekeni 361,300 kwa ajili ya mradi huo. Akijibu suala la nyongeza aliloulizwa na Mwakilishi wa Jimbo la Chonga Abdullah Juma, Waziri Fereji amesema Ofisi pekee haiwezi kudhibiti kina cha maji ya bahari kwani ni suala la maumbile, hivyo wananchi wanapaswa waelimishwe athari za uharibifu wa mazingira ili waweze kuachana na vitendo hivyo.Wakati huo huo Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo amesema sera ya Serikali ya matibabu bure Zanzibar bado ipo na inaendelea kufanya kazi, licha ya kwamba wananchi wamekuwa wakichangia kwango kidogo cha huduma za afya.Akijibu suala la Mh Ali Salum Haji (Jimbo la kwahani ) aliyetaka kujua mpango wa Serikali wa kuanzisha sera ya msamaha kwa baadhi ya makundi ya watu wakiwemo wazee wenye umri mkubwa na watoto chini ya miaka mitano kupata matibabu bila malipo kama zilivyo nchi nyengine jirani.
Naibu Waziri amesema Wizara ya Afya inaandaa miongozo ya uchangiaji wa huduma za afya ambapo makundi maalumu yameainishwa kupatiwa msamaha wa kuchangia huduma hizo.
Ameyataja makundi hayo ni watoto wenye umri chini ya miaka 5 wazee wasiojiweza , walemavu wasiojiweza, watu wenye maradhi sugu kama vile ukimwi, kifua kikuu na saratani, na kwa wale wasiokuwa na uwezo bado wanaendelea kupata huduma za afya kulingana na taratibu zilizowekwa .

No comments:

Post a Comment