TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, January 27, 2015

SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR YAITAJI AFISA MUANDAMIZI WA CHEO CHA NAIBU KAMISHNA WA MAMLAKA WA MAPATO TANZANIA (TRA)

index
Na Maryam Kidiko/
Kijakazi Abdallah – 
 Maelezo Zanzibar .
    
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema Kuna umuhimu mkubwa Zanzibar kuwa na Afisa muandamizi wa cheo cha Naibu Kamishna wa Mamlaka wa Mapato Tanzania (TRA) kwa lengo la kusimamia ukusanyaji wa Mapato yatokanayo na  ushuru wa Fedha na ushuru wa bidhaa  katika juhudi za  kuimarisha shughuli  za uchumi wa Zanzibar.
Hayo yalisemwa na  Waziri wa Fedha Omar Yussuf Mzee wakati akijibu suali la Mh, Jaku Hashim Ayoub Jimbo la Muyuni alietaka kujua kama kuna  ulazima wowote wa TRA kuwa na Afisa muandamizi wa cheo  hicho Zanzibar.
Amesema Mamlaka ya Mapato Tanzania  ni Taasisi ya Muungano iliyoundwa kwa mujibu wa sheria Na.11 ya mwaka 1985 ambapo inapaswa kuwa na  Ofisi yake Zanzibar.
Amesema kuwa kazi ya TRA Zanzibar nikukusanya Mapato ya Muungano yanayotokana na kodi ya Mapato,  Ushuru wa Fordha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa nchini kama ilivyoainishwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Ameongeza kuwa kodi itokanayo na ushuru wa Forodha inasimamiwa na Sheria ya Ushuru wa Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya 2004 na kwa mujibu wa sheria hiyo Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ni moja kati ya sehemu ya nchi wanachma wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.
Waziri wa Fedha alieleza kuwa  sheria ya ushuru ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki imeweka utaratibu wa uwekaji thamani Bidhaa zinazotoka Nje na Ndani ya Nchi ya Wanachama wa Jumuiya hiyo.
Amesema kwa  vile Zanzibar ni kisiwa  kutumia Viwango vya Kodi moja kunaweza kuathiri Uchumi wake hivyo Serikali imeweka utaratibu wa viwango vya kodi tofauti kama ilivyoainiswa katika sheria ya ushuru wa Forodha wa bidhaa zinazoingizwa Zanzibar kwa madhumuni ya soko na matumizi ya ndani
Jumla ya skuli ishirini na moja (21) za sekondari zimejengwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzinar kwa kushirikiana na Benki ya Dunia na Benki ya Kiarabu kwa Maendeleo ya Afrika (Badea)
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mh. Zahra Ali Hamad  ameeleza hayo katika ukumbi wa Baraza la Wawakilshi Chukwani wakati akijibu suali la Mwakilishi  wa Rahaleo Nassor Salim Ali  aliyetaka kufahamu   mpango  wa Serikali  wa kujenga majengo mapya ya kisasa ya ghorofa katika skuli  ya  Mwembeshauri iliyondani ya Jimbo lake kama bado upo.
Bi. Zahra amemuhakikishia Mwakilishi huyo kwamba mpango wa kujenga skuli ya ghorofa katika eneo la skuli hiyo upo kutokana na kubainika kuwepo kwa idadi kubwa ya wanafunzi katika mitaa ya karibu na skuli hiyo.
Alisema kuwa mbali na utekelezaji wa mpango  huo,  Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kushirikiana na mfuko wa OPEC inakusudia kujenga skuli kumi  10 za ghorofa ambapo mradi huo ulichelewa kuanza kutokana na kutokamilika  taratibu za kisheria kuhusu makubaliano ya mkopo.
Wakati huo huo Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati  inakusudia kumaliza  tatizo la upatikanaji wa huduma za maji ifikapo mwaka 2017 kwa Wananchi wa Mji mkogwe na Ng’ambu.
Hayo yameelezwa na Naibu  Waziri wa wizara hiyo   Mh. Haji Mwadini Makame wakati akijibu suali la Muwakilishi Ali Salum Haji (Jimbo la Kwahani) alitaka kujua  juhudi za serikali za kuondoa tatizo hilo linalowakabili wananchi wengi hasa sehemu za mjini.
Amesema kuwa wanakusudia kumaliza tatizo kwa kuimarisha huduma hiyo kwa kuimarisha miundo mbinu ikiwemo kubadilisha  Mabomba ya zamani  ambayo yamechoka na kushindwa kuhimili ongezeko kubwa la wahamiaji.
Aidha alisema kuwa hali ya upatikanaji wa maji katika Mkoa wa Mjini inaendelea kuimarika siku hadi siku ambapo kuna baadhi ya maeneo yanapata Maji kwa muda mrefu na mengine yanapata maji kwa mgao hasa wakati wa kiangazi  na maeneo machache hukosa kabisa.
Alisema kupitia Mamlaka ya maji wamekuwa wakifanya juhudi kutafuta  ufumbuzi  wa suala hilo ikiwa ni pamoja na  uchimbaji wa Visima  vipya katika maeneo mbali mbali.                                                                           
IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

No comments:

Post a Comment