TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, March 7, 2015

MMILIKI WA KAMPUNI YA URBAN AND RULAR ENGINEERING PAMOJA NA WAJUMBE WAKE WAMTEMBELEA BALOZI LIBERATA MULAMULA



 Mkurugenzi na mmiliki wa kampuni ya urban and rular engineering ndugu Awadh Zuberi pamoja na ujumbe wake pichani wamemtembelea Balozi Liberata Mulamula, Kuanzia kushoto ni  ndugu Paula Mwafongo (Afisa Ubalozi uchumi),Bwa. Joseph Mnzanilla ,Mh.Bbalozi Mulamula,Bwa. Awadh Zuberi,Shemuni Halahala pamoja na ndugu Majid Zuberi wakiwa katika picha ya pamoja.


Mkurugenzi wa Urban and Rular  Engineering wa kwanza kulia ndugu Awadh  Zuberi na msaidizi wake Shemuni Halahala wakiwasili  Tanzania house ,ubalozini Washington, D.C.

MGOGORO KUHUSU MAGARI YA TANZANIA UTATATULIWA HIVI KARIBUNI- WAZIRI NYALANDU

itb1Waziri wa Maliasili na Utalii wa Tanzania Mh.Lazoro Nyalandu akizungumza wakati wa hafla ya siku ya Jumuia ya Afrika Mashariki iliyofanyika katika banda la Tanzania katika maonesho ya ITB berlin Ujerumani
itb2Waziri Nyalandu katika picha ya pamoja na Mawaziri wenzake Mh. Phylis Kandie (Wa pili kushoto), Waziri wa Maliasili na Mambo ya Kale wa Ugand Mh. Maria Mutagamba (wa pili kulia) na wageni wengine mashuhuri katika banda la Tanzania.

Wadau wa Utamaduni washauriwa kutoiga tamaduni za nchi nyingine

UT1Kaimu Mkuu wa Idara ya Utamaduni Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Afisa Bw. Habibu Msami akimkaribisha Mgeni rasmi kufunga kikao kazi cha kumi cha sekta ya Utamaduni jana Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mgeni rasmi akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi.
UT2Mgeni rasmi wakati wa kufunga kikao kazi cha sekta ya utamaduni akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi akizungumza na wadau wa utamaduni kuwapongeza kuwa na ushirikiano katika kutekeleza majukumu yao. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Idara ya Utamaduni Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Afisa Bw. Habibu Msami

WAFANYAKAZI WA RADIO 5 WANOLEWA NA BBC MEDIA ACTION

???????????????????????????????
Wafanyakazi wa kampuni ya Tan Communication Media  inayo miliki kituo cha  Radio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha wakiwa katika picha ya pamoja jana katika mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kitaaluma ili waweze kuandika habari za kuboresha maisha ya jamii kwa kupata maendeleo kuelekea uchaguzi mkuu,mafunzo hayo yanaendeshwa na shirika lisilo la kiserikali la BBC Media Action, aliyevalia shati la blue ni mkufunzi mwandamizi Pendael Omari wa shirika hilo(Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
???????????????????????????????
Mkufunzi mwandamizi Pendael Omari wa shirika lisilo la kiserikali la BBC Media Action akiwa anatoa ufafanuzi katika mafunzo hayo yaliyokuwa yakifanyika katika ofisi za Radio 5,mafunzo hayo yalidumu kwa takribani wiki mbili

Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) lazindua mauzo ya nyumba zake za Victoria Place, Dar

 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akifanya mahojiano na Ephraim Kibonde wa Kipindi cha Maisha ni Nyumba cha Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwenye uzinduzi wa nyumba za makazi za Victoria jana jioni kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria kwenye uzinduzi wa nyumba za makazi za Victoria jana jioni kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Nyumba hizo za makazi zitaanza kuuzwa rasmi Jumatatu.

Spika Makinda, Wenyeviti wa Bunge Watembelea Miradi ya NSSF Dar

Meneja Mradi wa NSSF, Mhandisi John Msemwa (mwenye kipaza sauti) akielezea maendeleo ya mradi wa ujenzi wa nyumba za kisasa zinazojengwa na shirika hilo Kigamboni jijini Dar es Salaam kwa Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge walipo tembelea mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa ubia na Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa Kigamboni.
Meneja Mradi wa NSSF, Mhandisi John Msemwa (mwenye kipaza sauti) akielezea maendeleo ya mradi wa ujenzi wa nyumba za kisasa zinazojengwa na shirika hilo Kigamboni jijini Dar es Salaam kwa Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge walipo tembelea mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa ubia na Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa Kigamboni.
Meneja Mradi wa NSSF, Mhandisi John Msemwa (mwenye kipaza sauti) akielezea maendeleo ya mradi wa ujenzi wa nyumba za kisasa zinazojengwa na shirika hilo Kigamboni jijini Dar es Salaam kwa Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge walipo tembelea mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa ubia na Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa Kigamboni.
Meneja Mradi wa NSSF, Mhandisi John Msemwa (mwenye kipaza sauti) akielezea maendeleo ya mradi wa ujenzi wa nyumba za kisasa zinazojengwa na shirika hilo Kigamboni jijini Dar es Salaam kwa Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda pamoja na wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge walipo tembelea mradi wa daraja la kisasa linalojengwa na NSSF kwa ubia na Serikali kuunganisha Jiji la Dar es Salaam na mji wa Kigamboni.

KANUNI KUWABANA WAKWEPA KODI

kit5
* Kitwanga aagiza wachimbaji madiniwasiolipa wanyang’anywe leseni
Veronica Simba na Rhoda James Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Madini), Charles Kitwanga amewataka Maofisa wa Serikali katika sekta ya madini nchini kutumia kanuni zinazoongoza sekta hiyo kuwabana wachimbaji wadogo wa madini wanaokwepa kulipa kodi mbalimbali zilizowekwa na Serikali. Kitwanga ametaka kanuni husika zitumike kuwachukulia hatua kali wakwepa kodi hao ikiwa ni pamoja na kuwanyang’anya leseni za uchimbaji madini wanazomiliki.

Gharama za kuunganisha umeme shilingi 177,000. Atakayetoza zaidi ya hapo kufikishwa polisi – Ndassa

NDA1\Meneja Miradi kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Mhandisi Khalid James (kulia) akiieleza Kamati ya   Bunge ya Nishati na Madini hatua iliyofikiwa ya   ujenzi wa miundombinu ya umeme katika   mikoa ya Iringa, Dodoma, Singida hadi   Shinyanga inayosimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Awamu ya Pili. Kamati ya Bunge inafanya ziara katika mikoa ya Dodoma, Singida, Arusha na Kilimanjaro kwa ajili ya kukagua miradi ya umeme   ili kujionea maendeleo yake pamoja na kuzungumza na wananchi
NDA2Meneja Miradi kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Mhandisi Khalid James (katikati) akitoa maelezo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuhusu maendeleo ya ujenzi wa njia kuu za umeme unaofanywa na kampuni ya Jyoti Structures Limited kutoka India katika eneo la Nara mkoani Dodoma
………………………………………………………………………….

Stara T aachia wimbo wa Siku ya Wanawake Duniani

Msanii Stara T, ametoa wimbo mpya UWEZESHWAJI WA MWANAMKE ambao ni maalum kwa ajili ya siku ya kinamama dunia inayoadhimishwa Machi 8 ya kila mwaka.

MKURUGENZI MKUU MPYA WA TBL AKAGUA MAJENGO YAO WALIYOYAKABIDHI KWA CHUO KIKUU CHA STEPHANO MOSHI

 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bia Tanzania TBL,Roberto Jarrin akiongozwa na mkufunzi katika Chuo Kikuu Kishiriki cha kumbukumbu ya Stephano Moshi,Gasper Mpehongwa kutembelea vyumba vya madarasa ambavyo vinatumika kwa ajili ya masomo pamoja na mitihanikatika eneo la TBL mjini Moshi.Eneo hilo limetolewa na TBL kwa chuo hicho ikiwa ni kurudisha sehemu ya faida inayopatikana kwa wananchi.
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bia Tanzania TBL,Roberto Jarrin akiwa ameambatana na mkuu wa chuo Kikuu Kishiriki cha kumbukumbu ya Stephano Moshi,Profesa Anord Temu,wakati akitembelea majengo ya jengo hilo mjini Moshi.

KATIBU MKUU WA CCM NDG. ABDULRAHMAN KINANA KATIKA ZIARA KONGWA

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Kongwa na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Job Ndugai wakati alipowasili katika eneo la Kongwa Junction akitokea wilayani Mpwapwa ambako ndiko alikoanzia ziara yake ya mkoa wa Dodoma kabla ya kuanza katika jimbo wilaya ya Kongwa, Kinana yuko katika ziara ya mikoa ya Dodoma, Arusha na Kilimanjaro akikagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 na kuhimiza uhai wa Chama cha Mapinduzi CCM  na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi ili kuzipatia ufumbuzi, Akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa Itikadi na Uenezi.(PICHA NA KIKOSIKAZI  CHA FULLSHANGWE-KONGWA)

WAZIRI NYALANDU AKUTANA NA WAZIRI MWENZAKE WA KENYA ITB BERLIN

laz1Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akiwa na Waziri wa Biashara na Utalii wa Kenya Bibi Phylis Kandie mara baada ya mazungumzo yao.

SERIKALI YAANZISHA MFUMO WA KIELEKTONIKI KUSIMAMIA UTOAJI WA HUDUMA ZA ARDHI NCHINI.

unnamedWaziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akitoa ufafanuzi wa mfumo wa kielektroniki utakaosimamia utoaji wa huduma katika sekta ya ardhi. 
……………………………………………………………………………
Na. Aron Msigwa –MAELEZO.
 Dar es salaam.

SERIKALI YA JAPAN YAIPATIA MSAADA WA DOLA LAKI 1.4 HALMASHAURI YA WILAYA YA MONDULI

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiongozana na mwenyeji wake ambaye ni Kaimu Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Kazuyoshi Matsunaga wakati alipowasili nyumbani kwa Balozi huyo,Masaki Jijini Dar es salaam,kulikofanyika hafla fupi ya kusaini mkataba wa makubaliano wa kufanikisha Miradi miwili iliyopo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Monduli,jijini Arusha.Serikali ya Japan imeipatia Halmashauri hiyo dola za kimarekani 142,251 (sawa na Shilingi Milioni 250) kwa ajili ya kufanikisha miradi hiyo.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
Kaimu Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Kazuyoshi Matsunaga (kushoto) akionyesha kitu kwenye karatasi kwa Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa pamoja Mbunge wa Viti Maalum – Monduli,Mh. Namelock Sokoine,wakati wa hafla fupi ya kusaini mkataba wa makubaliano wa kufanikisha Miradi miwili iliyopo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Monduli,jijini Arusha.Serikali ya Japan imeipatia Halmashauri hiyo dola za kimarekani 142,251 (sawa na Shilingi Milioni 250) kwa ajili ya kufanikisha miradi hiyo.

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA UZINDUZI WA STUDIO ZA AZAM ULIOFANYWA NA RAIS JAKAYA KIKWETE

AZA1Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitangaza rasmi kuzinduliwa kwa studio mpya za stesheni ya Azam TV  Tabata Relini jijini Dar es salaam leo Machi 6, 2015. Pamoja naye kwenye kilinge cha utangazaji ni mmiliki wa stesheni hiyo Bw. Saidi Salim Bakhressa.(PICHA NA IKULU)
AZA2 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Naibu Mkurugenzi wa Azam TV Bw. Dunstan Tido Mhando wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa studio mpya za stesheni hiyo iliyopo Tabata Relini jijini Dar es salaam leo Machi 6, 2015. 

Mashabiki wamtaka Rose Muhando .Msama apata kigugumizi

indexNa Mwandishi Wetu
MASHABIKI   kadhaa  wa  muziki  wa Injili  Tanzania  wametamka kumtaka  muimbaji  nguli  wa  muziki  wa  Injili  kuwemo  katika  orodha  ya  waimbaji  watakaopanda  jukwaani  kwenye  Tamasha  la  Pasaka  linalotarajia  kufanyika  mwezi  ujao hapa nchini.
Voster  Maulid  na Kassim Mtolea wa  jijini  Mwanza  wanampenda kwa kiasi kikubwa muimbaji huyo hasa anapokuwa jukwaani.
Mashabiki  hao  walisema  muimbaji  huyo  akifanikiwa  kupanda  jukwaani anasaidia  kuteka  idadi  kubwa ya mashabiki  wanaohudhuria matamasha anayohudhuria.

Rais Jakaya azindua studio za Azam Media jijini Dar leo

AZ1Rais Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akikata utepe kuzindua rasmi studio za kisasa za Azam Media jijini Dar es Salaam leo. Rais Kikwete alizindua studio hizo ambazo ni  za kisasa zaidi zilizowahi kufunguliwa katika nchi za Afrika Mashariki na Jangwa la Sahara zilizogharimu sh Bilioni 53. Wengine kutoka kushoto ni Naibu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Tido Mhando, Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Fenella Mukangara na Mwenyekiti Mtendaji wa  Makampuni ya Bakhresa, Said Salim Bakhresa.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA KWA MWENYEKITI WA CCM MKOA WA IRINGA

Mwenyekiti  wa CCM mkoa  wa Iringa  Jesca Msambatavangu  akionyesha kanuni  za  uongozi na maadili za CCM leo  alipozungumza na  wanahabari mkoa  wa Iringa
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa  Jesca Msambatavangu  akizungumza na  wanahabari leo  ofisi ya  chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC()
Wanahabari  Iringa  wakimsikiliza mwenyekiti wa CCM mkoa
…………………………………………………………………………….
ILIYOJITOKEZA BAADA YA MAAMUZI MBALI MBALI
KUFANYIKA NA KUTANGAZWA KUHUSU MAADILI YA UONGOZI.
UTANGULIZI
Mtakumbuka kuwa tarehe 2/3/2015 kuna kauli ambayo ilitolewa na Katibu wa wilaya ya Mufindi Ndugu Mtaturu.
 Ambayo ilielekeza baadhi ya hatua
zilizochukuliwa na Chama cha Mapinduzi kwa baadhi ya wanachama wetu,
ikiwa ni pamoja na kufukuzwa uanachama kwa baadhi ya makada wetu.
 Akiwemo Shukuru Luhambati, Clara Shirima na Hosea Kaberege. Swala hili
limeamusha malalamiko na mjadala miongoni mwa wanaCCM na wapenzi na
wakereketwa wa CCM. Kila mtu akiwa na mtizamo wake kuhusu swala hili,
ambalo pia kimepelekea kuamsha malumbano katika vyombo mbali mbali vya
habari.

Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni, Utamaduni na Michezo wawakutanisha Wanachama wa Timu ya Pan Afican

indexNa Happy Shirima – Maelezo.
Wizara ya Habari , Vijana, Utamaduni na Michezo imeandaa mkutano mkuu wa wanachama wote wa klabu ya mpira wa miguu ya Pan-African utayofanyika Machi 7 ,mwaka huu saa 3 asubuhi katika ukumbi wa mikutano Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.
Taarifa hiyo imetolewa na Wizara hiyo leo Jijini Dar es salaam ambapo imesema kuwa mkutano huo unatokana na uwepo wa mgogoro wa muda mrefu miongoni mwa wanachama wa klabu hivyo kupelekea ofisi ya msajili kutaka kupata taarifa za kina kutoka kwa wanachama wa makundi  yote.

MKE WA RAIS MAMA SALMA KIKWETE KUWA MGENI RASMI SIKU YA WANAWAKE DUNIANI.

index
Na Happy Shirima – Habari Maelezo.
 Dar es salaam.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo [WAMA] anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yatakayofanyika Machi 8 mwaka huu katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam .

WANAWAKE CUF WETE WAWA NA MWITIKIO MDOGO WA KUGOMBEA UONGOZI

index
Na Masanja Mabula -Pemba
Mchakato wa uchukuwaji wa fomu za kugombea nafasi mbali mbali za Uongozi wa Majimbo na Wadi ndani ya Chama Cha Wananchi (CUF)  katika Wilaya ya Wete  unaendelea vyema huku kukiwa na mwitiko mdogo wa wanawake kuchukua fomu  kuwania nafasi hizo .
Ikiwa zimebakiwa siku nne (4)  kufungwa kwa zoezi hilo katika Majimbo ya Gando na Mtambwe  jumla ya wanachama kumi na tano (15) wa chama hicho wamejitokeza kuchukua fomu za kugombea nafasi za ubunge .
Katika nafasi ya uwakilishi jumla ya wanachama sita (6) ndiyo waliochukua fomu hizo ambapo kwa upande wa nafasi ya diwani waliochukua fomu ni wanachama sita (6) huku wadi ya Bopwe na Fundo hakuna mwanachama aliyechukua fomu .
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Katibu wa CUF Jimbo la Gando Khelef Mohammed amesema kuwa nafasi ya Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi ambayo inashikiliwa na Said Ali Mbarouk ni mwanachama mmoja ndiye aliyechukua fomu .

TAARIFA YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KWA KUTUMIA TEKNOLOJIA YA BIOMETRIC VOTER REGISTRATION (BVR) KATIKA KATA TISA (9) ZA HALMASHAURI YA MJI WA MAKAMBAKO KUANZIA TAREHE 23/2/2015 HADI 3/3/2015


imagesTume ya Taifa ya Uchaguzi imeanza rasmi zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura baada ya kukamilika kwa maandalizi muhimu ya Uboreshaji wa Daftari, ikiwemo manunuzi ya vifaa na upatikanaji wa fedha kutoka Serikalini.

Tanesco na Helios Tower Tanzania wafanya warsha ya siku moja juu ya usambazaji wa Umeme

 
Eranus Thompson, Mkuu wa uendeshaji wa Kanda ya Dar Es Salaam na Pwani kutoka Kampuni ya Helios Tower Tanzania akizungumza jinsi Helios Tower wanavyoweza kusambaza umeme unaozalishwa na Tanesco wakati wa warsha ya siku moja na Wafanyakazi wa Shirika la Umeme la Tanzania (Tanesco) iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwl Nyerere.

Kitwanga aagiza wachimbaji madini wasiolipa wanyang’anywe leseni

kit1Kaimu Kamishna Msaidizi wa Madini, Sehemu ya Uchumi na Biashara ya Madini, Aloyce Tesha (Kulia) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Madini), Charles Kitwanga (Kushoto) kuhusu utendaji kazi katika sekta hiyo. Naibu Waziri Kitwanga aliwatembelea Watumishi wa Idara ya Madini kuzungumza nao na kukagua utendaji kazi wao.
kit2Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Madini), Charles Kitwanga (wa kwanza Kulia), akifafanua jambo kwa Viongozi wa Idara ya Madini alipokutana nao kujadili utendaji kazi katika sekta hiyo. Naibu Waziri Kitwanga aliwatembelea Watumishi wa Idara ya Madini kuzungumza nao na kukagua utendaji kazi wao.
kit3 Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Madini), Charles Kitwanga (Katikati) akizungumza na baadhi ya Wafanyakazi wa Idara ya Madini alipowatembelea kujionea utendaji kazi katika Idara hiyo.
…………………………………………………………………………… Veronica Simba na Rhoda James Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Madini), Charles Kitwanga amewataka Maofisa wa Serikali katika sekta ya madini nchini kutumia kanuni zinazoongoza sekta hiyo kuwabana wachimbaji wadogo wa madini wanaokwepa kulipa kodi mbalimbali zilizowekwa na Serikali. Kitwanga ametaka kanuni husika zitumike kuwachukulia hatua kali wakwepa kodi hao ikiwa ni pamoja na kuwanyang’anya leseni za uchimbaji madini wanazomiliki. Aliyasema hayo hivi karibuni alipokutana na Viongozi wa Idara ya Madini katika Wizara husika hivi karibuni jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuzungumza nao na kujionea utendaji kazi wao. Akizungumza na Viongozi hao, Kitwanga alisema wachimbaji wadogo wa madini, kama walivyo wafanyabiashara wengine nchini, wanawajibika kulipa kodi zote zilizowekwa na Serikali ikiwa ni pamoja na kodi ya huduma, mrahaba na nyingine ili kuiwezesha Serikali kupata mapato stahiki kwa lengo la kuwaletea wananchi wake maendeleo. “Inabidi tujenge nidhamu katika kazi, vinginevyo hatutafika kwenye uchumi wa kati tunaoutarajia ifikapo mwaka 2025. Kama mtu anakaa na leseni bila kulipa, tutumie kanuni kumnyang’anya. Kwa mfano, mtu asipolipa TRA kwa biashara yake, watamwacha kweli?” alisisitiza Naibu Waziri. Akifafanua zaidi, Kitwanga alisema ili kupata matokeo chanya katika kazi yoyote, inabidi kutenda yale yaliyo sahihi na siyo kutenda mambo kwa usahihi, akitumia msemo maarufu wa lugha ya kiingereza ‘Do the right thing, don’t do things right.’ “Inapotokea kuna sheria imepitwa na wakati, si sahihi kuendelea kuifuata tu bila kutafuta namna ya kuirekebisha kwa manufaa ya wananchi,” alisisitiza Kitwanga na kuongeza kuwa ni lazima kutumia kanuni mbalimbali zilizopo kubadilisha mambo inapobidi na kutenda mambo sawa sawa kwa manufaa ya wananchi. Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Kitwanga aliwataka Watendaji katika Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kuwasaidia wachimbaji wadogo wa madini ili watoke katika uchimbaji mdogo na kuwa wachimbaji wa kati na kuendelea, hivyo kukuza kipato chao na uchumi wa nchi kwa ujumla. “Ni lazima ifike mahala madini yetu yachimbwe na Watanzania wenyewe hali itakayosaidia mzunguko wa fedha nchini kuwa mkubwa zaidi,” alisema. Aidha, Naibu Waziri Kitwanga aliwataka Stamico watakapokuwa wanachimba madini, wahakikishe faida yote inarudi nchini ili kukuza mzunguko wa fedha na hivyo kuinua uchumi wa nchi. “Hata wenzetu wanapeleka fedha zote za faida kwao. Wanazobakiza hapa, ni zile tu wanazohitaji kuendeshea biashara,” alitoa mfano. Akizungumza na Wafanyakazi wa Wakala wa Ukaguzi Madini Tanzania (TMAA), Naibu Waziri Kitwanga aliwataka kufanya kazi kwa juhudi ili kuhakikisha mapato ya Serikali yanakusanywa kikamilifu. “Leteni maoni kuhusu nini zaidi kifanyike ili kuhakikisha mapato ya Serikali katika sekta ya madini yanaongezeka,” alisisitiza Kitwanga.

Naibu Katibu Mkuu wa UDP Zanzibar amvaa Maalim Seif

index 


kuu wa UDP Zanzibar Juma Khamis Fakih amemvaa Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Maalim
 Seif Sharif Hamad na kuigwaya kauli yake ya kuwataka wananchi kutoshiriki zoezi la upigaji wa kura ya maoni juu ya katiba inayopendekzwa .
Amesema kuwa kauli ya Katibu Mkuu wa CUF haina nia njema na wananchi wa Zanzibar na haifai kutolewa na Kiongozi wa juu wa Serikali kama huyo ambaye amepewa dhamana ya kuwaongoza na kuwatumikia wazanzibar .

MAFUNZO YA SIKU TATU KWA WAFANYAKAZI WA SEKTA YA AFYA ZANZIBAR JUU YA KUKABILIANA NA UGONJWA WA EBOLA YAFUNGWA.

af1 Mkuu wa kitengo cha kufuatilia mwenendo wa maradhi Zanzibar Dkt. Salma Masauni akitoa neno la shukrani mara baada ya kumaliza mafunzo ya siku tatu juu ya kukabiliana na ugonjwa wa Ebola, mafunzo hayo yamezaminiwa na Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) huko Hoteli ya Zanzibar Beach Resort.

ZI 10000 KUNUFAIKA NA UKARABATI BWAWA LA KALEMAWE

DSC_0001Mshehereshaji wa kongamano la siku moja lililofanyika jijini Dar kuzungumzia ukarabati na uendeshaji wa bwawa la Kalemawe lililopo wilayani Same mkoani Kilimanjaro, Mtaalamu wa masuala ya fedha wa UNCDF, Bw. Imanuel Muro akisherehesha kongamano hilo. Katikati ni mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Same, Herman Kapufi akifuatiwa na Mkuu wa ushauri wa ufundi wa Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF), Bw. Peter Malika.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)
Na Mwandishi Wetu

MSANII WA NYIMBO ZA INJILI, MKOANI IRINGA REHEMA CHAWE AACHIA ALBAMU YAKE YA GOSPEL

Muimbaji wa Nyimbo za Injili Rehema Chawe
………………………………………………………

Thursday, March 5, 2015

WADAIWA SUGU BILI WASABABISHA WANANCHI KUKOSA MAJI KATIKA MJI WA MPWAPWA, WAMO NMB

18Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Mpwapwa huku akiwa ameshikilia nyaraka za wadaiwa sugu wa bili za maji katika mji wa Mpwapwa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji katika mji huo Bw. Shadrack Mtemba.
Nyaraka hizo zina orodha kubwa ya wadaiwa zikiwemo taasisi za serikali , makampuni zikiweno benki kama vile NMB inayodaiwa fedha ndogo ambayo jumla yake ni shilingi  elfu 79.179.50 fedha ambayo ni ndogo sana ikiwa ni bili ya mwezi wa pili 2015.
Sauala hilo limekuja baada ya malalamiko ya wananchi katika mkutano huo ambapo walimweleza Katibu Mkuu wa CCM kuwa maji hayatoki, lakini kila mwezi wanadaiwa bili ya maji jambo ambalo limekuwa kero kubwa kwao, Akielezea sakata hilo mbele ya Katibu Mkuu wa CCM, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Mpwapwa Bw. Shadrack Matemba amesema mradi huo ni mkubwa na unatosheleza mahitaji ya maji kwa  wananchi wa mji wa Mpwapwa. tatizo ni kwamba Taasisi na makampuni mengi hayalipi bili zao kwa wakati jambo ambalo linafanya uendeshaji kuwa mgumu huku akikabidhi nyaraka za wadaiwa hao mbele ya Kinana

Sekereti ndani ya Tamasha la Pasaka Dar

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama (kulia) akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusiana na maandalizi ya tamasha hilo litakalofanyika Aprili 5. (Picha na Francis Dande)

Balozi wa Marekani Nchini amtembelea mwanasheria Mku wa Serikali

mar1Balozi wa Marekani nchini Tanzania Bw. Mark Childress akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Leo Jijini Dar es Salaam.
mar2Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. George Masaju (mwenye tai nyekundu) akiwa katika picha ya pamoja na balozi   wa Marekani nchini Tanzania Bw. Mark Childress(wa pili kulia) mara baada ya mazungumzo.

KIJIJI CHA GONGONI WILAYANI KILOSA WAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI, WANAWAKE WAPATA HATI MILIKI ZA ARDHI

Angelina Mziray Katibu Mkuu wa Women and Poverty Alleviation in Tanzania  , Akiwakaribisha wageni Mbalimbali waliofika katika Sherehe za Kuazimisha Siku ya Wanawake Duniani ambapo wao wameadhimisha mapema,Katika Ufunguzi Alisema kuwa Shirika lisilo ka Kiserikali la Waupata wakishirikiana na OXFAM wamesaidia Kijiji hicho katika kuleta maendeleo mbalimbali Tangu mwaka 2006 ikiwa ni pamoja na Kilimo cha mpunga, Matumizi Bora ya Ardhi, Ambapo Pia aliwashukuru OXFAM kwa kuleta ufugaji bora wa kuku wa kienyeji, na ujenzi wa masoko mawili ya kisasa, Pia kusaidia wanawake kupata hati milili za Ardhi ambapo wanawake 186 watapata Hati hizo. Mwisho alishukuru taasisi zengine zisizo za Kiserikali ikiwemo Mviwata,Ungo,Tupawaki pamoja na Mwayodeo kwa jitihada zao za kusaidia wanawake na wanakijiji cha Gongoni katika maendeleo ya kijiji hicho.
 Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster