TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, March 7, 2015

KATIBU MKUU WA CCM NDG. ABDULRAHMAN KINANA KATIKA ZIARA KONGWA

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Kongwa na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Job Ndugai wakati alipowasili katika eneo la Kongwa Junction akitokea wilayani Mpwapwa ambako ndiko alikoanzia ziara yake ya mkoa wa Dodoma kabla ya kuanza katika jimbo wilaya ya Kongwa, Kinana yuko katika ziara ya mikoa ya Dodoma, Arusha na Kilimanjaro akikagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 na kuhimiza uhai wa Chama cha Mapinduzi CCM  na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi ili kuzipatia ufumbuzi, Akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa Itikadi na Uenezi.(PICHA NA KIKOSIKAZI  CHA FULLSHANGWE-KONGWA)

2
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia moja ya vikundi vya ngoma vilivyomlaki wakati wa mapokezi eneo la Kongwa Junction huku mmoja wa wanakikundi akipiga ngoma huku akiwa amembeba mtoto wake mgongoni.
3
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupalilia shamaba la kijiji pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mheshimiwa Bituni Msangi na mkuu wa mkoa wa Dodoma Luteni Mstaafu Chiku Galawa kulia pamoja na wananchi wengine katika kata ya Iduo
4
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akirejea mara baada ya  kupalilia shamaba la kijiji pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mheshimiwa Bituni Msangi na wananchi wengine katika kata ya Iduo
5
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  na mbunge wa jimbo la Kongwa Mh. Job Ndugai wakifungua maji kwenye kituo cha Mlali wilaya ya Kongwa.
6
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimtwisha ndoo ya maji Bi. Subiraga Bukuku mkazi wa kijiji cha Mlali mara baada ya kuzindua mradi wa maji katika kijiji hicho
8
 Mwenyekiti wa CCM Ndugu Adam Kimbisa akishiriki ufyatuaji wa matofali ya kujengea mabweni ya watoto wenye mahitaji maalum katika shule ya msingi Mlali B akishirikiana na Mkuu wa mkoa  wa Dodoma Ndugu Chiku Galawa.
10
Mbunge wa Jimbo la Kongwa na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Job Ndugai akihutubia wakati wa mkutano wa kuwasalimia wananchi wa kijiji cha Njoge na kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kushiriki ujenzi wa Zahanati.
11
Kikundi cha Ngoma kikitumbuiza wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipowasili kijijini kijijini  Njoge ili kushiriki ujenzi wa Zahanati ya kijiji hicho na kuzungumza na wananchi.

12
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Njoge pamoja na Mbunge wa jimbo la Kongwa Mh. Job Ndugai na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Mh. Adam Kimbisa.
14
Baadhi ya vikundi vikitoa burudani katika maeneo kadhaa ambayo Kinana ameyatembelea na kuzungumza na wananchi katika jimbo la Kongwa.
16 17
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Nape Nnauye Katibu wa Itikadi na Uenezi wakipungia wananchi mikono yao mara baada ya kuwasili katika eneo la mkutano katika kijiji cha Mkoka wilayani Kongwa.
18
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Luteni Mstaafu Chiku Galawa akizungumza na wananchi kabla ya viongozi wengine kupanda jukwaani.
19
Mbunge wa Jimbo la Kongwa Ndugu Job Ndugai akihutubia maelfu ya wananchi waliojitokeza kwa kwenye mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye yupo kwenye ziara ya kujenga na kuimarisha Chama.
20 21
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Mkoka wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma ambapo aliwaambia wananchi hao CCM ni Chama pekee chenye kujali Watanzania kinachosimamia na kuitunza amani iliyopo
22 23
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Adam Kimbisa akihutubia wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara ambao Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alikuwa mgeni wa Heshima, Kimbisa aliwaambia wana CCM kuwa Dodoma itakuwa mfano katika kutenda haki wakati wa uchaguzi mkuu ujao ndani ya chama .
24
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Mkoka wilayani Kongwa na kuwaambia moja ya sifa muhimu na ya kipekee kwa kiongozi anayefaa kuongoza wananchi ni Uadilifu.
26
28
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Mkoka wilayani Kongwa na kuwaambia moja ya sifa muhimu na ya kipekee kwa kiongozi anayefaa kuongoza wananchi ni Uadilifu.
Aliyekuwa Katibu Mwenezi Kata ya Ngomae na Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Chadema wilaya ya Kongwa Ndugu Makang’ata Nyanje akimkabidhi kadi yake ya Chadema Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya Msingi Mkoka wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma
29

No comments:

Post a Comment