TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, March 7, 2015

Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni, Utamaduni na Michezo wawakutanisha Wanachama wa Timu ya Pan Afican

indexNa Happy Shirima – Maelezo.
Wizara ya Habari , Vijana, Utamaduni na Michezo imeandaa mkutano mkuu wa wanachama wote wa klabu ya mpira wa miguu ya Pan-African utayofanyika Machi 7 ,mwaka huu saa 3 asubuhi katika ukumbi wa mikutano Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.
Taarifa hiyo imetolewa na Wizara hiyo leo Jijini Dar es salaam ambapo imesema kuwa mkutano huo unatokana na uwepo wa mgogoro wa muda mrefu miongoni mwa wanachama wa klabu hivyo kupelekea ofisi ya msajili kutaka kupata taarifa za kina kutoka kwa wanachama wa makundi  yote.
Aidha taarifa imefafanua kuwa wanachama wote waliopo Dar es Salaam wanaoweza kufika kwenye mkutano na wale ambao sio hai kwa sababu mbalimbali kama kutolipa ada kutohudhuria vikao na kutokuwa na kadi wanatakiwa kuhudhuria wote.
“Wanachama wote wanashauriwa kuwa wawe wamefika ukumbini saa tatu kamili asubuhi tayari kwa kikao hicho”ilieleza taarifa hiyo.
Hata hivyo Wizara imewaomba wanachama wote kushirikiana kwa maendeleo ya klabu ya Pan African na mpira wa miguu kwa ujumla.    

No comments:

Post a Comment