TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, March 7, 2015

MGOGORO KUHUSU MAGARI YA TANZANIA UTATATULIWA HIVI KARIBUNI- WAZIRI NYALANDU

itb1Waziri wa Maliasili na Utalii wa Tanzania Mh.Lazoro Nyalandu akizungumza wakati wa hafla ya siku ya Jumuia ya Afrika Mashariki iliyofanyika katika banda la Tanzania katika maonesho ya ITB berlin Ujerumani
itb2Waziri Nyalandu katika picha ya pamoja na Mawaziri wenzake Mh. Phylis Kandie (Wa pili kushoto), Waziri wa Maliasili na Mambo ya Kale wa Ugand Mh. Maria Mutagamba (wa pili kulia) na wageni wengine mashuhuri katika banda la Tanzania.

itb3Kikundi cha ngoma kutoka Kenya kikitumbuiza mawaziri, Mabalozi na wageni mbalimbali waalikwa katika siku ya Jumuia ya Afrika Mashariki katika banda la Tanzania.
……………………………………………………………….
Na: Geofrey Tengeneza – Berlin
Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Lazaro Nyalandu amesma kuwa serikali ya Tanzania inaamini kuwa zuio lililowekwa na Serikali ya Kenya kwa magari ya utalii kutoka Tanzania kuingia katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyata litatatuliwa na kuondolewa muda si mrefu kutokana na utayari wa kila nchi kukaa pamoaja na kuzungumzia suala hilo kwa lengo la kuona kuwa ushirikiano katika biashara ya utalii unaendelea kustawi kwa manufaa ya nchi hizi mbili na jumuia ya Afrka Mashariki kwa ujumla. Hayo yamesemwa na Waziri Nyalandu katika hafla ya siku ya Afrika Mashariki katika maonesho ya Kimataifa ya Utalii ya ITB Berlin Ujerumani iliyofanyika katika banda la Tanzania na kuhudhuriwa na Waziri wa Biashara na Utalii wa Kenya Mheshimiwa Phylis Kandie, Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale wa Uganda Mheshimiwa Maria Mutagamba,mabalozi wanaowakilisha nchi za Afrika Mashariki nchini Ujerumani na wageni wengine mashuhuri. “Napenda kuchuka nafasi hii kuwahikishieni mliopo hapa na dunia kwa ujumla kwamba hakuna tatizo lolote ambalo Tanzania na Kenya hatuwezi kulitatua katika meza ya mazungumzo” alisema. Waziri Nyalandu amedokeza kuwa tarehe 20 mwezi huu anatarajia kukutana Waziri Kandle wa Kenya kuzungumzia suala hili ambapokabla ya hapo tarehe 18 Machi Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na utalii Dk. Adelhelm Meru atakutana na katibu wa Wizara ya Biashara na Utalii ya Kenya.

No comments:

Post a Comment