TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, March 7, 2015

MSANII WA NYIMBO ZA INJILI, MKOANI IRINGA REHEMA CHAWE AACHIA ALBAMU YAKE YA GOSPEL

Muimbaji wa Nyimbo za Injili Rehema Chawe
………………………………………………………


MSANII wa nyimbo za Injili, nyanda za juu kusini Rehema Chawe ambaye ni Mwanachama wachama cha Muziki wa Injili Tanzania (CHAMUITA), anatarajia kuzindua albamu yake ya kwanza, inayoitwa Kusamehe ni afya.
Uzinduzi huo unatarajia
kufanyika Jumapili, March 8, mwaka katika kanisa la EAGT, Frelimo kwa mchungaji
Mwenda, ambaye ni Mwenyekiti wa makanisa ya Kipentekoste mkoani Iringa.
Akizungumza na wanahabari,
Chawe alisema uzinduzi huo utapambwa na waimbaji wengi toka nje na ndani ya
mkoa wa Iringa.
Alisema mgeni rasmi katika
uzinduzi huo atakuwa, ni mhadhiri wa chuo kikuu cha Iringa, Enock Ugulumo.
Mwenyekiti wa CHAMUITA mikoa
ya nyanda za juu kusini, Tumaini Msowoya Kibiki aliwataka wanachama wote kuwepo
kwenye uzinduzi huo ili kumsindikiza mwenzao.
“Ni jukumu la waimbaji wote
hususani wanachamuita kuhakikisha wanakuwepo siku ya uzinduzi ili kumuunga
mkono mwanachama wenzetu,”alisema Kibiki

No comments:

Post a Comment