TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, March 7, 2015

KANUNI KUWABANA WAKWEPA KODI

kit5
* Kitwanga aagiza wachimbaji madiniwasiolipa wanyang’anywe leseni
Veronica Simba na Rhoda James Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Madini), Charles Kitwanga amewataka Maofisa wa Serikali katika sekta ya madini nchini kutumia kanuni zinazoongoza sekta hiyo kuwabana wachimbaji wadogo wa madini wanaokwepa kulipa kodi mbalimbali zilizowekwa na Serikali. Kitwanga ametaka kanuni husika zitumike kuwachukulia hatua kali wakwepa kodi hao ikiwa ni pamoja na kuwanyang’anya leseni za uchimbaji madini wanazomiliki.

Aliyasema hayo hivi karibuni alipokutana na Viongozi wa Idara ya Madini katika Wizara husika hivi karibuni jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuzungumza nao na kujionea utendaji kazi wao. Akizungumza na Viongozi hao, Kitwanga alisema wachimbaji wadogo wa madini, kama walivyo wafanyabiashara wengine nchini, wanawajibika kulipa kodi zote zilizowekwa na Serikali ikiwa ni pamoja na kodi ya huduma, mrahaba na nyingine ili kuiwezesha Serikali kupata mapato stahiki kwa lengo la kuwaletea wananchi wake maendeleo. “Inabidi tujenge nidhamu katika kazi, vinginevyo hatutafika kwenye uchumi wa kati tunaoutarajia ifikapo mwaka 2025. Kama mtu anakaa na leseni bila kulipa, tutumie kanuni kumnyang’anya. Kwa mfano, mtu asipolipa TRA kwa biashara yake, watamwacha kweli?” alisisitiza Naibu Waziri. Akifafanua zaidi, Kitwanga alisema ili kupata matokeo chanya katika kazi yoyote, inabidi kutenda yale yaliyo sahihi na siyo kutenda mambo kwa usahihi, akitumia msemo maarufu wa lugha ya kiingereza ‘Do the right thing, don’t do things right.’ “Inapotokea kuna sheria imepitwa na wakati, si sahihi kuendelea kuifuata tu bila kutafuta namna ya kuirekebisha kwa manufaa ya wananchi,” alisisitiza Kitwanga na kuongeza kuwa ni lazima kutumia kanuni mbalimbali zilizopo kubadilisha mambo inapobidi na kutenda mambo sawa sawa kwa manufaa ya wananchi. Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Kitwanga aliwataka Watendaji katika Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kuwasaidia wachimbaji wadogo wa madini ili watoke katika uchimbaji mdogo na kuwa wachimbaji wa kati na kuendelea, hivyo kukuza kipato chao na uchumi wa nchi kwa ujumla. “Ni lazima ifike mahala madini yetu yachimbwe na Watanzania wenyewe hali itakayosaidia mzunguko wa fedha nchini kuwa mkubwa zaidi,” alisema. Aidha, Naibu Waziri Kitwanga aliwataka Stamico watakapokuwa wanachimba madini, wahakikishe faida yote inarudi nchini ili kukuza mzunguko wa fedha na hivyo kuinua uchumi wa nchi. “Hata wenzetu wanapeleka fedha zote za faida kwao. Wanazobakiza hapa, ni zile tu wanazohitaji kuendeshea biashara,” alitoa mfano. Akizungumza na Wafanyakazi wa Wakala wa Ukaguzi Madini Tanzania (TMAA), Naibu Waziri Kitwanga aliwataka kufanya kazi kwa juhudi ili kuhakikisha mapato ya Serikali yanakusanywa kikamilifu. “Leteni maoni kuhusu nini zaidi kifanyike ili kuhakikisha mapato ya Serikali katika sekta ya madini yanaongezeka,” alisisitiza Kitwanga.

No comments:

Post a Comment