TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, March 5, 2015

WADAIWA SUGU BILI WASABABISHA WANANCHI KUKOSA MAJI KATIKA MJI WA MPWAPWA, WAMO NMB

18Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Mpwapwa huku akiwa ameshikilia nyaraka za wadaiwa sugu wa bili za maji katika mji wa Mpwapwa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji katika mji huo Bw. Shadrack Mtemba.
Nyaraka hizo zina orodha kubwa ya wadaiwa zikiwemo taasisi za serikali , makampuni zikiweno benki kama vile NMB inayodaiwa fedha ndogo ambayo jumla yake ni shilingi  elfu 79.179.50 fedha ambayo ni ndogo sana ikiwa ni bili ya mwezi wa pili 2015.
Sauala hilo limekuja baada ya malalamiko ya wananchi katika mkutano huo ambapo walimweleza Katibu Mkuu wa CCM kuwa maji hayatoki, lakini kila mwezi wanadaiwa bili ya maji jambo ambalo limekuwa kero kubwa kwao, Akielezea sakata hilo mbele ya Katibu Mkuu wa CCM, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Mpwapwa Bw. Shadrack Matemba amesema mradi huo ni mkubwa na unatosheleza mahitaji ya maji kwa  wananchi wa mji wa Mpwapwa. tatizo ni kwamba Taasisi na makampuni mengi hayalipi bili zao kwa wakati jambo ambalo linafanya uendeshaji kuwa mgumu huku akikabidhi nyaraka za wadaiwa hao mbele ya Kinana

Kinana amemkabidhi suala hilo mkuu wa mkoa wa Dodoma Kapteni Chiku Galawa na Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Dr. Jasmine Tisekwa ili kulishughulikia huku akiahidi pia kulifuatilia yeye mwenyewe kwa makini ili kuhakikisha wananchi wa mji wa Mpwapwa wanapata huduma nzuri ya maji safi na salama.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ameanza ziara ya kikazi ya siku 9 mkoani Dodoma akizna na wilaya ya Mpwapwa kabla ya kuendelea na wilaya zingine na mikoa ya Arusha na Kilimanjaro, Katika ziara hiyo Kinana anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi kulia katika picha ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji katika mji wa Mpwapwa Bw. Shadrack Matemba.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MPWAPWA). 19Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji katika mji wa Mpwapwa Bw. Shadrack Matemba akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Mh. Adam Kimbisa mara baada ya kukabidhi orodha hiyo ya wadaiwa sugu wa bili za maji kwa Mkuu wa mkoa wa Galawa ambaye anaonekana akiipitia orodha hiyo.
1Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishuka kwenye mfereji wakati alipokuwa akivuka mfereji huo akielekea akishiriki kupalilia shamba la karanga la Bi. Anna Mlewa katika kijiji cha Berege Mpwapwa huku akiwa ameongozana na Bi Anna Mlewa na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Dodoma ,  3Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupalilia shamba la karanga la Bi. Anna Mlewa wa pili kutoka kushoto na, wengine anayefuata ni Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Chiku Galawa (kulia) ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Mh. Adam Kimbisa 4Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiondoka mara baada ya kushiriki kupalilia shamba la karanga la Bi. Anna Mlewa katika kijiji cha Berege kulia ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi na katikati ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Mh. Adam Kimbisa. 5Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kujenga mfereji wa maji katika shamba la kilimo cha umwagiliaji cha Mpunga kijiji cha Msagali. 6Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa zahanati katika kijiji cha Mazae kata ya Kisokwe kushiriki ujenzi wa zahanati. 7Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua jengo la bweni  katika shule ya sekondari ya Mpwapwa lililoungua ambapo pia ameshiriki kufyatua matofali kwa ajili ya ukarabati wa bweni hilo. 8Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida Mh. Adam Kimbisa akishiriki kufyatua matofali kwa ajili ya ukarabati wa bweni hilo. 9Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana hiku Galawa  wakishiriki kufyatua matofali kwa ajili ya ukarabati wa bweni la shule ya sekondari ya Mpwapwa lililoungua moto na kuteketeza mali zote za wanafunzi. 10Mkuu wa mkoa wa Dodoma akitoa maelekezo kwa mmoja wa wanausalama katika msafara wa Katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi. 11Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa kwa ngoma wakati alipowasili katika kijiji cha Berege na kusalimia wananchi. 12Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wanafunzi katika shule ya sekondari ya Mpwapwa mara baada ya kukagua bweni lililoungua kwa moto katika shule hiyo. 13 14Baadhi ya wananchi waliohudhuria katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mashujaa mjini Mpwapwa. 15Mkuu wa mkoa wa Dodoma Kapteni mstaafu Chiku Galawa akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mashujaa mjini Mpwapwa. 16Umati wa wananchi wakiwa katika mkutano huo. 17Nape Nnauye Katibu wa Itikadi na Uenezi akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa  Mashujaa mjini Mpwapwa.

No comments:

Post a Comment