TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, March 7, 2015

SERIKALI YAANZISHA MFUMO WA KIELEKTONIKI KUSIMAMIA UTOAJI WA HUDUMA ZA ARDHI NCHINI.

unnamedWaziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akitoa ufafanuzi wa mfumo wa kielektroniki utakaosimamia utoaji wa huduma katika sekta ya ardhi. 
……………………………………………………………………………
Na. Aron Msigwa –MAELEZO.
 Dar es salaam.
SERIKALI imeanza kutekeleza mpango wa kusimika mfumo funganishi wa kielektroniki (Intergrated Land Management Information Systeam) utakaosimamia sekta ya ardhi nchini na kupunguza muda, gharama za upimaji na upatikanaji wa hati miliki za ardhi kwa wananchi.
Akizungumzia uanzishwaji wa mfumo huo leo jijini Dar es salaam, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amesema  mfumo huo wa kisasa utawawezesha wananchi kupata hati za umiliki  wa ardhi na taarifa zao za malipo na matumizi ya ardhi katika ngazi za vijiji, wilaya, kanda hadi taifa.
 Amesema utekelezaji wa mradi huo utasimamiwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa ufadhili wa Benki ya dunia kupitia ofisi ya Waziri Mkuu na kuongeza kuwa utekelezaji wa mradi huo utafanyika kwa awamu mbili itakayohusisha uundwaji wa programu hiyo na majaribio ya mfumo huo katika kanda zilizochaguliwa za mikoa ya Dar es salaam,Pwani na Morogoro.
Mhe. Lukuvi ameeleza kuwa utekelezaji wa mradi huo mkubwa pia utaambatana na utoaji wa hati mpya za umiliki wa ardhi na kufuta za zamani,  upigaji wa picha za anga kwa mfumo wa Satelite, ujenzi wa kituo cha kutunza kumbukumbu za ardhi kitaifa pamoja na uelimishaji wa jamii kuhusu matumizi ya mfumo huo.
Amesema awamu kwanza itatekelezwa kwa muda wa miaka miwili kuanzia Machi 2015 hadi 2016 na kugharimu kiasi cha dola za Kimarekani milioni 35 huku awamu ya pili ikihusisha uboreshaji wa mfumo huo kutokana na matokeo mazuri yatakayopatikana kwenye awamu ya kwanza ili kuwezesha mfumo huo kusambazwa nchi nzima.
Akitaja faida za kusimikwa kwa mtambo huo nchini amesema utasaidia kuhifadhi  taarifa za wananchi kwa uhakika  na usahihi pamoja na matumizi ya ardhi kote nchini pia  utarahisisha upatikanaji wa hati za umiliki wa ardhi kwa wananchi wengi zaidi tofauti na ilivyo sasa kutokana na ongezeko la kasi ya upimaji wa ardhi
Aidha, amesema mfumo huo utaondoa vitendo vya utoaji wa hati zaidi ya moja kwenye viwanja, kuondoa hati pandikizi na kuongeza uwazi wa taarifa kwa kuwawezesha wananchi wanaomiliki ardhi kupata taarifa zao kupitia  simu za mkononi.
“Nawahakikishia watanzania kiama cha matapeli wa ardhi kimefika ,teknolojia hii ni ya kisasa na Tanzania itakua nchi ya pili barani Afrika kuwa na mfumo wa aina hii, Serikali tumelenga kuondoa kabisa kero na ukiukaji wa maadili  uliokuwa ukifanywa na baadhi ya watendaji wa serikali wasio waaminifu katika utoaji wa hati za viwanja nchini” Amesisitiza.
Amefafanua kuwa kufungwa kwa mitambo hiyo ya kielektroniki katika kanda 7 nchini kutawezesha kila sehemu ya ardhi kupimwa  na kuongeza thamani ya ardhi na mapato ya Serikali yatokanayo na ardhi huku na kueleza kuwa nchi ya Uganda ambayo sasa inatumia mfumo huo imenufaika kwa kiasi kikubwa kutokana na kuwa na taarifa sahihi za ardhi na matumizi yake.
Amewataka wananchi na watendaji wanaosimamia sekta ya ardhi kote nchini wajiandae kupokea mabadiliko hayo kwa kuanza kutunza kumbukumbu  sahihi za za viwanja wanavyomiliki ambazo zitaingizwa kwenye mfumo huo na wao kupewa hati mpya za kielektroniki.
Pia amewatoa hofu wananchi kuwa zoezi la upimaji wa maeneo ambayo bado hajapimwa hususani yale yenye hati zilizotolewa na vijiji na zile za kimila katika maeneo mbalimbali nchini litaenda sambamba na utoaji wa hati mpya za kielektroniki.
Katika hatua nyingine Mhe. Lukuvi amesisitiza kuwa zoezi la bomoa bomoa linalosimamiwa na wizara yake katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam sasa litafanywa katika mikoa mingine kwa lengo la kusimamia sheria ya ardhi namba 4 ya mwaka 1999 kifungu namba 175(1) inayozuia mwananchi yeyote kuingia na kuendeleza  kwenye ardhi asiyoimiliki kisheria. 
“Naomba wananchi watupe ushirikiano,haki lazima itendeke kazi hii tumeianza katika jiji la Dar es salaam na tunaendelea nayo katika maeneo mengine nchini ambako kuna vitendo vya dhuruma na uvamizi wa ardhi unaofanya na baadhi ya watu kinyume cha sheria”

No comments:

Post a Comment