TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, March 7, 2015

WAFANYAKAZI WA RADIO 5 WANOLEWA NA BBC MEDIA ACTION

???????????????????????????????
Wafanyakazi wa kampuni ya Tan Communication Media  inayo miliki kituo cha  Radio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha wakiwa katika picha ya pamoja jana katika mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kitaaluma ili waweze kuandika habari za kuboresha maisha ya jamii kwa kupata maendeleo kuelekea uchaguzi mkuu,mafunzo hayo yanaendeshwa na shirika lisilo la kiserikali la BBC Media Action, aliyevalia shati la blue ni mkufunzi mwandamizi Pendael Omari wa shirika hilo(Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
???????????????????????????????
Mkufunzi mwandamizi Pendael Omari wa shirika lisilo la kiserikali la BBC Media Action akiwa anatoa ufafanuzi katika mafunzo hayo yaliyokuwa yakifanyika katika ofisi za Radio 5,mafunzo hayo yalidumu kwa takribani wiki mbili
???????????????????????????????
Mtangazaji maarufu wa kituo hicho Ernest Matundiro a.k.a Prince de la ville kushoto akiwa anaandika vipengele muhimu katika uandishi wa habari,kulia ni Mhariri wa kituo hicho Monica Nangu
???????????????????????????????
Msimamizi mkuu wa vipindi vya Radio 5  kulia Mathew Philip akiwa anafatilia mafunzo kwa ukaribu zaidia,kushoto ni mtangazaji wa kituo hicho Wilberd Kiwale
???????????????????????????????
Mkufunzi mwandamizi Pendael Omari akiwa anatoa ufafanuzi kwa Mhariri Mkuu Philip Magesse katika mafunzo hayo jana
???????????????????????????????
Mtangazaji wa kituo hicho Yakubu Simba
???????????????????????????????
Mtangazaji machachari wa kituo hicho Godfrey Thomas a.k.a GT
???????????????????????????????
Mmiliki wa mtandao wa kijamii wa http://jamiiblog.co.tz/ Pamela Mollel akiwa anafanya mahojiano na mkuu wa vipindi vya Radio 5  Mathew Philip kuhusu mafunzo hayo
???????????????????????????????
Mtangazaji wa kituo hicho Clara Moita wakiwa katika majadiliano na mkuu wa vipindi vya Radio 5 Mathew Philip
???????????????????????????????
Wafanyakazi wa Radio 5 katika pozi
Wafanyakazi wa Radio 5 jijini A rusha wamepatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kitaaluma ili waweze kuandika habari za kuboresha maisha ya jamii kwa kupata maendeleo kuelekea uchaguzi mkuu,mafunzo hayo yanaendeshwa na shirika lisilo la kiserikali la BBC Media Action,
Akizungumza mapema jana katika mafunzo hayo Mkufunzi mwandamizi Pendael Omari wa shirika lisilo la kiserikali la BBC Media Action alisema kuwa lengo la kufanya mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wa kitaaluma pindi wanapokuwa katika kazi zao
Alisema kuwa mafunzo hayo yatawezesha pia upatikanaji wa utawala bora kwa kuwa vyombo vya habari vitaelimisha wananchi umuhimu wa kuchagua viongozi watakaoleta maendeleo
Kwa  upande wake Msimamizi mkuu wa vipindi vya radio hiyo  Mathew Philip  alisema kuwa mafunzo hayo yamewajengea uwezo wa kufanya kazi kwa kuwa walikuwa wakifanya mafunzo kwa vitendo zaidi 
Pia alisema kuwa kupitia mafunzo hayo wamepata ufahamu wa namna ya kutafuta habari za kupigia kura maoni pamoja na uchaguzi mkuu bila upendeleo kwa kumpa msikilizaji nafasi ya kusikika na kumpa elimu
Mafunzo hayo yalifanyika katika ofisi za radio 5 kwa muda wa wiki mbili 
(Habari na Picha Pamela Mollel wa jamiiblog)

No comments:

Post a Comment