TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, April 18, 2014

MAMA AMSAMEHE NA KUMFUNGUA KITANZI MFUNGWA ALIYE HUKUMIWA KUFA KWA KUMUUA MWANAE

Wanasema uchungu wa mwana aujuae mzazi! Na kutokana na uchungu huo wa mama, ni vigumu kumshawishi akae meza moja na mtu aliyemuua mwanae kwa makusudi tena kwa kumpiga hadi kuhakikisha anakata roho.

Lakini imekuwa tofauti na jambo lililowaacha mdomo wazi umati wa watu uliohudhuria kushuhudia kunyongwa kwa mwanaume aliyemuua kijana mwenye umri wa miaka 18 nchini Iran ambako hukumu ya kunyongwa hadharani ni kawaida kwa mtu aliyepatikana na hatia ya kuua kwa kukusudia, pale ambapo mama mzazi wa marehemu alipoingilia na kumfungua kitanzi muuaji huyo sekunde ya mwisho.
Kwa mujibu wa The Guardian, mwanaume huyo aliyejulikana kwa jina la Balal alikuwa tayari amefungwa kitambaa cheusi na kuvalishwa kitanzi akisubiri amri ya kitanzi kufyatuliwa, ghafla mama huyo alimzaba kibao usoni na kuanza kumfungua kitanzi akisaidiana na mumewe!

“Mimi ni mtu wa imani.” Alisema mama huyo aliyefahamika kwa jina la Samereh Alinejad. “Nilipata ndoto ambayo mwanangu alikuwa ananiambia kuwa yuko katika sehemu nzuri na yenye amani…baada ya hapo, ndugu zangu wote, hata mama yangu, wakaanza kunihimiza nimsamehe muuaji huyu.”
Balal alihukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya kumpiga vibaya Abdollah Hosseinzadeh (18) hadi kumuua katika ugomvi uliotokea mtaani kati yao mwaka 2007.

Tuesday, April 15, 2014

Fredy Tony added 2 new photos. 7 hrs · Haya yaligongana moja likaingia chaka moja likapinduka ..kila moja na upande wake wa barabara Fredy Tony's photo. Fredy Tony's photo. Like · · Share Bana Kang'ata likes this. Mpalule Shaban Mwezi huu nimeshuhudia ajali nyingi sana barabara ya kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro na ile ya kwenda Mbeya baada ya Mikumi, lakini nahisi sema zilitokana na utelezi uliokuwa umeambatana na mvua za hapa na pale. lakini pia nawashauri madereva kwenda mwendo wa kawaida. kwani mwendo kasi ndo chanzo cha ajali.

Fredy Tony added 2 new photos.
7 hrs ·
Haya yaligongana moja likaingia chaka moja likapinduka ..kila moja na upande wake wa barabara
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Like · ·
  • Bana Kang'ata likes this.
  • Mpalule Shaban Mwezi huu nimeshuhudia ajali nyingi sana barabara ya kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro na ile ya kwenda Mbeya baada ya Mikumi, lakini nahisi sema zilitokana na utelezi uliokuwa umeambatana na mvua za hapa na pale. lakini pia nawashauri madereva kwenda mwendo wa kawaida. kwani mwendo kasi ndo chanzo cha ajali.

TIZAMA HAPA JINSI LOWASSA ALIVYOMKARIBISHA RAIS MSTAAFU MKAPA WILAYANI MONDULI

Rais mstaafu wa awamu wa tatu Mh Benjamin Mkapa amefanya ziara kutembelea shule ya msingi ya Manyara Ranchi inayofadhiliwa na shirika la kimataifa la uhifadhi wa wanyamapori la African Wildlife Foundation  Wilayani Monduli. Mzee Mkapa ni Makamu Mwenyekiti wa shirika hilo lenye makao yake mjini Washington Marekani. picha mbalimbali zinamuonesha Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akimuongoza Rais Mkapa kuzuru shule hiyo.
 Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akizungumza Mzee Mkapa Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akiagana na  Mzee Mkapa
 
NA: RWEYEMAMU BLOG

AJALI BARABARANI

:Liliacha njia
 
 
 
 
 
 
 
Like · ·

MAZIKO YA GUROMO ANGALIA MATUKION KATIKA PICHA

Monday, April 14, 2014

MKUU WA MKOA WA ARUSHA AZUNGUMZIA TUKIO LA BOMU KULIPUKA KWENYE BAA USIKU APRILI 13, 2014

Usiku wa April 13 2014 kwenye baa iitwayo ‘Arusha night park’ iliyopo Mianzini Arusha ambayo siku zote ni miongoni mwa sehemu zinazokua na mkusanyiko wa watu wengi kuanzia jioni, limerushwa bomu wakati watu mbalimbali wakitazama mpira.
Blog hii imepata nafasi ya kuongea na mkuu wa mkoa wa Arusha ambae ni kiongozi
wa Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa ambae amethibitisha kwamba ni
watu 15 wamejeruhiwa kwenye mlipuko huo.
Anasema
wote wamepelekwa hospitali ambapo uchunguzi wa awali umeonyesha bomu
hilo ni la kutengenezwa kwa mkono na mpaka sasa hajajulikana
alietekeleza shambulio hilo.
Kwenye sentensi nyingine pia amesema hakuna aliepoteza maisha kwenye shambulio hilo ambalo uchunguzi wa awali umeshatoka, ila baadae itatoka taarifa rasmi pale uchunguzi kamili utakapokamilika.

ANGALIA PICHA ZA MUONEKANO WA DARAJA LA MTO RUVU LLILOJAA MAJI NA KUSABABISHA MAGARI KUSHINDWA KUPITA