TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, February 28, 2012

Mashujaa Band waandaa Listening Party



 wanamuziki  Mafumu Bilali, Anania Ngoliga na Hamza kalala, John Kitime leo walikaribishwa na uongozi wa Mashujaa Band katika ukumbi wao wa  nyumbani kule Vinginguti ili kusikiliza nyimbo mpya za Mashujaa Band. kwa lengo la kupata ushauri toka kwa wapenzi na waalikwa kuhusu nyimbo zao mbili mpya. Ushauri ulitoka mwingi toka kwa viongozi mbalimbali wa bendi na wapenzi waliokuwa wameruhusiwa kuingia na kusikiliza nyimbo hizo.
 Baada ya utambulisho wa  shughuli toka kwa Chalz Baba, Mashujaa Band ilileta show yao mpya
Baada ya show nyimbo ya kwanza ambayo ni utunzi wa Chalz Baba iliyoenda kwa jina la Kidole Risasi ilipigwa. Maoni baada ya wimbo yalihusu urefu wa wimbo, ambao ulionekana kutokana na uwingi wa waimbaji katika bendi na wote kuwa na vipande vya kutuma katika wimbo, hivyo kuufanya wimbo uwe mrefu sana. Jingine lilikuwa ni kugundua kuwa wapiga magita walikuwa wakipiga bila ya kutyuni magitaa. Kulikuweko na mawazo kuhusu uchezaji wa show, ambapo wengi walikubaliana kuwa show ilikuwa safi katika onyesho hilo tofauti na kawaida katika madansi mengine. Pia ulitolewa ushauri kuwa mafundi mitambo walikuwa hawajiipatia kazi yao ya kurekibisha vyombo sawasawa. Mpiga tumba na wale mabingwa wa kurap waliambiwa waongeze ubunifu.

Wacheza Shoo wa Bendi hiyo, Rose Masaki (kushoto) na Sweety Baby wakiongoza wenzao kuteka mashabiki waliofulika usiku wa jumanne kwenda jumatano.
Wakurugenzi wa Bendi hiyo, Mama Sakina wa Pili kushoto, na Mumewe Hosea Hopaje(Maisha) kati ,Mkurugenzi wa Blogu hii na ambaye aliwahi kuwa  Meneja Mstaafu wa Bendi hiyo, Shaaban Mpalule(kushoto) na Mdau wa Mziki kutoka Uingereza mzee wa Ulaya(kulia) wakifuatilia kwa makini onyesho hilo

Rais wa Bendi hiyo Kajo Litunguru
Mwanamuziki Mkongwe Mafumo Bombenga  na Mkewe wakifuatilia kwa makini
Rais Mstaafu wa Bendi hiyo, Mwimbaji Nguli , Jembe, Mbishi wa Maisha asiyeogopa Vita(Jado Fid) kulia na Pasia Budansi Kengere
Makamu wa Rais wa Bendi hiyo Charlz Baba,
Mwimbaji wa Bendi hiyo, Raja Radha mbele na Masooud
Rapa wa Bendi hiyo 33 akiwa wenzake
Mpiga Gitaa Bes(Profa)
Kutoka kulia, Jado Fid, Pasia Budansi, Charz Baba, na Masoud
Mpiga Kinanda wa Bendi hiyo Fredy Manzaka
Mpiga Gitaa la Solo Amosi Mkono wa Nabii
Mpiga Ngoma(Dram) Sele Kadanser

Mwimbaji wa Bendi hiyo Masoud
Wacheza Shoo wa Kike na wa Kiume wakichuana vikali