TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, July 4, 2016

MULTICHOICE TANZANIA YATOA MSAADA WA VITU MBALIMBALI KWA KITUO CHA WATOTO YATIMA TANDALE JIJINI DAR


Misaada ambayo imetolewa kwa watoto hao ni Cherehani 4, kapeti 12, vikombe 60, sahani 40, magodoro 11, shuka 40, tenga za nguo 3, jagi 6, beseni kubwa 3, sufuria 9, chupa za chai 4 na mikeka 6.Akizungumzia misaada hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande alisema msaada huo ni mwendelezo wa misaada ambayo Multichoice imekuwa ikitoa kwa kituo hicho kwa lengo la kuwasaidia kuishi maisha bora lakini pia kuwapatia msaada ambao unaweza kuwasaidia kuwa na uwezo wa kuingiza kipato.

Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande akizungumza kuhusu msaada ambao wameutoa kwa kituo cha Al--Madina.

"Multichoice tumekuwa tukitoa misaada yetu kwa kituo hiki tangu 2009 na leo tumewaletea mwingine ikiwa ni kila mwaka tunafanya hivyi lakini kwa mwaka huu tumeleta pia Cherehani ambazo zitawasaidia kupata kipato,
"Pamoja na hayo pia tumewafungia king'amuzi ambacho watoto watakuwa wakiangalia vipindi balimbali baada ya kurejea nyumbani na tuna chaneli mbalimbali za vipindi vya watoto na burudani kwahiyo tunaamini kuwa watoto watafurahi," alisema Chande.

MRADI WA USAID WA UIMARISHAJI MIFUMO YA SEKTA ZA UMMA (PS3) WAZINDULIWA MKOANI KIGOMA


Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali (Rt), Emmanuel Maganga akizindua mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) katika mkoa wake wa Kigoma leo. Mradi huo wa miaka mitano unafadhiliwa na Shirika la Misaada la Kimataifa la Marekani (USAID) na utatekelezwa katika mikoa 13 nchini na kushirikisha Halamashauri 93.
Mkuu wa Mkoa aliwataka watendaji wa Halamashauri hizo kufanya kazi kwa bidii kuhakikisha mradi unaleta manufaa kwa jamii na mkoa.
Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma Charles Pallangyo, akizungumza wakati wa uzinduzi huo. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mjini Samsoni Anga, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali (Rt), Emmanuel Maganga, Kiongozi wa Mradi wa PS3, Dk Conrad Mbuya na Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi.
Kiongozi wa mradi wa PS3, Dk Conrad Mbuya akizungumza na kueleza dhumuni la mradi huo. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma,Brigedia Jenerali (Rt), Emmanuel Maganga.
Mwakilishi kutoka Tamisemi, Mrisho Mrisho akizungumza kuhusiana na mradi huo na namna ambavyo serikali imejipanga kuhakikisha utekelezaji wake unafanikiwa.
Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Kigoma wakifuatilia kwa makini uzinduzi huo. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Kanali. Elisha Marco Gaguti, Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali.Hosea Malonda Ndagala na Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Luis Peter Bura.
Mkuu wa Wilaya Kasulu, Kanali. Martin Elia Mkisi akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mwanamvua Hoza Mlindoko, wakifuatilia mada katika uzinduzi huo. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.

WANANCHI WAZIDI KUMIMINIKA BANDA LA PSPF, MKURUGENZI MKUU AWASAIDIA WAFAMYAKAZI WAKE KUHUDUMIA WATEJA


Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, akiyekaa, akimuonyesha Mwanachama huyu wa Mfuko huo michango yake papo kwa hapo kwenye banda la Mfuko huo lililoko jengo la Wizara ya Fedha na Mipango, wakati wa maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, Julai 4, 2016. Mamia ya Wananchi wamekuwa wakimiminika kwenye banda hilo, ambapo jambp la kuvutia Mkurugenzi Mkuu huyo aliungana na wafanyakazi wake kutoa huduma kwa wananchi. Maonyesho hayo yanashirikisha jumla ya nchi 30 ambapo banda la PSPF limekuwa na idadi kubwa ya wananchi wanaotembelea kujua huduma zitolewazo kwa wananchi ambao si wanachama lakini pia kuwahudumia wanachama wake. (PICHA NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID)
Mama Anna Mkapa, (kulia), Mke wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa, ambaye ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa Kwa Wote (EOTF), akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, (kushoto) na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Abdul Njaidi, wakati Mkurugenzi huyo alipotembelea banda la EOTF linalokusanya wajasiriamali kutoka mikoa yote ya bara na vuisiwani. Kupitia mpango wa uchangiaji wa hiari yaani PSS, wajasiriamali hao wanaweza kujiunga na Mfuko huo na hivyo kufaidika na mafao mbalimbali yakiwemo ya kuboresha biashara zao
Mama Salma Kikwete, (kulia), Mke wa Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete, akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, walipokutana kwenye banda la EOTF kwenye maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, Julai 4, 2016.


Mamia ya wananchi wakiwa kwenye banda la PSPF Julai 4, 2016
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, akimkabidhi kadi yake ya uanachama wa Mfuko huo, Mwanaidi Msangi baada ya kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS), Julai 4, 2016
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, akimkabidhi kadi yake ya uanachama wa Mfuko huo, Baturi J. Msusi, baada ya kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS), Julai 4, 2016

WAKUU WAPYA WA WILAYA ZA MKOA WA MWANZA WAPEWA MAJUKUMU MARA BAADA YA KUAPISHWA


Akizungumza baada ya kuwaapisha wakuu hao wa wilaya zote saba za mkoa wa Mwanza, Mongella amesema kwa muda mrefu mkoa wa Mwanza umekumbwa na matukio ya mauaji ya watu wenye ualbino na vikongwe kutokana na imani za kishirikina na kwamba wakati umefika kuhakikisha matukio hayo yanakwisha.Amesema mkoa huo umejipanga vyema kuhakikisha matukio hayo yanakuwa historia kwa kuwa hakuna binadamu mwenye mamlaka ya kutoa uhai wa binadamu mwenzake kwa sababu yoyote ile.

Mkuu huyo wa mkoa amewapa mwezi mmoja wakuu hao wapya wa wilaya kumaliza tatizo la madawati pamoja na kuwachukulia hatua watumishi hewa 1,057 waliogundulika kwenye wilaya zote za mkoa wa Mwanza.Mongella amewata wakuu hao wa Wilaya kuhakikisha kwamba matumizi ya dawa za kulevya katika wilaya zao yanakomeshwa ambapo amepiga marufuku matumizi ya shisha katika hoteli na klabu zote za muziki pamoja uchezaji wa "pool table" na unywaji wa pombe saa za kazi huku akitanabaisha kwamba atakaeshindwa kutekeleza maagizo hayo ni dhahiri shahiri kwamba atakuwa ameshindwa kusimamia majukumu yake.

Aidha Mongella amemtaka mkuu wa Wilaya ya Nyamagana kuhakikisha kwamba hadi ifikapo Agosti mosi mwaka huu awe amewaondoa wafanyabiashara ndogondogo waliosambaa kwenye maeneo mbalimbali ya katikati ya jiji Mwanza.Wakuu wapya wa Wilaya za Mkoa wa Mwanza walioapishwa, wamesema wamejipanga vyema kushirikiana na viongozi wengine pamoja na wananchi katika Wilaya zao ili kuhakikisha kwamba wanatekeleza vyema majukumu yao ikiwemo kuimarisha suala la ulinzi na usalama katika jamii.

Wakuu wapya wa Wilaya saba za Mkoa wa Mwanza walioapishwa hii leo ni Mary Onesmo Tesha wa Nyamagana, Estomin Francis Chang’a wa Ukerewe, Hadija Rashid Nyembo wa Magu, Juma Samwel Sweda wa Misungwi, Emmanuel Enock Kipole wa Sengerema, Dkt.Leonard Moses Masale wa Ilemela na Mhandisi Mtemi Msafiri Simion wa Kwimba ambapo wote wamekabidhiwa vitendea kazi ikiwemo Katiba ya Tanzania pamoja na Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015/20.
Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Mh.Emmanuel Enock Kipole (kulia), akiapa mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella (kushoto).
Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Mhe.Estomin Francis Chang’a (kushoto) akiapa mbele ya mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella (kulia).
Mkuu wa Wilaya ya Magu, Mhe.Hadija Rashid Nyembo, akiapa hii leo
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Mhe.Juma Samwel Sweda, akiapa mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella (kushoto).

Vyama Vya Siasa Zanzibar Kuhakikiwa


==================================================

EPZA YATENGENEZA AJIRA 36,000

==============================================

AGIZO LA KUZUIA UVUTAJI WA SIGARA NA MATUMIZI YA BIDHAA ZA TUMBAKU KATIKA MAENEO YA UMMA.

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inampongeza Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa kupiga marufuku matumizi ya Shisha na uvutaji wa Sigara hadharani kama afua ya kupunguza madhara ya tumbaku na madawa ya kulevya katika jamii.

Uchunguzi wa kitalaam uliofanyika umebaini kuwa Shisha ina madhara kwa afya ya watumiaji hasa vijana na watoto. Watumiaji wa Shisha wanatumia kiwango kikubwa cha tumbaku kwa muda mfupi, hali inayoongeza madhara yatokanayo na tumbaku kama vile: – Saratani, Magonjwa ya Mapafu, Kibofu cha mkojo, Tezi dume, Koo, Mdomo na Kiywa, Ngozi, Ini, Ubongo.

Pia imebainika kwamba matumizi ya Shisha huambatana na kuongezewa dawa nyingine za kulevya na hivyo hufanya watumiaji wa Shisha kupata uraibu wa dawa za kulevya. Matumizi ya dawa hizo za kulevya ni kosa la jinai.

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inapenda kurejea na kusisitiza agizo lake la tarehe 12 Machi 2015 la kuzuia matumizi ya sigara na matumizi ya bidhaa za tumbaku katika maeneo ya umma

Inakumbushwa kwamba agizo hili limezingatia utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa Bidhaa za Tumbaku, Sura ya 121 T.L 2002, ya Sheria za Tanzania kipengele cha 12 (1) ambacho kinakataza matumizi ya Tumbaku katika Maeneo ya Umma.

Madhumu ya Agizo hili ni kuilinda Jamii kwa ujumla kutokana na madhara yatokanayo na moshi wa sigara. Wizara inawakumbusha wananchi wanaotumia bidhaa za tumbaku kupunguza au kuacha kabisa matumizi ya tumbaku. Aidha, agizo hili linaijumuisha jamii yote katika kubaini madhara ya tumbaku na umuhimu wa kuzuia matumizi ya tumbaku katika maeneo ya kazi na maeneo yote ya umma.

RC MAKONDA AWATAKA WAKUU WA WILAYA KUIMARISHA ULINZI NA USALAMA

MPALULEBLOGS:
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda (kushoto) akimuapisha Mhe.Sophia Mjema (kulia) kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala leo katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam. Mhe.Sophia Mjema (kulia) akionesha Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) aliyokabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto) mara baada ya kuapishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala leo katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto) akimuapisha Mhe.Hashim Mgandilwa (kulia) kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni leo katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto) akimuapisha Mhe.Felix Lyaniva (kulia) kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke leo katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe.Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wapya wa Wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam (mbele) pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam (nyuma)mara baada ya kuisha kwa zoezi la kuapishwa lililofanyika leo nje ya Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto) akimuapisha Mhe.Ally Hapi (kulia) kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni leo katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam. Picha zote na Jacquiline Mrisho – MAELEZO

Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda amewataka Wakuu wapya wa Wilaya kuimarisha ulinzi na usalama kwa wananchi waliopo katika Wilaya zao ili kudumisha amani.

Makonda alisema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na Wakuu wa Wilaya juu ya kuwalinda wananchi na mali zao na kuhakikisha usalama unakuwepo katika Wilaya wanazozisimamia.Alieleza kuwa kwa kuwa wao ndio wanaomuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika Wilaya zao, wanatakiwa kuhakikisha wametekeleza ahadi zilizotolewa na Mhe. Rais wakati wa kampeni.

“Ningependa wakuu wangu wa Wilaya mchukiwe kwa kusimamia Haki na Sheria kuliko kukumbatia uovu kwa kuhitaji furaha ya muda mfupi, hakikisheni Sheria na Kanuni zilizopo kwenye Katiba ndio ziwe muongozo wenu”, alisema Makonda.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Dar es Salaam aliwataka Wakuu wa Wilaya zake kuwasimamia Wakurugenzi wao ili kuhakikisha wanatumia bajeti waliyopewa katika kutatua changamoto zilizopo katika Wilaya zao.Aidha, Makonda amewasisitiza kuhakikisha kuwa kuanzia Julai 11 mwaka huu maeneo yote yanayofanya biashara ya shisha kufungwa na kuweka maeneo maalumu kwa ajili ya kuvutia sigara.

Wakuu wa Wilaya wapya wamepewa wiki mbili za kutengeneza mpango kazi kwa kusoma ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Hotuba ya Mhe.Rais John Magufuli aliyoisoma wakati wa ufunguzi wa Bunge la 11 la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na mazingira ya kazi katika maeneo yao.