TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, January 25, 2012

Ambassador H.E J BISWARO in Adds Ababa


The Tanzania Parmanent representative and ambassador H.E J BISWARO(with glasses) leaving the meeting at the 2nd day of the 18th ordinary session of the assembly of heads of stae and goverrnment at the AU headquaters in Addis Ababa.

MRADI WA KUDHIBITI MAAMBUKIZI YA VVU/UKIMWI ULIOFADHILIWA NA SERIKALI YA JAPAN KWA KUSHIRIKIANA NA WIZARA YA AFYA WAFUNGWA RASMI JIJINI DAR ES SALAAM.

Mwakilishi mkuu wa Shirika la Kimataifa la ushirikiano wa kimaendeleo la Japan (JICA) Bw. Yukihinde Katsuta akitoa maelezo juu ya ukamilishwaji wa mradi wa kudhibiti maambukizi ya Virusi vya Ukimwi nchini Tanzania uliofadhiliwa na serikali ya Japan kwa lengo la kupunguza maambukizi ya VVU sanjari na usambazaji wa vifaa vya kupimia maambukizi hayo na kuahidi kuendeleza ushirikiano na serikali ya Tanzania katika utoaji wa vifaa vya kutolea huduma za afya. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
Katibu mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi. Blandina Nyoni akimkabidhi Zawadi iliyoandaliwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii mwakilishi mkuu wa JICA wakati wa hafla fupi ya ukamilishaji wa mradi wa kudhibiti maambukizi ya Virusi vya Ukimwi nchini uliofadhiliwa na serikali ya Japan jijini Dar es salaam.
Baadhi ya watendaji wa wizara ya afya na wawakili kutoka Shirika la kimataifa la maendeleo la Japan (JICA) wakifuatilia taarifa mbalimbali zilizokuwa zinatolewa wakati wa hafla fupi ya ukamilishaji wa mradi wa kudhibiti maambukizi ya Virusi vya Ukimwi nchini uliofadhiliwa na serikali ya Japan jijini Dar es salaam.
Katibu mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi. Blandina Nyoni akizungumza watendaji wa Wizara hiyo na wawakilishi wa Shirika la Kimataifa la ushirikiano wa kimaendeleo la Japan (JICA) wakati wa hafla fupi ya ukamilishaji wa mradi wa kudhibiti maambukizi ya Virusi vya Ukimwi nchini ulioanza mwaka 2009 chini ya ufaufadhili wa serikali ya Japan, jijini Dar es salaam.

Airtel yatoa vitabu Kilimanjaro

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Siha,Bw.Rashid Kitambulo akizungumza na kuishukuru kampuni ya Airtel kwa msaada mkubwa wa vitabu ilioutoa kwa shule nne za sekondari zailizopo wilayani hapo, mwisho kushoto ni Mwalimu mkuu wa sekondari ya Oshara Elieta Kaaya akifatiwa na wawakilishi wa Airtel Pascal Bikomagu na Jane matinde (kulia) ni Afisa Elimu Taaluma wa sekondari Wilaya ya Siha,Bw. Mussa Shaban Ally.hafla hiyo ya makabidhiano iliyofanyika shule ya sekondari Oshara jana.
Airtel yatoa msaada wa vitabu shule 4 za secondari wilaya ya SIHA - Kilimanjaro Chini ya mpango wake wa Airtel Shule Yetu kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imetoa vitabu vya ziada na kiada kwa shule 4 za sekondari zilizoko wilaya ya Siha ili kusaidia maendeleo ya elimu wilayani hapo. Hafla hiyo fupi imefanyika katika shule ya sekondari Oshara ambapo shule zilizonufaika na msaada huo ni za sekondari ya Oshara,Kilingi,Magadini na Namwai zote za wilayani humo ambapo wawakilishi wa shule hizo walikabidhiwa msaada huo na Mkurugenzi wa Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Siha bw, Rashid Kitambulo ambaye alikabidhiwa vitabu hivyo na Afisa Uhusiano wa kampuni ya airtel bi, Jane Matinde. kila shule imepewa msaada wa vitabu vyenye thamani ya shilling milio moja. Akiongea katika hafla ya makabithiano iliyofanyika katika shule ya sekondari Oshara Afisa Uhusiano wa Airtel Tanzania Jane Matinde alisema" Airtel kwa kupitia programme ya shule yetu imeweza kuwafikia wanafunzi wengi na shule nyingi nchini Tanzania na leo tunafurahi kuwa sehemu ya maendeleo ya shule hizi 4 za sekondari wilayani Siha na kuweza kuchangia vitabu zitakavyotumika katika kufundishia na kuwa nyenzo muhimu kwa walimu na wanafunzi wa shule hizi” “Tutaendelea kushirikiana na Serikali chini ya Wizara ya Elimu katika kuinuia na kuboresha kiwango cha elimu nchini kwani tunatambua elimu ndio ufunguo wa maisha na vijana ndio nguvukazi ya kesho” Aliongeza Matinde. Mgeni rasmi katika halfa hiyo Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Siha bwana Kitambulio Rashidi alisema tunayo fuhara kuona Airtel inajitoa katika kusaidia kuinua kiwango cha elimu nchini, moja kati mikakati ya elimu halmashauri yetu iliyojiwekea ni kuhakikisha kwamba kila nyumba moja ya mkazi wa siha anatoka graduate na ili kufikia malengo yake kuna mahitaji ya vitabu vya kufindishia, tunashukuru sana Airtel kwa kutusaidia katika kutimiza malengo tuliojiwekea Bw Rashidi pia alichukua fulsa hiyou kuwaasa wanafunzi kuvitumia vizuri vitabu hivyo ili vilete matokeo vizuri kwa wanafunzi na kufikia lengo halmshauri hiyo iliyojiwekea Kwa upande wake Afisa Elimu Taaluma wa sekondari wilaya ya Siha Mussa Shaabani Ally wameishukuru Airtel kwa kuwawezesha vitendea kazi na kuongeza kuwa wilaya hiyo mpya bado inakabiliwa na changamoto nyingi katika elimu hivyo kuiomba kampuni hiyo kuendelea kuisaidia katika mambo mengine. Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imekuwa ikitoa misaada mbalimbali kama vile Vitabu vya shule ya sekondari, wiki iliyopita Airtel ilitoa msaada wa kutoa computer 4 kwa shule ya sekondari mlangarini iliyoko wilaya ya Arumeru mkoani na pia kuchangia katika sekta ya afya ambapo Airtel iligawa baskeli kumi kwa vituo vya afya wilayani misungwi Mkoani Mwanza. Hii ikiwa nikatika kurudisha faida inayoipata na kuchangia katika huduma kwa jamii.

NSSF YAFANIKIWA KUKUSANYA ZAIDI YA BILIONI 16


Na Gladness Mushi -Arusha
MFUKO wa hifadhi ya jamii( NSSF)mkoani Arusha umefanikiwa kukusanya shilingi bilioni 16.745 kwa kipindi cha Jully hadi desemba 2011 ambapo fedha hizo ni sawa na asilimia 92 ya lengo walilokusudia Hayo yalisemwa na meneja kiongozi wa mfuko huo mkoani hapa Bw Jackton Ochieng' alipokuwa akiongea na gazeti hili kuhusiana na hali ya mfuko huo .ilivyo kwa sasa. Aidha alisema kuwa mfuko huo umeweza kuandikisha wanachama 3582 ambapo ni sawa na asilimia 49.8 ambapo hilo ndilo lengo hailsi Vile vile aliongeza kuwa kwa kipindi hicho pia wameweza kuandikisha waajiri 72 ambapo ni sawa na asilimia 79 ya lengo Hata hivyo bw Ochieng' alieleza kuwa mfuko huo umeweza kulipa mafao kwa wanachama wake 2416 ambapo kifedha wamelipwa shilingi bilioni 4033.65. Alieleza changamoto zinazoukabili mfuko huo kuwa ni pamoja na watu kutojua dhana ya elimu ya mfuko wa jamii na hivyo kuwafanya kuwa waoga kujiunga na mfuko huo ambapo alisema kuwa hadi sasa wamejitahidi kutoa elimu hiyo kwa waajiri 53 . Aliitaja changamoto nyingine kuwa ni pamoja na baadhi ya wafanyakazi kurubuniwa na waajiri hali ambayo inaleta matatizo katika mfuko huo. Aliwataka wanachama na wasio wanachama kutokubali kurubuniwa na waajiri kwa kuwa ni haki ya mfuko kuhudumia wanachama wake kuanzia sasa na hata uzeeni

WACHOMA MAHINDI WAPEWA MAJIKO KUJIKWAMUA KIUCHUMI JIJINI ARUSHA


NA GLADNESS MUSHI- ARUSHA
Kikundi cha akinamama wapatao 50 kinaojishughulisha na biashara ya kuchoma mahindi katika jiji la Arusha kinatarajia kuongeza kipato kupitia biashara hiyo baada ya wanachama wake kupatiwa majiko yaliyosanifiwa kwa tenknolojia ya kisasa.
Upatikanaji wa majiko hayo yaliyotengenezwa kwa teknolojia ya aina yake unaelezwa kuiongezea dhamani biashara hiyo ya uchomaji mahindi ambayo akinamama wengi na vijana wamekuwa wakiifanya.
Kwa msaada mkubwa wa mtandao wa vijana nchini,kikundi kinachofahamika kama Wamama Wachoma Mahindi Arusha kimeweza kufadhiliwa na kupata majiko sita yenye dhamani ya shilingi milioni mbili ambapo mwenyekiti wa kikundi hicho Bi Sophia Juma anasema yatasaidia kuongeza ufanisi katika biashara hiyo.
Mwenyekiti wa mtandao wa vijana nchini YDN,Bw.Elipokea Urio amesema upatikanaji wa majiko hayo ni sehemu ya mikopo midogomidogo ambayo imekuwa ikitolewa na halmashauri ya jiji la Arusha katika kuinua vipato cha vya wafanyabiashara wadogo na wakati.
Naye Fundi aliyesanifu majiko hayo Bw.John Werema amesema kitaalamu aina hiyo ya majiko ni rafiki wa mazingira kutokana na muundo wake
Biashara ya uchomaji wa mahindi licha ya kutengeneza ajira kwa baadhi ya kinamama na vijana imekuwa ikielezwa kuchangia uchafuzi wa mazingira katika baadhi ya maeneo nchini lakini sasa aina hii ya majiko inaelezwa kuwa tiba sahihi katika kukabiliana na hali hiyo.

SIMBA YAPATA MTEREMKO TANGA- YAIFUNGA COASTAL UNION 2-1

Mchezaji wa timu ya Simba akikokota mpira baada ya kumtoka beki wa timu ya Coastal Union ya Tanga Felix Stanley katika mchezo wa Ligi kuu ya Vodacom mzunguko wa pili unaoendelea kwenye uwanja wa Taifa jioni hii,Mpira umekwisha Simba imeshinda goli 2-1goli la kwanza limefungwa na mchezaji Haruna Moshi "Boban" katika kipindi cha kwanza na goli la pili likafungwa na mchezaji Gelvas Kago akipokea pasi nzuri ya Haruna Moshi. Timu ya Coastal Union ilifanikiwa kupata goli katika kipindi cha pili kwa njia ya penati lililofungwa na mchezaji Hamis Shengo, mpaka mpira unakwisha simba 2 na Coastal Union 1.
Mashabiki wa timu ya Simba wakishangilia mara baada ya timu yao kupata goli la kuongoza dhidi ya Coastal Union katika mchezo huo.

Baadhi ya Maafisa Kilimo wa Halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga na wakulima wakikagua shamba katika kijiji cha Kaoze.
NA :Ramadhani Juma, Afisa habari wilaya ya Sumbawanga 
VIKUNDI vya wakulima katika Halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga Mkoani Rukwa vimeanza kufaidika na miradi ya kilimo kupitia Mashamba Darasa inayodaiwa kuwaongezea mbinu za kisasa za kilimo bora hali inayotarajiwa kuwaongezea mavuno na kipato ikiwa ni juhudi za kujikwamua kutoka katika lindi la umasikini.
Baadhi ya wanachama wa kikundi cha CHEMKA kilichopo katika kijiji cha Kaoze kilichopo bonde la ziwa Rukwa walisema wamenufaika sana na elimu ya mradi wa shamba darasa uliotekelezwa katika kijiji hicho na kwamba wamekuwa wakipoteza mazao mengi kwa kulima kilimo cha kiasili.
Walisema kuwa, kwa kipindi kirefu wamekuwa wakivuna magunia matatu mpaka matano kwa hekari moja walipokuwa wakilima kilimo cha asili lakini kwa kilimo bora cha kisasa wanategemea kupata magunia 25 mpaka 30 kwa hekari moja hivyo wanategemea kujiongezea kipato na kujikwamua katika umasikini.
Kwa mujibu wa Afisa Kilimo wa wilaya hiyo Shaaban Bahari, Halmashauri hiyo ina jumla ya mashamba Darasa 151 katika vijiji mbalimbali wilayani humo na kwamba hali hiyo inatarajiwa kuwafaidisha wakulima.
“Tunategemea miradu hii itawasaidia wakulima wetu kujiongezea mbinu mbalimbali za kilimo cha kisasa ikiwemo matumizi ya mbolea, kupanda kwa kuzingatia nafasi, pamoja na kutumia mbegu bora” alisema Juma.
Miradi hiyo ya mashamba darasa inatekelezwa na wilaya hiyo katika vijiji na Kata mbalimbali kwa lengo la kuwaongezea ujuzi wakulima wilayani humo, ikiwa ni pamoja na matumizi ya mbolea pamoja na mbinu nyingine za kilimo cha kisasa.

President Jakaya Kikwete is received by the Minister for Agriculture, Food Security and Cooperatives Professor Jumanne Maghembe as he arrives at the Davos Sheraton ahead of the four day World Economic Forum held annually in the mountainous health resort. The forum, that goes under the theme: " The Great Transformation: Shaping New Models", Ais being attended by mong others President Kikwete is also scheduled to hold a number of private meetings and bilateral talks with prominent world leaders and entrepreneurs, besides attending interactive sessions on different issues.
President Jakaya Kikwete holding a preparatory meeting with his delegations soon after arrival at the Davos Sheraton ahead of the start of the four day World Economic Forum held annually in the mountainous health resort. The forum, that goes under the theme: " The Great Transformation: Shaping New Models", Ais being attended by mong others President Kikwete is also scheduled to hold a number of private meetings and bilateral talks with prominent world leaders and entrepreneurs, besides attending interactive sessions on different issues. (PHOTOS BY STATE HOUSE)

Tuesday, January 24, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AANZA ZIARA YA MKOA WA TANGA LEO, AKAGUA UKUTA WA KUZUIA MAJI YA BAHARI PANGANI

Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua rasmi Jengo la Ofisi ya Idara ya Maji, lililopo Wilaya ya Pangani, wakati alipoanza ziara yake ya Mkoa wa Tanga leo, Januari 24, 2012. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa (kushoto) ni Mkurugenzi wa Maji wa wilaya hiyo, Mohamed Hamis.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kuhusu ukuta huo unaozuia maji ya Bahari unaobomoka kutokana na mabadiliko ya Tabia nchi na kutishia amani ya wakazi wa maeneo hayo. Pangani Kivukoni.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya Viongozi wa Wilaya ya Pangani wakati akitoka kukagua ukuta wa kuzuia maji ya Bahari unaobomoka Pangani Kivukoni.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia ukuta unaozuia maji ya Bahari eneo la Pangani Kivukoni, unaozidi kubomoka kutokana na kujengwa miaka 100 iliyopita na kutishia amani kwa wakazi wa maeneo hayo. Makamu wa Rais ameanza ziara yake ya Mkoa wa Tanga leo Januari 24, 2012.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, amekutana na watendaji wa Wizara Afya, Ikulu Mjini Zanzibar leo,katika mpangilio wake wa kuzungumza na kila Wizara ya Serikali ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza na watendaji wa Wizara Afya katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar jana,katika mpangilio wake wa kufanya mazungumzo na kila Wizara ya Serikali. Picha na Ramadhan Othman IKULU.

KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma(PAC), imeagiza kwamba sheria inayoruhusu Mamlaka ya Nishati na Madini(EWURA) kulipa mishahara ya watumishi wa Baraza Ushauri na Watumaji la Nishati na Madini (EWURA CCC) ibadilishwe ili baraza hilo liweze kufanya kazi ipasavyo.
Hayo yalisemwa leo na Makamu Mwenyekiti wa PAC, Deo Filikunjombe wakati akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye ofisi ndogo za Bunge jijini Dares Salaam kuhusu shughuli zilizofanywa na kamati yake , ambapo alisema baraza hilo hesabu zake zinakwenda vizuri.
“Baraza hili hesabu zake ni nzuri , lakini halifanyi kazi ipasavyo kwa kuwa halimtendei kazi ipasavyo liko pamoja na EWURA tumeagiza sheria ibadilishwe ili liweze kufanya kazi kwa kuzingatia pande zote,” alisema Filikunjombe.
Makamu Mwenyekiti huyo alishauri kuwa ni vyema mishahara hiyo ilipwe na wizara husika ili baraza hilo lifanye kazi bila kuegemea upande mmoja.
Akizungumzia kuhusu upandaji wa umeme kwa asilimia 40 alihojia upanda kwa sababu zipi je mlaji wa chini wamemsikiliza wanasemaje, hivyo alisema haitakuwa sahihi ikiwa hakusikilizwa.
Aliongeza kuwa baraza hilo pia linatakiwa kuacha kulipa malipo ya kila baada ya miaka mitano mtumishi anapostaafu badala yake yawe katika mfumo ya mifuko ya hifadhi ya jamii, ikiwemo kuwaingiza watumishi wake katika Mfuko wa Bima ya Afya ili kuepuka utumiaji wa risiti za malipo ya matibabu.
Alitaka baraza hilo kutumia fedha kulingana na bajeti yake.
Wakati huohuo Filikunjombe alisema kamati hiyo imemfukuza mwakilishi wa Shirika Hodhi la Mali za Umma (CHC) kwa kuwa ni mtendaji wa chini hawawezi kuzungumza naye hivyo wanamtaka Ofisa Mtendaji Mkuu.
Alisema mwakilishi aliyetumwa ni Ofisa Uhusiano ambayo ameitumwa na Kaimu Mkurugenzi.

Na. Aron Msigwa –MAELEZO.
Kuanzishwa kwa mkakati wa kitaifa wa mabadiliko ya Tabia nchi kutaiwezesha na kuiongezea uwezo nchi ya Tanzania kushirikiana na mataifa mbalimbali katika kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchini yanayoendelea kuikumba dunia.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Mazingira, Ofisi ya makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi wakati akifungua mkutano wa wadau wa mazingira kujadili mkakati wa kitaifa wa mabadiliko ya Tabia nchi.
Amesema hivi sasa mabadiliko ya tabia nchi yameleta athari kubwa duniani ikiwemo ongezeko la gesi joto angani jambo ambalo linahitaji juhudi za mtu mmoja mmoja, vikundi, Taasisi na Jumuiya za kimataifa kushirikiana kwa pamoja kuinusuru dunia kutokana na athari za mabadiliko hayo.
“ Tanzania na watanzania wote kwa ujumla watapata fursa ya kushiriki katika fursa za miradi ya kupunguza gesi joto kupitia sekta binasfi hasa fursa za miradi ya kupunguza gesi joto inayoanzishwa nchini na kuwawezesha watanzania kupata fedha huku wakiendelea kufanya shughuli zao za kila siku”
Amefafanua kuwa mkakati huo wa kitaifa wa mabadiliko ya Tabia nchi utaisaidia nchi ya Tanzania kushiriki katika masuala mbalimbali ya kimataifa na kuiwezesha kuwa na msimamo kama nchi kupinga vitendo vyote vinavyofanywa na mataifa mbalimbali yaliyoendelea kiviwanda ambayo yanachangia kwa kiwango kikubwa ongezeko la gesi joto duniani.
Pia amefafanua kuwa licha ya mkakakati huo kuanzishwa kwa mara ya kwanza kwanza nchini utaiwezesha Tanzania kuwa ushirikiano na nchi nyingine za Afrika, jumuiya mbalimbali za kimatifa ndani na nje ya bara la Afrika na kuongeza kuwa ukamilishwaji wa mkakati huo utaiwezesha nchi kupanga na kuamua masuala mbalimbali yahusuyo mabadiliko ya Tabia nchi.
Aidha amefafanua kuwa sanjari na kuwepo mkakati huo ambao ni mkubwa masuala ya mazingira yataendelea kuongozwa na mkakati wa kitaifa wa mwaka 2006 na ule wa 2007 unaotoa mwongozo kuhusu masuala mbalimbali ya mazingira yakiwemo uzuiaji wa uchafuzi na uharibifu wa vyanzo vya maji katika mito na uharibifu wa misitu na mazingira.
Kwa upande wake mshiriki wa mkutano huo kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam Prof. Richard Kangalawe amefafanua kuwa mabadiliko ya tabia nchi yanendelea kuathiri kwa kiasi kikubwa uchumi wan chi yetu na hata kutishia maisha ya kila siku.
Amezitaja baadhi ya changamoto ambazo Tanzania kwa sasa inakabiliana nazo kutokana na mabadiliko ya Tabia nchi kuwa ni pamoja na ukame katika baadhi ya maeneo, mafuriko yanayojitokeza katika maeneo mbalimbali nchini kutokana na mvua zinazonyesha kwa muda mfupi na ongezeko la magonjwa mbalimbali.
“Kama tunavyoona kuna dalili mbalimbali ambazo zinaonyesha kuwa hali ya mabadiliko ya tabia nchi imekuwa kubwa sana tofauti na miaka 30 iliyopita na inaliathiri taifa hasa baadhi ya matukio mbalimbali yaliyotokea hivi karibuni ikiwemo mvua kubwa zilizonyesha na kusababisha mafuriko katika maeneo mbalimbali nchini na kusababisha madhara makubwa katika jiji la Dar es salaam.

Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja (kushoto) akiwekeana saini na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Motherland Industries Limited kutoka India Bw, V. K. Sood (Kulia) uwekaji saini wa mikataba mitatu ya utafiti wa mafuta nchini, umefanyika leo jijini Dar es Salaam, (Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO)
Kamishna Msaidizi wa Nishati kutoka Wizara ya Nishati na Madini Bw, Prosper Victus (alisimama mbele na Kabrasha) akitoa maelezo ya awali wakati wa uwekaji wa saini mikataba mitatu ya utafii wa mafuta kutoka kampuni za nje leo wakati wa hafla hiyo kwenye jengo la Wizara ya hiyo jijiji Dar es Salaam. (Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO).
Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja (kulia) akifafanua jambo wakati wa uwekaji saini wa mikataba mitatu ya uatafiti wa mafuta kutoka kampuni za nje jijini leo DSM (Kulia) ni Kamishna Msaidizi wa Nishati (Petroleum na Gas ) Bw, Prosper Victus, (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).
Waziri wa Nishati na Madini Wiliam Ngeleja (kushoto) akibadilisha hati za makubaliano ya utafiti wa mafuta nchini na Mkurugenzi Mtendaji wa kampun i ya Petrobras kutoka Brazil Bw, Samuel Bastos de Miranda (kulia) , hafla hiyo imefanyika leo jijini Dar es Slaam wakati wa hafla ya uwekaji saini wa mikataba mitatu ya utafiti wa mafuta wa kampuni kutoka nje, (Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO).
Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja (katikati) akiweka saini mkataba wa utafiti wa mafuta nchini kwa kampuni tatu kutoka nje, (kushoto) ni Mkurugenzi mtendaji wa TPDC Bw, Yona Killagane na (kulia) Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Matherland industries LTD kutoka India, Bw. V.K. Sood .(kulia). Mkataba huo umewekwa saini leo kwenye jingo la Wizara ya Nishati na Madini, (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza na watendaji wa Wizara ya Ardhi,Makaazi,Maji na Nishati, Ikulu Mjini Zanzibar,katika mpangilio wake wakuzungumza na kila Wizara ya Serikali ya Zanzibar,katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo. Picha na Ramadhan Othman IKULU.
Baadhi ya Watendaji wa Wizara ya Ardhi,Makaazi,Maji na Nishati,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza na watendaji hao Ikulu Mjini Zanzibar,katika mpangilio wake wakuzungumza na kila Wizara ya Serikali ya Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akisalimiana na ujumbe wa Mabalozi wa Tanzani Nchi za Nje,ambao wanakwenda nchi mbali mbali kiwakilisha Tanzania,walipofika kumuaga Rais Ikulu Mjini Zanzibar.(24 Jan 2012)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akisalimiana na ujumbe wa Mabalozi wa Tanzani Nchi za Nje,ambao wanakwenda nchi mbali mbali kiwakilisha Tanzania,walipofika kumuaga Rais Ikulu Mjini Zanzibar.(24 Jan 2012) Picha na Ramadhan Othman IKulu.

Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kupitia kitengo chake cha utatuzi wa migogoro (Dispute Resolution Chamber- DRC) limeagiza klabu ya Yanga kumlipa mchezaji John Njoroge sh. 17,159,800 ikiwa ni fidia kwa kuvunja mkataba wake kinyume cha taratibu.
Uamuzi huo wa DRC chini ya Jaji Theo van Seggelen ambaye ni raia wa Uholanzi ulifanywa Desemba 7 mwaka jana jijini Zurich, Uswisi na kutumwa TFF kwa njia ya DHL, Januari 17 mwaka huu.
Njoroge ambaye ni raia wa Kenya aliwasilisha kesi yake FIFA kupinga Yanga kuvunja mkataba alioingia wa kuichezea timu yao kinyume na makubaliano. Mchezaji huyo hivi sasa anachezea timu ya Tusker ambayo ni mabingwa wa Kenya.
Yanga ina siku nne za kukata rufani kupinga uamuzi huo kuanzia tarehe iliyoupokea kama inataka kufanya hivyo. Klabu hiyo inatakiwa iwe imeshamlipa Njoroge ndani ya siku 30 tangu ilipopokea uamuzi huo. Ikishindwa kulipa ndani ya muda huo, itatozwa riba ya asilimia 5 kwa mwaka ya fedha hizo.
Ikiwa Yanga itashindwa kulipa ndani ya muda huo vilevile suala hilo litafikishwa mbele ya Kamati ya Nidhamu ya FIFA kwa hatua zaidi.
Powered by Sorecson : Creation de site internet

Kiingilio cha chini kwa mechi ya kufuzu kwa fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC) kati ya Twiga Stars na Namibia itakayochezwa Jumapili (Januari 29 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kitakuwa sh. 2,000.
Kiwango hicho ni kwa washabiki kwa viti vya bluu na kijani. Viti hivyo kwa pamoja vinachukua jumla ya watazamaji 36,693 kwenye uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua washabiki 60,000.
Pia kutakuwa na kiingilio cha watoto wenye umri wa chini ya miaka 10 ambacho ni sh. 1,000. Watoto watakaotumia tiketi hizo wanatakiwa kuingia uwanjani wakiwa na wazazi au walezi wao.
Viingilio vingine kwa mechi hiyo ni sh. 3,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 5,000 kwa VIP B na C n ash. 10,000 kwa VIP A.
Namibia inatarajia kuwasili nchini Ijumaa (Januari 27 mwaka huu) saa 12.45 jioni kwa ndege ya South Africa Airways.

Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imefanya marekebisho madogo kwenye ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom kutokana na Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kutumika kwa sherehe za kitaifa za kuzaliwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mechi namba 111 kati ya Toto Africans na African Lyon ambayo kwa mujibu wa ratiba ilikuwa ichezwe Februari 5 mwaka huu Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza sasa itachezwa Aprili 18 mwaka huu.
Mabadiliko hayo yamefanyika baada ya wamiliki wa Uwanja wa CCM Kirumba, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kueleza kuwa watautumia kwa sherehe za kuzaliwa chama chao, hivyo hautakuwa na nafasi kwa Februari 4, 5 na 6 mwaka huu.
Uamuzi huo umesababisha pia mabadiliko kwa mechi nyingine mbili. Mechi namba 168 kati ya Villa Squad na African Lyon iliyokuwa ichezwe Aprili 18 mwaka huu Uwanja wa Chamazi jijini Dar es Salaam, sasa itachezwa Aprili 22 mwaka huu.
Pia mechi namba 170 kati ya Azam na Toto Africans iliyokuwa ichezwe Aprili 29 mwaka huu jijini Dar es Salaam sasa imerudishwa nyuma hadi Aprili 26 mwaka huu ambayo ni Sikukuu ya Muungano.

Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Mazingira,Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi akizungumza na wadau wa mazingira kutoka Taasisi mbalimbali,wizara na wadau kutoka nchi wahisani wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau hao unaojadili mabadiliko ya Tabia nchi na mkakati wa kitaifa kuhusu mabadiliko ya Tabia nchi leo jijini Dar es salaam. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
Mshauri wa masuala ya mabadiliko ya Tabia nchi kutoka Idara ya Kimataifa ya Maendeleo (DFID) nchini Tanzania Bi. Magdalena Banasiak (kushoto) akizungumzia athari za mabadiliko ya Tabia nchi duniani na mchango wa wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi katika kuhakikisha kuwa athari za mabadiliko ya tabia nchi zilizoanza kujitokeza zinadhibitiwa.
Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Mazingira,Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi akiwasilisha mada kuhusiana na mabadiliko ya Tabia nchi na ripoti ya tafiti ya athari za kimazingira iliyofanyika katika baadhi ya maeneo yakiwemo Zanzbar, Mbeya, Tanga, Manyara, Shinyanga na Mwanza leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wadau wa Mazingira kutoka ndani na nje nchi wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa mkutano wa wadau wa mazingira kuhusu mkakati wa kitaifa kuhusu mabadiliko ya Tabia nchi leo jijini Dar es salaam.
Wadau wa Mazingira kutoka, Taasisi mbalimbali,wizara na wadau wa mazingira kutoka nchi wahisani wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa mkutano unaojadili Mkakati wa Kitaifa kuhusu mabadiliko ya Tabia nchi leo jijini Dar es salaam.

Ayoub Mzee at the Africa Union Summit to attend the 18th ordinary session of the assembly of heads of state and governments
The advent of the African Union (AU) can be described as an event of great magnitude in the institutional evolution of the continent. On 9.9.1999, the Heads of State and Government of the Organisation of African Unity issued a Declaration (the Sirte Declaration) calling for the establishment of an African Union, with a view, inter alia, to accelerating the process of integration in the continent to enable it play its rightful role in the global economy while addressing multifaceted social, economic and political problems compounded as they are by certain negative aspects of globalisation.
The main objectives of the OAU were, inter alia, to rid the continent of the remaining vestiges of colonization and apartheid; to promote unity and solidarity among African States; to coordinate and intensify cooperation for development; to safeguard the sovereignty and territorial integrity of Member States and to promote international cooperation within the framework of the United Nations.
Indeed, as a continental organization the OAU provided an effective forum that enabled all Member States to adopt coordinated positions on matters of common concern to the continent in international fora and defend the interests of Africa effectively.
Through the OAU Coordinating Committee for the Liberation of Africa, the Continent worked and spoke as one with undivided determination in forging an international consensus in support of the liberation struggle and the fight against apartheid.

HII siyo bahati nasibu wala Bingo bali ni msaada wa kumuwezesha Mchungaji Deogratius Mosha wa Kanisa la Elishadai Gospel Ministry katika kumuwezesha kujikwamua kiuchumi kwenye Kanisa lake, hii ni sehemu ya mkakati wa Kanisa la Amri kuu za Mungu (Akuzamu) lililoko Jijiji Dar es salaam katika jengo la IPS,linalofundisha watu masuala ya uchumi na kuwawezesha kwa mahitaji mbalimbali ambapo tukio hili lilifanyika katika semina ya uchumi iliyofanyika kwenye ukumbi wa Nadd's uliko Salender Bridge juzi (picha na Salesi Malula)
Na salesi Malula
Mchungaji Edward Amri wa huduma ya Amri Kuu za Mungu (AKUZAMU) amewapiga marufuku waumini wake kuacha kuilaumu Serikali kwani haisaidii chochote katika maisha yao na kufanya hivyo ni kinyume na Neno la Mungu.
Ameyasema hayo alipokua akifundisha Neno la Mungu katika ibada ya Jumapili, ambapo aliwaasa wakristo kufuata Kanuni ya Neno la Mungu, ili waweze kufanikiwa katika kila eneo na kuepuka kuilaumu serikali kila mara, jambo ambalo haliwezi kuleta majibu katika maisha yao ya Kila siku.
Alisema ifikie mahali Watanzania wajiulize nini wataifanyia nchi yao kwani sisi kama Kanisa lazima tuwe Baraka kwa Taifa na siyo kugeuka wapinzania kwa kuilaumu serikali; kinachotakiwa kila Kanisa liwe na utaratibu wa kuwasaidia waumini wake kwa kuwapa mafundisho ya namna ya kujikwamua kiuchumi, likiwepo suala la kuwahamasisha waweze kujiajiri ili waweze kuisaidia serikali katika kutoa ajira na kulipa kodi kwa usashihi.
“Kazi ya Kanisa ni kuisaidia serikali na siyo kuipinga na kuwatengeneza watu wake yaani waumini kuwa raia wema wenye kuipenda nchi yao likiwepo suala la kuwakwamua watu kiuchumi kwa kuwafundisha mafundisho sahihi ya uchumi katika ufalme wa Mungu, kama ambavyo kanisa letu linafanya ambapo muda si mrefu sisi tutakuwa Baraka katika Taifa kwani waumini wetu wengi wataajiri na watakuwa na walipakodi wazuri katika nchi yetu”.
Akiongea kwa kujiamini alisema kwa sasa uchumi wa dunia nzima umekwama na sababu yake ni kwamba ni vigumu sana uchumi wa mfumo huu kufaulu kwa sababu hauna mbadala, yaani ziada kwani masomo hayo ya uchumi yanayofundishwa shuleni miaka 20 iliyopita ndio hayo hayo yanafundishwa hivyo wachumi wetu hawawezi kuwa na la ziada zaidi ya kujifunza masomo ambayo wenzao waliyagundua zamani na ndio maana hadi hivi sasa hawawezi kutoa majibu ya kuboresha maisha ya wananchi.
Akitoa mfano alisema kwa sasa nchini kwetu hatuna vitu ambavyo tumegundua. Kwa mfumo wa uchumi wa kwenye makaratasi hauwezi kutoa majibu kwani hata hao wachumi endapo masomo yangekuwa na hatimiliki nadhani sisi tusingekuwa na kitu kwani masomo hayo tunakopi kutoka kwa wenzetu ambapo hatuwezi kuwa na mbadala na ndio maana unaweza kukuta tunao wasomi wengi wa uchumi wasipoajiriwa hawawezi kuishi wanachanganyikiwa maana hawana mbadala
Akieleza mikakati ya Kanisa lake amesema wao wameamua kuisaidia serikali badala ya kuilaumu kwa kuwaelimisha waumini wao masuala ya uchumi katika ufalme wa Mungu kwa kutumia Neno la Mungu, pamoja na kuwahamasisha juu ya umuhimu wa kujiajiri ili waweze kuwaajiri wengine.
Akijitolea mfano yeye alisema kabla hajaanza kumtumikia Mungu alijiajiri kwa kufungua biashara ambapo miaka hivi sasa anao wafanyakazi wasiopungua mia moja wanaofanyakazi katika biashara zake hivyo amekua msaada kwa serikali kwa kuipunguzia kero ya ajira kwani ameajiri na analipa kodi serikalini hivyo amekua Baraka kwa nchi.
Mbali na hilo amekuwa na mkakati wa kuwahamasisha wale aliowaajiri kutojisahahu badala yake nao wafungue biashara zao nao waweze kuajiri watu wengine kwani ifikie hatua tuipunguzie mzigo serikali badala ya kuilaumu.
Amekemea tabia ya baadhi ya watumishi pamoja na waumini kuilaumu serikali kwa kusema eti inasababisha hali ngumu jambo ambalo amesema si kweli kwani mazingira ya sasa karibu nchi zote zimekwama ni wakati wa Kanisa kuisaidia serikali kwa kuwafundisha waumini Neno la Mungu kwa usahihi pamoja na kuwasaidia kujiajiri badala ya kutumia muda mwingi kuilaumu serikali jambo ambalo si sahihi.
Tangu mwaka 2012 Kanisa la Akuzamu chini ya kiongozi wake Mchungaji Edward Amri limeanzisha kampeni kabambe kuisaidia serikali kwa kuiombea pamoja na kuwahamasisha waumini wake kujiajiri na kuwaajiri wale ambao bado hawana ajira ambapo pia limekuwa likitoa mafundisho ya uchumi kila siku katika ukumbi wa IPS Jijini Dar es salaam na kila mwezi, ambapo mwezi ujao linatarajia kuendesha semina kubwa itakayofanyika katika ukumbi wa Nadd’s ulioko salender bridge jijini Dar es salaam tarehe ishirini na tano mwezi ujao ambapo wengi wamekuwa wakihudhuria na mara baada ya mafundisho wengi wamebadilika katika ufahamu wao na wameanza kuchukua hatua ya kujiajiri.