TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, January 2, 2014

MAN UNITED YAVURUGWA TENA, YAFUMULIWA 2-1 NA SPURS, ARSENAL, MAN CITY, CHELSEA, LIVERPOOL MWENDO MDUNDO EPL!!

In form: Adebayor (left) has scored four goals in five games since Tim Sherwood took over as manager 
Yupo kwenye kiwango: Adebayor (kushoto) amefunga mabao matano mpaka sasa katika mchezo mitano tangu Tim Sherwood apewe mikoba ya kocha aliyetimuliwa AVB
Doubling up: Eriksen's header leaves De Gea stranded at Old Trafford as Tottenham edge further in front 
La pili: Eriksen akifunga kwa kichwa bao la pili  na kumwacha kipa wa Man United De Gea akiambulia manyoya katika uwanja wa  Old Trafford
Down and out? Manchester United prepare to take kick off after conceding the second goal 
Ebwana daaah! mwaka majanga? Manchester United wakijiandaa kuanzisha mpira baada ya kufungwa bao la pili.
Matokeo ya mechi za leo ni kama hapo chini 
   
Finished
 
 Swansea
2-3
Manchester City 
 
(1-1)        
   
Finished
 
 West Bromwich Albion
1-0
Newcastle United 
 
(0-0)        
   
Finished
 
 Sunderland
0-1
Aston Villa 
 
(0-1)        
   
Finished
 
 Stoke
1-1
Everton 
 
(0-0)        
   
Finished
 
 Arsenal
2-0
Cardiff 
 
(0-0)        
   
Finished
 
 Crystal Palace
1-1
Norwich 
 
(1-1)        
   
Finished
 
 Southampton
0-3
Chelsea 
 
(0-0)        
   
Finished
 
 Liverpool
2-0
Hull 
 
(1-0)        
   
Finished
 
 Fulham
2-1
West Ham 
 
(1-1)        
   
Finished
 
 Manchester United
1-2
Tottenham 

KIVUMBI MAPINDUZI 2014: SIMBA SC YAITAFUNA LEOPARD 1-0, KIEMBA AIBUKA SHUJAA, KMKM YALIZWA, MBEYA CITY YATOA SARE GOMBANI!!


BAO pekee la kiungo mtata wa Wekundu wa Msimbazi, Simba sc, Amri Ramadhan Kiemba limetosha kuibuka na pointi 3 muhimu za kwanza usiku jana katika mechi yao ya kwanza  kombe la Mapinduzi 2014 iliyoanza kutimua vumbi leo hii viwanja viwili vya Amaan, Unguja na Gombani, Pemba.
Mgeni rasmi katika mchezo huo alikuwa kocha wa Timu ya Taifa ya  Italia, Cesare Prandelli ambaye alikagua timu zote na kwenda katikati ya dimba la Amaan na kuudunda mpira ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa michuano ya mwaka huu.
Mchezo huo wa kundi B ulioanza majira ya saa 2:00 usiku ndio uliochaguliwa kuwa wa ufunguzi katika michuano ya mwaka huu ambayo ni maalumu kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
blogger-image--1657134963

Amri Kiemba amewaliza AFC Leopard
Fundi Kiemba aliyeanzia benchi leo hii na kuingia dakika ya 47 kuchukua nafasi ya Kiungo mpya wa Simba aliyesajiliwa kutoka Mtibwa Sugar dirisha dogo mwaka jana, Awadh Juma Issa, alifunga bao hilo baada ya kuuwahi mpira uliookolewa na beki wa AFC Leopard kufuatia Amisi Tambwe kujaribu kuunganisha krosi maridadi uliochongwa na Ramadhan Singano `Messi` dakika ya 77 ya mchezo.
`Messi` huyu mtoto ni nuksi tupu!, alifanya vitu vyake vya Nani Mtani Jembe baada ya kumlamba chenga ya aibu beki mrefu zaidi na mkongwe, Joseph Shikokoti na kupiga krosi iliyosababisha bao hilo muhimu.
Ushindi wa leo kwa Simba sc umewapatia nguvu zaidi katika harakati zao za kuusaka ubingwa ambao kwa mara ya mwisho kuutwaa ni mwaka 2011.
Kwasasa Azam fc ndio mabingwa watetezi mara mbili mfululizo, yaani walitwaa `ndoo` hiyo 2012 na 2013.
Hata hivyo imekuwa neema kwa kocha msaidizi wa Simba, Suleiman Matola `Veron` ambaye alisimama kwenye benchi la ufundi wakati akimsubiri bosi wake Mcroatia, Zdravko Logarusic ambaye atawasili kesho Zanzibar.
Mechi ya leo ilijigawa kwa timu zote kwani Leopard walicheza vizuri dakika 45 za kwanza, lakini Simba SC walichachamaa kipindi cha pili na kucheza soka safi, lakini kukosa umakini kwa washambuliaji wa klabu hiyo kumewanyima ushindi mnono.
Simba sasa wanashika nafasi ya pili kundi B wakijikusanyia pointi tatu sawa na KCC ya Uganda wenye pointi 3, lakini wao wanawastani mzuri wa mabao ya kufunga.
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Ivo Mapunda, Haruna Shamte, Issa Rid, Joseph Owino, Donald Mosoti, Jonas Mkude, Haruna Chanongo, Ramadhani Chombo/Uhuru Suleiman dk89, Amisi Tambwe/Betram Mombeki dk81, Ramadhan Singano, Awadhi Juma/Amri Kiemba dk47.
AFC Leopard; Martin Masalia, Etenesy Augustin, Abdallah Juma, Saleh Jackson, Joseph Shikokoti, Imbalebala Martin, Okwemba Charles, Mussa Mude, Kelly Jacb, Mang’ole Benard/Seda Edwin dk86 na Oscar Kadenge/Hassan Mohamed dk86.
Awali katika dimba hilo, mabingwa wa Zanzibar KMKM walilala kwa mabao 3-2 dhidi ya KCC kutoka nchini Uganda katika mchezo wa Kundi A.
Mabao ya KCC yalifungwa na Herman Waswa dakika ya 10, Tony Odur katika dakika ya 20 na William Waoro dakika ya 82, wakati ya KMKM yalifungwa na Hamisi Ali dakika ya saba na Maulid Ibrahim dakika ya 79.
Huko uwanja wa Gombani, Pemba, vijana wa Juma Mwabusi, Mbeya City wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Clove Stars. 
Bao la Mbeya City lilifungwa dakika ya 13 na Deus Kaseke, lakini dakika ya 24 kipindi hicho cha kwanza, Clove Stars.

BONY MWAITEGE AFANYA KWELI TAMASHA LA KRISMAS DODOMA

  1. 1Mwimbaji wa muziki wa injili nchini Bony Mwaitege akiimbisha mashabiki wake kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma wakati akiimba kwenye tamasha la Krismas lililofanyika leo na kushirikisha waimbaji wa muziki wa injili kutoka maeneo mbalimbali nchini  Tanzania , Tamasha hilo linaandaliwa na kampuni ya Msama Promotion ya jijini Dar es salaam na tamasha la leo lilikuwa linahitimisha ziara ya mikoa minne ya Tanzania ambako matamasha hayo yamefanyika ambayo ni Dar es salaam, Morogoro, Tanga, Arusha na tamasha la  leo mjini Dodoma 2Mwimbaji wa muziki wa injili nchini Bony Mwaitege akisalimiana na mashabiki wake wakati alipokuwa akiimba kwenye uwanja waJamhuri Mjini Dodoma leo. 4Mgeni rasmi Mbunge wa jimbo la Tarime na Mwandishi wa vitabu Nyambari Nyangwine akitoa neno kwa mashabiki  waliohudhuria kwenye tamasha la Krismas kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, kulia ni Alex Msama Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion. 5 
  2. aadhi ya mashabiki waliohudhuria kwenye tamasha la Krismas wakiimba pamoja na mwimbaji Upendo Nkone hayupo pichani wakati akifanya vitu vyake jukwaani. 6 
  3. Hapa ni kusifu na kuabudu tu. 7Ikafika saa ya maombi 9Mashabiki wakitoa ushirikiano kwa mwimbaji Upendo Nkone hayupo piuchani. 10Upendo Nkone akifanya vitu vyake mbele ya mashabiki wake kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo. 11Upendo Nkone akicheza na mashabiki wake. 12Mwimbaji Rose Muhando akikata kiu ya mashabiki wake mjini Dodoma leo. 13 
  4. Hii ni sataili ya kucheza kiduku kwa kumsifu yesu kaazi kwelikwe. 15Upendo Kilahiro akiimba na waimbaji wenzake kutoka kushoto ni Edson Mwasabwite, Tumaini Njole na  Faraja Ntaboba. 18kutoka kulia ni Edson Mwasabite, Tumaini Njole na Faraja Ntaboba kutoka DRC Kongo wakiimba kwa pamoja.19Baadhi ya mashabiki wakiwa katika tamasha hilo.  20Mwimbaji Tumaini Njole akifanya vitu vyake. 21
  5. Vijana wa kazi The Voice wakifanya vitu vyao katika tamasha hilo.


TASWA FC YAANZA MWAKA MPYA KWA KUICHAPA TWANGA PEPETA 1-0!!


 Beki wa timu ya Taswa Fc Sufianimafoto (kulia) akiwania mpira na mshambuliaji wa Twanga Fc, wakati wa mchezo wa kirafiki wa Bonanza la kufunga mwaka na kuukaribisha mwaka mpya wa 2014, lililofanyika kwenye Viwanja vya Leaders Club Kinondoni, leo jioni. Katika mchezo huo Taswa ilianza mwaka mpya kwa ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Juma Pinto katika kipindi cha pili.
 Mshambuliaji wa Taswa Fc, Juma Pinto (katikati) akiwatoka mabeki wa Twanga Pepeta Fc, wakati wa mchezo huo.
 Beki wa Taswa Fc, Athuman (kulia) akiwatoka wachezaji wa Twanga Pepeta.
 Winga wa Taswa Fc, Zahro Milanzi (kulia) akimiliki mpira……
 Kocha wa Twanga Pepeta Fc, ambaye pia ni Mkurugenzi wa bendi hiyo Asha Baraka, akitoa mawaidha kwa wachezaji wake wakati wa muda wa mapumziko.
 Wachezaji wa Taswa Fc, wakimsikiliza Kocha mchezaji Ally Mkongwe, wakati wa mapumziko.
 Benchi la Twanga likiwa haliamini kilichotokea uwanjani…
 Hapa utaenda wewe mpira utabaki………tulia kama ulivyooooo…..
 Hapiti mtu hapa……..
 Mwamuzi wa mchezo huo akichezesha huku akiwa na chupa ya soda ya Novida iliyo na kinywaji cha Konyagi ndani yake……

MAISHA PLUS/MAMA SHUJAA WA CHAKULA

Haya sasa… Mchakato wa Kupata Washiriki 30 wa Maisha Plus
Na washiriki 10 wa Mama Shujaa wa Chakula , 2014 Umeanza!
Fomu zinapatikana:
IRINGA – EBONY FM 87.8
SONGEA- JOGOO FM 93.0
SHINYANGA- FARAJA FM 21.3
ZANZIBAR – ZENJI FM 96.8
MOROGORO- ABOOD RADIO 89.7
MWANZA- PASSION FM 99.9
MTWARA- PRIDE FM 87.8
BUKOBA- RADIO VISION 98.0FM
MBEYA- BOMBA FM 104.0
TABORA- CG FM 89.5
DODOMA – IMPACT FM 94.4
ARUSHA- RADIO 5 104.5
Pamoja na ofisi  zifuatazo: ….. ACTIONAID,ADGL KIVULINI, CONCERN, COWEA, CVM/APA, KICKSTAR-Money Maker, LBTIC, INADES FORMATION, NORWEGIAN CHURCH AID, OXFAM, SHDEPHA+, RISE TANZANIA,TREE OF HOPE, SASA Foundation, PWC, UZIKWASA, ADP Mbozi, VSO Tanzania, WOPATA, WOWAP, WOMEN PARALEGALS, KAWOCONET, MZALENDO PUB kwa Dar es Salaam.
Nani Anapaswa kuchukuwa Fomu:
Mama Shujaa:  Wakina Mama na wasichana Wakulima na Wafugaji, kuanzia miaka 18 na kuendelea
Maisha Plus:  Vijana, wasichana na wavulana kuanzia umri wa miaka 21 mpaka 26
fomu hizi zinaweza kujazwa moja kwa moja kupitia tovuti yetu ya www.maishaplus.tv na kupitia Facebook.com/MaishaPlus
Mwisho wa kurudisha Fomu ni: Tarehe 24 Mwezi wa Kwanza 2014
Mwaka huu kutakuwa na washiriki Maisha Plus kutoka Burundi, Rwanda, Uganda, Kenya pamoja na Tanzania.
Wahi kuchukua fomu yako sasa ujishindie Mamilioni ya Pesa.  
MAISHA PLUS/MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2014

DK.Shein aongoza Matembezi ya Bonanza la Vikundi vya mazoezi ya Viungo!!

TA1A5708  
Kikundi cha Barssband cha Mafunzo kikiwa mbele ya Matembezi ya Bonanza la 5 la Vikundi vya Mazoezi ya Viungo,yanayoongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein,na viongozi mbali mbali wakishiriki,matembezi  hayo yameanzia Uwanja wa Kisonge,hadi uwanja wa Amaan Wilaya ya Mjini Unguja,[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]TA1A5718  
Wanavikundi vya mazoezi ya Viungo wa Zone A,wakiwa katika  Matembezi ya Bonanza la 5,yanayoongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein,na viongozi mbali mbali wakishiriki,matembezi  hayo yaliyoanzia Uwanja wa Kisonge,na kumalizia  Uwanja wa Amaan Wilaya ya Mjini Unguja,[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]TA1A5759 
Kikundi cha Mchezo wa Judo,wakiwa katika Matembezi ya Bonanza la 5,yanayoongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein,na viongozi mbali mbali wakishiriki,matembezi  hayo yaliyoanzia Uwanja wa Kisonge,na kumalizia  Uwanja wa Amaan Wilaya ya Mjini Unguja,[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]TA1A5795 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein,(katikati) na viongozi mbali mbali walioshiriki,Matembezi  ya Bonanza la 5 la Vikundi vya Mazoezi ya Viungo,  yaliyoanzia Uwanja wa Kisonge,hadi uwanja wa Amaan Wilaya ya Mjini Unguja,[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
TA1A5823  
Wazee wa Mchezo wa Bao la kete,wakipita mbele ya Jukwaa la Uwanja wa Amaan,wakitoa heshma kwa mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein,katika Bonanza la 5 la vikundi vya mazoezi ya Viungo,lililofanyika leo,Wilaya ya Mjini  Unguja,katika shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar,.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
 TA1A5828 
Watu wenye ulemavu wa Miguu,wanotumia baskeli za maringi wakipita kutoa heshma kwa mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein,katika Bonanza la 5 la vikundi vya mazoezi ya Viungo,lililofanyika leo,Wilaya ya Mjini Unguja,katika shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar,.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
TA1A6211  
Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Wanamichezo wa Vikundi vya Mazoezi ya Viungo katika Bonanza la 5,Vikundi vya mazoezi ya Viungo,lililofanyika katika Uwanja wa Amaan,Wilaya ya Mjini Unguja,katika shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi ya zanzibar.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]TA1A6321 
Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,akionesha Cheti alichokabidhiwa na Waziri wa Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo Said Ali Mbarouk,  katika Bonanza la 5,lililofanyika katika Uwanja wa Amaan,Wilaya ya Mjini Unguja,katika shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi ya zanzibar.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

SALAMU ZA MWAKA MPYA KUTOKA MWANALIBENEKE MPALULE SHAABAN

Kwanza kabisa Napenda kuchukua nafasi hii Kumshukuru sana Mwenyezi Mungu Mwingi Wa Rehema Kwa Kuweza Kunijalia Uwezo,Nguvu na Afya na Bahati Pia ya Kuweza Kufika Mwaka 2014, Siwezi Kujidanganya Wala Kudanganya Kuwa nimefika Hapa Leo Mnamo tarehe 1 Jan 2014 Kwa ujanja wangu au uwezo hapana Nimefika hapa Kwa Neema Na Rehema Zake Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema, Na pIa sio Kwasababu ameniwezesha Kuuona na kuingia leo tarehe 1 Jan 2014 basi mimi ni mwema, msafi na mtiifu sana mbele zake kuliko wengine hapana Ila Ni Kwa Neema na Makusudi yake Pia Wapo waliopenda kuiona Siku kama ya Leo Lakini kwa mapenzi yake Muumba Hawakuweza kufika na Pia wapo walioweza Kufika lakini wakiwa sio wazima Kiafya Na Sio kwamba wao ni wakosaji sana mbele za Mungu hapana Bali yote hayo Hutokea Kwa Makusudi yake na
Mipango yake Pia.

Tuna kila sababu ya Kumbuomba Mwenye Mungu Mwingi wa Rehema Kila Dakika itupitayo na Sio Kusubiri Mwaka Mpya ndio Tumuombe, Tuna kila sababu ya kufanya kila siku iendayo kwake basi iwe ni Mwaka Mpya Kwake Kwa Kuomba, Kusali na KUmwabudu maana ni yeye Pekee ndiye Muweza wa Kila Jambo.

Napenda Kuchukua Nafasi hii Kuwatakia Watanzania wote na Dunia Nzima wakiwemo Wazazi Wangu, Ndugu zangu, kaka zangu, Dada zangu ,Wajomba, Mashangazi, Mama Wadogo, baba Wadogo, Marafiki zangu, Watembeleaji wa Blogu zenu wote, Marafiki zenu, Ndugu zenu, Bila kuwasahau Maadui zangu Wote maana na wao pia ni sehemu ya mimi kupata mafanikio madogo sana maana Usijisifie Kuwa Unaweza kukimbia Sifa pia Kilichokukimbiza au aliyekukimbiza pia…Kwa Kuweza Kufika Mwaka 2014 wakiwa na afya na wazima wa afya, Na Hata wale waliokuwa wagonjwa Basi Mwenyezi Mungu Awatie Nguvu ili waweze kupona na Kurejea majumbani Mwao wakitokea Mahospitalini kwaajili ya Kuungana na Familia zao pia.

Mwaka 2014 umeanza ikiwa ndio siku ya Kwanza kabisa ya Mwaka 2014, Tuzidi Kumuomba Mungu Mwingi wa Rehema Azidi Kutuepusha na Kutupigania katika Vita ya Kiroho dhidi ya Mwovu Shetani na Mawakala zake kama CHuki, Roho Mbaya, Majungu, Masimango, Uchawi, Na vingine vingi vya namna hiyo.

Vilevile napenda Kuchukua nafasi Hii Kuwashukuru wote kwa kuendelea Kuwa nami katika Kipindi hiki chote cha Mwaka 2013 na naomba tuendelee kushikamana, Kupendana, Kuombeana Mazuri na yenye heri na Kuweza Kufika Pale tulipojiwekea malengo yetu tena Kwa Mwaka 2014.

Namwomba Pia Mwenye Mungu Mwingi wa Rehema Azidi kunipa Nguvu, Afya , Hekima na Busara katika Kazi zote za halali nizifanyazo na hatimaye kuweza kufanikiwa hadi pale apendapo yeye nifike.

Mwisho Nachukua Nafasi hii Kuwatakia Wote Heri ya Mwaka Mpya 2014. Tufanye kazi Kwa Bidii na Tuzidi Kumuomba Yeye Kwa Ni yeye ndie atupaye Nguvu na kututia uwepesi wa Kila Jambo

KAMANDA WA POLISI MBEYA AITAKA JAMII KUSHEREHEKEA SIKUKUU YA MWAKA MPYA KWA AMANI

ahmed-msangi 
>KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA, KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI AHMED. Z. MSANGI ANAWATAKA WANANCHI WOTE WA MKOA WA MBEYA KUENDELEA KUSHEREHEKEA SIKUKUU YA MWAKA MPYA, 2014 KWA AMANI NA UTULIVU KWA KUFUATA SHERIA/KANUNI NA TARATIBU TULIZOJIWEKEA.
>AIDHA ANAENDELEA KUSISITIZA USHIRIKIANO KUTOKA KWA WANANCHI HASA KATIKA MWAKA HUU MPYA.
>MWISHO KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA, ANAWATAKIA KHERI YA MWAKA MPYA 2014, NA WENYE MAFANIKIO.

UMOJA WA WACHUNGAJI ZANZIBAR WAMTEMBELEA RAIS MSTAAFU MHE DKT. SALMIN AMOUR JUMA

01 (1) 
wa Dua Maalum ya kuiyombea Zanzibar kwenye mkesha wa mwaka mpya Allen Mbaga kutoka kanisa la Tanzania fellowship of churches (TFC) aliesimama kulia akiwatambulisha wachungaji waliofika nyumbani kwa Rais mstaafu wa Zanzibar Dkt Salmin Amour Juma kwa lengo la kumtembele na kumuomea huko Migombani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.02 
Rais mstaafu wa Zanzibar Dkt. Salmin Amour Juma wakuli alievaa kofia akiwapa historia ya Bara la Afrika kabla ya ukombozi wachungaji wa Zanzibar walipofika nyumbani kwake kumtembele jana huko nyumbani kwake Migombani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.04 
Wachungaji wakiongozwa na Askofu Fabian Obedi kutoka kanisa la Sentekoste Zanzibar wa tatu kushoto wakimuaga Rais mstaafu wa Zanzibar Dkt. Salmin Amour Juma mara baada ya kumaliza kumuombea nyumbani kwake Migombani Zanzibar Dec 31/2013.
(Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).

TUME YA SHERIA YAUKARIBISHA MWAKA MPYA 2014

KEKI 
maalum kwa ajili ya kuukaribisha mwaka mpya
 zainabna japhece   
Maafisa Sheria waTume Zainabu Chanzi (Kulia) na Japhace Daudi wakikata keki.km 
Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Bi. Winfrida Korosso akizungumza na wafanyakazi wa Tume wakati wa kuukaribisha mwaka mpya 2014.wana Tume 
Wafanyakazi wa Tume  wakishiriki katika kuukaribisha mwaka mpya 2014muziki 
Watumishi wakishiriki katika kutakiana heri ya mwaka mpya 2014

WAZIRI WA FEDHA DR. WILLIAM MGIMWA AFARIKI DUNIA NCHINI AFRIKA KUSINI

Dr. William
TANZIA: TAARIFA ZILIZOTUFIKIA KATIKA KITENGO CHA HABARI KUPITIA MITANDAO MBALIMBALI YA KIJAMII ZINAELEZA KUWA WAZIRI WA FEDHA MHE. DR. WILLIAM MGIMWA AMEFARIKI DUNIA JIONI HII NCHINI AFRIKA KUSINI KATIKA HOSPITALI YA MILLPARK ALIPOKUWA AMELAZWA KUPATIWA MATIBABU. 
LAKINI SERIKALI BADO HAIJATHIBITISHA TAARIFA HIZO.
MTANDAO HUU UNAFANYA JITIHADA KUBWA KUWASILIANA NA WAHUSIKA ILI KUPATA UHAKIKA WA  TAARIFA HIZO.

RAIS KIKWETE AMWAPISHA IGP MPYA PAMOJA NA NAIBU WAKE

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Ernest Mangu katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jana jioni 
 
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpatia nyenzo za kazi baada ya kumuapisha Naibu  Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Abdulrahman Kaniki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali na Katibu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika picha ya pamoja na Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Ernest Mangu na naibu wake Naibu IGP Afande Abdulrahman Kanini katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali Mawaziri na Katibu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika picha ya pamoja na Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Ernest Mangu na naibu wake Naibu IGP Afande Abdulrahman Kanini katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na IGP mpya Afande Ernest Mangu,  Naibu  Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Abdulrahman Kaniki pamoja na IGP mstaafu Afande Saidi Mwema katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na IGP mpya Afande Ernest Mangu,  Naibu  Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Abdulrahman Kaniki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii. PICHA NA IKULU
IDARA YA HABARI MAELEZO
Rais Dk. Jakaya Kikwete amemwapisha Mkuu mpya wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Generali wa Polisi Ernest Jumbe Mangu na Naibu wake Kamishna  Abdulrahan Omar Juma Kaniki katika viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam jana jioni 
Katika hafla fupi hiyo iliyoshuhudiwa na Makamu wa Rais, Dk Mohamed Ghalib Bilal, mawaziri kadhaa, viongozi wa Serikali na baadhi ya makamanda wa jeshi la polisi kiongozi huyo baada ya kiapo cha  kulitumikia jeshi hilo na Katiba ya Jamhuri ya Muungano Tanzania, amewaambia waadishi wa habari kuwa kazi yake kubwa itakuwa ni kupambana na uhalifu na kufuatailia migogoro miongoni mw a jamii na makundi mbalimbali, pia ameahidi kuendelea kushirikiana na serikali katika kuboresha mifumo ndani ya jeshi lake.  
Kwa upande wa naibu wake, Bw. Kaniki amesema mbali na majukumu yake ya kumsaidia Mkuu wake wa kazi ataongeza juhudi za ufuatiliaji katika ngazi ya tarafa na vijiji ili kujenga uwezo wa ulinzi shirikishi na kusisistiza kuwa jamii ina fursa kubwa katika kufanikisha suala la ulinzi katika maeneo wanayoishi. 
Naye aliyekuwa Inspekta Jenerali wa Polisi , Said Mwema ameishukuru jamii kwa ujumla kwa ushirikiano mkubwa ambao amekuwa akiupata, kadhalika kumtakia mwenzake aliyempokea kazi ya mafanikio na amesihi jamii iendelee kumpa ushirikiano.
Kuhusu maendeleo ya jeshi hilo Bw. Mwema amesema pamekuwepo na kasi ya uimarishaji wa vitendea kazi katika kipindi kifupi, uimarishaji wa miundombinu ndani ya jeshi hilo na amesema kuna kazi mbili za utafiti wa kisayansi kuhusu mwenendo wa utendaji zilizo katika hatua ya mwisho kukamilishwa zitakazobaini ufanisi na changamoto za jeshi la polisi na kutoa mapendekezo ya kuboresha upande wa jeshi la polisi kadhalika kubaini kiwango cha mahusiano ya jeshi hilo na umma.