| Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya ujenzi wa barabara mkoani Iringa Ya GNSM Contractrors Co. Ltd Bw Geofrey Mungai akiwa na watoto yatima wa kituo cha Tosamaganga wilaya ya Iringa jimbo la kalenga ambako alifika kukabidhi msaada wa chakula chenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 1.5 kwa ajili ya mwaka mpya kwa watoto hao | 
| Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya ujenzi wa barabara mkoani Iringa Ya GNSM Contractrors Co. Ltd Bw Geofrey Mungai akiwa karibu na gari lililobeba msaada wa chakula | 
| Baadhi ya watoto yatima wa kituo cha Tosamaganga Iringa wakiwa wamepumzika | 
| Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya ujenzi wa barabara mkoani Iringa Ya GNSM Contractrors Co. Ltd Bw Geofrey Mungai kulia akiwa amemshika mmoja kati ya watoto yatima kituo cha Tosamaganga kushoto ni diwani wa viti maalum tarafa ya Kalenga Shakra Kiwanga ambae alikuwa ni mwenyeji wa Mungai katika kukabidhi msaada wa chakula kwa yatima hao | 
| Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya ujenzi wa barabara mkoani Iringa Ya GNSM Contractrors Co. Ltd Bw Geofrey Mungai akiwa na mmoja kati ya watoto yatima wa kituo cha Tosamaganga Iringa leo | 
| Mlezi wa watoto hayo Sisita Herena Kihwele kushoto akiwa na ugeni uliofika kituoni Tosamaganga kwa ajili ya kushuhudia tukio la Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya ujenzi wa barabara mkoani Iringa Ya GNSM Contractrors Co. Ltd Bw Geofrey Mungai kulia kukabidhi msaada wa chakula xcha mwaka mpya kwa watoto kituoni hapo | 
| Watoto hao yatima wakiimmba mbele ya ugeni | 
| Mtoto aliyefahamika kwa jina la Nyota akimsalimia Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya ujenzi wa barabara mkoani Iringa Ya GNSM Contractrors Co. Ltd Bw Geofrey Mungai ambae alifika kituoni hapo leo kuwapa watoto hao chakula cha sikukuu ya mwaka mpya ,mtoto huyo alitelekezwa porini na mzazi wake baada ya kujifungua kabla ya kituo hicho kumuokota na kumtunza kituoni hapo | 
| Baadhi ya yatima kituo cha Tosamaganga | 
| Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya ujenzi wa barabara mkoani Iringa Ya GNSM Contractrors Co. Ltd Bw Geofrey Mungai kulia akiwa na mlezi wa kituo hicho sisita Herena Kihwele | 
| Watoto yatima wa kituo cha Tosamaganga wakimpongeza Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya ujenzi wa barabara mkoani Iringa Ya GNSM Contractrors Co. Ltd Bw Geofrey Mungai kulia kwa kuwajali kwa mwaka mpya | 
| Diwani wa viti maalum tarafa ya Kalenga Shakra Kiwanga kushoto akimpongeza Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya ujenzi wa barabara mkoani Iringa Ya GNSM Contractrors Co. Ltd Bw Geofrey Mungai kulia kwa kusaidia yatima | 
 Mkurugenzi
  mtendaji  wa  kampuni  ya ujenzi  wa barabara mkoani  Iringa ya  GNSM 
Contractrors Co. Ltd Bw  Geofrey Mungai   amekabidhi  msaada  wa chakula
  cha mwaka  mpya chenye thamani  ya  zaidi ya Tsh milioni 1.5 kwa 
 kituo cha kulelea  watoto yatima  cha  Tosamaganga katika   jimbo la 
kalenga wilaya ya  Iringa vijijini .
Akikabidhi
  msaada  huo  leo  Mungai  alisema  kuwa  amelazimika  kufika katika 
 kituo  hicho  ambacho  kinasimamiwa na masisita  wa kanisa la RC  kama 
 sehemu ya  mwendelezo wa kampuni  yake kuendelea  kuzungukia  vituo 
mbali mbali vya kulea yatima  na  kuwapa faraja  hasa katika msimu huu 
wa sikikuu.
Alisema
  kuwa miongoni mwa vituo ambavyo amepata  kuvikumbuka katika msimu  huu
 wa sikukuu ya Krismas na Mwaka mpya ni pamoja na  kituo cha Daily Bread
 Life (DBL) kilichopo jimbo la Iringa mjini na kituo hicho cha 
Tosamaganga  kilichopo jimbo la Kalenga huku lengo likiwa ni 
 kuwakumbuka  yatima  hao  na  kuihamasisha  jamii  kuelekeza nguvu  zao
 kwa  yatima kama  hao.
Bw 
 Mungai alisema  kuwa   takwimu  za maambukizi ya VVU katika  mkoa  wa 
Iringa zimeendelea  kuongezeka na iwapo  jamii haitajenga  utamaduni  wa
 kujali  yatima  vifo vya watoto  yatima ambao watakosa chakula baada ya
 kupoteza wazazi  wao kwa VVU pia  vitazidi  kuongezeka   hivyo lazima 
 misingi  ya  kuwajali  yatima ikaanzwa kuwekwa mapema  zaidi. 
” 
Hawa  watoto  iwapo  jitihada za vituo vya  kusaidia yatima visinge kuwa
 na moyo huo  leo yawezekana  baadhi yao  wasingekuwepo hapo  tungekuwa 
 tumewazika  ila kazi nzuri  ya  kujitolea  inayofanywa na vituo  vya 
yatima  ndio  imewafikisha hapa leo ….hivyo lazima  sisi kama  jamii 
 kuunganisha  nguvu zetu na vituo vya yatima”
Pia
  alisema  kuwa  hata  viongozi  wa vyama vya siasa na serikali ni vema 
wakaweka utaratibu  wa  kufanya ziara  za mara kwa mara katika  vituo 
 vya yatima na  kujifunza mazingira ambayo  watoto hao  wanaishi ikiwa 
ni  pamoja na  kusaidia  kutatua changamoto  zinazovikabili vituo vya 
yatima mkoani Iringa .
Kwani
  alisema kwa upande wake kama  mkandarasi ambae amekuwa akifanya kazi 
ya ujenzi wa barabara  mkoani Iringa na nje ya mkoa ameona  ni vema 
 katika fedha  kiasi ambazo anazipata  kuweka utaratibu wa kusaidia 
watoto yatima kama njia ya  kuwahamasisha pia wenzake  kujitoa kwa 
yatima  katika maeneo yao ama  kusaidia kuchangia maendeleo ya maeneo 
yao. 
Katika
  hatua  nyingine Mungai aliwapongeza  walezi  wa  vituo vya  yatima 
katika mkoa  wa Iringa kuwa kutokana na mchango wao  wa kulea yatima 
hata  idadi ya yatima  na  watoto wa mitaani katika mji wa Iringa 
imeonekana  kupungua zaidi  
Kwa
  upande  wake  diwani  wa viti  maalum tarafa  ya Kalenga Shakra 
 Kiwanga  akimpongeza  Mungai  alisema  kuwa ameonyesha upendo mkubwa 
kwa  yatima  hao na kuwataka makandarasi  wengine  kuiga mfano  huo. 
Kiwanga
  ambae pia ni mmoja kati ya makandarasi wadogo mkoani Iringa alisema 
 kuwa alichofanya Mungai ni somo kwao pia katika kutoa sehemu ya 
makusanyo wanayoyapata  kupitia kazi mbali mbali. 
Awali
 mlezi  wa  kituo  hicho Herena Kihwele  alisema kuwa kituo hicho kina 
 watoto zaidi ya 100 na  kuwa kwa  sasa kituo kinakabiliwa na changamoto
 kubwa ya kushindwa  kuwalipia ada  sekondari   watoto zaidi ya 10 
 waliofaulu darasa la  saba ila kituo hakina uwezo wa  kuwasomesha . 
Iwapo
 umeguswa kuchangia  kituo hicho ada ama msaada  wowote  ule waweza 
 kuwasiliana na mlezi wa kituo hicho Sisita Herena Kihwele kwa simu 
 0768831477 pia  waweza  kutumia namba hiyo kwa kutuma M-PESA.
No comments:
Post a Comment