Na Kiza Sungura-MAELEZO
Wakazi
 wa Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya wanakusudia kuanzisha Kituo cha Redio 
ya kijamii kwa ajili ya kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii na 
shughuli nyingine za maendeleo katika eneo hilo ili kuongeza kipato kwa 
wananchi wake na taifa kwa ujumla.
Kauli
 hiyo imetolewa jana jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Kamati ya 
Mandalizi ya Harambee ya uanzishaji wa  Redio Rungwe FM Bw. Christopher 
Andendekisye  wakati akizungumza  waandishi wa habari .
Alisema
 kuwa Mkoa wa Mbeya na husasani Wilaya ya Rungwe inavyo vivutio vingi 
ambavyo kwa sababu ya kukosa chombo cha mawasiliano kama vile Redio 
vimekuwa havifahamiki kwa wananchi wengi wan je ya Wilaya hiyo na hivyo 
kuikosesha Serikali mapato ambayo yangetokana na sekta ya utalii.
Bw. 
Andendekisye alisema kuwa  kutokana na changamoto mbalimbali 
zinazoikabili Wilaya Rungwe, Uongozi wa Christian na Gospel Ministry 
umeamua kuanzisha mchakato wa usajili Redio inayoitwa Rungwe FM, ikiwa 
ni Redio ya kijamii kwa ajili  ya kuhamasisha shughuli mbalimbali za 
kiuchumi, kijamii na kisiasa ndani ya Wilaya ya Rungwe.
Alisema
 Redio hii tayari ipo katika orodha ya redio zilizoomba usajili wa 
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania [TCRA], imesajiliwa mwezi septemba mwaka
 2013.
Kufuatia
 hali hiyo Bw. Andendekisye aliwaomba wananchi na wakazi wa Wilaya ya 
Rungwe kusaidia upatikanaji wa shilingi milioni 170 zinahitaji 
kukamilisha ununuzi wa vifaa vitakavyosaidia uanzishwaji wa redio hiyo 
mapema.
Aliongeza
 kuwa hadi hivi sasa wameshapata ahadi ya shilingi milioni 92 na 
kuongeza kuwa ili kumalisha kiwango chote wanatarajia kufanya harambee 
mwezi Machi 2014 katika ukumbi wa Diamond Jubilee.
Bw. 
Andendekisye alisema kuwa kwa mwananchi atakayehitaji kuwachangia 
anaweza  kutuma fedha zake kupitia akaunti 038201043087 Tukuyu Christian
 Fellowship –NBC Bank

No comments:
Post a Comment