TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, January 17, 2015

TAARIFA YA MSIBA WA DADA LETICIA MATTEI RWECHUNGURA

 Tunasikitika kutangaza kifo cha ghafla cha  dada yetu mpendwa Leticia Mattei Rwechungura kilichotokea hapa Ujerumani tarehe 06.01.2015.Mazishi yatafanyika hapa Ujerumani Königswinter, karibu na mji wa Bonn tarehe 24.01.2015. Misa itaanza saa tano asubuhi (11:00 a.m.), katika Kanisa la St. Michael Niederdollendorf, Petersbergerstr. 14, 53639 Königswinter.

Dada Leticia Mattei alikuwa mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa huko South Sudan (UNMIS) - United Nations Mission in Südan, Eastern Equatoria State of Torit-Sudan. Aliugua muda mfupi na kufariki dunia katika hospitali iliyoko mjini Bonn hapa Ujerumani. 

Watanzania wote walioko hapa Ujerumani, nyumbani Tanzania na ulimwenguni kote wameshtushwa na kifo hiki cha ghafla cha kuondokewa na mama yetu na dada yetu mpenzi Leticia Mattei. Tutamkumbuka daima kwa kazi kubwa alizoifanyia nchi yetu ya Tanzania, bara la Afrika na dunia nzima kwa ujumla. Mungu amlaze mahali pema Peponi - Amin!
Kwa yeyote atakayependa kutoa sanda yake, tunaomba michango itumwe moja kwa moja kwa mtoto wa marehemu:

Diana Kajuna
IBAN: DE76 3806 0186 5501 3030 13
BIC: GENODED1BRS
Kreditinstitut: Volksbank Bonn Rhein-Sieg eG

Tunaomba sana ili tuweze kutekeleza mipango hii vizuri ya kumsindikiza dada yetu kwa heshima zote, wale wanaopenda kuhudhuria mazishi haya wawasiliane na mratibu wa shughuli hizi Nd. Majura, ili tupate orodha kamili ya wale wanaokuja ili itusaidie kuandaa mambo mengi ya muhimu. Kwa wale watakaopenda kupata malazi (ya hoteli), kadhalika tunaomba wawasiliane na Dr. Isack Majura kuanzia sasa kupitia:

Tel. +49 173 7089513
e-Mail: IMajura@aol.com
Germany

Historia ya Tanzania na nchi za GCC yawa chachu ya uwekezaji nchini.

 
 Na Eleuteri Mangi- MAELEZO

Serikali ya Tanzania itaendelea kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji na kuendeleza ushirikiano na mahusiano mzuri uliopo kati yake na nchi zinazounda umoja wa nchi za Ghuba (GCC).

Kauli hiyo imetolewa jana jijini Dar es salaam na Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima alipokuwa akifunga mkutano wa siku mbili wa wafanyabishara kutoka Tanzania na nchi za GCC ambao ulianza Januari 15 hadi 16 mwaka huu.

Malima alisema kuwa Watanzania umefika wakati wa kuboresha biashara zetu ili kuweza kuuza bidhaa bora ndani na nje ya nchi na kukabiliana na changamoto za soko la kimataifa.

“Viwango vya mazao yetu vinapaswa viewe bora, ambapo ubora huo utaruhusu bidhaa zetu ziuzike nchi nyingine” alisema Malima.

Akitolea mfano, Malima alisema Tanzania imejaliwa kuwa na mifugo mingi inayoweza kuzalisha nyama ambayo soko lake tunalo tayari ambalo ni nchi za GCC na kusisitiza kuwa nyama hiyo inapaswa kuandaliwa  katika machinjio salama na ya kimataifa ili kufungua fursa ya kuuza nyama hiyo maana milango sasa ipo wazi kwa serikali ikishirikiana na wafanyabiashara nchini.

Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Shirikisho la Wafanyabiashara kutoka nchi za Ghuba (FGCCC) Abdulrahman Bin Saleh Al- Otainshan alisema kuwa jumuiya ya wafanyabiashara wan chi za Ghuba  wameona na wanatarajia kufanya biashara Tanzania katika sekta ya kilimo na mifugo ambapo wanategemea kupata mzao mbalimbali yanayohitajika nchi za Uarabuni.

Mazao hayo yanayohitajika ni pamoja na mchele, matunda, mboga mboga, asali na nyama.Zaidi ya hayo, Rais hyo wa FGCCC alisema kuwa nchi zianazounda umoja huo zinatarajia kuwekeza Tanzania katika sekta za  kilimo, mifugo, elimu, maji, afya, ufundi na utalii.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa benki ya BADEA alisema kuwa Abdel Aziz Khelef alisema kuwa benki yake itaendelea kuwa kiunganishi muhimu kati ya wafanyabiashara wa Tanzania na nchi za GCC ambapo wamekuwa na uhusiano mzuri kwa zaidi ya miaka 40.

Nchi zinazounda umoja wa GCC ni Kuwait, Oman, Bahrain, Qatar, UAE na Saud Arabia zinauhusiano wa karibu na Tanzania kihistoria, lugha pamoja mila na desturi.

VIJANA WATAKIWA KUJITUMA NA KUFANYA KAZI KWA KWA MAENDELEO YAO

Ndugu Elly David Akitoa Mada Kuhusu Vijana kujituma na kufanya kazi kwa Bidii Kwa maendeleo ya taifa.Mtoa Mada huyo amesema kutokana na Ukosefu wa ajira hususani kwa vijana ni vyeme vijana kujituma na kuwa wabunifu na waweze kujiajiri kwa lengo la Kupambana katika Maisha.Katika Kongamano hilo la Vijana lililofanyika Jijini dar es salaam Liliwapa Fursa vijana kueleza Changamoto zinazowakabili na namna ya Kuzikabili.Kongamano hilo lililoandaliwa na Elly David mara baada ya ya kuona changamoto zinazowakabili vijana wa kitazania ili kuwapa fursa vijana kukutana kubadilishana mawazo Pamoja na Kuangalia namna ya kutatua changamoto zinazowakabili vijana wa Kitanzania/

MSAJILI WA VYAMA AVIAS VYAMA VYA SIASA

NA MAGRETH KINABO – MAELEZO.

MSAJILI wa Vyama Vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amevitaka vyama vyote vya siasa kutekeleza wajibu wao kwa mujibu wa sheria , katiba na kanuni ili kuepusha migogoro. Aidha msajili huyo amevitaka vyama hivyo mfano mzuri wa kwa jamii kwa kudumisha amani na utulivu ndani ya vyama vya siasa.

Kauli hiyo imetolewa leo na Msajili huyo katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari kufuatia kuwepo kwa wimbi kubwa la migogoro ndani ya vyama hivyo. “Endapo kwa bahati mbaya mgogoro ukiibuka, unatakiwa utatuliwe kwa utaratibu na namna ambayo itadumisha amani na utulivu ndani ya chama,” alisema Jaji Mutungi.

Jaji Mutungi amewataka wanachama wa kawaida wa vyama vya siasa kupenda amani na utulivu ndani ya chama na kuepuka migogoro kwa kuheshimu na kufuata mfumo au taratibu za kuwasilisha malalamiko uliopo ndani ya chama au taasisi husika. Pia wawe wavumilivu mpaka watakapopata majibu ya malalamiko yao kutoka katika utaratibu huo uliowekwa na taasisi husika.

Aliongeza kuwa ofisi yake inajitahidi kuepusha na kutatua migogoro ndani ya vyama kwa kuchukua hatua zifuatazo, ambazo ni kuvihimiza vyama vya siasa kuheshimu sheria,kuzingatia misingi ya demokrasia na utawala bora,katiba na kanuni zake, kusuluhisha mgogoro unapoibuka, “Na hivi sasa tumewasilisha Serikalini mapendekezo ya marekebisho ya sheria yatakayosaidia kuepusha migogoro ndani ya vyama,” alisisitiza.

Ameiomba jamii ikemee tabia ya migogoro isiyo na tija ,inapoona vyama vya siasa havitekelezi wajibu wake, badala yake vinajikita katika migogoro ndani ya ndani.

KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI CHA KWANZA KWA MWAKA HUU WA 2015 JIJINI DAR ES SALAAM.

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri cha kwanza kwa mwaka huu wa 2015 Ikulu jijini Dar es salaam January 16, 2015. Kulia kwake ni Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali na kushoto kwake ni Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda. PICHA NA IKULU

KUNA MATUMAINI MAKUBWA YA KUFIKIWA MAKUBALIANO YA KUKIUNGANISHA CHAMA CHA SPLM -KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana jana  aliwasili Arusha kwa lengo la kufanya mazungumzo na makundi matatu ya chama cha SPLM ya Sudani ya Kusini, mashauriano hayo yalilenga kukamilisha makubaliano baina ya makundi hasimu. 
Baada ya Mazungumzo Ndugu Kinana alisema ana matumaini ya kufikiwa makubaliano ya kukiunganisha chama cha SPLM katika siku chache zijazo  Kutoka kushoto ni Balozi David Kapya,Abdulrahman Kinana,Mwenyekiti wa Mazungumzo Dk.John Samuel Malecela na Makamu Mwenyekiti wa mazungumzo Dk. Hassan Kibelloh mazungumzo hayo yalifanyika Ngurdoto Arusha. 
Viongozi wa Makundi matatu kutoka chama cha SPLM kutoka Sudani ya Kusini wakiwa kwenye mazungumzo ya kufikia makubaliano ya kuunganisha chama chao cha SPLM. Hapa wakiwa  na viongozi wa Tanzania wanaosaidia kumaliza tofauti na yakiwa yanasimamiwa na Chama Cha Mapinduzi chini ya uongozi wa Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana.
======  ======  ===== =======
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alitangaza kuwa Tanzania imekubali kuwa msuluhishi wa mgogoro wa kisiasa ndani ya chama tawala cha Sudan Kusini cha Sudanese People’s Liberation  Movement (SPLM), mgogoro ambao ulisababisha kuzuka kwa vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

Hata hivyo, Rais Kikwete alisema kuwa usuluhishi huo utakuwa wa kichama na Chama cha Mapinduzi (CCM) ndicho kitaongoza usuluhishi huo katika mazungumzo yatakayofanyika Arusha na kuwa jitihada hizo za Tanzania hazitaingilia mazungumzo ya kujaribu kusimamisha mapigano nchini humo yanayoendelea huko Addis Ababa, Ethiopia.

Rais Kikwete alisema kuwa ulikuwa uongozi wa SPLM na hasa Mwenyekiti wa Chama hicho, Rais Salva Kiir ambao wameiomba Tanzania kusaidia jitihada za kisiasa za kupatanisha pande ambazo zinavutana na kutofautiana ndani ya SPLM wakiamini kuwa mapatano ndani ya chama yatafanikisha kumaliza mgogoro wa kisiasa katika Serikali ya nchi hiyo ambayo  imegawanyika na kusababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Rais Kikwete alitangaza jitihada hizo za upatanishi za Tanzania wakati alipohutubia maelfu kwa maelfu ya wananchi na kupitia kwao Taifa kwenye Sherehe ya Kuzima Mwenge wa Uhuru, Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na Kilele cha Wiki ya Vijana kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.

“Ni fahari kwetu kwamba wananchi wa Msumbiji, Zimbabwe, Angola, Namibia na Afrika Kusini nao wako huru na tumetoa mchango wetu.  Ni jambo la faraja kubwa kwamba nchi yetu imeweza kupatia hifadhi ndugu zetu wa nchi jirani na hata mbali wakati maisha yao yalipokuwa hatarini kwa sababu ya kukosekana kwa amani ama kukimbia mateso ya uongozi wa kidikteta. Ndugu zetu wa Kongo, Burundi, Rwanda, Kenya na Comoro wanaujua ukweli huo. Na, kwa Uganda tuliwasaidia kuling’oa Dikteta Idd Amin na Comoro tulisaidia kuunganisha nchi yao tena.”

AP Interview: Miss Univers reflects as her reign winds down Associated Press

CORRECTS CROWNING DATE TO JAN 25 - FILE - In this Oct. 2, 2014 file photo, Miss Universe, Gabriela Isler, of Venezuela, speaks during a news conference in Doral, Fla. Isler's reign is in its final days, with the next woman to wear the crown to be selected Jan. 25 in Miami. The classic tiara _ the one that slipped off her head on the night she was crowned _ soon will be gently placed atop someone else and after touring the world almost nonstop, Isler is ready to see what the next chapter brings. (AP Photo/Wilfredo Lee, File)
CORRECTS CROWNING DATE TO JAN 25 - FILE - In this Oct. 2, 2014 file photo, Miss Universe, Gabriela Isler, of Venezuela, speaks during a news conference in Doral, Fla. Isler's reign is in its final days, with the next woman to wear the crown to be selected Jan. 25 in Miami. The classic tiara _ the one that slipped off her head on the night she was crowned _ soon will be gently placed atop someone else and after touring the world almost nonstop, Isler is ready to see what the next chapter brings. (AP Photo/Wilfredo Lee, File)
MIAMI (AP) — When Gabriela Isler wakes up on Jan. 25, it will mark the 441st and final time that she will begin a day while wearing the title of Miss Universe.
Then, as she put it, she becomes "just Gabby" again.
Isler's reign is in its final days, with the next woman to wear the crown to be selected Jan. 25 in Miami. The classic tiara — the one that slipped off her head on the night she was crowned — soon will be gently placed atop someone else and after touring the world almost nonstop, Isler is ready to see what the next chapter brings.
"Before all this, I was just a simple girl, no makeup, no hair, no heels, just a normal girl finishing my education," Isler said in an interview with The Associated Press. "This just changed my life. This made me feel confidently beautiful. ... Now I'm happy with myself every day. I learned to be happy. I grew up in every way, as a daughter, as a sister, as a girlfriend, as a friend. It transformed my life."
The 5-foot-10 Venezuelan carries her country's flag with intense pride, even as her nation continues to battle over economy and politics. Being an example for women in her country was a top priority during her time as Miss Universe, and once it ends Isler plans to step up her efforts by combating a massive problem with teen pregnancy in her homeland.
"During my reign, I discovered myself," Isler said. "I want to continue doing a lot of things related to humanitarian efforts, so one of my new chapters will be maybe becoming a spokesperson for different organizations, but my first one is my baby — starting my own foundation in Venezuela that can help create awareness and bring education and family values to young girls and young women."
Choking levels of inflation and shortages of basic goods are part of the norm in Venezuela, where beauty pageants are big business and a source of national pride.
"With all that's happening in Venezuela, to have a chance to be a good-news person for my country I feel so satisifed," Isler said. "I did as much as I can — not just to represent the Miss Universe organization but also my country."
There is symmetry to her reign ending South Florida, which has a massive Latin population and is the place that Isler says will be her second home.
The Miss Universe pageant itself will be at Florida International University in Miami, but many of the preliminary events leading up to the big night will be in the nearby suburb of Doral, Florida — which has an enormous Venezuelan population.
"I was dreaming to give my crown in Venezuela," Isler said. "But to have this opportunity to end this reign and close a chapter in my life around the Venezuelan community, this Latin environment, this Latin energy, I couldn't ask for a better place."
When asked if one day stood out among all others during her reign, Isler didn't hesitate. She quickly chose Sept. 3, the day she went to the Vatican, heard Pope Francis speak about the role of women in the church and received a blessing from the pontiff.
"I was not able to sleep the day before because I was so excited," Isler said. "I couldn't believe it was real. I was like, 'Really, I'm going to meet the Pope?' I went to the Vatican and I couldn't stop crying and I could cry again. It was a dream. ... I was in tears. I didn't know I was awake. ... That day I realized, this was real."
Isler expects to shed tears on pageant night, not because her time as Miss Universe will be over but out of both fear and excitement for whatever will happen next.
"I can't wait to wake up and just enjoy the day," Isler said. "Have a breakfast in bed and just have the opportunity to have the first official day where I can make my own decisions and start my dreams."
She won't sit idle for long.
Her first meeting is already scheduled — for Jan. 26.

Friday, January 16, 2015

Waisilamu waandamana dhidi ya C.Hebdo

Maandamano nchini Pakistan kuonyesha kero la waumini wa kiisilamu kuhusu Charlie Hebdo
Polisi nchini Pakistan wamekabiliana na waandamanaji, walioghadhabishwa na uamuzi wa jarida na Ufaransa la Charlie Hebdo wa kuchapisha vibonzo vya mtu wanayedai ni Mtume Mohammad.
Baada ya maombi ya ijumaa, maafisa wa ulinzi walitumia magari yenye majai kuwamwagia maji waandamanaji katika juhudi za kuwatwanya.
Walikuwa wamekusanyika nje ya ubalozi wa Ufaransa mjini Karachi.
Baadhi ya waandamanaji inaarifiwa walikuwa wamebeba bunduki. Watu watatu walijeruhiwa katika maandamano yenyewe.
Mwandishi wa BBC mjini Islamabad amesema idadi ya waandamanaji hao, kwa mujibu wa idadi ya wasisilamu nchini Pakistan, ilikuwa ndogo.
Maandamano kama hayo yameitishwa katika nchi zingine zilizo na idadi kubwa ya waumini wa Kiislamu kama vile Uturuki, Ufilipino,Kuwait, Mauritania na Sudan.

Cameroon kupambana na Boko Haram

Wapiganaji wa Boko Haram wamekuwa kero kubwa kwa wananchi wa Nigeria kwa miaka mingi sasa
Serikali ya Cameroon imesema Chad itatuma kikosi kikubwa cha wanajeshi wake kupambana na wapiganaji wa kiisilamu wa Boko Haram mpakani mwa Nigeria na nchi hio.
Tangazo hili limetolewa siku moja baada ya Chad kusema kwamba itaunga mkono jirani yake Nigeria katika harakati dhidi ya wapiganaji wa kiisilamu wa Boko Haram.
Hakuna taarifa zozote zimetolewa kuhusu idadi kamili ya wanajeshi watakaopelekwa huko au siku.
Mnamo siku ya Jumanne, Cameroon ilisema kwamba iliwaua wapiganaji 143 wa Boko Haram, ambao walishambulia kambi zake katika eneo la Kolofata karibu na mpaka na Nigeria.
Ilisema kuwa mwanajeshi mmoja alifariki wakati wa mashambulizi hayo ambayo yalisababisha ufyatulianaji risasi mkali kati ya wanajeshi na waasi hao kwa muda wa saa tano.
lilikuwa shambulizi la kwanza kubwa kufanywa na Boko Haram dhidi ya Cameroon tangu kundi hilo kutishia kiongozi wa nchi hio katika kanda ya video waliyoiweka kwenye mtandao mapema mwezi huu.
Wanamgambo hao wameteka miji na vijiji kadhaa ambavyo wanavidhibiti Kaskazini Mashariki mwa Nigeria katika harakati zao ambazo wameziendeleza kwa miaka sita sasa.

Dubai inatisha kwa uaminifu

mavumba yaliyokuwemo hayakuguswa
Dubai imejinyakulia sifa ya kipekee katika kupima Imani za jamii kwa pochi iliyoangushwa mtaani,na mara ikarejeshwa kwa mhusika mara moja.
Katika utafiti uliofanywa na mtengeneza Filamu mwenye asili ya Uingereza katika mitaa ya Dubai, alijaribu mara arobaini na tano kuidondosha kwa makusudi na katika kila tukio msamaria aliyeiokota aliirejesha pochi hiyo kwa mmiliki wake.
Daniel Jarvis, mwenye miaka 26,akiwa ameificha kamera yake na kurekodi mfululizo wa matukio hayo ya makusudi akiwa pamoja na rafikiye aliyejipachika jina la utani la 'Digi' ama Dan, mwenye miaka 25, walibarizi katika viunga vya Downtown na Bur vilivyoko Dubai,siku za karibuni na kuweka swali je unaweza kuiba Dubai? Kutaka kuichunguza jamii na kurushwa vipande vyake katika YouTube ambapo mpaka kufikia jana usiku watazamaji walikuwa ni zaidi ya 70,000 .
Jarvis aliiambia 7DAYS walishangazwa na utafiti huo na kikubwa kilichowasangaza ni kwamba waliookota pochi hiyo hawakujishughulisha kutazama ndani kuna nini? Wakati pochi hiyo ilikuwa imesheni euro za kutosha na fedha ya Falme za Kiarab dirham kadhaa.
Mtaa wa kwanza walioufanyia majaribio ni mtaa uliko katika barabra ya Sheikh Zayed karibu na soko kuu la kibiashara na jirani kabisa na mnara wa Emirates lakini kila aliyeiona pochi hiyo aliirejesha,lakini baadaye tukafikiri sababu ya kurejeshwa pochi hiyo kuwa walioko eneo hilo ni matajiri.
Basi utafiti wetu tukauhamishia eneo la Bur ,Dubai, mahali ambapo palionekana duni kidogo cha ajabu watu waliendeleza utamaduni ule ule wa kurejesha pochi kama ilivyo, na hali eliendelea hivyo mara kadhaa.
Jarvis anasema wameshafanya utafiti kama huo katika mji wa London nchini Uingereza. Na huko walistaajabu walipoidondosha tu aliyeiokota alianza kukimbia nayo wa nako hakuna aliyethubutu kuichukua pochi hiyo.
Jarvis, alivalia suti nadhifu na kuigiza kudondosha pochi anaonekana kwenye video hiyo anaeleza hisia za kurejeshewa kitu ulichondondosha kuwa ni raha iliyoje .lakini akaendelea kusema kuwa anadhani vyombo vya habari hupotosha ukweli,kwakuwa kulikuwa na kichwa cha habari kuwa kuna mtu alihukumiwa miaka 15 jela kwa kuiba mdoli wenye taswira ya dubu, utafiti wetu umegundua tofauti na wayasemayo.
Trollstation ina wanachama wapatao 230,000 na utafiti wao kutoka Falme za Kiarab unaelekezwa Ulaya, Marekani na hatimaye Afrika .
Inawezekana katika maeneo watakayopita kuvunja rekodi ya Dubai tusubiri wakati uwadie, ni kauli yake Jarvis .

Mavazi ya mhubiri yawaacha vinywa wazi

Bwana Khademiana akiwa kwenye TV
Mhubiri mmoja nchini Iran amewaacha watu vinywa wazi kwa kuvalia vazi la rangi ya manjano.
Hoseyn Khademian alionekana kwenye televisheni akivalia shati la manjano , viatu na hata saa ya rangi hiohio. Taarifa hii ni kwa mujibu wa shirika la habari la Mehr.
Wahubiri nchini Iran, kwa kawaida huvalia mavazi meupe na joho la rangi isiyong'aa sana huku viatu vyao vikiwa vyeusi au vya hudhurungi.
Lakini mavazi ya Khademian yalikejeliwa na kufanyiwa gumzo sana kwenye mitandao ya kijamii.
Wakati baadhi ya watu kwenye Facebook walimzomea wakisema anajitakia tu sifa, wengine walimfananisha na ndizi lilioivaa kupitiliza. ''
Msomaji mwengine alisema, '' angependeza zaidi ikiwa angevalia kilemba cha waridi,basi angependeza sana''.
Wakati mwonekano wake umegonga vichwa vya habari nchini Iran, bwana Khademian anasema yeye haoni kwa nini watu wanamsema sana kwani sio mara yake ya kwanza kuvalia mavazi ya manjano.
Mara ya mwisho alionekana kwenye TV akiwa amevalia mavazi ya waridi, anahoji ''kwa nini watu hawakunisema sana wakati huo,''ikilinganishwa na sasa rangi ya mavazi yangi sio kitu kipya,'' alisema Bwana Khademian. Rangi ya manjano ni rangi ya kawaida kama rangi nyinginezo''.

Ethiopia yawafunga waingereza 2 kwa 'ugaidi'

Waziri mkuu wa Ethiopia (kulia) Hailemariam Desalegn amekuwa akikosolewa na kuwa na sheria kali za kupambana na ugaidi
Raia wawili wa Uingereza na msomali mmoja wamefungwa jela nchini Ethiopia kwa kupanga njama ya kuunda dola ya kiisilamu.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa kituo cha redio kinachounga mkono serikali.
Taarifa hii imethibitishwa na ofisi ya mambo ya nje ya Uingereza.
Wanaume hao watatu waliohukumiwa kifungo cha kati ya miaka minne na saba walidaiwa kuwa na uhusiano na kundi la wapiganaji wa kiisilamu.
Ethiopia ina sheria kali sana za kupambana na ugaidi.
Kwa mda mrefu imekuwa ikiendesha harakati dhidi ya kundi la wapiganaji wa kiisilamu wa Al shabaab nchini Somalia.
Nchi hio pia imekuwa ikikabiliwa na madai ya kuwafunga jela wakosoaji wa serikali wakiwemo wanablogu maarufu nchini humo ambao wanakabiliwa na tisho la kufungwa jela kwa madai ya kuhusika na ugaidi na wamekuwa wakizuiliwa tangu Aprili mwaka 2014.
Hata hivyo kiongozi wa nchi hio ametetea sana sheria kali za ugaidi ambazo nchi hio hutumia.
Kulingana na FBC, washukiwa wawili waingereza, Ali Adros Mohammad na Mohammad Sharif Ahmed walikuwa wanaishi mjini London wakati Mohammad Ahmed akiwa na mizizi yake Hargeisa eneo la Somaliland.
Watuhumiwa hao watatu inaarifiwa walikuwa na mawasiliano na wanachama wa kundi la wapiganaji wa kiisilamu tangu mwezi Disemba mwaka 2012 na walisafiri kwenda mjini Adama, ambako walikuwa wanapanga kufanya mashambulizi ya kigaidi.
Mahakama kuu mjini Addis Ababa, iliarifiwa kuwa Ali Adros aliingia nchini Ethiopia kutoka Kenya kwa mafunzo ya kijeshi na kwamba pia alikuwa na makubaliano na kundi la waasi la (OLF), kufanya mashambulizi nao.

Viatu vinavyojifunga kamba vyenyewe

Viatu hivi vina uwezo wa kujifunga kama vyenyewe
Ni miaka 26 tangu tuone viatu vikijifunga kamba zenyewe kama ilivyokuwa kwenye matangazo ya biashara ya viatu vya Nike vyake Marty McFly vikijifunga miaka hiyo. hio
Hilo lilikuwa tu tangazo la bishara zamani sana lakini kuna mtu ambaye aliwaza hivyo miaka hiyo na kusema atakuja kuzindua viatu vyenye uwezo wa kujifunga kamba. Na kwake ndoto hio imetimia.
Wahandisi nchini Ujerumani wamebuni viatu ambavyo vina uwezo wa kujifunga kamba.
Walifanikiwa kufanya hivyo kwa kuweka 'cherger'mfano kama ile ya simu kwenye viatu hivyo ambavyo vinatumia kawi kujionea wenyewe itakavyokuwa kwenye miguu tofauti.
Pindi unapovaa kiatu hicho, sensa ya kiatu inakiambia kwamba mguu uko sawasawa na kuchochea kawi kwenye kiatu kile kuamrisha kamba kujifunga zenyewe.
Wakati unataka kuvua viatu utahitajika kubonyeza au kugonga wayo wa kiatu kile mara mbili na vile vile kuna miale inayoamrisha kamba za viatu vile kujifungua kwa kuzilegeza kamba.
Wanasema kiatu hicho hakihitaji kuwekwa kwenye charger au kubadilisha betri kwa sababu kawi inatokana na hatua za kuukanyaga mguu chini kwa mvaaji au anapotembea zile hatua ndizo zinakipatia kiatu nguvu au kawi.
Mmoja wa wahandisi waliokitengeza kiatu hicho, anasema kwamba kiatu hicho kitawasaidia watu wengi.
Miongoni mwa watakaofaidi ni watu wanaokumbwa na ulemavu wa miguu au wenye matatizo ya kutembea lakini pia vinaweza kuwasaidia watoto au kwa wanaotaka tu kubadili mfumo wao wa maisha.
Saa moja ya kutumia viatu hivyo inatosha kuweza kurejesha kawi ya kufunga kamba.
Bwana Ylli na kikundi cha wahandiisi wengine wanashughulikia kifaa kingine ambacho kitawezesha viatu kumuonyesha mvaaji mwelekeo anakokwenda.

PROIN PROMOTION YAZINDUA MPANGO WA KUUZA FILAMU ZAKE KWA NJIA YA MTANDAO

Waziri wa habari, vijana, utamaduni na michezo Dkt Fenella Mukangara akizungumza jambo kwenye hafla fupi iliyoandaliwa na Proin Promotion kwa ajili ya kuzindua mpango wa kuuza filamu kupitia njia ya mtandao. 


Waziri wa habari, vijana, utamaduni na michezo Dkt Fenella Mukangara akizindua rasmi mpango wa kuuza filamu zake kwa njia ya mtadao wa kwanza kulia ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania, Bi Joyce Fissoo pamoja na Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin, Johnson Lukaza(wa kwanza kushoto)
 Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin, Johnson Lukaza akizungumza jambo kwenye uzinduzi wa  mpango wa kuuza filamu zake kwa njia ya mtandao 

Waziri wa habari, vijana, utamaduni na michezo Dkt Fenella Mukangara akizungumza jambo baada ya kuzindua mpango wa kuuza filamu kwa njia ya mtandao. Wa kwanza kulia ni  Rais wa shirikisho la filamu nchi Tanzania (TAFF), Bw. Simon Mwakifamba na kulia ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania, Bi Joyce Fissoo
Waziri wa habari, vijana, utamaduni na michezo Dkt Fenella Mukangara akitazama moja ya filamu iliyonunuliwa kwenye uzinduzi wa kuuza filamu kwenye mtandao wa kwanza kulia ni  Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania, Bi Joyce Fissoo
Msanii wa maigizo Elizabeth Diana Michael "Lulu" akieleza jambo kwa  Waziri wa habari, vijana, utamaduni na michezo Dkt Fenella Mukangara kwenye uzinduzi wa kuuza filamu kwa kutumia mtandao katikati ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania, Bi Joyce Fissoo  
Baadhi ya wadau waliofika kwenye hafla hiyo
Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin, Johnson Lukaza(kulia) akibadishana mawazo na baadhi ya wadau waliofika kwenye hafla hiyo fupi iliyofanyika jana kwenye Hoteli ya Southern sun ya jijini Dar
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kazini

Naibu waziri wa maliasili na utalii MAHAMUOD MGIMWA amewataka vijana kujitumakufanya kazi

Naibu waziri wa maliasili na utalii MAHAMUOD MGIMWA ambaye ni mbunge wa jimbo la mufindi kusini akiwa ziarani 
Na Fredy Mgunda ,Iringa
Naibu waziri wa maliasili na utalii MAHAMUOD MGIMWA ambaye ni mbunge wa jimbo la mufindi kusini amewataka vijana kujituma na kutumia fursa mbalimbali ambazo zinatolewa na serikali.
“Eti asubuhi unawakuta vijana wamekaa kwenye vijiwe wakizungumza siasa na kucheza mabao wakati hawajui mchana watakula wapi na jioni watarudi na nini nyumbani”alisema MAHMOUD MGIMWA
MGIMWA ameendelea kuwaomba vijana wengi wenye fursa ya kurudi au kuingia shuleni upya warudi kwa kuwa dunia ya sasa inataka wasomi wengi kutokana na mabadiliko ya kiuchumi na sayansi na teknolojia na ndio sababu inayopelekea hata watu wazima kurudi shuleni.
“Vijana mnatakiwakujifunza kutoka kwa watu wazima ambavyo wamekuwa wakijituma kufanya kazi kwa bidii na kujituma ilimradi kuwatengenezea watoto maisha mazuri pamoja na kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla”alisema MAHMUOD MGIMWA
Lakini Naibu waziri wa maliasili na utalii MAHAMOUD MGIMWA
ambaye ni mbunge wa jimbo la mufindi kusini amewataka wakinamama kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi wa kumi mwaka huu.
MGIMWA ameeleza kuwa wanawake waondoe hofu ya kugombea hasa kukiwa na ushindani wa wagombea wanaume kwa kuogopa kuchafuliwa kwa mambo yasiyokuwepo.
Ameendelea kusema kuwa wananchi wasishawishiwe na propaganda za wanasiasa na badala yake wachague viongozi bora wenye uwezo wa kuongoza kutoka katika chama chochote.
Aidha ameongeza kuwa viongozi wawe na sera za kutekelezeka ili kuwatendea haki wapiga kura wao hali itakayowafanya waaminike katika jamii.
Mbali na hayo MGIMWA amewakumbusha vijana kutokubali kutumiwa na baadhi ya wanasiasa katika kuleta vurugu hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu na badala yake wachague kiongozi mwenye weredi na sifa za kuwa kiongozi kutokana na sera za chama chake.
Ameendelea kusema kuwa vijana wajitokeze kwa wingi katika kupiga kura ndiyo katika katiba iliyopendekezwa ili kuweza kufanya uchaguzi ulio wa haki na amani pia kujitokeza katika kujiandikisha katika daftari la wapiga kura pamoja na kupiga kura.
Amemaliza kwa kuwataka wananchi wa jimbo la mufindi kusini kuwa na imani nae kwa kuwa amefanya yote ambayo aliwaahidi katika uchaguzi wa mwaka wa 2010 na amewaomba waendelee kuwa na imani naye katika kutekeleza mambo mapya ambayo wamejitokeza kwa lengo la kuleta maendeleo ya jimbo hilo.

PINDA AKUTANA NA VIONGOZI WA BENKI YA BADEA

unnamed2Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na viongozi wa Benki ya Arab Bank  for Economic Development  in Africa (BADEA) baada ya kukutana nao  kwenye Ofisini kwake jijini Dar es salaam Januari 16, 2015.Kutoka kushoto ni Abdulrahman Bin Saleh Al-Otaishan na Abdelaziz Khelef.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
unnamed3Waziri wa Fedha Saada Mkuya (kushoto) akiteta na Kiongozi  wa Benki ya Arab Bank  for Economic Development  in Africa (BADEA) , Abdulrahm Hassan Naq baada ya mazungumzo kati ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na ujumbe wa Benki hiyo, Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Januari 16, 2015.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
unnamedWaziri Mkuu, Mizengo Pinda na Waziri wa Fedha Saada Mkuya (wapili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Benki ya Arab Bank  for Economic Development  in Africa (BADEA) baada ya mazungumzo kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Januari 16, 2015.Kutoka kushoto ni Abdulrahm Hassan Naq,Abdulrahman Bin Saleh Al-Otaishan na Abdelaziz Khelef.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

SKYLIGHT BAND WAZIDI KULITIKISA JIJI LA DAR WASAJILI VIFAA VIPYA AKIWEMO JOHN MUSIC

Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK47 akitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band Ijumaa iliyopita kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar
Kifaa kipya ndani ya Skylight Band John Music akiimba kwa hisia kaliii huku akipewa sapoti na Wenzake wa kwanza kushoto ni Baby na wa pili kutoka kushoto ni Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK47 na kulia ni Jessie
Wanaume wa shoka wa Skylight Band kutoka kushoto ni Joniko Flower, Sony Masamba na Sam Mapenzi wakionyesha mbwembwe zao za kulisakata sebene kwa mashabiki wao, ambapo jioni ya leo watakuwepo kama kawaida kwenye kiota cha maraha Thai Village
Jessie(katikati) akiimba kwa raha zakee ndani ya Thai Village akipewa sapoti na Baby pamoja na Aneth Kushaba AK47
John Music akiiendelea kutoa burudani ya nguvu huku akipewa sapoti na Wenzake wa kwanza kushoto ni Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK47 na wa pili kutoka kushoto ni Baby na kulia ni Jessie
Sam Mapenzi akiimba Naija Flava njoo leo umshuhudie kwa macho yako…Skylight Band ndio kila kitu huna haja ya kwenda disco unapata kila kitu hapa hapa.
Kikosi kazi cha Skylight Band kikiongozwa Meneja wa Band Aneth Kushaba AK47, Sam Mapenzi na Sony Masamba kwa pamoja wakiwapa raha mashabiki wa bendi hiyo (hawapo pichani) kwenye kiota cha maraha cha Thai Village Masaki jijini Dar Ijumaa iliyopita ambapo leo wataendelea kutoa kuwaburudisha mashabiki wake kama kawaida kuanzia saa tatu usiku.
DSC_0021Mashabiki wa Skylight Band wakiburudika na muziki safi kabisa wa ladha na vionjo vya kila aina ikiwemo Reggae, Kwaito, Naija Flava, R&B, Zouk na zingine kibao bila kusahau sebene pale kati Joniko Flower anahusika sana sambamba na Sony Masamba.