TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, January 16, 2015

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI PROFESA SOSPETER MUHONGO AFANYA ZIARA KATIKA MKOA WA TABORA

 Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amekamilisha  rasmi  ziara yake katika mkoa wa Tabora. Waziri  Muhongo alifanya ziara katika mikoa  ya  Shinyanga, Simiyu na  Tabora lengo likiwa ni kukagua miradi ya umeme  vijijini pamoja na kuzungumza na wananchiunnamedWaziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akitoa maelekezo kwa uongozi wa kijiji cha Tura wilayani Uyui mkoani Tabora kuhakikisha umefanya mkutano na wananchi ili kufanya makubaliano jinsi ya kusimamia mradi wa umeme wa kontena ili wananchi waanze kunufaika mara moja.
unnamed1Mtendaji wa kijiji cha Tura wilayani Uyui mkoani Tabora Gundi Igonzo (kulia aliyevaa koti la kijani) akitoa maelezo juu ya mradi wa umeme wa kontena kijijini hapo mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati)
unnamed2Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akitoa maelekezo kwa uongozi wa kampuni ya kusambaza umeme katika wilaya ya Uyui na Mirambo ya Chico – CCC ya China mara baada ya kutembelea eneo palipohifadhiwa vifaa kwa ajili ujenzi wa miundombinu ya umeme katika wilaya za Uyui na Mirambo.
unnamed3Mtaalamu kutoka Kampuni ya Chico – CCC, Luo Xiaoyong (kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) juu ya hatua iliyofikiwa ya utekelezaji wa mradi wa kusambaza umeme katika wilaya za Uyui na Urambo mara Waziri alipotembelea eneo palipohifadhiwa vifaa kwa ajili ya kazi hiyo.
unnamed4Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akisalimiana na wakazi wa Inala mkoani Tabora kabla ya kufanya mkutano nao ili kusikiliza kero zao.

No comments:

Post a Comment