TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, January 14, 2015

TAKWIMU SAHIHI NA ZA WAKATI ZITASAIDIA KULETA MAENDELEO KWA HARAKA BARANI AFRIKA.

images
NA: VERONICA KAZIMOTO
14 JANUARI, 2015
KAMPALA.
 
WITO umetolewa kwa washiriki wote wa Mkutano wa Kumi wa Maendeleo ya Takwimu Afrika kuelendelea kutoa takwimu sahihi na kwa wakati ili kuleta maendeleo yanayokusudiwa ya kiuchumi na kijamii barani Afrika.
 
Wito huo umetolewa jana na Waziri Mkuu wa Uganda Mhe. Dkt. Ruhakana Rugunda wakati akifungua Mkutano wa Kumi wa Maendeleo ya Takwimu Afrika uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Speke Munyoyo Kampala, Uganda.
 
Dkt. Rugunda amesema kuwa, ili kupata maendeleo kwa haraka, ni lazima takwimu zitolewe kwa wakati na ziwe sahihi kwa ajili ya kusaidia kupanga mipango mbalimbali ya maendeleo.
 
“Ili Bara la Afrika liweze kuendelea kwa haraka, linahitaji takwimu sahihi na zinazotolewa kwa wakati ili takwimu hizo zisaidie katika kupanga mipango mbalimbali ya maendeleo”, amesema Waziri Mkuu Rugunda.
 
Dkt. Rugunda ameongeza kuwa ili kuweza kufanikisha hilo, kuna umuhimu kwa nchi za Afrika kusaidia program mbalimbali za uzalishaji wa takwimu na matumizi yake kwa ajili ya kupanga mipango ya maendeleo.
 
Kwa upande wa Waziri wa Fedha wa Uganda Matia Kasaija amesema kuwa, ili kuweza kulinganisha takwimu za nchi mbalimbali, ni vyema takwimu zinazozalishwa zikafuata mbinu bora za uzalishaji wa takwimu.
 
Matia Kasaija amesema mbinu bora za uzalishaji wa takwimu ni zile  zinazofuata viwango vinavyopendekezwa na Umoja wa Kimataifa – Kitengo cha Takwimu.  
 
Mkutano wa Kumi wa Maendeleo ya Takwimu Afrika umewakutanisha washiriki takribani 400 kutoka nchi mbalimbali za Afrika ikiwemo Tanzania. Mkutano huu ni wa siku tatu na unatarajia kumalizika kesho tarehe 15 Januari, 2015.

No comments:

Post a Comment