TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, January 16, 2015

CHUO KIKUU CHA SUMAIT ZANZIBAR CHAFANYA MAHAFALI YA KUMI NA NNE.

unnamed (12)
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ali Juma Shamhuna akiongoza wahadhiri na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sumait   Chukwani kuingia katika kiwanja cha Mhafali. Wa kwanza (kulia) kaimu Makamu Mkuu wa chuo hicho Prof. Hamad Rashid Hikmany (kushoto) Mwenyekiti wa Baraza la chuo Dkt. Abdulrahman Al Muhailan. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
unnamed (13)Baadhi ya wahitimu wa chuo Kikuu cha Sumait  wakiwa kwenye maandamano  kuingia uwanja wa mahafali.
unnamed (15)Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ali Juma Shamhuna akiwahutubia wanafunzi na wageni waalikwa katika mahafali ya 14 ya chuo Kikuu cha Sumit Chukwani. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
unnamed (16)Baadhi ya wageni waalikwa wa mahafali ya 14 ya chuo Kikuu cha Sumait wakifuatilia sherehe hizo zilizofanyika Chukwani Wilaya ya Magharibi Unguja.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
……………………………………………………………………..
Na Miza Othman- Maelezo Zanzibar 
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ali Juma Shamuhuna amewashauri wahitimu wa vyuo vikuu nchini kutumia elimu na ujuzi wanaopata  kujiajiri wenyewe badala ya kusubiri ajira Serikalini.
Hayo aliyasema   Chuo Kikuu cha Abrahaman Al-Sumaait Memorial  Chukwani  (Sumait University) wakati wa  kuwatunuku shahada   ya uwalimu wanafunzi waliohitimu mafunzo hayo katika  mahafali ya 14 ya chuo hicho.
Amesema kumekuwa na upungufu mkumbwa wa ajira  Serikalini, huku wahitimu wakiendelea kuongeza kila mwaka.  hivyo amewataka  kutumia taaluma  yao  kujiajiri wenyewe na kuisaidia jami zao.
“Nnawakumbusha  kwamba kuna baadhi ya taaluma soko lake la ajira limepungua, hivyo msikae  kusubiri ajira Serikalini  bali itumieni  elimu na ujuzi wenu ili kujitengezea ajira”, Alisisitiza Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali..
Waziri Shamhuna ameupongeza uongozi wa chuo hicho kwa kukipanua na kukipa hadhi zaidi kutoka Chuo cha Elimu na sasa kuwa chuo Kikuu kamili na kupewa jina jipya la Sumait University.
Alisema anaamini kazi hiyo haikuwa rahisi  kwa uongozi na wafanyakazi kuitekeleza  bali ni matokeo ya kazi ngumu  na ushirikiano uliokuwepo kwa kipindi cha miaka mitatu ya mageuzi hayo.
Katika kukiimarisha Chuo Kikuu cha Sumait Waziri Shamhuna ameshauri  kuongezwa fani za utafiti na masuala ya ushauri ili kukipa hadhi zaidi na kutoa wanafunzi waliobora.
Aidha aliutaka uongozi wa Chuo hicho kutafuta njia mbadala za kukiendesha  badala ya  kutegemea  zaidi malipo ya wanafunzi na misaada ya wahisani.
Akimkaribisha mgeni rasmi kutunuku shahada kwa wahitimu, Mwenyekiti wa Baraza Kuu la chuo Dkt. Abdulrahman Al-Muhailan  alimpongeza Kaimu Makamu Mkuu wa chuo hicho Professa Hamad Rashid Hikmany na wasaidizi wake kwa kazi kubwa waliofanya katika kukifanyia mageuzi chuo hicho..
Aliishukuru Serikali ya Muungano wa Tanzania kupitia Kamisheni ya Vyuo Vikuu  Tanzania (TCU)  kwa  ushauri  na maelekezo mazuri  waliowapa na hatimae kupata usajili katika Kamisheni hiyo.
Alisema sera za chuo hicho katika kipibndi cha miaka mitano inayomalizika mwaka 2017 ni kuwekeza miradi ambayo itaingiza mapato na tayari wameanzisha jingo la ofisi itakayokuwa na ehemu ya kutoa huduma kwa wageni  mjini Dar es salaam.
Ameongeza kuwa hivi sasa wanaimarisha Idara ya Uchapaji  ya chuo hicho na kuiendesha  kibiashara  ili kuwavutia wateja kutoka taasisi za umma na binafsi.
Jumla ya wahitimu 266 walikabidhiwa shahda  zao katika mahafali hiyo na kufikisha idadi ya wahitimu 1704 tokea kuanzishwa mwaka 1998.

No comments:

Post a Comment