TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, January 17, 2015

KUNA MATUMAINI MAKUBWA YA KUFIKIWA MAKUBALIANO YA KUKIUNGANISHA CHAMA CHA SPLM -KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana jana  aliwasili Arusha kwa lengo la kufanya mazungumzo na makundi matatu ya chama cha SPLM ya Sudani ya Kusini, mashauriano hayo yalilenga kukamilisha makubaliano baina ya makundi hasimu. 
Baada ya Mazungumzo Ndugu Kinana alisema ana matumaini ya kufikiwa makubaliano ya kukiunganisha chama cha SPLM katika siku chache zijazo  Kutoka kushoto ni Balozi David Kapya,Abdulrahman Kinana,Mwenyekiti wa Mazungumzo Dk.John Samuel Malecela na Makamu Mwenyekiti wa mazungumzo Dk. Hassan Kibelloh mazungumzo hayo yalifanyika Ngurdoto Arusha. 
Viongozi wa Makundi matatu kutoka chama cha SPLM kutoka Sudani ya Kusini wakiwa kwenye mazungumzo ya kufikia makubaliano ya kuunganisha chama chao cha SPLM. Hapa wakiwa  na viongozi wa Tanzania wanaosaidia kumaliza tofauti na yakiwa yanasimamiwa na Chama Cha Mapinduzi chini ya uongozi wa Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana.
======  ======  ===== =======
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alitangaza kuwa Tanzania imekubali kuwa msuluhishi wa mgogoro wa kisiasa ndani ya chama tawala cha Sudan Kusini cha Sudanese People’s Liberation  Movement (SPLM), mgogoro ambao ulisababisha kuzuka kwa vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

Hata hivyo, Rais Kikwete alisema kuwa usuluhishi huo utakuwa wa kichama na Chama cha Mapinduzi (CCM) ndicho kitaongoza usuluhishi huo katika mazungumzo yatakayofanyika Arusha na kuwa jitihada hizo za Tanzania hazitaingilia mazungumzo ya kujaribu kusimamisha mapigano nchini humo yanayoendelea huko Addis Ababa, Ethiopia.

Rais Kikwete alisema kuwa ulikuwa uongozi wa SPLM na hasa Mwenyekiti wa Chama hicho, Rais Salva Kiir ambao wameiomba Tanzania kusaidia jitihada za kisiasa za kupatanisha pande ambazo zinavutana na kutofautiana ndani ya SPLM wakiamini kuwa mapatano ndani ya chama yatafanikisha kumaliza mgogoro wa kisiasa katika Serikali ya nchi hiyo ambayo  imegawanyika na kusababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Rais Kikwete alitangaza jitihada hizo za upatanishi za Tanzania wakati alipohutubia maelfu kwa maelfu ya wananchi na kupitia kwao Taifa kwenye Sherehe ya Kuzima Mwenge wa Uhuru, Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na Kilele cha Wiki ya Vijana kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.

“Ni fahari kwetu kwamba wananchi wa Msumbiji, Zimbabwe, Angola, Namibia na Afrika Kusini nao wako huru na tumetoa mchango wetu.  Ni jambo la faraja kubwa kwamba nchi yetu imeweza kupatia hifadhi ndugu zetu wa nchi jirani na hata mbali wakati maisha yao yalipokuwa hatarini kwa sababu ya kukosekana kwa amani ama kukimbia mateso ya uongozi wa kidikteta. Ndugu zetu wa Kongo, Burundi, Rwanda, Kenya na Comoro wanaujua ukweli huo. Na, kwa Uganda tuliwasaidia kuling’oa Dikteta Idd Amin na Comoro tulisaidia kuunganisha nchi yao tena.”

No comments:

Post a Comment