TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Sunday, January 11, 2015

VIJANA WASHAURIWA KUUNGANA NA KUTUMIA RASIRIMALI ZILIZOPO NCHINI

2
Ayubu Lihunga Mkurugenzi wa Shirika la Vijana wajasiriamali na Uwezeshaji Tanzania (TYEEO) akizungumza na wajasiriamali wakati alipokuwa akimkaribisha mgeni rasmi kwenye sherehe ya uzinduzi wa taasisi hiyo niliyofanyika kwenye viwanja vya maonyesha vya Sabasaba jijini Dar es salaam leo, Katikati ni Sadiki Kusiama Mhadhiri Msaidizi Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya.
3
Baadhi ya wana VICOBA wajasiriamali wakiwa katika sherehe hiyo
4
Baadhi ya wana VICOBA wajasiriamali wakiwa katika sherehe hiyo
………………………………………………………………………………………………
VIJANA wameshauriwa kuungana pamoja na kuweza kutumia rasilimali zilizopo hapa nchini kwa lengo la kujiendeleza na kujitoa katika lindi la umasikini.
Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam leo katika uzinduzi wa Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya TEEYO na Mhadhiri msaidizi wa Chuo kikuu cha sayansi na Teknolojia Mbeya Sadiki kusiama.
kusiama alisema kuwa hakuna njia nyingine kwa vijana ya kuweza kuyafikia maendeleo kama si kujiunga katika vikundi ili kuweza kupata fursa zinzojitokeza katika jamii.
“Binafsi nimefarijika kwa hatua hii ambayo taasisi hii ya TEEYO ilichokifanya katika jamii ni dhahiri kuwa vijana wengi wataweza kupata fursa na mwisho wasiku kuweza kujinasua katika umasikini hivyo watanzania wanapaswa kuchangia jitihada hizi,”alisema Sadick
Alisema kuwa kupitia taasisi kama hizo ambazo zinafanya kazi kubwa kwa ajili ya kuwanasua watanzania kuondoka katika umasikini serikakali ingeweka mazingira mazuri na hasa katika kupunguza bei ya vifaa vya ujenziu vinavyo zalishwa hapa nchini ili kutoa fursa kwa wajasiliamali kuweza kuwa na nyumba za kisasa.
Pia Sadick aliipongeza taasisi hiyo kwa kazi kubwa ambayo wanaifanya ikiwemo kuunga juhudi za serikali za kuhakikisha watanzania wanakuwa katika maisha bora na ya uhakika.
Mbali na uzinduzi huo pia mgeni rasmi huyo aliweza kuchangia Sh. milioni tano huku akiiwataka wadau na taasisi zingine kuunga mkono jitihada hizo zinazofanywa na Taasisi ya jana wajasiliamali na uwezeshaji (TEEYO).
kwaupande wake Murugenzi wa taasisi hiyo Luhunga Ayubu alisema kwanza taasisi yake ina mwaka mmoja tangua imeazishwa na imekuwa na mafanikio makubwa kwani hadi hivi sasa inawachama hai zaidi ya 2000 na vikundi 132.
Alisema kuwa pamoja na mafanikio hayo taasisi inahitaji Sh.milioni 342 kwa ajili ya kuweza kutoa mikopo kwa wananchama wake katika vikundi mbalimbali vya biashara.
“dhamira yetu ni kuona tuna wainua wanachama wetu kibiashara pamoja na kuwapa elimu ya ujasialiamali ili waweze kujimudu kimaisha na kupiga vita umasikini ambao umeonekana kukithiri katika nchi yetu,’alisema Luhunga.
Akizungumzia malengo ya Taasisi ni kuweza kuwasaidia wajasiliamali zaidi pamoja na kuanzisha mtandao wa biashara kutoa uelewa binafsi ili kuepukana na magonjwa ambukizi.

No comments:

Post a Comment