TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, September 27, 2016

HIVI NDIVYO SAFARI YA MWISHO YA MPIGANAJI MWENZETU ADOLF SAIMON KIVAMWO ILIVYOKUWA,TULIMPENDA SANA LAKINI MUNGU AMEMPENDA ZAIDI

 
Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP-Media ambapo marehemu aliwahi kufanyika kazi kwenye Kampuni ya The Guardian Ltd akimwombea marehemu baada ya kuweka shada la maua.
Wabunge Saed Kubenea wa ubungo (kushoto), Zitto Kambwe Kigoma Mjini na Shy-Rose Bhanji wa Bunge la Afrika Mashariki wakiweka maua kwenye kaburi wakati wa mazishi.
Mwenyekiti wa 'Media Car Wash for Cancer' aliyeongoza kampeni ya matibabu ya Kivamwo, Benjamin Thomson na Mwana habari mwenzake Grace Nackso wakiweka maua kwenye kaburi wakati wa mazishi.
Mwana habari Amy Cunningham aliyewahi ufanya kazi na Kivamwo akiweka ua wenye kaburi wakati wa mazishi.

MAFUNZO KUHUSU MWONGOZO WA USIMAMIZI WA UWEKEZAJI WA MIRADI YA UMMA KANDA YA MOROGORO YAFUMGULIWA RASMI

Mgeni Rasmi, Bi. Lorah Madete, Kaimu Naibu Katibu Mtendaji, Klasta ya Uchumi Jumla, Tume ya Mipango, akitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tano kuhusu Usimamizi wa Uwekezaji wa Miradi ya Umma Kanda ya Morogoro kwa Maofisa na Watendaji wa Idara za Sera na Mipango. Waliokaa ni Bi. Anna Kimwela, Mchumi, Tume ya Mipango na Dr. Jehovaness Aikaeli, Mhadhiri Mwandamizi na Mkuu wa Idara ya Uchumi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Washiriki wa Mafunzo kuhusu Mwongozo wa Usimamizi wa Uwekezaji wa Miradi ya Umma ambao ni Maofisa na Watendaji wa Idara za Sera na Mipango kutoka Kanda ya Morogoro wakimsikiliza Mgeni Rasmi (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yanayofanyika katika Ukumbi wa Mkutano katika Chuo Kikuu cha Kilimo Morogroro (SUA). 

Muwezeshaji Dr. Jehovaness Aikaeli, Mhadhiri Mwandamizi na Mkuu wa Idara ya Uchumi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akitoa elimu kwa washiriki wa mafunzo hayo.

Washiriki pamoja na wakufunzi wa mafunzo juu ya Mwongozo wa Usimamizi wa Uwekezaji wa Miradi ya Umma ambao ni Maofisa na watendaji wa Idara za Sera na Mipango kutoka Kanda ya Morogoro wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi, Bi. Lorah Madete, Kaimu Naibu Katibu Mtendaji, Klasta ya Uchumi Jumla, Tume ya Mipango (aliyekaa wa pili kushoto) mara baada ya ufunguzi wa mafunzo hayo.