TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, August 2, 2014

LIVE MUDA HUU : WAZIRI MKUU MH.PINDA AZINDUA RASMI KITUO KIPYA CHA MABASI NANENANE MKOANI MBEYA MUDA HUU.

                        Na Mbeya yetu Blog

Meza kuu Muda huu katika Kituo kikuu cha Mabasi Nane nane 
 Waziri Mkuu Mh. Pinda akiwa anaongea na wananchi katika kituo kikuu cha mabasi  Nane nane na Kukizindua Rarmi 
Kazi ya Uzinduzi ikiwa inaendelea .. 

Dunia nzima lazima iifuate Azam Mbagala

Wachezaji wa Azam wakijadiliana jambo wakati wa mechi ya kirafiki dhidi ya Kombaini ya jeshi jana Ijumaa kwenye uwanja wa Azam Complex. Azam ilifungwa mabao 3-0. 
By DORIS MALIYAGA  (email the author)

Posted  Agosti2  2014  saa 12:13 PM
SHARE THIS STORY
0
Share

KATIKA kujiweka sawa, Mabingwa wapya wa Ligi Kuu Bara  klabu ya Azam FC, itakipiga na Zesco ya Zambia Uwanja wa  Azam Complex Agosti 10 na imetamka rasmi kuwa itacheza  mechi zake zote za Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye Uwanja  wao na siyo Taifa.
Katibu Mkuu wa Azam, Idrissa Nassor ameliambia Mwanaspoti  kuwa: “Baada ya mechi yetu na Mtibwa, tutacheza mechi ya  kirafiki na Zesco ya Zambia siku hiyo mipango yote  imeshakamilika.”
Muivory Coast  wa Azam, Kipre Tchetche ameondolewa  kikosini kutokana na kusumbuliwa na majeruhi ya shingo na  anatarajiwa kuanza mazoezi na wenzake, wiki ijayo.
Pia Mhaiti Leonel Saint-Preux anasumbuliwa na majeruhi  kwenye mguu wa kulia. Omog amesema: “Tchetche  nimempumzisha hadi wiki ijayo, anamatatizo mgongoni kwenye  shingo na Leonel hayuko vizuri nafikiri ataanza mazoezi na  wenzake kesho (leo),”alisema Omog. Azam leo itafanya  mazoezi ya ufukweni Coco.

TWIGA AFA BAADA YA KUJIGONGA DARAJANI


Shirika la kutetea haki za wanyama la Afrika Kusini limeanza uchunguzi kuhusiana na kifo cha twiga baada ya kuumia wakati akisafirishwa kwenye gari. Watu walioshuhudia tukio hilo wanasema twiga mmoja kati ya wawili waliokuwa kwenye lori, aligonga kichwa chake katika barabara moja mjini Johannesburg. 
Gari hilo baadaye liliharibika na kulazimika kusubiri kwa saa kadhaa kabla ya kutengenezwa. Wanyama wote wawili walipelekwa kwa daktari wa wanyama, lakini shirika la kutetea haki za wanyama la NSPCA limesema twiga mmoja alikufa. 
Tukio hilo limeleta mjadala mkubwa kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter. 
Meneja wa NSCPA Rick Allen amethibitisha kuwa twiga huyo alipata majeraha ya kichwani lakini amesema uchunguzi ni muhimu ufanyike kutafuta sababu hasa ya kifo hicho.

WENGER: MESSI ALIMFANYA SANCHEZ AHANGAIKE BARCELONA KAMA ILIVYO KWA NEYMAR

Wenger: Messi made Alexis suffer at Barcelona
NA BARAKA MPEJA
ASERNE Wenger anaamini Alexis Sanchez aliathirika kama anavyoathirika Neymar wakati akiwa Barcelona kutokana na uwepo wa Lionel Messi.
Asernal ilitumia Euro milioni 40 kumsajili nyota huyo wa kimataifa wa Chile majira haya ya kiangazi na leo hii anatarajia kucheza mechi yake ya kwanza ya maandalizi ya msimu mpya.
Licha ya kucheza kama winga akiwa Barca, Alexis atachezeshwa kama mshambuliaji Emirates na Wenger anaamini atang`ara zaidi katika nafasi hiyo kutokana na kutokuwepo kwa ‘mchawi’ wake Messi.
“Kwa mara ya kwanza alitinga katika rada zangu alipokuwa Udinese na baadaye Barcelona”. Alisema Mfaransa huyo alipozungumza na The Dail Mirror.
“Ni mshambuliaji. Ni mmaliziaji mzuri ambaye alikuwa na kiwango kizuri Italia. Nilimuona pale na alikuwa amesimama vizuri. Lakini mambo yalikuwa magumu alipoenda Barcelona kama ilivyo kwa Neymar sahizi”.
“Unapomuona Neymar wa Brazil na Neymar wa Barcelona sio mtu mmoja. Naamini kuwa Alexis anaweza kucheza kushoto, kulia na mbele na ndio maana nilimfuata”.

MBUNGE NASSARI ASHIRIKI MDAHALO ULIOANDALIWA MAKAO MAKUU YA BENKI YA DUNIA.

Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari (wa pili toka shoto) akiwa ni miongoni mwa wawasishaji wa mada katika mdahalo maalumu uliofanyika Makao Makuu ya Benki ya Dunia.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari (katikati) akichangia mada iliyosema "The Fundamental Role of Education and Skills ,addressing the Challenge of Youth Education " katika mdahalo maalumu uliofanyika Makao Makuu ya Benki ya Dunia ambapo Mh Nassari alikuwa ni miongoni mwa wawasilishaji wa mada. Wengine ni Waziri Msaatfu wa Mambo ya nje wa Liberia na baadhi ya maofisa wa Benki ya Dunia ambapo Nassari pia alipata fursa ya kukutana na rais wa Benki ya Dunia kwa maswala ya Afrika.

BREAKING NEWS: BASI LA HOOD LAUA WATANO ARUSHA


Ajali iliyohusisha basi la HOOD na daladala maeneo ya Usa River mkoani Arusha muda huu...Ambapo dereva wa dala dala kafariki hapo hapo
atu 5 wamekufa baada ya basi la Hood kwenda Mbeya kugongana na Hiace eneo la Kilala, Arusha asubuhi hii, wengi wajeruhiwa. Taarifa zaidi baadaye.

TETESI ZA SOKA ULAYA

Salim Kikeke's photo.

Salim Kikeke's photo.
Salim Kikeke's photo.

Arsenal wameambiwa Juan Quintero, 21, ataruhusiwa tu kuondoka Porto iwapo kifungu cha pauni milioni 32 cha uhamisho kitatenguliwa (Daily Express) Manchester United wanakaribia kufanikisha uhamisho wa pauni milioni 20 wa Mats Hummels, 25, huku Borussia Dortmund wakiwa na matumaini ya kuziba pengo hilo kwa kumchukua Tiago IIori, 21, kutoka Liverpool kwa mkopo (Daily Mirror), rais wa Napoli Aurelio De Laurentiis amethibitisha kuwa klabu yake inamtaka kiungo wa Manchester United Marouanne Fellaini, 26, ingawa kuna wachezaji wengine pia inawafuatilia (Daily Telegraph), Liverpool inatazama kuwachukua mabeki kutoka Spain Alberto Moreno, 22, wa Sevilla na Javier Manquillo, 20 kutoka Atletico Madrid (Daily Star), West Ham wamekuwa na mazungumzo na mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Samuel Eto'o, 33, na pia Hugo Almeida, 30 kutoka Besitkas (Times), kocha wa Atletico Madrid Diego Simione yuko tayari kupanda dau kumchukua kiungo wa Manchester United Shinji Kagawa, 25 (Daily Express), QPR wameelekeza macho yao kumfuatilia kiungo
Salim Kikeke's photo.
Morgan Amalfitano, 29 kutoka Marseille, aliyeichezea West Brom kwa mkopo msimu uliopita (Daily Mail), Arsenal wanamfuatilia beki wa Real Madrid Alvaro Arbeloa iwapo Thomas Vermaelen ataondoka Emirates (AS), Arturo Vidal wa Juventus amepita katika vipimo vya afya na anasubiri makubaliano ya mwisho kusaini mkataba na Manchester United (Metro), kiungo wa Porto Juan Quintero amesafiri kwenda London kukamilisha uhamisho wake wa kwenda Arsenal (Marca). Share tetesi hizi na wapenda soka wote. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Cheers!

Friday, August 1, 2014

MTUHUMIWA WA MAUWAJI YA AYOUB MLAY KWA BASTOLA AMBROSIA CLUB AONJA JOTO YA JIWE MAHAKAMANI KISUTU.


Mtuhumiwa  wa kesi ya Mauaji, Conrad Leo (33)akiwa chini ya ulinzi wa polisi mara baada ya kuachiwa na kukamatwa tena katika mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam jana.Mtuhumiwa huyo anashitakiwa kwa kosa la kumuua kwa kutumia silaha Ayubu Mlai.
Mtuhumiwa  wa kesi ya Mauaji, Conrad Leo (33)akiwa ndani ya gari ya polisi akipelekwa Mahabusu baada ya kuachiwa na kukamatwa tena katika mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam .Mtuhumiwa huyo anashitakiwa kwa kosa la kumuua kwa kutumia silaha Ayubu Mlai 
Mtuhumiwa  wa kesi ya Mauaji, Conrad Leo (33)akizibitiwa na Polisi

Rais Kikwete awasili Washington kuhudhuria Mkutano wa Viongozi wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Amerika na Africa (US-Africa Leaders summit)

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya maafisa waliofika kumpokea wakati akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dulles tayari kwa Mkutano wa Viongozi wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Amerika na Africa (US-Africa Leaders summit) uliondaliwa na Rais Barack Obama wa unaotaraji kuanza Agosti 4-hadi 6, 2014, ambao utatanguliwa na mikutano mingine ya maendeleo ya sekta mbalimbali na uwekezaji (2-3 Agosti, 2014) jijini Washington DC. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani,Balozi Liberata Mulamula.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakisalimiana na baadhi ya maafisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani wakati walipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dulles.PICHA NA IKULU.

Maadhimisho ya siku ya Mwanamke wa Afrika yaliyo ratibiwa na -WiLDAF yafana jijini Dar es salaam

Maadhimisho ya siku ya Mwanamke wa Afrika yaliyo ratibiwa na Women in Law and Development in Africa-WiLDAF yafana jijini Dar es salaam. Ni siku ya Mwanamke wa Afrika na husheherekewa kila mwaka tarehe 31 July toka ilipotamkwa rasmi mwaka 1963 July 31 na wanawake wa Pan African waliokutana Dar es Salaam kwa wakati huo.Mada mbalimbali zilitolewa ikiwemo mchakato mzima wa katiba mpya na changamoto zake. Kulikuwa na watoa mada mbalimbali wakiwemo Dr Khoti Kamanga na Mh. Getrude Mongela.

Mbunge wa jimbo la Ukonga Eugen Mwaiposa akabidhi kombe kwa washindi wa shindano la Airtel Rising Stars

  Mbunge wa jimbo la Ukonga Eugen Mwaiposa akimkabidhi kombe la ubingwa nahodha wa timu ya Ilala Academy Maisala Adam baada ya timu hiyo kuibuka mabingwa wa Airtel Rising Stars mkoa wa kisoka wa Ilala juzi.
 Mbunge wa jimbo la Ukonga Eugen Mwaiposa akimkabidhi kombe la ubingwa nahodha wa timu ya Temeke All Stars Maulid Jamal baada ya timu hiyo kuibuka mabingwa wa Airtel Rising Stars mkoa wa kisoka wa Temeke juzi.
 Mbunge wa jimbo la Ukonga Eugen Mwaiposa akimkabidhi kombe la ubingwa nahodha wa timu ya Kinondoni Academy Jafali Said baada ya timu hiyo kuibuka mabingwa wa Airtel Rising Stars mkoa wa kisoka wa Kinondoni juzi.

CHUO CHA CBE CHAZINDUA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 JIJINI DAR, WADAU MBALIMBALI WAPONGEZA UBORA WA ELIMU INAYOTOLEWA

Mbunge wa Ilala Mh. Mussa Zungu ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa Uzinduzi wa Maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) akikata utepe kuashiria uzindunzi wa maadhimisho ya chuo hicho kutimiza miaka 50 tangu kuanzishwa kwake katika hafla iliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) wakiangalia moja ya picha ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyopigwa wakati akifungua Chuo hicho Januari, 1965. Kutoka kushoto ni Mkuu wa chuo hicho Prof. Emanuel Mjema, Mh. Musa Zungu (Mb) jimbo la Ilala,Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda,Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho Prof. Mathew Luhanga na Prof.Eliuta Mwageni Makamu Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha.
Viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) wakiwa katika picha ya pamoja wakiongozwa na Mbunge wa Ilala Mh. Mussa Zungu na Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda (katikati). Nyuma ni bango lenye picha ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyopigwa wakati akifungua Chuo hicho mwaka 1965.
Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Tunu Pinda kwa niaba ya wanafunzi waliosoma katika chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam akizungumza na wadau na wanajumuiya wa Chuo hicho wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo hicho jijini Dar es salaam.

MH ZITTO KABWE ATOA MSIMAMO WAKE KUHUSU KATIBA NA UKAWA..

Jana tarehe 29 Julai, 2014 nimefanya mahojiano katika kipindi cha PowerBreakFast kinachorushwa na Clouds FM. Baadhi ya vyombo vya habari vimeandika mahojiano yale. Napenda nitoe ufafanuzi kidogo kuhusu msimamo wangu kuhusu mchakato wa Katiba.Kwanza, Mimi sijawahi kuwa UKAWA wala kundi lolote lile katika Bunge Maalumu la Katiba isipokuwa kundi linalotaka maridhiano. Msimamo wangu kuhusu Muungano ni Serikali Tatu Zilizoboreshwa (S3z) ili kuwa na Muungano imara usio tegemezi wala egemezi kwa Washirika wake.  Pili, Mimi niliunga mkono ‘protest’ ya baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kupinga lugha za matusi na lugha za kibaguzi zilizokuwa zinaendelea ndani ya mkutano ule. Vilevile niliunga mkono kwamba Rasimu inayopaswa kujadiliwa ni Rasimu iliyotokana na Tume ya Marekebisho ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Sinde Warioba.
Nasisitiza umuhimu wa kupata Katiba BORA itakayoimarisha DOLA ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tatu, kwa hali ya sasa kuna mkwamo katika kupatikana kwa Katiba Bora. Mkwamo unaotokana na kutokuwepo kwa nia ya dhati ya kupata maridhiano ya pande zinazopingana. UKAWA hawataki mazungumzo na Viongozi wa Bunge la Katiba badala ya kujenga maridhiano kila siku wanawabeza UKAWA jambo ambalo kamwe haliwezi kujenga mwafaka.Ushauri wangu ni kuahirisha mchakato mzima wa kuandika Katiba mpaka mwaka 2016 baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Katiba ya sasa ifanyiwe marekebisho machache kama ifuatavyo;  
i) Tume ya Uchaguzi ili iwe huru na ionekane kuwa huru, ikiwemo kuwaondoa watumishi wa Halmashauri za Wilaya, Miji na Majiji katika kusimamia uchaguzi
ii) Kuruhusu mgombea binafsi 
iii) Kuondoa Mafuta na Gesi kama Jambo la Muungano ili Zanzibar ianze mara moja kusimamia kwa uhuru utafutaji wa Mafuta katika vitalu vilivyopo upande huo wa Muungano 
Mkutano wa Bunge Maalumu utakaofanyika bila kuwepo kwa maridhiano utakuwa hauna maana yeyote na itakuwa ni sawa na kupoteza muda na fedha za walipa kodi ambazo zingeweza kununua madawa vijijini.

MARAIS WASTAAFU THABO MBEKI, FESTUS MOGAE NA BENJAMIN MKAPA WAKUTANA DAR ES SALAAM

1a
Marais wastaafu Thabo Mbeki wa Afrika Kusini na Festus Mogae wa Botswana wakiigia kwenye chumba cha Mkutano katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo wakati wa mkutano wa mwaka wa Africa Readership Forum ulioandaliwa na Taasisi ya Uongozi Institute jijini Dar es salaam ambao ulikuwa unajadili changamoto mbalimbali zinazozikabili nchi za Afrika na kuangalia masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na hatua za kushughulikia changamoto hizo.
2a
Rais mstaafu wa wa Afrika Kusin Thabo Mbeki akizungumza katika mkutano huo uliojumuisha viongozi mbalimbali wa afrika na taasisi mbalimbali kweye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo.
3a
Marais wastaafu Thabo Mbeki wa Afrika Kusini katikati ,Festus Mogae wa Botswana kushoo na Rais Mstaafu wa Tanzania Mh. Benjamin William Mkapa wakiwa wakiongoza mkutano huo.
4a
Baadhi ya viongozi kutoka taasisi mbalimbali waliohudhuria katika mkutano huo.
5a
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh. Zitto Kabwe katikati ni mmoja wa viongozi waliohudhuria katik mkutano huo uliofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
6a
Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Fredrick Sumaye kulia ni Mh. Balozi Ali Karume walikuwa ni miogoni wa viongozi waliohudhuria katika mkutano huo pia.

Thursday, July 31, 2014

RAIA WANNE WAPOTEZA MAISHA JIJINI MBEYA, YUMO ALIYEANGUKIWA NA KIFUSI. WATU WANNE WAFARIKI DUNIA NA WENGINE 51 KUJERUHIWA KATIKA AJALI YA GARI MATUNDASI- CHUNYA


TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 31.07.2014.

WATU WANNE WAFARIKI DUNIA NA WENGINE 51 KUJERUHIWA KATIKA AJALI YA GARI MATUNDASI WILAYANI CHUNYA.

MTU MMOJA AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA BARABARANI JIJINI MBEYA.

MTOTO WA MIAKA MITATU AFARIKI DUNIA BAADA YA KUANGUKIWA NA KIFUSI CHA MCHANGA WILAYANI CHUNYA.

MTOTO WA MIAKA KUMI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUPIGWA NA SHOTI YA UMEME.

KATIKA TUKIO LA KWANZA:
WATU WANNE WALIOTAMBULIKA KWA MAJINA YA 1. PAULO MWASANGA (18) MKAZI WA KITONGOJI CHA MATUNDASI ‘B’ 2. WEDI ANGOLWISE (21) MKAZI WA MATUNDASI 3. SALOME MWAKIBETE (13) MWANAFUNZI WA DARASA LA SABA SHULE YA MSINGI SAMBILIMWAYA NA 4. OBEDI MWAKAMELA (25) MKAZI WA MATUNDASI WAMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.595 CHU AINA YA FUSO TIPPER LIKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA KIPINDUKA KATIKA KIJIJI CHA MATUNDASI WILAYANI CHUNYA.

AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 30.07.2014 MAJIRA YA SAA 16:00 JIONI HUKO KATIKA KITONGOJI CHA MATUNDASI “B”, KIJIJI CHA MATUNDASI, KATA YA MATUNDASI, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA CHUNYA/MAKONGOLOSI.
GARI HILO LILIKUWA LIKITOKEA KIJIJI CHA SAMBILIMWAYA KUELEKEA KIJIJI CHA MATUNDASI LIKIWA LIMEBEBA WACHEZAJI WA MPIRA WA MIGUU NA MASHABIKI. AIDHA KATIKA AJALI HIYO WATU 51 WALIJERUHIWA, KATI YAO 26 WALITIBIWA NA KURUHUSIWA NA WENGINE 25 WAMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA CHUNYA WAKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI, DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO NA JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL .N. MASAKI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO HASA KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA WILE PETER AMBAYE ALIKUWA ABIRIA KATIKA PIKIPIKIAMEFARIKI DUNIA BAADA YA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI DFP 0036 AINA YA BENZ MALI YA SHIRIKA LA UMEME TANESCO LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA PATRICK MHAGAMA (46) MKAZI WA ILOMBA JIJI MBEYA KUMGONGA MPANDA PIKIPIKI ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE NA KUSABABISHA KIFO KWA ABIRIA HUYO.

AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 31.07.2014 MAJIRA YA SAA 16:45 JIONI HUKO NZOVWE, KATA YA NZOVWE, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. DEREVA AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUONI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL .N. MASAKI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO HASA KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. 

KATIKA TUKIO LA TATU:
MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA MITATU ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA PASCALIA JIFULA NGASA AMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUANGUKIWA NA KUFUNIKWA NA KIFUSI CHA MCHANGA KATIKA KITONGOJI CHA CHIZYA WILAYANI CHUNYA.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 30.07.2014 MAJIRA YA SAA 08:300 ASUBUHI HUKO KATIKA KITONGOJI CHA CHIZYA, KIJIJI CHA MWAMBANI CHINI, KATA YA MWAMBANI, TARAFA YA KWIMBA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. WAKATI TUKIO HILO LINATOKEA, MTOTO HUYO ALIKUWA AKICHEZA NA WATOTO WENZAKE KWENYE GEMA LA MCHANGA NA NDIPO KIFUSI KUMUANGUKIA NA KUMFUNIKA.

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL .N. MASAKI ANATOA WITO KWA WAZAZI NA WALEZI KUWA MAKINI NA WATOTO WADOGO KWA KUANGALIA MAZINGIRA YA MAENEO YAO ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA KUJITOKEZA. 

KATIKA TUKIO LA NNE:
MTOTO WA MIAKA KUMI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JERRY JESTED, MWANAFUNZI NA MKAZI WA MLOWO WILAYANI MBOZI ALIKUTWA AMEKUFA CHUMBANI KWAKE BAADA YA KUPIGWA NA SHOTI YA UMEME.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 30.07.2014 MAJIRA YA SAA 06:00 ASUBUHI HUKO KATIKA KATA YA MLOWO, TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA CHANZO CHA TUKIO HILO NI BAADA YA MAREHEMU KULAMBA NYAYA ZA UMEME AMBAZO ZILIKUWA KARIBU NA KITANDA CHAKE HALI ILIYOPELEKEA KUPIGWA SHOTI NA KUSABABISHA KIFO CHAKE.

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL .N. MASAKI ANATOA WITO KWA WAZAZI NA WALEZI KUWA MAKINI NA WATOTO WADOGO KWA KUANGALIA MAZINGIRA YA MAENEO YAO ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA KUJITOKEZA IKIWA NI PAMOJA NA KUWEKA MBALI VITU VYA HATARI KWA WATOTO.

Imetolewa na kusainiwa na:
[BARAKAEL .N. MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais Dkt Mahenge azindua tovuti ya mabadliko ya tabia nchi.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira Mh. Dkt. Eng Binilith Satano Mahenge akizindua rasmi tovuti ya mabadiliko ya tabianchi itakayotumika kutoa taarifa mbalimbali za utunzaji wa Mazingira. 
Mheshimiwa      Eng  Dkt. Binirithi S.  Mahenge  (mbunge)  Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa  Rais (mazingira) azindua tovuti ya mabadiliko ya tabia  nchi. Katika hotuba yake fupi ya uzinduzi wa tovuti hiyo, aliyoandaliwa kwa ufadhili wa serikali ya Denmark Mh. Binirithi  Mhenge amesema kuwa mabadiliko ya tabia ya nchi huangaliwa kwa muda wa miaka 30 hivyo kwa kipindi hiki chote kumekuwa na madhara mengi yatokanayo na athari za mabadiliko ya tabia Nchi ikiwa ongezeko la joto, kina cha bahari kuongezeka pamoja na ongezeko la majanga ya mvua zisizo na viwango,  kutoka na shughuli za binadamu katika uzalishaji hasa viwanda vikubwa
Alisema kwa tovuti inayozinduliwa ina umuhimu mkubwa kwani inaelezea maeneo ya hali ya mabadiliko ya tabia  nchi na juhudi za serikali katika kukabiliana na athari zinazoletwa na mabadiliko hayo.
“ziko sababu za kuungana na wenzetu ili kuondoa      tatizo hili la mabadiliko ya nchi ambapo tovuti hii WWW.climatechange.go.tz inatuunganisha na tovuti mbali mbali katika kupunguza gesi joto hapanchini pia inaelezea fursa zilizopo katika miradi na program mbali mbali. Alisisitiza”
Alibaini kuwa tovuti hii itachangia kwa kiasi kikubwa kuongeza uelewa na weledi kuhusu mabadiliko ya tabia  nchi nchini kwa wananchi na wadau kwa ujumla.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira Mh. Dkt. Eng Binilith Satano Mahenge (wa kwanza kushoto) akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) katika ukumbi wa mkutano wa  Ofisi ya Makamu wa Rais leo jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa "tovuti ya mabadiliko ya tabianchi" huku akieleza malengo ya tovuti hiyo. kushoto ni Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Julius Ningu.
 sehemu ya wadau waliyoudhulia katika mkutano huo kushuhudia makubaliano ya mkataba huo.
 Mkuu Msaidizi wa Chuo cha kilimo SUA Prof. Gerald Monella (aliyesimama) akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wadau mbalimbali kuhusu mkataba huo unaofanyika baina ya Ofisi ya Makamu wa Rais na chuo cha SUA.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Sazi Salula (wa kwanza kushoto) na Mkuu Msaidizi wa Chuo cha SUA Prof. Gerald Monella wakisaini mkataba wa uwanzishwaji wa kituo cha Taifa cha kukusanya na kuratibu takwimu za hewa ukaa  uliofanyika katika ukumbi wa mkutano Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dar es Salaam.
 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Sazi Salula wakipeana Mkataba na mkuu msaidizi wa wa chuo cha kilimo SUA Prof. Gerald Monella baada ya kusaini.
 Sehemu ya waandishi wa habari waliyoudhulia katika uzinduzi huo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.