TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, July 28, 2014

TANZANIA IJIPANGE TENA JUMUIYA YA MADOLA.

Timu ya Tanzania ilipo wasili kwenye michezo ya jumuiya ya madola jijini Glasgow Scotland 
 =================================================
Fabiano mshindi wa medali ya fedha ya mita 10,000 kwenye michezo hiyo mwaka 2006 nchini Australia alikuwa tegemeo la Tanzania, lakini alishika nafasi ya 11 huku Mtanzania mwingine John Leonard akiishia njiani.
NYOTA ya Tanzania katika michezo ya Jumuiya ya Madola inayoendelea huko Glasgow, Scotland imeendelea kufifia baada ya jana Jumapili mwanariadha tegemeo Fabiano Joseph (pichani) kushindwa kwenye marathoni.
Fabiano mshindi wa medali ya fedha ya mita 10,000 kwenye michezo hiyo mwaka 2006 nchini Australia alikuwa tegemeo la Tanzania, lakini alishika nafasi ya 11 huku Mtanzania mwingine John Leonard akiishia njiani.
Kushindwa kwa Fabiano ni mwendelezo wa wanamichezo wa Tanzania kwenye michezo hiyo kuondoshwa mapema ambapo tayari, baadhi ya mabondia, waogeleaji na timu ya mpira wa meza wameaga michezo hiyo.
Fabiano alitumia muda wa 2:15.21 kumaliza mbio hizo, wakati mshindi Michael Shelley wa Australia alitumia muda wa 2:11.15 na Stephen Chemlany wa Kenya alikuwa wa pili akitumia 2:11.58 huku Mganda, Abraham Kiplimo alikimbia kwa 2:12:23. Wakati huohuo, juzi jioni, bondia Nasser Mafuru aliondoshwa kwenye michezo hiyo na kuungana na Seleman Kidunda aliyeugua tumbo na kushindwa kupigana.

No comments:

Post a Comment