TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Sunday, July 27, 2014

Loga amvizia Hamis Kiiza

By  MWANDISHI WETU
 
Kocha wa Simba,Zdravko Logarusic ‘Loga’ alisema; “Nawajua hao wachezaji Okwi na Kiiza ni wachezaji wazuri niliwaona msimu uliopita, sina pingamizi kama nitaletewa hapa, ninachotaka ni mchezaji mzuri mwenye uwezo wa kunifanyia kazi ninayotaka.”

UONGOZI wa Simba umegawanyika wapo ambao hawataki kusikia usajili wa mchezaji yoyote kutoka Yanga lakini wapo mabosi watatu huwaambii kitu kuhusu Emmanuel Okwi.
Kocha wa Simba,Zdravko Logarusic ‘Loga’ alisema; “Nawajua hao wachezaji Okwi na Kiiza ni wachezaji wazuri niliwaona msimu uliopita, sina pingamizi kama nitaletewa hapa, ninachotaka ni mchezaji mzuri mwenye uwezo wa kunifanyia kazi ninayotaka.”
“Sina uhakika kama viongozi wangu wanataka kuwasajili, lakini mimi isingekuwa hii kanuni ya shirikisho hata ukiniletea wote hakuna shida, siwezi kumkataa mchezaji mzuri sababu ikiwa ni klabu anayotoka, nitamchukua mchezaji yeyote kutoka Yanga na hata Azam.” Mwanaspoti linajua kwamba Yanga wanafikiria kuachana na Hamis Kiiza ingawa na Okwi na mwenyewe yuko kwenye wakati mgumu.
Kocha wa Yanga, Marcio Maximo amesema hataki wachezaji wabinafsi kwenye kikosi chake na hababaishwi na majina makubwa hivyo atahitaji muda wa kuwatazama Okwi na Kiiza ili kuona uwezo wao uwanjani kabla ya kumtema mmoja.
“Nasubiri waje kwanza, wacheze ili niwaone wanavyocheza na uwezo wao kwa ujumla na baada ya hapo nitafanya maamuzi sahihi yatakayokuwa na mafanikio.
“Kwa kifupi sitaki mchezaji mbinafsi, mchezaji anayewaza nafsi yake pekee bali nataka mchezaji anayewaza mafanikio ya Yanga na anayejituma kuhakikisha timu inanyakua kombe kwani mchezaji anashinda mechi lakini timu ndiyo inayoshinda makombe,” alisema Maximo.

No comments:

Post a Comment