TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, October 18, 2014

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI- NISHATI MHE. CHARLES KITWANGA ATEMBELEA MIRADI YA UMEME INAYOFADHILIWA NA WAKALA WA NISHATI VIJIJINI (REA) KATIKA MKOA WA PWANI

Picha Na 1
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantum Mahiza (aliyesimama mbele) akielezea mchango wa nishati ya umeme katika ukuaji wa uchumi wa mkoa huo, katika kikao chake na Naibu  Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya  nishati Mhe. Charles Kitwanga. Mhe. Kitwanga  yuko ziarani mkoani humo ambapo anatembelea miradi ya umeme inayofadhiliwa na Wakala wa Nishati  Vijijini (REA) pamoja na kuzungumza na wananchi.
Picha Na 2Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantum Mahiza (kulia) akisisitiza jambo katika kikao hicho. Katikati ni  Naibu  Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya nishati Mhe. Charles Kitwanga. Kushoto ni Meneja Mwandamizi wa Tanesco Kanda ya  Dar es  Salaam na Pwani Mhandisi Mahende Mugaya.
Picha Na 3Naibu  Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya nishati Mhe. Charles Kitwanga, (aliyesimama) akielezea mikakati ya  Serikali katika kufikisha umeme vijijini katika kikao kilichoshirikisha  Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantum Mahiza  na watendaji wa Tanesco, wataalamu pamoja na waandishi wa habari.
Picha Na 4Naibu  Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya nishati Mhe. Charles Kitwanga, akisisitiza jambo katika kikao hicho
Picha Na 5Meneja Mwandamizi wa Tanesco Kanda ya  Dar es  Salaam na Pwani Mhandisi Mahende Mugaya (aliyesimama) akielezea mikakati ya  shirika hilo katika kukabiliana na changamoto ya kukatika kwa umeme kutokana na matengenezo yanayofanyika
Picha Na 6Naibu  Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya nishati Mhe. Charles Kitwanga, akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika kituo cha umeme cha Chalinze.
Picha Na 8Naibu  Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya nishati Mhe. Charles Kitwanga (katikati) akitoa maelekezo kwa wataalamu wa shirika la Tanesco katika kituo cha Chalinze ya jinsi ya kuboresha hali ya umeme katika mji wa Chalinze
Picha Na 11Naibu  Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya nishati Mhe. Charles Kitwanga (kushoto) akizungumza na mkazi wa Kiwangwa wilayani Bagamoyo, Said Ramadhani ili kupata maoni yake kuhusiana na utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini.
Picha Na 10Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya nishati Mhe. Charles Kitwanga (katikati) akifurahia jambo na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo,  Ahmed Kipozi (kushoto). Kulia ni Diwani wa Kerege, Tabia Juma.
Picha Na 9Naibu  Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya nishati Mhe. Charles Kitwanga (katikati) akifurahia jambo na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo,  Ahmed Kipozi (kushoto). Kulia ni Diwani wa Kerege, Tabia Juma.

Tanesco kuunganishia wateja wake wa umeme ndani ya siku moja

Picha Na 8
Naibu  Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya nishati Mhe. Charles Kitwanga (katikati) akitoa maelekezo kwa wataalamu wa shirika la Tanesco katika kituo cha Chalinze ya jinsi ya kuboresha hali ya umeme katika mji wa Chalinze
……………………………………………………………………….
Na Greyson Mwase, Pwani
Ili kuhakikisha wananchi wananufaika na nishati ya umeme na kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi, Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini imeagiza Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) kufanya kazi kwa weledi na ufanisi lengo likiwa ni kuwaunganishia wateja wake umeme ndani ya siku moja mara baada ya kukamilika kwa taratibu za malipo.
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya nishati Charles Kitwanga alipokutana na mkuu wa mkoa wa Pwani Mwantum Mahiza, watendaji wa Tanesco katika ziara yake ya kutembelea miradi ya umeme inayofadhiliwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) awamu ya pili.
Waziri Kitwanga alisema kuwa ili kuendana na kasi ya ukuaji wa uchumi wa nchi, shirika la Tanesco linatakiwa litoe huduma kwa ubora wa hali ya juu, wa kuridhisha na kwa wakati.
“ Inabidi ifikie mahali iwapo mteja atalipia umeme kabla ya saa nne asubuhi na ambaye haitaji nguzo, basi aunganishiwe umeme ndani ya siku hiyo hiyo, na hili linawezekana.” Alisema Kitwanga.
Kitwanga aliendelea kusema kuwa kwa wateja wanaohitaji huduma ya nguzo za umeme, shirika linatakiwa liwe limewaunganishia umeme kwa kipindi cha siku tatu.
Waziri Kitwanga aliongeza kuwa shirika la Tanesco linatakiwa kuondoa mfumo wa wateja kulipa madeni yao kwa foleni badala yake, walipe kwa kufuata mfumo wa kielektroniki ili kurahisisha ulipaji wake na wananchi kupata huduma kwa wakati.
Aidha, Kitwanga aliongeza kuwa ili kuondokana na adha ya kukatika kwa umeme mara kwa mara kutokana na sababu za matengenezo ya miundombinu ya umeme, shirika la Tanesco linatakiwa kubuni mifumo mbadala ya kuwezesha huduma ya umeme kuendelea kupatikana wakati matengenezo yakiendelea pasipo kukwamisha shughuli za uchumi.
“ Inatakiwa ifike umeme uwe ni kama oksijeni katika mwili wa binadamu, mwili wa binadamu ukikosa oksijeni kwa muda mfupi unapoteza uhai, tukielewa umuhimu wa umeme kwa mantiki hii, zitatumika mbinu mbadala za kuzuia kukatika umeme wakati wa matengenezo hivyo kupelekea uchumi wa nchi kukua kwa kasi.” Alisisitiza Kitwanga.
Kitwanga aliendelea kusema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini imejipanga kuhakikisha kuwa nishati ya umeme inachangia katika kutimiza lengo la Dira ya Maendeleo ya Taifa ya Mwaka 2025 ya kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2025 nchi ya Tanzania inaondoka kwenye kundi la nchi masikini duniani na kuwa nchi ya kipato cha kati.
Alisema kuwa katika nchi nyingi zilizopiga hatua kubwa katika ukuaji wa uchumi wake, nishati ya umeme imechangia kwa kiasi kikubwa mno na kusisitiza kuwa Wizara ya Nishati na Madini imejizatiti kuhakikisha kuwa uchumi wa nchi unakua kupitia mchango wa sekta ya nishati.
Wakati huo huo akielezea hali ya umeme katika mkoa wa Pwani, Meneja Mwandamizi wa Tanesco Kanda ya Dar es Salaam na Pwani Mhandisi Mahende Mugaya alisema kwa kipindi cha kuanzia Januari hadi Septemba mwaka huu Shirika la Tanesco lilifanikiwa kuwaunganishia umeme wateja 10, 100 katika mkoa wa Pwani na kufikisha asilimia 21.3 lengo likiwa ni kufikisha asilimia 30 ifikapo mwaka 2015.
Mhandisi Mahende aliongeza kuwa kwa sasa shirika la Tanesco linaendelea na zoezi la ukarabati wa miundombinu ya umeme iliyochakaa na kuongeza kuwa ifikapo Februari mwakani tatizo la kukatika umeme mara kwa mara litakuwa limekwisha kabisa.
Akielezea changamoto Shirika la Tanesco linalokumbana nazo katika shughuli zake katika mkoa huo, Mhandisi Mahende alitaja kuwa ni pamoja uchakavu wa miundombinu ya umeme na kusisitiza kuwa ukarabati bado unaendelea katika maeneo yaliyoathirika.
Mhandisi Mahende aliendelea kusema kuwa changamoto nyingine ni pamoja na madeni sugu kwa wateja na kuongeza kuwa hadi sasa Shirika linadai shilingi bilioni 16 wateja mbalimbali na kusisitiza kuwa Tanesco imepanga mikakati mipya ya ukusanyaji wa madeni hayo.
Alibainisha changamoto nyingine kuwa ni pamoja na wizi wa umeme, na madai ya fidia katika utekelezaji wa mradi wa umeme wa awamu ya kwanza uliokuwa unafadhiliwa na Wakala wa Umeme Vijijini (REA) na kuongeza kuwa wananchi walidai fidia iliyokuwa kubwa kuliko gharama za mradi.

MISA TANZANIA YAKUTANA NA MAAFISA HABARI KUJADILI CHANGAMOTO ZA UTOAJI TAARIFA

Afrika(MISATAN) Bwana Andrew Marawiti  akizungumza jambo wakati akifungua kongamano na maafisa habari wa taasisi za serikali zilizofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi wetu
Maafisa habari mbalimbali
kutoka wizara na mihimili tofauti ya nchi, jana walikutana katika hoteli ya JB
Belmont hapa Dar es Salaam kujadili changamoto wanazo kumbana nazo wakati kwa kutoa taarifa kwa wananchi.
Kongamano hilo linafuatia matokeo ya utafiti wa upatikanaji taarifa kwenye taasisi za umma uliofanywa na  Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) nakuzinduliwa rasmi siku ya tarehe 28 Septemba, ambayo pia ni Siku ya Kimataifa ya Haki ya Kupata  Taarifa.
Miongoni mwa taasisi  zilizoshiriki katika kongamano hilo ni Bunge, Mahakama, Wizara ya Katiba na Sheria, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Wizara ya Nishati na Madini, Idara ya Habari Maelezo, Mamlaka ya Taifa ya Vitambulisho (NIDA) na Idara ya Taifa ya Takwimu. Wizara za Afya na Mambo ya Nje hazikuweza kuwakilishwa licha ya kupata mwaliko. 
 Organization of Legal Assistance-nola)  Bwana James Malenga akisisitiza jambo alipokuwa anawasilisha mada yake kwenye kongamano hilo la maafisa habari wa taasisi za kiserikali lililoandaliwa na Misa-Tanzania.
Gasirigwa akitoa ufafanuzi kwenye mada aliyokuwa anaiwasilisha kwenye kongamano la maafisa habari wa taasisi za kiserikali(hawapo picha)  
anazozipata anapokuwa anakwenda taasisi na idara mbalimbali za serikali kupeleka barua ama maombi ya taarifa.
yake ilivyopokea Tuzo ya Kufuli na ambavyo imekuwa chachu ya mabadiliko katika kutoa taarifa kwa umma.
Nyantori akielezea changamoto za utoaji taarifa katika taasisi na idara za serikali.


Maafisa habari wakifuatilia kwa umakini mada ya Umuhimu wa Kutoa/Kupata
Taarifa serikalini kutoka kwa mwanasheria wa kujitegemea Bwana James Marenga.
Bwana Andrew Marawiti  akitoa shukrani wa wageni waliofika kwenye kongamano hilo.

NHC yaelezea namna ilivyosaidia vijana kupitia mradi wa ufyatuaji wa matofali na ujenzi wa nyumba za gharama nafuu

 Meneja wa Mkoa wa Tabora Bw. Erasto Chilambo,  akimpa maelezo ya ujenzi wa nyumba za gharama nafuu Mkuu wa Mawasiliano na Huduma kwa Jamii Bi Susan Omari alipotembelea mradi huo ulioko eneo la Isikizya Wilayani Uyui jana. (Picha kwa hisani ya Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa Jamii cha Shirika la Nyumba la Taifa)
 Mwonekanao wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC eneo la Isikizya Mkoani Tabora.
 Meneja wa Mkoa wa Tabora Bw. Erasto Chilambo akiendelea kutoa maelezo ya mradi kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii, Bi Susan Omari
 Nyumba 38 zilizojengwa karibu kabisa na Makao Makuu ya Wilaya ya Uyui eneo la Isikizya. Nyumba zingine 12 zimejengwa upande wa pili wa barabara eneo la Isikizya.
 Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii wa NHC, Bi Susan Omari akitoa maelekezo kwa Meneja wa Mkoa wa Tabora Bw. Chilambo
 Msimamizi wa mradi wa NHC isikizya Bw. Tokimu Mondo akitoa maelezo ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu eneo la Isikizya jana.
 Sehemu ya nyumba zilizojengwa katika mradi wa nyumba za gharama nafuu eneo la Isikizya Wilayani Uyui zinavyoonekana.
 Meneja wa Mkoa wa Tabora Bw. Chilambo akitoa maelezo kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii Bi. Susan Omari yanayohusu viwanja vya Shirika vilivyoko eneo la Itetemia Manispaa ya Tabora.
 Meneja wa Mkoa wa Tabora Bw. Erasto Chilambo akielezea hatua mbalimbali zilifikiwa na Mkoa huo za kutengeneza nyumba za Shirika. Hili ni mojawapo ya jengo la Hoteli ya Golden Eagle baada ya kufanyiwa matengenezo.
 Sehemu ya mtaa wa Jamhuri/Shule wenye nyumba zilizofanyiwa matengenezo makubwa na NHC Mkoa wa Tabora
 Mojawapo wa jengo lililofanyiwa matengenezo na NHC Mkoa wa Tabora linavyoonekana kwa sasa
Sehemu ya Maafisa Vijana wakisikiliza mada iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii wa NHC, Bi Susan Omari (hayuko pichani) alipoelezea mpango wa NHC wa kugawa mashine kwa ajili ya kusaidia vijana kwenye Halmashauri zote za Wilaya hapa nchini. Jumla ya mashine 656 zimeshambazwa kwa ajili hiyo.
 Washiriki wa semina iliyotolewa na NHC wakisikiliza mada kwa makini
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii wa NHC, Bi Susan Omari akitoa mada juu ya mpango wa NHC wa kusaidia vijana mashine za kufyatulia matofali katika Halmashauri zote za  Wilayanchini.
Mmoja wa washiriki wa semina hiyo akilishukuru Shirika la Nyumba la Taifa kwa uamuzi wake wa kizalendo wa kusaidia vijana mashine ili waweze kujiajiri alipochangia mada iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii wa NHC.
Katibu  Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, , Bibi Sihaba Nkinga akitoa maelezo wakati wa semina iliyotolewa na NHC mjini Tabora.

MKURUGENZI MKAZI WA UNESCO AMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA DODOMA

DSC_0206Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues (katikati) akiongoza na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mtungi (kulia) baada ya kuwasili ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi. Kushoto ni Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Bw. Al Amin Yusuph.
DSC_0209Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi akimkaribisha ofisini kwake Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues alipomtembelea na kufanya naye mazungumzo. Kushoto ni Msajili wa Vyama vya Siasa nchini. Jaji Francis Mtungi na kushoto ni Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Bw. Al Amin Yusuph na Nyuma kabisa ni Msajili Msaidizi kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Sisty Leonard Nyahoza.
DSC_0232Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Rehema Nchimbi alipomtembelea leo na kufanya nae mazungumzo juu masuala mbalimbali ya maendeleo likiwemo suala la elimu na changamoto zake katika mkoa wa Dodoma.
DSC_0237Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mtungi (wa pili kulia) akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi (kushoto), Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues (wa pili kushoto) pamoja na Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Bw. Al Amin Yusuph, Msajili Msaidizi kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Sisty Leonard Nyahoza walipomtembelea Mkuu huyo wa mkoa ofisini kwake leo.
DSC_0248Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues (wa pili kushoto) akitoa maelezo ya kazi mbalimbali zinazofanywa na shirika lake ikiwemo Mradi wa Micro Science Kits (MSKs) ulioendeshwa kwa miaka minne wa kusaidia ufundishaji wa masomo ya sayansi kwa kufanikisha majaribio ya maabara uliokuwa ukifadhiliwa na Shirika lake na kuendeshwa na Wizara ya Elimu nchini katika shule 180 zilizopo katika wilaya 34 ambao umemalizika hivi karibuni kwa mafanikio makubwa.
DSC_0280Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi katika picha ya pamoja na ugeni huo ofisini kwake mjini Dodoma leo.
DSC_0330Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues akisisitiza jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi alipokuwa akigana nae mara baada ya mazungumzo ofisini kwake mjini Dodoma.

SSRA yajipanga kuboresha Sekta ya Hifadhi ya Jamii.

Mkurugenzi  Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) Bi. Irene Isaka akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusu  hatua zilizochukuliwa na mamlaka hiyo katika kuboresha sekta ya Hifadhi ya Jamii hapa nchini. Kushoto ni Mkuu wa  Mahusiano na Uhamasishaji wa SSRA Bi. Sarah Kibonde Msika.
Mkurugenzi wa Huduma za Sheria kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) Bw. Ngabo Ibrahimu(Katikati)akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu maboresho ya Sheria ya Hifadhi ya Jamii na Miongozo iliyotolewa na Mamlaka hiyo inayolenga kuboresha sekta ya Hifadhi ya Jamii.Kushoto ni Mkuu wa Mahusiano na Uhamasishaji Bi. Sarah Kibonde Msika na Kulia ni Mkurugenzi wa Usajili na Matekelezo wa SSRA Bi. Lightness Mauki.
Mkuu wa Mahusiano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) Bi. Sarah Kibonde Msika akieleza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu Mikakati ya Mamlaka hiyo katika kutetea na kulinda maslahi ya wanachama ikiwemo kuboresha Kikokotoo cha Mafao ya Pensheni.Kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria kutoka SSRA Bw. Ngabo Ibrahimu.
Baadhi ya waaandishi wa habari wakiwasikiliza wawasilishaji kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) wakati wa Mkutano uliofanyika leo kwenye Ofisi za Mamlaka hiyo Jijini Dar Es Salaam.
Picha na Fatma Salum

Mkoa wa Katavi kuzindua kampeni ya kutokomeza magonjwa ya surua rubella

unnamed
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Rajabu Rutengwe akiongea na waandishi wa Habari ofisini kwake  hawapo pichani wakati akielezea mkoa kufanyakuzindua kampeni ya chanjo ya magonjwa ya surua na Rubella  kuzinduliwa leo nchini ambapo mikoa 16 inshiriki na katavi ikiwemo,katika mkoa wa Katavi zinafanyika Halmashauri ya wilaya ya Nsimbo.
………………………………………………………………
Na Kibada Kibada-Katavi.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi  Dkt Rajabu Rutengwe amesema Mkoa wa Katavi  kupitia  mpango  wa Taifa  wa chanjo  na  wadau  mbalimbali  utaendesha  kampeni  shirikishi ya  chanjo  dhidi  ya Surua Rubella, matone ya vitamin A, utoaji wa  dawa za minyoo na kinga dhidi  ya magonjwa yasiyopewa kipaumbele.
Akizungumza katika mkutano wa Waandishi wa Habari   Dkt Rajabu Rutengwe  ameeleza kuwa katika kampeni  hiyo chanjo ya  surua-rubella itatolewa kwa watoto wote wenye umri kati ya miezi tisa hadi miaka mitano.
Matone ya Vitamini A’yatatolewa kwa watoto wenye umri kati ya miezi sita na miaka mitano, dawa dhidi  ya minyoo itatolewa kwa watoto wenye umri kati ya mwaka mmoja na miaka mitano, kinga tiba dhidi ya matende, mabusha au ngiri maji na usubi kwa wenye umri wa miaka mitano na kuendelea.
Mkuu wa Mkoa alisema Kampeni ya Chanjo ya surua inaendeshwa ikiwa ni muendelezo wa utaratibu wa kufanya kampeni kila baada ya miaka mitatu, utaratibu huu unaotokana na ukweli kwamba baadhi ya watoto hukosa chanjo ya surua  katika utaratibu wa kawaida  ,pia watoto 15 kati ya 100 wanaopewa chanjo ya surua hawajijengei kinga ya mwili ya dhidi ya surua, hali hii husababisha kutokea milipuko ya surua.
Amesema Wizara ya Afya  na ustawi wa Jamii kupitia Mpango wa Chanjo imekuwa ikifanya ufuatiliaji wa ugonjwa wa surua,kila mtu anayejitokeza na dalili za surua sampuli huchukuliwa kwa ajili ya uchunguzi wa kimaabara,sampuli huchukuliwa kwa ajili ya uchunguzi wa kimaabara, Sampuli nyingi zilizochukuliwa zilithibitika kuwa ni ugonjwa wa Rubelle .
Akaongeza kuwa ugonjwa wa Rubella una dalili zinazofanana na surua ingawa husababishwa na vimelea  tofauti, njia za kuthibiti magonjwa haya mawili zinafanana ,kwa kuzingatia haya shirika la Afya ulimwenguni (WHO) liliamua kuunganisha chanjo ya surua na Rubella ili kuongeza ufanisi wa rasilimali na pia ni mkakati wa kidini kutokomeza surua na Rubella kwa pamoja ifikapo mwaka 2020.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Yahaya Husein anaeleza kuwa lengo kuu la kufanya kampeni hii ni kudumisha upungufu wa magonjwa ulemavu na vifo vinavyotokana na surua na Rubella,pamoja na kutoa matone yaVitamini A’na dawa ya kukinga ugonjwa minyoo tumbo,usubi,mabusha na matende,ngirimaji ili kutibu maradhi na kuimarisha afya.
Naye Katibu Tawala mkoa wa Katavi Mhandisi Emmanuel Kalobelo ameleza kuwa katika kampeni hiyo Mkoa wa Katavi umelenga kutoa chanjo ya surua –Rubella kwa watoto wapato 392,174,walengwa wa matone ya vitamin A’watoto 107,609,walengwa,wa kinga tiba dhidi ya magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ni watu 451,683,na walengwa wa dawa dhidi minyoo ni 95,652.
Huduma hizi zitatolewa katika vituo maalum ambavyo vitahusisha vituo vya kutolea huduma za Afya ,Shule za Msingi,Sekondari na maeneo mengine yaliyopangwa.