TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, May 26, 2012

Mkutano wa CHADEMA LEO





Umati wa wananchi wakiwa wamefurika Viwanja vya Jangwani.

ICD yazindua mtandao wa taarifa kuhusu walemavu

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Habari Kuhusu Ulemavu nchini Tanzania (ICD), Fredrick Mkatambo akizungumza na wageni waalikwa katika hafla hiyo. Kushoto ni Kamishna kutoka Wizara ya Ustawi wa Jamii, Danford Makala aliyekuwa mgeni.
 Baadhi ya wageni waalikwa na wafanyakazi wa ICD wakiwa katika hafla hiyo
Picha ya pamoja ya wafanyakazi wa ICD mara baada ya uzinduzi.
 
KITUO cha Habari Kuhusu Ulemavu (ICD) nchini Tanzania kimezindua mtandao (Blogu) ambayo itakuwa ikikusanya taarifa mbalimbali kuhusiana na masuala ya walemavu na kuziweka katika mtandao huo ili wadau anuai waweze kujua taarifa hizo.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam katika hafla ya uzinduzi wa mtandao huo ambao utakuwa ukisimamiwa na ICD, Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho, Fredrick Mkatambo amesema kwa muda mrefu imekuwa ni vigumu kupata taarifa zote juu ya masuala ya walemavu jambo ambalo ni moja ya vikwazo.
Alisema kuanzishwa kwa mtandao huo utasaidia wadau wa masuala ya walemavu ikiwemo Serikali kuingia na kupata taarifa mbalimbali zikiwemo changamoto inayokumbana nayo jamii hiyo na ikiwezekana wahusika kuwasaidia kundi hilo.
Aidha alisema “Najua kwa sasa kazi ni ngumu kupata taarifa muhimu juu ya masuala mbalimbali ya ulemavu…lakini naamini kwa sasa itakuwa ni rahisi maana tunasehemu ambayo unaweza kupata taarifa zote muhimu juu ya walemavu,” alisema Mkurugenzi.
Akifafanua namna mtandao huo utakavyokuwa ukifanya kazi, Mshauri wa Kiufundi kutoka kituo cha ICD, Natalia Lintner alisema katika blogu hiyo walemavu wanaweza kupata taarifa mbalimbali zinazowagusa kama ufadhili wa masomo, vyuo vikuu rafiki wa walemavu, matangazo muhimu yanayowagusa walemavu na habari za kawaida kuhusu watu wenye ulemavu.
Alisema taarifa nyingine ambazo zitakuwa zikioneshwa katika mtandao huo ni mashirika na taasisi mbalimbali zinazofanya kazi na watu wenye ulemavu na shughuli zake, pamoja na wadau anuai kuwa na uwezo wa kuchangia/kusaidia walemavu kupitia mtandao huo.
Naye Kamishna kutoka Wizara ya Ustawi wa Jamii, Danford Makala akizindua mtandao huo pamoja na kitabu cha ‘Maisha Yangu’ ambacho kimeandaliwa na ICD na wafadhili wengine, alisema mtandao na kitabu hicho vitakuwa ni vyanzo vizuri vya taarifa kuhusu watu wenye ulemavu.
Alisema mtandao huo ambao ni sawa na jukaa la taarifa kuhusu watu wenye ulemavu litaisaidia Serikali pia kupata taarifa anuai juu ya masuala ya watu wenye ulemavu, ambazo zitakuwa chachu ya maboresho ya sera mbalimbali kila uchao.
“Hii ni njia ambayo watu wenye ulemavu wanaweza kupaza sauti yao kwa pamoja…kwa kutumia mtandao huu, tujitokeze kuchangia basi ili kweli mtandao huu uweze kufanya kazi ipasavya,” alisema Makala.
Kitabu cha maisha yangu ambacho kimezinduliwa pia katika hafla hiyo kimekusanya mahojiano ya watu wenye ulemavu jijini Dar es Salaam nia kuainisha changamoto mbalimbali katika maisha yao, hivyo kuleta picha halisi ya walemavu Tanzania.
*Habari hii imeandaliwa na Mtandao wa Thehabari.com (www.thehabari.com)  

VIKUNDI VYA KUWEKA NA KUKOPA VINAVYOSAIDIWA NA TAASISI YA WAMA VYAPEWA SEMINA YA UMUHIMU WA KUJIUNGA NA MFUKO WA BIMA WA AFYA (NHIF)

 Tabu Likoko Mkurugenzi wa Idara ya Uwezeshaji Wanawake katika Taasisi ya (WAMA) akifungua rasmi semina ya wanawake kutoka vikundi mbalimbali vya kuweka na kukopa vinavyosimamiwa na Taasisi ya (WAMA) kuhusu huduma za Mfuko wa Bima wa Afya NHIF inayofanyika kwenye viwanja vya Taasisi ya WAMA asubuhi hii jijini Dar es salaam kutoka kulia  pichani ni Rehani Athumani Mkurugenzi mifuko ya Afya ya Jamii (CHF), Michael Mhando Mkurugenzi wa Tathmini ya Uhai wa Mfuko na Utafiti na Eugen Mikongoti Mkurugenzi wa Uendeshaji.
Eugen Mikongoti Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF) akizungumza katika semina hiyo jinsi mfuko huo unavyosaidia jamii kupata matibabu, kulia ni Rehani Athumani Mkurugenzi mifuko ya Afya ya Jamii (CHF) na katikati ni Michael Mhando Mkurugenzi wa Tathmini ya Uhai wa Mfuko na Utafiti na
 Afisa wa Masoko na Elimu kwa Umma NHIF Grace Michael akifuatilia mada katika semina hiyo, kushoto ni Philomena Marijani Afisa Uraghibishi na Mawasiliano Taasisi ya (WAMA).
Rehani Athumani Mkurugenzi mifuko ya Afya ya Jamii (CHF) akitoa mada mbalimbali juu ya huduma za mfuko wa bima ya Afya, huku washiriki wa semina hiyo wakimsikiliza kwa makini, katikati ni  Michael Mhando Mkurugenzi wa Tathmini ya Uhai wa Mfuko na Utafiti na kulia Eugen Mikongoti Mkurugenzi wa Uendeshaji.
 Washiriki wa semina hiyo wakiandika mambo muhimu yaliyojadiliwa katika semina hiyo inayofanyika katika viwanja vya Taasisi ya (WAMA).
Washiriki wa semina hiyo wakiandika mambo muhimu yaliyojadiliwa katika semina hiyo inayofanyika katika viwanja vya Taasisi ya (WAMA).
Washiriki wa semina hiyo wakiandika mambo muhimu yaliyojadiliwa katika semina hiyo inayofanyika katika viwanja vya Taasisi ya (WAMA).
 Tabu Likoko Mkurugenzi wa Idara ya Uwezeshaji Wanawake katika Taasisi ya (WAMA) kulia na Philomena Marijani Afisa Uraghibishi na Mawasiliano Taasisi ya (WAMA) ambao ndiyo wenyeji wa wanasemina wakiwa katika semina hiyo.

ZIARA YA NAPE BUKOBA MKOANI KAGERA

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimsalimia Mwenyekiti wa Chama Cha Walemavu wilaya ya Misenyi mkoani Kagera, Simon Andrea, baada ya kufungua Baraza la Vijana wa CCM wilaya hiyo, jana, May 25, kwenye Uwanja wa Mashujaa, wilayani humo. Waliosimama ni baadhi ya viongozi wa CCM na UVCCM walioshiriki ufunguzi huo.
Nape akiwa ka Katibu wa CCM mkoa wa Kagera Avelyne Mushi baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Bukoba, kuanza ziara a kikazi ya siku moja mkoani Kagera.
Nape akizungumza na viongozi katika Ofisi ya CCM mkoa wa Kagera.
Nape akitoa salam za Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kwenye msiba wa mtumishi wa siku nyingi waserikali,  Balozi, Dk. Vedasto Kyaruzi, mjini Bukoba, baada ya kwenda kwenye msiba huo wakati wa kuaga mwili wa marehemu tayari kwa mazishi yaliyofanyika jana mjini Bukoba.
Nape akikata utepe kuingia kwenye kambi ya Baraza la Umoja wa Vijana wa CCM, wilaya ya Missenyi mkoani Kagera, kwa ajili ya kufungua baraza hilo la mwaka.

Vijana wa CCM waliopiga kambi hiyo ya Baraza la Vijana, Missenyi, wakimsikiliza Nape alipowahutubia.
Nape  akimkabidhi cheti Kamanda wa Vijana wa CCM mkoa wa Kagera, Dioniz Malinzi kwa kuwa mmoja wa waliowezesha kambi hiyo ya Baraza la Vijana kufanyika.
Baadhi ya viongozi kwenye kambi hiyo wakimpungia mkono Nape wakati akiondoka

Rais Kikwete apokea ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Angola

Mjumbe maalum wa Rais wa Angola Dr.Andre de Oliveira Sango akiwasilisha ujumbe maalum kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu ndogo mjini Dodoma leo asubuhi(picha na Freddy Maro)

Mama Asha Bilal akizungumza na Watanzania wanaoishi Botswana

Mke wa  Makamu wa Rais Mama Asha Bilal, akiwa katika picha ya pamoja
na Watanzania wanaoishi nchini Botswana baada ya kuzungumza na
Watanzania hao jana jioni mjini Gaborone Botswana.
PICHA NA VPO.
Mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal akizungumza na Watanzania
wanaishi Nchini Botswana jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Mohammed Gharib
Bilal, akizungumza na Makamu wa Rais wa For Conervation Policy kulia
na Waziri wa Fedha wa Kenya Mhe. Robinson Njeru baada ya kumalizika
kwa mkutano wa siku mbili kwa wakuu wa nchi za Afrika kuhusu maendeleo
endelevu kwa nchi za bara la Afrika uliomalizika mjini Gaborone
Botswana jana jioni.

MBALI NA SHUGHULI ZA CHAMA PIA NAPE AKACHEZA GOFU KWENYE VIWANJA VYA DIONIZ MALINZI

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akiwasili na ujumbe wake kwenye Uwanja wa ndege wa Bukoba, kwa ajili ya ziara ya siku moja ya kikazi mkoani Kagera ambako pamoja na shughuli nyingine alifungua Baraza la Vijana wa CCM, Wilaya ya Missenyi mkoani humo.
Nape alipata fursa pia kucheza gofu kwenye viwanja vya mchezo huo vya Dioniz Malizni (kulia) nje kidogo ya mji wa Bukoba

RAIS KIKWETE KUFUNGUA MKUTANO WA AFDB AMBAO UTAGARIMU BILIONI 12


Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkutano wa (AFDB) Bw. Ngosha Magonya  katikati akiongea na waandishi wa habari mapema leo jijini Arusha.
Baadhi ya wanakamati wa kamati ya maandalizi ya mkutano wa AFDBwakiwa katika viwanja vya AICC jijini Arusha leo.
NA GLADNESS MUSHI-ARUSHA
 Benki ya maendeleo ya Afrika (AFDB)inatarajia kutumia kiasi cha Shilingi bilioni 12 katika mkutano wake unaoanza Jumatatu jijini Arusha na kufunguliwa na Raisi Jakaya Kikwete  huku kiasi cha fedha hizo zikitumika kukarabati Kumbi mbalimbali za jengo la Kimaitaifa la ukumbi wa AICC kwa kuwa baadhi ya kumbi za jengo hilo zinaonekana kupitwa na wakati kutokana na utandawazi uliopo kwa sasa ndani ya nchi zilizoendelea
Akizungumza jijini hapa na waandishi wa habari mwenyekiti wa kamati ya kitaifa ya mkutano wa benki ya AFDB kwa mwaka 2012 Bw Ngosha  Magonya  ambapo alisema kuwa mkutano huo utakuwa na faida kubwa sana

Alifafanua kuwa kupitia mkutano huo ambao utaanza Jumatatu ijayo utakuwa na faida kubwa sana kwa jiji la Arusha kwa kuwa hata kiwango cha uchumi kitaaimarika sana kwa kuwa wageni mbalimbali kutoka katika maeneo ya nchi mbalimbali duniani watabadilishana hata uzoefu

“kwa kipindi hiki ambacho kuna mikutano ndani ya jiji la Arusha tunatarajia kuwepo na utoafuti wa khali ya juu sana hasa katika mchakato wa uchumi na kwa hali hii pia tunatarajia hata kufanya maendeleo mbalimbali  ikiwemo kufanya marekebisho kwa jengo la kimataifa la AICC”alisema bw Magonya

Katika hatua nyingine alifafanua kuwa mbali na kuweza kuimarisha uchumi wa mkoa wa Arusha pia wanatarajia kutumia fursa mbalimbali za kuhakikisha kuwa wanakutanisha wafanyabiashara mbalimbali huku malengo yakiwa ni kuendeleza uchumi kwa walengwa.

Pia alifafanua kuwa mbali na kuweza kuwasaidia wafanyabiashara hao katika michakato ya kukuza uchumi pia benki hiyo ina mikakati mbalimbali ya kuendeleza barabara ambazo zitaweza kutumika kama njia ya mawasiliano hapa Tanzania hali ambayo nayo itachangia kwa kiwango kikubwa sana hata kuimarisha uchumi wa nchi ya Tanzania

Aliongeza kuwa hapo awali benki hiyo ilikuwa imeshajenga barabara ya Arusha –Namanga kwa sasa ana mpango wa kujenga barabara ya Arusha – Holile ndani ya Mkoa wa Kilimanjaro hali ambayo itachangia sana maendeleo hasa ya mawasiliano

Alimalizia kwa kusema kuwa wafanyabiashara hasa wa mkoa wa Arusha wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanatumia vema fursa za mkutano huo ili kuweza kuimarisha biashara zao za kila siku.

SERIKALI YATAKIWA KUJENGA VYUO ZAIDI KWA AJILI YA KUTOA WALIMU WA WATOTO WENYE ULEMAVU

MWANDISHI WETU
 
SERIKALI imetakiwa kujenga Vyuo vitakavyozalisha walimu wakutosha kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa ‘Viziwiwasiona’.
Kauli hiyo ilitolewa jijini  Dar es Salaam leo , na Mwalimu wa Kitengo cha walemavu katika shule ya Uhuru Mchanganyiko, Anjelica Mtwale wakati alipokutana Mwakilishi Mkazi wa Shirika la ‘Sense International’ lenye makao yake makuu nchini Uingereza.
Alisema pungufu huo wa walimu maalum umetokana na kukosekana kwa vyuo vya kutosha, ambavyo vingesaidia kutoa taaluma hiyo na kupatikana walimu wengi ambapo wangetumika kutoa elimu kuanzia elimu ya awali hadi elimu ya juu.
Aidha, Anjelica alisema kutokana na baadhi ya wazazi kupata mwamko wa kuwapeleka watoto hao shule kwa ajili ya kupata elimu, bado kitengo chake kinashindwa kumudu kutoa mafunzo  kwa kiwango kinachohitaji kutokana na upungufu huo.
“Unajua katika kuwaelimisha watoto hawa yani Viziwiwasiona kunahitajika walimu wa kutosha kwa kuwa uelimishaji wao ni kwamba kila mtoto mmoja mwalimu mmoja”alisema Mwalimu Anjelica.
Anjelica alisema katika shule hiyo, kuna wanafunzi 13 huku walimu wakiwa 8 na walezi wa kujitolea wanne ambapo kwa utaratibu mzima wa kuwatuza watoto hao hawatoshi.
Akitaja mafanikio tangu kuanzishwa kitengo hicho mwaka 1994, Anjelika alisema wapo watoto waliofanikiwa kupata elimu ya sekondari hadi kidato cha pili, kuishia kidato hicho kumetokana na kukosekana walimu wenye elimu hiyo ya watu maalumu katika shule mbalimbali.
Aidha, Anjelica alitoa shukran kwa shirika la Sense International  kwa kushiriki katika kutoa misaada mbalimbali ya kielimu na afya kwa watoto hao.
Alisema Shirika hilo limekuwa la kwanza nchini katika kujishughulisha katika utoaji wa mafunzo kwa walimu wa watu wa aina hiyo pia limehusika katika kuwapeleka walimu katika mafunzo ndani na nje ya nchi.
Naye Mwakilishi Mkazi wa Shirika hilo, Christopher Andendekisye alisema Shirika hilo limekuwa likifanya shughuli zake kwa kushirikiana na serikali.
Alitoa wito kwa Watanzania kuwafikiria watu hao kwa huruma kwani ni watu wenye ulemavu wakusikitisha, alisema “Hebu fikiria mtu huyo haoni hasikii na hawezi kusema hivyo ni wakati kwa baadhi ya taratibu za upatikanaji wa elimu ya walimu kuekebishwa ili iwe rahisi katika kupatikana walimu  wingi”

Hatimaye Redd's Miss IFM huyu hapa

 
Redds Miss IFM -Fina  Revocatus katikati akiwa na mshindi wa pili Jane Augustino na mshindi wa tatu Theresia Issaya wakiwa katika Picha ya Pamoja baada ya  kuibuka washindi katika fainali za Redds Miss Tanzania ngazi ya Vitongoji iliyofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar Es Salaam.Ambapo watashiriki fainali ya ngazi ya kanda ya Dar Es Salaam.

USHINDI WA CHADEMA UBUNGO

MAJIRA - GAZETI HURU LA KILA SIKU:



Posted: 25 May 2012 12:37 AM PDT

Posted: 25 May 2012 12:35 AM PDT

JANA Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam,ilitoa hukumu ya kesi iliyokuwa imefikishwa mbele yake na aliyekuwa mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bi. Hawa Ng'umbi, akipiga matokeo yaliyompa ushindi Mbunge wa Jimbo la Ubungo,Bw. John Mnyika.

Hukumu hiyo ilisomwa na jaji Bi. Upendo Msuya, na  kubainisha kuwa mdai katika kesi hiyo ameshindwa kuithibitishia mahakama pasipo kuacha shaka juu ya madai aliyokuwa akiyalalamikia.  Kesi ya kupinga matokea
zisifunguliwe kwa jazba

Jaji Msuya alisema kuwa katika madai hayo ushahidi wa mashahidi wa mdai haukuwa na nguvu na kwamba mdai hakuleta mashahidi wa kuunga mkono madai  yake.

Hii ni moja kati ya kesi nyingi ambazo zimefunguliwa na baadhi ya wabunge wakipinga matokeo dhidi ya wapinzani hao. Tunakumbuka wakati uchaguzi ulipomalizika aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusuf Makamba, aliwataka wagombea wote wa chama hicho walioshindwa kufungua kesi za kupinga matokeo kwa ahadi kuwa chama kitawasaidia.

Ahadi hiyo ya Bw. Makamba inatufanya tuamini kuwa iliwafanya baadhi ya wagombea wa chama hicho walioshindwa kufungua kesi hata kama hawakuwa na ushahidi wa kutosha.

Japokuwa ni haki yao ya msingi kufanya hivyo,lakini kesi zinazotupiliwa mbali na mahakama zinatakiwa kuwa ushahidi kwetu kuwa baadhi yao walifungua kesi kwa shinikizo, bila ushahidi wa kutosha.

Mfano mzuri ni kama kesi hiyo ambayo hukumu iliyotolewa jana. Kesi kama hizi mara nyingi zinafunguliwa kwa jazba bila watu kutafakari,

Kwa msingi huo tunaiomba Serikali sasa ifikiri upya namna ambavyo inaweza kutunga sheria itakayosaidia kuwabana watu wanaokimbilia mahakamani kufungua kesi baada ya kushinda bila kuwa na ushahidi wa kutosha.

Tunasema hivyo kwa kutambua kuwa Serikali inatumia fedha nyingi kuendesha kesi za aina hiyo. Wote tunakumbuka kuwa kuna wakati mahakama ilikwama kusikiliza kesi hizo kutokana na uhaba wa fedha, lakini baada ya mahakama kulalamika ilitoa fungu hilo ili zianze kusikilizwa.

Lakini baadhi ya kesi zinaonekana hazikuwa na kichwa wala miguu, matokeo yake zimesababisha fedha za walipa kodi kupote, ambapo zingetumika kwa ajili shughuli zingine za maendeleo.

Tunatoa mwito itungwe sheria yenye meno makali itakayosaidia kuwabana wanaoshindwa na kukimbilia mahakamani bila kuwa na ushahidi wa kile wanachokidai. Kwa kufanya hivyo tutaokoa fedha za wananchi zinazotumika kuendesha kesi hizo.
Posted: 25 May 2012 12:34 AM PDT

Kaimu Mkurugenzi wa Idala ya Kinga katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Geoffrey Kiangi, akizungumza wakati akifungua warsha ya siku moja kwa waandishi wa habari (hawapo pichani), Dar es Salaam jana, iliyohusu mafunzo ya uelewa wa ugonjwa wa Malale unaoambukizwa na Mbung'o. (Picha na Charles Lucas)
Posted: 25 May 2012 12:29 AM PDT


Na Stella Aron

NI miaka mingi sasa tangu kupata uhuru, kumekuwa na harakati mbalimbali za kuwawezesha wananchi kutambua ama kushiriki mambo mbalimbali ya kuboresha maisha ya jamii.

Serikali na asasi zisizo za kiserikali zimeshiriki kwa namna moja au nyingine katika kuendesha harakati hizo.

Pamoja na mafanikio mbalimbali yaliyopatikana katika kuhamasisha wananchi, bado kuna mambo mengi  ambayo yanahitaji kufanyiwa kazi zaidi hasa katika kipindi hiki cha utandawazi pamoja na kukabiliana na mfumo wa soko huria.


Bi. Mayrose Majinge ni mwanaharakati mwenye elimu ya juu anazungumzia zaidi kuhusiana na nini Watanzania wanahitaji katika kuboresha na kupatikana kwa maendeleo nchini na hasa katika kipindi hiki cha utandawazi pamoja na kukabiliana na mfumo wa soko huria.

Anasema harakati za kuwahamasisha vijana wajue namna ya kukabiliana na umaskini itasaidia ili kuwawezesha kuendana na utandawazi na kukabiliana na mfumo wa soko huria.

Mwanaharakati huyo anasema kuwa, asilimia kubwa ya watanzania bado wanafikiri kwamba jitihada za kuleta maendeleo ni jukumu la serikali peke yake kwani ni tofauti na mtazamo walionao wananchi wa mataifa mengine yaliyoendelea kwani hilo ni jukumu la kila mtu katika nafasi yake.

Bi. Mayrose anasema,  mwananchi ana uhuru wa kuchangia mawazo yake katika kuboresha mipango ya maendeleo bila ya kuvunja sheria za nchi. Anasema kuwa ili mwananchi aweze kuwa huru zaidi sasa imefika wakati wa kila mtu kushiriki vema katika mchakato wa uandaaji wa katiba mpya.

Anasema kuwa kwanza Rais Jakaya Kikwete anapaswa kupongezwa kwa kukubali kubadilishwa kwa katiba na kuunda kwa tume ya watu 30 iliyo chini ya Jaji Joseph Warioba kwa ajili ya kukusanya maoni kwa wananchi kuhusiana na mabadiliko ya Katiba mpya.

Kuundwa kwa tume hiyo kumeleta sura mpya miongoni mwa wananchi kutokana na kilio cha muda mrefu ambapo wengi walikuwa wakilia na baadhi ya vipengele ambavyo inadaiwa kuwa vimepitwa na wakati na vinatakiwa vifanyiwe marekebisho kulingana na wakati tuliopo sasa.

Historia ya Katiba yetu tuliyonayo hivi sasa, inaonyesha kulikuwa na ushirikishwaji hafifu wa wananchi. Hii inaanza kujidhihirisha tangu kupatikana kwa uhuru Katiba ya kwanza iliandikwa na Waingereza na kuikabidhi kwa serikali ambao ni wazalendo jambo ambalo lilionyesha kuwa katiba hiyo ilisheheni mapendekezo ya upande mmoja.

Katiba hiyo ilionyesha dhahiri kumkera Mwalimu Julius Nyerere kutokana na muundo wa uongozi ambapo mwaka 1962 aliifuta na kuiunda upya huku ikionyesha kumpa zaidi yeye madaraka badala ya ile ya awali ambayo watawala wa juu walikuwa ni Waingereza na yeye alikuwa kama ni Waziri Mkuu.

Kwa historia hii inaonyesha kuwa maamuzi hayo yalikuwa ni ya busara lakini hayakuwashirikisha wananchi ambao ndiyo wadau wakuu wa katiba hiyo.

Pia tume maalum ya Katiba iliyoundwa mwaka 1977 chini ya uongozi wa Sheikh Thabit Kombo na Pius Msekwa nayo ilionyesha kutokukidhi matakwa ya wananchi kwa kuwashirikisha vya kutosha katika kuchangia na kutoa maoni yao ya nini wanakihitaji na hawakitaki.

Katiba ya sasa, maana yake ni kwamba sasa tunafungua ukurasa mpya ambapo wananchi watashirikishwa tofauti na Katiba zilizopita ili kuondoa malalamiko na mapungufu yasiyo na lazima ambayo kwa kiasi fulani yamekuwa yakichangia kila kukicha kuibuka kwa mizozo isiyo ya lazima.

Wananchi ndiyo wenye Katiba hivyo wanapaswa kushirikishwa tangu mwanzo wa mchakato hadi mwisho, tukiangalia historia ya nyuma mwaka 1992, Rais mstaafu Ally Hassan Mwinyi aliunda Tume ya kuratibu maoni kuhusu mfumo wa vyama vingi vya siasa, tume hiyo iliyoongozwa na Jaji Francis Nyalali, ilifanya kazi na kutoa matokeo kwamba asilimia 80 ya Watanzania hawataki mfumo wa vyama vingi.

Bi. Mayrose anasema kuwa mbali ya mapungufu yaliyopendekezwa kufanyiwa marekebisho, Serikali ilikubali mfumo wa vyama vingi lakini ikaendelea kuzikumbatia sheria ambazo zinaonyesha zimepitwa na wakati.

Wakati ule pia Rais Mstaafu Benjamin Mkapa naye aliunda Tume ya Jaji Robert Kisanga ya mwaka 1998 ambapo baada ya kukusanya maoni hayakufanyiwakazi na serikali kwa madai kuwa tume hiyo imevuka mpaka.

Pia mwaka 2006 rais Mkapa aliunda Tume ya kuchunguza tatizo la rushwa nchini  chini ya Jaji Joseph Sinde Warioba mbali ya mapendekezo ya mchakato mzima ya nini kifanyike ili kukomesha tatizo hilo, mapendekezo hayo hayajashughulikiwa ipasavyo hadi leo rushwa imeota mzizi na inaendelea kulitafuna taifa.

Anasema kuwa ana imani kuwa kwa tume iliyoundwa hivi sasa itakuwa ni kwa ajili ya maslahi ya wananchi na taifa kiujumla hivyo kilichobaki kwa wananchi ni kutoa maoni yao bila ya woga kwani ni kwa faida yao. Na anaamini kwa dhamira aliyonayo Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete atasimamia vema mapendekezo yote yatakayotolewa na Tume ya Katiba.

Mwanaharakati huyo anaendelea kusema kuwa Watanzania wanapaswa kuelewa kuwa rais ndiye mkuu wa nchi hivyo anapaswa kuheshimiwa hata kama atakuwa amemteua mtu mwenye umri mkubwa zaidi yake.

"Huyu anapaswa kuheshimiwa hata kama kuna mtu mwenye umri mkubwa zaidi yake kwani ndiye mwenye mamlaka ya juu zaidi ndani ya nchi yetu,' 

Aliongeza "Rais anapaswa kupewa nguvu zaidi na ulinzi kwani ndiye mkuu wa nchi na asije akatokea mtu mwingine akawa mkuu zaidi yake na hiyo ni kwa ajili ya usalama wake ili isifike mahala akawa hana mamlaka ya kutoa maamuzi kwa baadhi ya vitu kwani taifa litakuwa lisilo kuwa na nguvu ya kutosha, " alisema.

Akizungumzia kuhusiana na matumizi ya lugha ya Kiswahili, anasema kuwa sasa ifike mahala kiswahili kitumike kwenye mikutano yote bila ya kujali ni mikutano ya kitaifa.

Anasema kuwa ni bora sasa kukawa na watu maalumu watakaokuwa wakifanyakazi ya kuwafundisha wageni lugha ya kiswahili badala ya kutumika lugha ya kiingereza.

Kutokana na kujali lugha ya kiingereza hivi sasa kwenye mikataba kumekuwa na utumikaji wa lugha ya kiingereza huku lugha yetu ikibaki nyuma kama mapambo.

Mwanaharakati huyo anasema kuwa ana imani kuwa kama Serikali itasimamia suala hilo kwa kushirikiana na Baraza la Kiswahi Tanzania (BAKITA) lugha hiyo inaweza kuendelea zaidi kuwa chimbuko la maendeleo.

Aidha mwanaharakati huyo amewashauri wanawake kujitokeza kwa wingi katika utoaji wa maoni kwenye katiba ili kwenye mapungufu yaweze kurekebishwa na kuwepo kwa uwiano sawa.

Anasema kuwa maendeleo ya taifa hili yanatokana na mwanamke kwani katika familia mwanamke anapokuwa ameyumba kwa asilimia moja kuhusiana na hali ngumu ya maisha basi mwanaume atakuwa na asilimia 2.

Aidha mwanaharakati huyo amewashauri wanaharakati wote nchini watilie mkazo suala la kila Mtanzania  kwa nafasi yake kutimiza wajibu wake kikamilifu, kwani kazi ndio msingi wa kupata haki zote kwani itaweza kusaidia kuwakomboa Watanzania ambao baadhi yao wanakabiliwa na hali ngumu na kupatikana kwa maendeleo nchini.
Posted: 25 May 2012 12:28 AM PDT

                                                      Bi. Mayrose Majige








Posted: 25 May 2012 12:22 AM PDT


Na Florah Temba, Kilimanjaro

JAMII imetakiwa kuondokana na mitazamo potofu juu ya watu wenye ulemavu, pamoja na kuzingatia mahitaji ya watu hao wakati wa ujenzi wa miundombinu ili kuwawezesha kupita kwa urahisi pasipo usumbufu.

Rai hiyo ilitolewa na Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu Tanzania (SHIVIWATA) mkoani Kilimanjaro wakati wa mafunzo ya kuvijengea uwezo vyama  vya watu wenye ulemavu Manispaa ya Moshi ambapo walijadili mambo mbalimbali ikiwemo vikwazo na mitazamo hasi iliyojengeka katika jamii juu ya watu wenye ulemavu.

Katibu wa shirikisho hilo mkoani Kilimanjaro Bw. Zacharia Masawe alisema walemavu katika mkoa huo na nchini kote wanakabiliwa na changamoto kubwa ya mtazamo hasi ambapo wamekuwa wakionekana kuwa ni watu ombaomba na watu wasioweza kufanya chochote jambo ambalo si sahihi.

Alisema, mitazamo hiyo katika jamii imekuwa ikisababisha walemavu kudharaulika na kukosa haki zao za kimsingi ikiwemo elimu ambapo hata wakati mwingine hukoseshwa haki ya msingi ya kuishi kwa kuuawa.

“Kumekuwepo na mitazamo hasi katika jamii kuhusiana na sisi watu wenye ulemavu, kwani katika jamii tumekuwa tukionekana kuwa sisi ni watu ombaomba na hata wakati mwingine unakuta unakwenda katika ofisi ya kiongozi ikiwemo za serikali, lakini unapotaka kumuona kiongozi huyo unashangaa unaletewa sh. 500 na kuambiwa uondoke kwa kweli hii ni udhalilishaji na uonevu kwetu sisi,” alisema Bw. Masawe.

Bw. Masawe alisema ufike wakati sasa jamii ibadilike na iwaone walemavu kama watu wengine ambao wanahitaji kuthaminiwa, kuajiriwa na wasiwanyanyapae kwani hakuna mtu aliyezaliwa na kutaka  kuwa mlemavu.

Kwa upande wake Bw. Rumisha Masam alisema walmavu wamekuwa wakikumbana na vikwazo mbalimbali ikiwemo miundombinu mingi kujengwa pasipokuzingatia mahitaji ya watu wenye ulemavu.

“Jamii kwa saa inapaswa kuthamini watu wenye ulemavu na kuondokana na ile dhana kuwa walemavu ni watu wa kusaidiwa na hawana msaada wowote kwa jamii na sasa ibadilike na iwathamini kwani walemavu ni watu kama watu wengine na wanaweza kufanya kazi endapo wataendelezwa, lakini pia ihakikishe miundombunu yote inayojengwa inazingatia mahitaji yao,”alisema Bw. Rumisha.

Aidha aliongeza kuwa ili kuwawezesha walemavu kuweza kuondokana na hali ya utegemezi katika jamii serikali iweke mpango mkakati maalumu wenye upendeleo chanya ili kupanua soko la ajira kwa watu wenye ulemavu hapa nchini.
Posted: 25 May 2012 12:19 AM PDT
Bibi akiwa na wajukuu zake walioacha baada ya mtoto wake wa kike kukimbiwa na mume.Ukatili unaofanywa na wanaume kutelekeza familia umekuwa kikwazo kwa maendeleo ya wanawake wengi.
Posted: 25 May 2012 12:09 AM PDT

 Na Reuben Kagaruki

MWAMKO wa wazazi kutambua umuhimu wa elimu unazidi kuongezeka nchini, ikilinganishwa na miaka ya nyuma. Umuhimu wa elimu kwa watoto umechangia uwekezaji katika sekta hiyo kuongezeka kwa kasi ya aina yake. Jambo hili ni kati ya mambo ya kujivunia.

Watu binafsi, mashirika ya dini na wadau wengine wameonesha wazi kusaidia juhudi za Serikali za kuinua elimu nchini. Kinachotia moyo zaidi wazazi wengi kuhitaji watoto wao wapate elimu bora si bora elimu.

Kwa kufahamu hilo, wazazi wamekuwa wakihaha kutafuta shule bora za kusomesha watoto wao hasa zile zitakazokidhi matakwa wanayohitaji. Mfano, miaka ya nyuma kulikuwa na kasi kubwa ya wazazi kupeleka watoto wao kusoma nje ya nchi.

Mfano mzuri ni kwenye nchi za Uganda na Kenya. Kasi hiyo inazidi kupungua baada ya shule zinazoanzishwa nchini kukidhi viwango ambavyo wazazi wengi wanahitaji. Katika eneo hili tunastahili kuipongeza Serikali kwa kufungua milango ili watu wawekeza katika sekta hiyo.

Kuanzishwa kwa shule hizo pia kumesaidia kuwapunguzia wazazi gharama, kwani awali walikuwa wakitumia fedha nyingi kwenda kusomesha watoto nje ya nchi.

Kinachodhihirisha kuwa shule zenye ubora zipo nchini ni matokeo ya mitihani yaliyotangazwa jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Mkoa wa  wa Dar es Salaam  ulitangaza shule 10 bora zilizofanya vizuri zaidi katika mtihani wa kumaliza darasa la saba mwaka 2011, ambapo Tusiime iliyopo Tabata iliongoza kimkoa.

Katika matokeo hayo rasmi ya Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam shule hiyo ilikuwa ya kwanza baada ya kufaulisha wanafunzi wake wote 139 waliofanya mtihani wa kuhitimu darasa la saba mwaka jana.

Matokeo hayo rasmi yanaonesha shule zilizofuatia kimkoa ni St Joseph,
Montfort, Masaka, Filbert Bayi, Azanaki, Mountain Hill,  Hollycross,
Moga na Canossa. Matokeo hayo yalitangazwa rasmi wakati wa mkutano kati ya Ofisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Benard Makali na Maofisa Elimu na walimu wakuu wa shule za msingi jijini Dar es Salaam.

Bw. Makali anasema matokeo rasmi yanaonesha kuwa shule ya Tusiime iliyopo Tabata ndiyo imekuwa ya kwanza kimkoa kwa  kufaulisha
wanafunzi wote wa shule ya msingi kwenye mitihani ya kumaliza darasa
la saba mwaka 2011.

Katika matokeo ya Wilaya ya Ilala Tusiime pia imekuwa ya kwanza
ikifuatiwa na shule za St Joseph, St Theresoflisieux, African, Agens
Michael, Mkoani, Boma, Christ The King, Al Madrasa-Tus Asaifiya na New Ambasador.

Akifafanua kuhusu taarifa ambazo zimekuwa zikiwachanganya Watanzania
kuhusu baadhi ya shule jijini Dar es Salaam kujitangaza kwamba
zimekuwa za kwanza kiwilaya na kimkoa wakati sio kweli, anasema; "Nitazichunguza shule hizo na kuchukua hatua."

Bw. Makali alionesha kuchukizwa na tabia ya shule hizo na aliahidi
kufuatilia taarifa hizo na itakapobainika kwamba ni kweli, hatua kali
zitachukuliwa kwa shule husika ili iwe fundisho.

“Mimi sitambui matokeo mengine zaidi ya haya yanayoonesha kuwa
Tusiime ndiyo imeongoza kimkoa na kiwilaya, hao wanaojitangaza kwenye vyombo vya habari kuwa wamekuwa wa kwanza hayo matokeo wameyatoa wapi? Huu ni uongo wa hali ya juu na itabidi nifanyie kazi tabia hii ili Watanzania wasiendelee kupotoshwa,” alisema.

Katika matokeo rasmi ya Wilaya ya Kinondoni shule 10 bora
ni Filbert Bayi ambayo ndiyo imekuwa ya kwanza ikifuatiwa na Drive Inn, Ali Hassan Mwinyi Elite, Sunray, Msisiri ‘B’, Sunrise, Sahara,
Mirambo, Bethel Mission na Anininduni.

Temeke shule ya kwanza ni Montfort, Hollycross, Al-Hikma,
Fraylouisamigo, Shalom, Chang’ombe, Minazini, St Marys International,
Kurasini na Mivinjeni.

Kutokana na kufanya vizuri zaidi, Manispaa ya Ilala jijini Dar es
Salaam, iliiipa tuzo maalum shule ya Tusiime kwa kufanikiwa kufaulisha wanafunzi.

Tuzo hiyo ilitolewa hivi karibuni na manispaa hiyo kwa mkuu wa shule
hiyo, kama ishara ya kutambua mchango wa shule hiyo katika kukuza elimu nchini.

Bw. Makali, alisema shule ya Tusiime inastahili kupewa tuzo hiyo maalum kutokana na kufaulisha wanafunzi wote na kwa kuwa ya kwanza kimkoa miaka miwili mfululizo.

“Wamekuwa wa kwanza kimkoa kwa miaka miwili mfululizo na tuzo
waliyopata ni kutokana na kufaulisha wanafunzi wote kwa asilimia 100,
haya ni mafanikio makubwa kielimu nawapongeza,” alisema.

Mwalimu wa taaluma wa shule hiyo, Bw. Philibert Simon, anasema wanafunzi 19 walichaguliwa kujiunga na shule za vipaji maalum.

Alitaja baadhi ya shule za vipaji maalum walizochaguliwa wanafunzi hao kujiunga nazo kuwa ni Ilboru, Kibaha, Tabora Boys, Mzumbe, Ifunda Ufundi na Iyunga Ufundi.

Aliongeza kuwa si mara ya kwanza kwa shule hiyo kupewa tuzo ya aina hiyo, kwani Julai 2010 ilipewa tuzo ya aina hiyo na manispaa hiyo hiyo kwa kufaulisha wanafunzi kwa daraja A mwaka 2009.

“Siri ya mafanikio ni uongozi wa shule kutoa  ushirikiano wa kutosha
kwa walimu, wazazi kwa upande wao wamekuwa wakitimiza wajibu wao na
haya ndiyo  yametufikisha hapa tulipo,” anasema.

Anasema mazingira mazuri ya shule nayo yamekuwa na mchango mkubwa
katika kuhakikisha wanafunzi wanapata muda wa kutosha wa kusoma na
kushiriki michezo mbalimbali.

"Tunaamini kwamba matokeo haya hayakuja kwa bahati mbaya, bali
kumetokana na moyo wa kujituma kwa wanafunzi na walimu wao.
Kufaulisha wanafunzi wote si jambo la bahati kwani tumeshuhudia shule
nyingi zikifelisha nusu ya wanafunzi katika mitihani ya mwisho," anasema.

Hakuna shaka kwamba ufaulu huo mkubwa umetokana na jitihada za walimu
kufuatilia wanafunzi kuhakikisha wanafuata misingi ya masomo na
kujisomea ili waweze kufanya vyema.

Anasisitiza kuwa walimu wa shule zingine nao wanapaswa kuwa na moyo wa uzalendo kwa kufundisha kwa ari na moyo wa kujituma ili kuboresha elimu nchini.

Anaongeza kuwa pamoja na mazingira magumu ya baadhi ya walimu kwenye shule mbalimbali hasa za serikali wajitaidi kusahau ugumu huo na kufanya kazi kwa bidii na maarifa ili kuinua kiwango cha taaluma.

Hata hivyo anakiri kuwa mazingira ya shule nayo yanachangia kwa kiasi kikubwa kiwango cha ufaulu kwa shule za binafsi na za Serikali
zinapaswa kuiga mfano huo.

Anasema vifaa vya kujifunzia kama maabara navyo vina nafsi yake, kwani mwanafunzi kujifunza bila vitendo haiwezi kumsaidia siku za usoni.

Mwanafunzi akiambiwa kuhusu kifaa sayansi ili aweze kukielewa
vyema ni muhimu zikawepo maabara za shule hiyo ili kuhakikisha
wanapata ufahamu wa hali ya juu.
Posted: 25 May 2012 12:08 AM PDT


Wananfunzi wakifuatilia moja ya matukio yaliyohusu mijadala ya elimu.
Posted: 24 May 2012 11:59 PM PDT

Na Mwali Ibrahim

NAIBU Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amos Makalla jana alikabidhi bendera ya taifa kwa timu ya taifa ya Wanawake ,Twiga Stars, kabla ya kuelekea Ethiopia kwa ajili ya Fainali za Nane za Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC), zitakazofanyika Novemba mwaka huu, Equatorial Guinea.

Twiga Stars waliondoka nchini jana saa 11 jioni  kwa ndege ya Shirikia la Ndege la Ethiopia, kikosi hicho kikiwa na msafara wa watu 24 wakiwemo wachezaji, benchi la ufundi na viongozi itacheza na Ethiopia katika mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya mchujo kwa ajili ya fainali hizo, ambapo mechi yao inatarajiwa kuchezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Addis Ababa, kabla ya kurudiana wiki mbili baadaye Dar es Salaam.

Timu ya Twiga Stars ikifanikiwa kuitoa Ethiopia itakuwa imepata tiketi ya kwenda Equatorial Guinea.

Wachezaji walioondoka na kikosi hicho ni Amina Ally, Asha Rashid (nahodha), Ester Chabruma, Ettoe Mlenzi, Evelyn Sekikubo, Fadhila Hamad, Fatuma Bashiri, Fatuma Khatib, Fatuma Mustafa, Fatuma Omari, Maimuna Said, Mwajuma Abdallah, Mwanahamisi Omari, Mwanaidi Tamba, Mwapewa Mtumwa, Rukia Hamis, Semeni Abeid na Zena Khamis.

Kwa upande wa Benchi la Ufundi ni Charles Mkwasa (Kocha Mkuu), Nasra Mohamed (Kocha Msaidizi), Furaha Francis (Meneja wa Timu), Mwanahamisi Abdallah (Mtunza Vifaa) na Christina Luambano (Daktari wa Timu).

Twiga Stars ambayo msafara wake uliongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu kwa Wanawake Tanzania (TWFA) ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Lina Mhando itarejea nyumbani siku moja baada ya mchezo huo  saa 6 mchana kwa ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia.

Kabla ya mechi hiyo, Twiga walishajipima nguvu na mechi za kimataifa dhidi ya Zimbabwe na kufungwa mabao 4-1 na Banyana Banyana ya Afrika Kusini ambayo iliwafunga mabao 5-2.


Posted: 24 May 2012 11:57 PM PDT



Na John Gagarini, Pwani

KITUO cha Afya wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani kinahitaji kiasi cha shilingi bilioni 13 kwa ajili ya upanuzi wa kituo hicho ili kuwa hospitali ya wilaya hiyo.

Akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake jana Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha Dkt. Kaniki alisema kuwa tayari ujenzi huo umeanza.

Dkt. Kaniki alisema kuwa wamepeleka maombi maalumu serikalini kwa ajili ya ujenzi huo ambapo waliomba kiasi cha shilingi milioni 500 na kuwapatiwa shilingi milioni 290.

“Kiasi hicho cha fedha kilitolewa mwaka 2008 na 2009 ambazo zilitumika kwa ajili ya kujenga jengo la wagongwa nje yaani OPD, ” alisema Dkt. Kaniki.

Alisema kuwa, majengo ambayo yataongezwa ni jengo la wazazi na watoto wachanga, upasuaji mkubwa na akinamama, jengo la maabara, exray, wodi za wagonjwa wanawake na wanaume, jengo la magonjwa ya kuambukizwa jengo la kuhifadhia maiti na jengo la usafi.

“Mbali ya kupeleka maombi maalumu pia tumepeleka kwenye balozi za Korea Kusini kitengo cha misaada kwa huduma za afya na ubalozi wa Ireland ambako kote kwa bahati mbaya fedha hazikuweza kupatikana,” alisema Dkt. Kaniki.

Mganga Mkuu huyo wa halmashauri ya mji Kibaha alisema kuwa eneo la hospitali hiyo lina ukubwa wa hekari zaidi ya 10 na kuwataka wadau mbalimbali kujitokeza kufanikisha ujenzi huo.

Aidha aliwaomba wafadhili kujitokeza kuwasaidia ili waweze kufanikisha ujenzi huo ambapo michango imekuwa ni changamoto kubwa kufanikisha upanuzi huo ili kuisaidia Hospitali ya Tumbi ambayo itakuwa ya mkoa.
Posted: 24 May 2012 11:56 PM PDT

Mchungaji wa Kanisa la Pentekoste la LIFT HIM UP lililopo eneo la SanawariJuu mkoani Arusha Orche Mgonja (kushoto) akimuiombea mmoja wa waumini wa kanisa hilo Sabrina Masirori, wakati wa Maombi kwenye Kituo cha Maombezi maarufu Hospitali ya Rufaa juzi, aliyekuwa katika matatizo mbalimbali ya kiimani. (Picha na Richard Konga)
Posted: 24 May 2012 11:53 PM PDT

Na Moses Mabula, Tabora

KATIBU Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya taifa (TUGHE) Bw. Ally Kiwenge ameitaka Serikali itekeleze kwa vitendo ahadi yake ya kupandisha mishahara kwa watumishi wa umma ifikapo Julai Mosi mwaka huu ili kuepusha mivutano baina ya pande hizo mbili.


Bw. Kiwenge alitoa kauli hiyo jana mjini Tabora alipokuwa akizungumza na watumishi wa afya katika Hospitali ya Mkoa wa Tabora Kitete.

Alisema kwamba, Serikali ni lazima itekeleze ahadi yake hiyo kwa watumishi wake kama ambavyo Rais Jakaya Kikwete alivyoahidi siku ya maadhimisho ya wafanayakazi Duniani Mei Mosi yaliyofanyika mkoani Tanga.

Alisema kuwa, kila mwaka Serikali imekuwa ikitangaza nyongeza hewa ya mishahara kwa watumishi wake hususan wale wa sekta ya afya hali ambayo inafanya watumishi kutokuwa na imani na ahadi za Serikali yao na kupekelekea kufanya kazi chini ya kiwango.

“Chonde chonde mheshimiwa Rais Kikwete ninakuomba ahadi yako iwe ya kweli, sisi hapa tunasubiri tu, ifikapo Julai mwaka huu 'kahela ketu' kawe kameongezeka kwenye akaunti zetu,” alisisitiza Bw.Kiwenge.

“Sisi hatuna ugonvi na Serikali hata kidogo ugonvi wetu ni masilahi duni, lakini 'kamshahara ketu' kakiongezeka' sisi hatuna mgogoro kabisa na Serikali,” alisema Bw. Kiwenge.

Akiwageukia watumishi wa afya Bw. Kiwenge aliwataka wauguzi wote hapa nchini kutoa huduma ya afya kwa wagonjwa kwa moyo wa upendo, huruma na kutowanyanyapaa.

Alisema kuwa, kiapo cha muuguzi ni kuwa na upendo, huruma kwa wagonjwa wanaowahudumia sanjari na kujiupusha na vitendo vinavyokwenda kinyume na viapo vyao vya kazi yao ya uuguzi.

Alisema kuwa, kazi ya muuguzi ni kutoa huduma bora kwa mgojwa anayefika kutibiwa hospitalini na kwamba kwenda kinyume na kiapo cha cha kazi yake ni kutenda dhambi kwa Mungu.

Katibu Mkuu huyo wa TUGHE taifa alieleza kuwa kazi ya mtumishi wa idara ya afya imebeba dhamana kubwa ya usalama wa afya katika taifa, hivyo ni lazima wahakikishe wanatoa huduma kwa jamii isiyokuwa na mashaka wala malalamiko.
Posted: 24 May 2012 11:52 PM PDT
Na Elizabeth Mayemba

SIMBA sasa imepania kufanya kweli katika usajili ambapo wanataka kuziba pengo la kiungo wao Patrick Mafisango aliyefariki katika ajali ya gari hivi karibuni, hivyo wameanza mazungumzo na viungo wanne kutoka Kenya na Uganda.

Mbali ya viungo hao, pia klabu hiyo inampango wa kuwasajili washambuliaji Juma Abdallah wa JKT Ruvu na Jerrson Tegete wa Yanga, lengo ni kuwa na timu bora katika michuano ya Kombe la Kagame na Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao.

Akizungumza na gazeti hili jana mmoja wa Wajumbe wa Kamati ya Usajili ya Simba, ambaye aliomba kuhifadhiwa jina lake kwa madai wakati wa kuweka hadharani usajili bado, alisema tayari wameanza mazungumzo na viungo watano ambapo wawili kutoka Kenya na wawili wanatokea Uganda, na kwa hapa nchini wameanza mazungumzo na washambuliaji wawili.

"Tutavunja rekodi katika usajili wetu wala hatutaki kukurupuka lengo ni kuwa na kikosi kilicho bora na si bora kikosi," alisema Mjumbe huyo.

Aliwataja viungo hao ambao mmoja wapo ataziba pengo la Mafisango kuwa ni kiungo wao wa zamani Jerry Santo ambaye kwa sasa anachezea Tusker ya Kenya, Salim Kije wa FC Leopard ya Kenya, Owen Kasule na Mike Muchaba wote wa Bunamwaya ya Uganda.

Mjumbe huyo alisema baada ya kamati yao kuorodhesha majina hayo wataanza mara moja kupeleleza rekodi ya mchezaji mmoja mmoja na watakayevutiwa naye watamsajili na kumtangaza moja kwa moja.

Pia kwa wachezaji wazalendo Abdallah Juma hana tatizo lolote ni makubaliano tu, ila Tegete kuna baadhi ya vitu wanamchunguza na wakijiridhisha watamsajili katika kikosi chao.