TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, May 24, 2012

Breaking News:Mnyika ashinda kesi ya Uchaguzi Ubungo.

Na:  Yericko Nyerere
Hali ya mambo ni nzuri watu hawana munkari kama ilivyotarajiwa hasa wale wa Chadema ndio wengi na wanaonyesha wana matumaini ya Ushindi,
Hukumui haijaanza kusomwa tunaelezwa itaanza mida ya saa 3 hivi,
Polisi kwa mida hii sio wengi sana kwa hesabu hawafiki 50. Kwa ujumla hali ni ya amani kabisa!
Tutawajuza hatua kwa hatua moja kwa moja toka ukumbini!
Updates:
- Basi aina ya coaster lililobeba mashabiki wa chadema ndio linaingia huku likishangiliwa na watu kwa alama ya vidole viwili alimaarufu Amani na Upendo!
- Naaaaam vijana wakazi (FFU) ndio wanaingia kwenye eneo la tukio wakiwa wamevalia kikazi yani kama Baghdad lakini wapo kwa usalama tu hakuna dalili ya vurugu yoyote hali ni yaamani tu!
- Kuna mabishano ya hapa na pale kati ya wananchi na wahudumu wa mahakama, watu wanalalamika kuwa mbona mda unakwenda na hawaruhusiwi kuingia mahakamani! Lakini wamefanikiwa kuwasihii na wananchi wametuliza munkali
- Tunaendelea kusubiri mda ufike tuanze kufuatilia kesi hii!
- Naaaaam tumeshaingia ukumbini tayari kuanza usikilizaji wa kesi hii uendelee! Tumeambiwa tuzime simu lakini MIMI sitazima mwanzo mwisho!
- Tunasubiri jaji aingie na jopo la mawakili wa pande zote wapo tayari!
UPDATES:
Kuna kichekesho kimejitokeza hapa, yani wakati wakuingia ukumbini kuna mbinu iliyotumika na mashabiki wa CDM kuwabana mlangoni wale wa Magamba na wakashindwa kupata siti kilichofuata ni afande kuwatoa nje, wakati wakitolewa nje kuna kuna mwanachadema mashuhuri akaingia ukumbini afande akataka kumuunganisha na wanachadema kutoka nje, unaambiwa ukumbi umelipuka na kusema huyo siti ipoo!
Naaaaaaaaaaam Mh Mnyika ndio anaingia ukumbini anashangiliwa kwa makofi na Pipooooooozi Pawaaaaaaaaaaaaaa!
Updates:
Wakili wa Mnyika ndugu Mbogolo ndio anaingia anasalimiana na mnyika waapiga picha wanaendelea kupiga picha!
Sasa kilichobaki ni kumsubiri jaji tu aingie ukumbini!
Updates: 
Jambo la kufurahisha ktk kesi hii nikuwa Mh Mnyika na Hawa Ng’umbi wamekaa pamoja na wanapiga stori kweli, hata alipotokea afisa usalama akataka kuwatenganisha mnyika amemwambia haina tatizo watu pipoooooooooooz!
UPDATES:
M/Kiti wa CHADEMA na Kiongozi wa Upinzani Bungeni Mh Freeman Mbowe aka Sauti ya Zege ndio anaingia anashangiliwa ile mbaya pipooooooozi
UPDATES: Mpaka dakika hii saa nne kamili bado Jaji haja ingia ukumbini, tunaendelea kumsubiri!
UPDATES:
Naaaam jaji ameingia na hukumu inaanza rasmi,
Jaji anaomba radhi kuwa ataisoma hukumu kwa lugha ya kitumwa! Twendeleeee!
Updates:
Jaji anaendelea na mapitio ya mwenendo wa kesi nzima tangu ilipoanza na mpaka ilipo, kimsingi ameanzia kwenye historia ya kampeni,uchaguzi, uhesabuji kura na utangazwaji wa mshindi, sasa anaingia kwenye malalamiko makuu ya mlalamikaji,
Vuteni subira naripoti kwa kificho maana tumeambiwa tuzime simu na kamera zote za wanahabari!
Mtanisamehe nitaripoti yale muhimu tu, longolongo za jiji sitaziripoti muda wa kutafsiri lugha ya kitumwa sina!
Jaji mwenyewe inamsumbua kusoma ana nasanasa tu wakati anaisoma kwenye karatasi utadhani kaambiwa aisome kichwani!
Bado anaendela kusoma mwenendo wa kesi! Hajaingia kwenye vifungu halisi vinavyosubiriwa!
UPDATES:
Naam Hoja ya kwanza ndio inaelekea ukingoni kuna dalili za jaji kuitupa nje! Pamoja sanaaaa!
HOJA zenyewe ni hizi:
1)Kwamba Mnyika alimtuhumu kuuza nyumba za UWT
2)Kutumia Laptop za Mnyika Kuhesabu kura
3)Kuingia watu wengi wa CHADEMA ktk chumba cha kuhesabia kura
4)Kuzidi kwa kura hewa 16,000
5)Kukosewa kwa karatasi za kujumulisha kura (form)
Shitaka la kwanza: Mnyika alimwita fisadi Nghumbi ktk mkutano wa hadhara kwa kuuza nyumba za UWT limetupiliwa mbali na mahakama!
Shitaka la Pili: Kura hewa nalo limetupiliwa mbali!Sambamba na shatak la 3! Sasa shtaka la nne juu ya laptop!
Mashtaka matatu ya mwanzo (dhidi yake) yametupiliwa mbali na mahakama; sasa ni shtaka la nne.
Shtaka la nne la laptop binafsi limetupwa mbali.Hivyo mashtaka manne yote yametupwa mbali.Bado moja na la mwisho!
Sababu kuu ya kutupilia mashtaka manne: 1.Wahusika walioshtaki kutokuwapo ktk matukio tajwa 2.Kushindwa kuwasilisha ushahidi
MNYIKA ameshinda!Hawa atatakiwa kulipa gharama zote!

No comments:

Post a Comment