Mkurugenzi
Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Dkt. Aloyce Nzuki (katikati),
akizungumza na Naibu Waziri wa Utalii wa Afrika Kusini, Bi. Tokozile
Xasa, alipotembelea banda la Tanzania, katika maonesho ya utalii ya
INDABA yaliyofanyika Durban, Afrika Kusini hivi karibuni. (Na Mpigapicha
Wetu)
|
Mkuu
wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Tanzania,(SACP), Simon Siro
,(kulia), akishirikiana na mwananchi wa Ikwiriri (jina halikufahamika),
kuondoa mawe katika Barabara ya Kilwa, eneo la Ikwiriri, wilayani
Rufiji, Mkoa wa Pwani jana, mawe hayo yaliwekwa na wananchi wenye hasira
ili kuzuia magari yanayopita wakati wa vurugu kati ya wakulima na
wafugaji. (Picha na Masau Bwire)
|
Waziri
wa Maliasili na Utalii Balozi, Khamisi Kagasheki, akiteta na Naibu
Waziri wa wizara hiyo, Bw. Lazaro Nyarandu, wakati wa uzinduzi wa Bodi
ya Huduma za Wakala wa Misitu (TFS) Dar es Salaam jana. (Picha na
Charles Lucas)
|
Naibu
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Bw. Seif Suleiman Rashid (katikati)
akiongozana na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa (NHIF),
Bw. Emmanuel Humba na Naibu Mkurugenzi wa mfuko huo, Bw. Hamis Mdee
wakati wa ziara ya kuangalia utendaji na kuongea na wafanyakazi wa mfuko
huo, Dar es Salaam jana. (Picha na Charles Lucas)
|
MKAZI
wa maeneo ya Kasanga wilayani Morogoro Mkoa wa Morogoro Bw. Lucas
Robert (48) amefariki dunia mara baada ya kulipukiwa na taa ya chemli
aliyokuwa akiiwasha.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Morogoro Bi. Adolphina Chialo tukio hilo lilitokea Aprili 17, mwaka huu,
majira ya saa 12.45 alasiri maeneo ya Kasanga na kusababisha kifo chake
wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya mkoa.
Hata hivyo, Kamanda huyo alisema chanzo cha tukio hilo kinachunguzwa zaidi. Wakati
huohuo Jeshi la Polisi mkoani Morogoro linaendelea kumfanyia uchunguzi
utingo wa gari anaedaiwa kulishwa chakula chenye madawa ya kulevya huko
maeneo ya Mikumi wilayani Kilosa. Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi
mkoani Morogoro Bi. Adolphina Chialo tukio hilo lilitokea Mei 20, mwaka
huu, majira ya saa 10.00 jioni huko maeneo ya Mikumi Wilaya ya Kilosa. Kamanda
Chialo alisema Bw. Ramadhani Salumu (33) ambaye ni dereva wa gari lenye
namba za usajili T 509 ARS aina ya Scania Trela, alikuwa akitokea
nchini Zambia kuelekea jijini Dar es Salaam na alitoa taarifa kuwa
utingo wake aliyefahamika kwa jina Bw. Saimon Mashaka (21) amelishwa
chakula kinachodaiwa kuwa na madawa ya kulevya. Hata hivyo
Kamanda huyo alisema utingo huyo amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa
Morogoro na uchunguzi zaidi unaendelea kuhusiana na tukio hilo.
|
Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Morogoro Bw. Jasson Shumbusho (kulia), akikabidhi
Hundi ya Sh Mil 5.1, kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Ngoma Afrika Bw.
David Kitururu (wa pilia kushoto), kwa ajili ya Tamasha la Paukwa kwa
Wanafunzi wa Shule za Msingi za Manispaa ya Morogoro, litakalofanyika
Uwanja wa Jamhuri wiki hii. Jumla ya shule 20 zitashiriki. (Picha na
Aziz Msuya)
|
Askari
Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani, akimwelekeza dereva wa gari la
polisi namba PT O152 kulisogeza mbele eneo la Mchicha Barabara ya
Nyerere Dar es Salaam jana, baada ya kugongwa na daladala (halipo
pichani) namba T 342 AWQ, linalosafiri kati ya Gongolamboto na Mwenge.
(Picha na Prona Mumwi)
|
Na Lilian Justice, Morogoro
MWENDESHA
pikipiki anaedaiwa kuwa Ofisa Usalama Manispaa ya Morogor mkoani
Mrogoro amefariki dunia baada ya kugongana na mwendesha pikipiki
mwenzake huko katika maeneo ya Mizani Kihonda katika manispaa hiyo.
Akizungumzia
tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoani hapa Bi. Adolphina Chialo alisema
tukio hilo lilitokea Mei 19, mwaka huu majira ya saa 11.30 jioni huko
katika maeneo ya Mizani Kihonda mjini hapa.
Bi. Chialo alisema
pikipiki yenye namba za usajili T 699 BFU SUNLG amabayo ilikuwa
ikiendeshwa na Bw. Richard Feliciana (35) mkazi wa Chamwino mjini hapa
ilikuwa ikitokea Mkundi kuelekea mjini na iligongana na pikipiki
nyingine yenye namba za usajili T 281 AQU Honda iliyokuwa ikendeshwa na
Bw. Singoli Elia, ambaye alifariki dunia na kudaiwa alikuwa Ofisa
Usalama na mkazi wa Forest.
Kwa mujibu wa Kamanda huyo, marehemu
alikuwa akitokea maeneo ya mjini kuelekea Mkundi na chanzo cha ajali
hiyo kinachunguzwa zaidi.
Hata hivyo, taarifa za awali za Kikosi
cha Usalama Barabarani kimebaini chanzo cha ajali hiyo ni marehemu
kuendesha pikipiki yake kulia zaidi mwa barabara.
Wakati huohuo,
mtembea kwa miguu amefariki dunia mara baada ya kugongwa na gari mali ya
Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kilichopo mjini hapa.
Kwa
mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoani Morogoro Bi. Adolphina Chialo, tukio
hilo lilitokea Mei 18 mwaka huu, majira ya saa 12.30 jioni huko maeneo
ya Magubike wilayani Kilosa.
Bi. Chialo alisema gari lenye namba
za usajili SU 36224 Toyota Land Cruiser ikiendeshwa na Bw. Kassim Urasa
(53) mkazi wa Kihonda, ilikuwa ikitokea Mkoani Singida na ilimgonga
mtembea kwa miguu Emanueli Godfrey (7), mwanafunzi wa darasa la Kwanza
katika Shule ya Msingi Magubike na kufariki dunia papo hapo.
Hata hivyo, Kamanda huyo alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva na uchunguzi zaidi unaendelea.
|
Shekhe
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaj, Alhad Salum, akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) Dar es Salaam juzi, mara baada ya
kufanyika ibada ya kumbukumbu (Hitma) ya mwaka mmoja tangu kufariki kwa
aliyekuwa Mtabiri wa Nyota Afrika Mashariki Shekhe Yahya Hussein. (wa
pili kushoto) ni mtoto wa marehemu Bw. Hassan Yahya Hussein na kulia ni
mmoja wa maofisa wa taasisi mtabiri huyo, Shekhe, Hamisi Kondo. (Picha
na Charles Lucas)
|
Kaimu
Mkurungenzi wa Shirika la (TANESCO),Bw. Boniface Njombe(aliyeinama)
akimwonesha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Bw. Said Mwambungu moja ya kifaa
kilichoharibika katika moja ya mashine za kuzalisha umeme na kusababisha
kupungua kwa uzalishaji wa umeme katika Mji wa Songea mkoani Ruvuma
juzi. Kwa sasa upatikanaji wa nishati hiyo muhimu katika mji wa huo
imekua kero kubwa.Picha na kassian Nyandindi
|
JESHI
la Polisi mkoani Morogoro linawashikilia wakazi wawili ambao ni ndugu
katika maeneo ya Kihonda Kilimanjaro Manispaa ya Morogoro mkoani humo
kwa kosa la kukutwa na nyara za Serikali kinyume cha sheria.Akizungumzia
tukio hilo jana Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Bi. Adolphina Chialo
alisema lilitokea Mei 19, mwaka huu, majira ya saa 9.00alasiri huko maeneo ya Kihonda mjini hapa.Alieleza
kuwa askari waliokuwa doria waliwakamata Bw. Omari Mohamedi (56), mkazi
wa Kilimahewa na Bw. Salumu Mohamed (52) mkazi wa Nunge ambao ni
wanandugu wakiwa na ngozi za chui nne kinyume cha sheria huku wakiwa
wamezipakia kwenye baiskeli.Hata hivyo, Kamanda huyo alisema
watuhumiwa hao wamekamatwa na thamani ya ngozi hiyo bado haijafahamika
kwani uchunguzi maalumu bado unasubiriwa kutoka Idara ya Maliasili
kuhusiana na tukio hilo ili kuweza kufanya tathimini halisi ya ngozi
hizo.Wakati huo huo imeelezwa Mei 19, mwaka huu majira ya 12.45
jioni huko maeneo ya Melela, Wilayani Mvomero, mkazi wa eneo hilo Bw.
Bakari Rombo (29) ambaye ni mfugaji alitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi
kuhusu kuibwa kwa ng'ombe wakewatano wenye thamani ya sh. milioni 2.5 wakiwa zizini.Hata
hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Bi. Adolphina Chialo alisema
chanzo cha tukio hilo kinachunguzwa na mpaka sasa hakuna aliyekamatwa
kuhusiana na tukio hilo.
|
No comments:
Post a Comment