MWANDISHI WETU
SERIKALI imetakiwa kujenga Vyuo
vitakavyozalisha walimu wakutosha kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa
‘Viziwiwasiona’.
Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam leo , na Mwalimu wa
Kitengo cha walemavu katika shule ya Uhuru Mchanganyiko, Anjelica Mtwale wakati
alipokutana Mwakilishi Mkazi wa Shirika la ‘Sense International’ lenye makao
yake makuu nchini Uingereza.
Alisema pungufu huo wa walimu maalum
umetokana na kukosekana kwa vyuo vya kutosha, ambavyo vingesaidia kutoa taaluma
hiyo na kupatikana walimu wengi ambapo wangetumika kutoa elimu kuanzia elimu ya
awali hadi elimu ya juu.
Aidha, Anjelica alisema kutokana na baadhi ya
wazazi kupata mwamko wa kuwapeleka watoto hao shule kwa ajili ya kupata elimu, bado
kitengo chake kinashindwa kumudu kutoa mafunzo kwa kiwango kinachohitaji kutokana na upungufu huo.
“Unajua katika kuwaelimisha watoto hawa yani
Viziwiwasiona kunahitajika walimu wa kutosha kwa kuwa uelimishaji wao ni kwamba
kila mtoto mmoja mwalimu mmoja”alisema Mwalimu Anjelica.
Anjelica alisema katika shule hiyo, kuna
wanafunzi 13 huku walimu wakiwa 8 na walezi wa kujitolea wanne ambapo kwa
utaratibu mzima wa kuwatuza watoto hao hawatoshi.
Akitaja mafanikio tangu kuanzishwa kitengo hicho
mwaka 1994, Anjelika alisema wapo watoto waliofanikiwa kupata elimu ya
sekondari hadi kidato cha pili, kuishia kidato hicho kumetokana na kukosekana
walimu wenye elimu hiyo ya watu maalumu katika shule mbalimbali.
Aidha, Anjelica alitoa shukran kwa shirika la
Sense International kwa kushiriki
katika kutoa misaada mbalimbali ya kielimu na afya kwa watoto hao.
Alisema Shirika hilo limekuwa la kwanza
nchini katika kujishughulisha katika utoaji wa mafunzo kwa walimu wa watu wa
aina hiyo pia limehusika katika kuwapeleka walimu katika mafunzo ndani na nje
ya nchi.
Naye Mwakilishi Mkazi wa Shirika hilo,
Christopher Andendekisye alisema Shirika hilo limekuwa likifanya shughuli zake
kwa kushirikiana na serikali.
Alitoa wito kwa Watanzania kuwafikiria watu
hao kwa huruma kwani ni watu wenye ulemavu wakusikitisha, alisema “Hebu fikiria
mtu huyo haoni hasikii na hawezi kusema hivyo ni wakati kwa baadhi ya taratibu
za upatikanaji wa elimu ya walimu kuekebishwa ili iwe rahisi katika kupatikana
walimu wingi”
No comments:
Post a Comment