TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Sunday, May 20, 2012

TWIGA STARS YAKATWA MTAMA MARA 5 -2 DHIDI YA BANYANA BANYANA YA AFRIKA KUSINI


Mchezaji wa timu ya Twiga Stars Ester Chaburuma kulia akichuana na mchezaji wa Banyana Banyana Janne Van Wyk  wakati wa mchezo wa kirafiki unaofanyika jioni hii kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, mpira umekwaisha na  Banyana Banyana imeshinda kwa  goli 5-2 dhidi ya Twiga Star.

Magoli ya timu ya Banyana Banyana yamefungwa na wachezaji Portia Modise  magoli mawili dakika ya 23 na 46, Sanah Mollo magoli mawili dakika za 73 na 79 Janine Van Wyk amefunga goli la tano dakika ya 86 ya mchezo huo

Magoli ya Twiga Stars yamefungwa na wachezaji Fatma Bashir dakika ya 63 kwa njia ya penati, huku goli la pili likifungwa na Asha Rashid dakika ya 77
Kikosi cha Banyana Banyana kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo huo kwenye uwanja wa Taifa.
Kikosi cha Twiga Stars  kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo huo kwenye uwanja wa Taifa

No comments:

Post a Comment