Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Dkt. Mohammed
Gharib Bilal amemwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika mkutano wa Maendeleo
Endelevu Afrika unaolenga katika kujumuisha thamani ya Rasilimali Asilia
katika kupima maendeleo ya kiuchumi katika nchi za Afrika.
Katika mkutano huo, Tanzania imeunga mkono kuanzishwa
kwa mfumo wa kujumuisha thamani ya raslimali asilia ambao utahusishwa
kwenye tathmini ya pato la taifa kwa manufaa ya vizazi vya sasa na
vijavyo.
Makamu wa Rais alisema wakati akihutubia mkutano
huo leo Alhamis Mei 24, 2012 kuwa, mchango wa rasilimali asilia zina
nafasi kubwa katika kuchangia katika pato la taifa lakini ili mchango
wake utambulike, nchi zinahitajika kuwa na utaratibu wa kuzifanyia tathmini
hasa kuhusu matumizi yake na faida zake katika uchumi huku pia athari
zake zikitazamwa hasa zile zinazotokana na kupoteza uhalisia wa mazingira
ama kuharibu mazingira ya nchi.
“Ni imani ya serikali ya Tanzania kuwa mpango huu
utasaidia kutoa nafasi ya nchi kujikagua hasa kwa kuzingatia rasilimali
zinazotumika na faida inayopatikana. Tena mpango huu utatoa nafasi kwa
nchi kujiuliza kama matumizi ya rasilimali zake yanalenga kutambua faida
ya sasa na siku zijazo ili kuhakikisha kuwa mazingira yanabakia kuwa
salama kwa ajili ya vizazi vijavyo,” anasema Mheshimiwa Makamu wa
Rais Katika hotuba yake.
MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AHUDHURIA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA KUHUSU MAENDELEO NDANI YA BARA LA AFRIKA GABORONE
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed
Gharib Bilal akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Nchi pamoja na
wawakilishi kutoka nchi za Afrika waliohudhuria mkutano wa Maendeleo
Endelevu katika Bara la Afrika.(PICHA NA VPO)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed
Gharib Bilal akizungumza na Rais wa Liberia Bibi Ellen Johnson Sirleaf
kwenye mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Maendeleo Endelevu
Barani Afrika leo mjini Gaborone
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed
Gharib Bilal akihutubia kwenye mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu
Maendeleo Endelevu katika Bara la Afrika leo mjini Gaborone.
No comments:
Post a Comment