Timu
za Taifa za Tanzania (Taifa Stars) na Malawi (The Flames) zinapambana
kesho (Mei 26 mwaka huu) katika mechi ya kirafiki itakayofanyika Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
Makocha
wa timu zote mbili, Kim Poulsen wa Taifa Stars na Kinnah Phiri wa The
Flames wamezungumzia umuhimu wa mechi hiyo katika Mkutano na Waandishi
wa Habari uliofanyika leo (Mei 25 mwaka huu) ofisi za Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Kim
ambaye hiyo itakuwa mechi yake ya kwanza tangu asaini mkataba wa kuinoa
Stars, amesema baada ya mazoezi ya siku kumi hicho ndicho kipimo chake
cha kwanza na cha mwisho kabla ya kucheza na Ivory Coast kwenye mechi ya
mchujo ya Kombe la Dunia itakayofanyika ugenini Juni 2 mwaka huu.
“Wachezaji
wangu wamekuwa wakipokea mafunzo vizuri ingawa Nurdin Bakari na Thomas
Ulimwengu hatakuwepo kwa vile ni majeruhi. Bila shaka baada ya mazoezi
ni lazima ujipime, hivyo mechi hii ni muhimu kwangu ukizingatia kuwa
kwenye ubora wa viwango vya FIFA, Malawi wako juu yetu,” amesema Kim.
Naye
Phiri ambaye ni mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Malawi amesema awali
aliombwa mechi na Misri, lakini akaamua kucheza na Taifa Stars kwa vile
anaamini kitakuwa kipimo kizuri kwake kabla ya kucheza mechi ya mchujo
ya Kombe la Dunia dhidi ya Kenya itakayofanyika Juni 2 mwaka huu jijini
Nairobi.
“Nimekuja
na wachezaji 20 ambapo nusu yao wanacheza mpira wa kulipwa nje ya
Malawi, wengi wakiwa Afrika Kusini lakini wapo pia kutoka Msumbiji na
mmoja anacheza Hispania katika timu ya vijana ya Atletico Madrid.
Tumejianda si kwa mechi hii tu, bali pia dhidi ya Kenya na baadaye
Nigeria ambao tutacheza nao numbani Juni 9 mwaka huu,” amesema Phiri
ambaye kwenye benchi lake la ufundi anasaidiwa na Young Chimodzi.
Viingilio
katika mechi hiyo ni sh. 3,000 kwa viti vya kijani, sh. 5,000 kwa viti
vya rangi ya chungwa, sh. 15,000 kwa VIP C na B wakati VIP A inayochukua
watazamaji 748 tu itakuwa sh. 20,000.
No comments:
Post a Comment