Wito
huo umetolewa leo (Jumatano, Mei 23, 2012) katika mada tatu zilizowasilishwa
leo kuhusu maadili kwa viongozi wa umma kwenye mafunzo
maalum ya siku 10 kwa Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala na Wakuu wa Wilaya.
Mafunzo hayo ambayo leo yamefikia siku ya tatu yanafanyika kwenye ukumbi wa St.
Gaspar mjini Dodoma.
Akitoa mada kwa viongozi hao, Kamishna
wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji (Mst.) Salome Kaganda
alisema uadilifu ni zaidi ya kuzingatia sheria, taratibu na kanuni na akawataka
viongozi hao kuonyesha njia kwa matendo na mwenendo mwema ili waweze
kuwasimamia watendaji walio chini yao.
Naye Askofu Mkuu Mstaafu, Mhashamu
Donald Mtetemelwa aliwataka washiriki wa mafunzo hayo kujiepusha na matumizi
mabaya ya mamlaka walinayo kwani wasipofanya hivyo wanaweza kujikuta
wakiwaumiza wengi. “Lengo la kiongozi ni kubeba maumivu ya watu na siyo kupeleka
maumivu kwa wananchi,” alisema.
Alisema Tanzania kwa sasa inakabiliwa
na tatizo la kukosa viongozi wengi walio waadilifu kwa sababu wengi wao
wamemuacha Mungu kwa kisingizio cha kuwa na majukumu mengi. “Watu wakipewa
madaraka wanajitenga na Mungu, lakini lazima wakumbuke kuwa uadilifu wao utategemea
ni kwa kiasi gani wanamcha Mungu,” aliongeza.
No comments:
Post a Comment