Na Miza Chande-Maelezo Zanzibar
WAANDISHI wa habari Zanzibar
wametakiwa kubadilika katika uandishi wao kwa kuandika habari
zinazogusa zaidi maslahi ya jamii badala ya kuandika habari za kupamba
viongozi na watu maarufu nchini.
Imefahamika kuwa kuna habari nyingi za kuziandikia zenye maslahi na jamii ya Zanzibar ambazo zitakapojulikana kunaweza kupelekea mabadiliko makubwa katika jamii jambo ambalo litachochea maendeleo na kasi ya uwajibikaji.
Wito huo umetolewa na Mshauri wa Wanahabari Zanzibar Salim Said Salim wakati wa mafunzo
ya siku nne iliyofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo
Zanzibar, juu ya uandishi bora na namna ya kuzingatia maadili.
Salim
amesema miongoni mwa mambo ambayo yamekuwa yakigusa hisia za wazanzibar
ni pamoja na uingizwaji wa bidhaa mbovu ambazo zinapelekea wananchi
kuwa na shaka katika matumizi na hata kupata maradhi mbalimbali.
Amesema kama waandishi watakuwa wakitekeleza kazi zao vizuri na kuweza kufichua masuala kama hayo Zanzibar
haitaweza kuingizwa bidhaa hizo mbovu na wale ambao watafanya hivyo
wataweza kufichuliwa na kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria za Nchi.
Hivyo waandishi wa habari ni watu muhimu katika jamii kwani kalamu yao wakiitumia vizuri kwa maslahi ya nchi basin nchi inaweza kupiga hatua za haraka sana na mambo maovu kama hayo na mengineyo hayataweza kutendeka.
Amewasisitiza waandishi kujiamini katika kazi zao kwa kuzingatia maadili ya taaluma yao ambayo ndio muongozo katika kutekeleza kazi zao vizuri bila ya kujali habari hizo imemgusa nani.
Akifunga mafunzo hayo Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Yussuf Omar Chunda amewataka waandishi hao kutekeleza yale yote waliyoyapata katika mafunzo hayo ili kutoa habari zenye kuvutia.
Amesema
kuwa anaamini kuwa Taaluma waliyoipata itasaidia Taifa na kuwajengea
hadhi waandishi na taasisi zao ili ziwe zinakubalika na jamii.
Chunda
amesema kuwa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar itaendelea kutoa mafunzo
kwa waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari nchini viwe vya Serikali
au binafsi kwani vyombo hivyo vyote ni vya Zanzibar na vinahudumia Wazanzibari hivyo niwajibu wote kupata elimu ya habari ya kisasa
Mafunzo hayo ni ya pili kutayarishwa na Idara ya habari Maelezo ZanzĂbar na yakwanza yalifanyika Jijini Dar es Salaam mwezi wa Machi mwaka huu ambayo yalikuwa yamejikita katika uandishi wa habari za kibiashara na uchumi kwa kushirikiana na Ubalozi wa Uingereza nchini
No comments:
Post a Comment