Wateja wa Vodacom kupata nyongeza ya asilimia 50 kila wanapoongeza muda wa maongezi kuanzia Tsh 1000
· Nyongeza hii inaweza kutumika kwa ajili ya a kutuma ujumbe mfupi SMS, kupiga simu au kuperuzi internet.
· Kujua Salio la nyongeza mteja anaweza kubonyeza *102*02#
Kampuni
ya mawasiliano inayoongoza Tanzania, Vodacom leo imezindua promosheni
kwa ajili ya wateja wake ambapo kuanzia leo hadi mwisho wa wikiendi
watapata nyongeza ya asilimia hamsini kila mara wanapoongeza muda wa
maongezi wa kuanzia Tsh1000.
Katika taarifa kwenye vyombo vya habari, Mkurugenzi Mtendaji wa
Vodacom Tanzania Bw. Rene Meza alisema promosheni hii imetokana na
kuguswa kwa wateja na kampeni iliyozinduliwa hivi karibuni ya WAJANJA
ambayo imeonyesha kupendwa na kutumiwa sana na wateja wao kwenye
matumizi ya kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi SMS na kuperuzi kwenye
internet.
“Tunajivunia
tunapowaona wateja wetu wakifurahi na kuendelea kutumia huduma zetu na
hii promosheni inanuia kuwapa thamani zaidi yapesa zao wakati huu wa
wikiendi ikiwa ni fursa kubwa kwa familia kufanya shughuli kadha wa
kadha,” alisema Bwana Meza.
Nyongeza
hii ya salio ya asilimia 50 inaweza kutumika kwa kutuma ujumbe mfupi,
kupiga simu na kuperuzi internet kupitia simu za mkononi na pia
promosheni hii ni kwa ajili ya wateja wanaotumia Mpesa kununua muda wa maongezi.
Wateja pia wanaweza kuangalia salio la nyongeza hii kwa kubonyeza *102*02#
No comments:
Post a Comment