TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, January 10, 2015

RIDHIWANI KIKWETE AKABIDHI AMBULANCE KITUO CHA AFYA CHALINZE

 Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete (katikati) akikabidhi gari jipya la kubebea wagonjwa (Ambulance), kwa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo,Dk. Mastidia Rutaihwa kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Chalinze, katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Chalinze jioni hii. Wanaoshuhudia kutoka kulia ni Mganga Mkuu wa kituo hicho, Dk. Bamba Victor na Diwani wa Kata ya Bwilingu, Nasa Karama.
 Muumini wa Dini ya Kikiristo, Heema Said akitoa neno la shukrani kwa Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Kikwete 9aliyevaa koti kushoto) alipokabidhi ambulance hiyo. Ridhiwani alisema kuwa yeye hivi sasa ni mbunge wa vyama vyote jimbo humo hivyo ambulance aliyoitoa itoe huduma kwa wakazi wote wa jimbo hilo bila kubagua watu kutokana na itikadi zao. Pia aliuasa uongozi wa kituo hicho cha afya na uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kuhakikisha wanatunza vizuri gari hilo.
 Dok Rtaihwa akimkabidhi ufunguo wa gari hilo Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha Chalinze, Dk.Victor baada ambulance hiyo kukabidhiwa na Mbunge Ridhiwani.
 Dk. Victor akitoa shukurani kwa Mbunge Ridhiwani kwa msaada huo wa ambulance
 Wakifurahia kwa pamoja kupata usafiri huo muhimu kwa wagonjwa
 Mbunge Ridhiwani Kikwete na Dk. Rutaihwa wakiangalia ndani ya ambulance hiyo
 Wakiwa na furaha baada ya kuangalia samani zilizomo ndani ya ambulance hiyo
 Ridhiwani  pamoja na viongozi wa dini ya kiislamu wakiliombea dua gari hilo. Kutoka kulia ni Alhaji  Sheikh Hussein Fuko na Alhajj Khamis Magula
 Ridhiwani 9katikati) na Mbuunge wa Jimbo la Mtera, Lusinde wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Kituo cha Afya cha Chalinze akiwemo Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Dk. Rutaihwa.
 Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Dk.Mastidia Rutaihwa akitoa shukurani kwa Ridhiwani kwa msaada wa Ambulance na kuahidi kuitunza
 Ridhiwani akipongezwa na wananchi kwa kuwapatia ambulance
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya Hafsa Kazinja akicheza muziki na mmoja wa wazee wa Chalinze alipotumbuiza katika mkutano huo
 Ridhiwani akihutubia katika mkutano huo
 Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria makabidhiano ya ambulance katika viwanja vya miembe saba mjini Chalinze
 Mbunge wa Jimbo la Mtera, Dodoma, Lusinde ambaye alikuwa safarini akitokea Dodoma kwenda Dar kwenye vikao vya Kamati za Bunge, aliamua kushiriki kwenye mkutano huo ambapo alimsifia Mbunge Ridhiwani kwa kipindi kifupi alichoaguliwa kuwa mbunge miezi sita iliyopita kutekeleza kwa kiasi kikubwa ahadi alizozitoa wakati wa kampeni ikiwemo ambulance hiyo, ujenzi wa visima katika vijiji mbalimbali na ujenzi wa barabara pamoja na zahanati
Lusinde akikumbatiana kwa furaha na Ridhiwani baada ya mkutano huo kumalizika

MAMA SALMA KIKWETE AWAANDALIA TAFRIJA YA MWAKA MPYA WENZA WA MABALOZI WA NJE WALIOPO TANZANIA

unnamed1FMke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa tafrija ya mwaka mpya aliyoiandaa huko Ikulu tarehe 10.1.2015 kwa ajili ya wenza wa mabalozi wa nchi za nje walioko hapa Tanzania. unnamed2FMke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa tafrija ya mwaka mpya aliyoiandaa huko Ikulu tarehe 10.1.2015 kwa ajili ya wenza wa mabalozi wa nchi za nje walioko hapa Tanzania. unnamed3FMke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa tafrija ya mwaka mpya aliyoiandaa huko Ikulu tarehe 10.1.2015 kwa ajili ya wenza wa mabalozi wa nchi za nje walioko hapa Tanzania. unnamed4F Baadhi ya wageni waalikwa wakiongozwa na Mke wa Makamu wa Rais Mama Zakhia Bilal (wa kwanza kushoto)  wakisikiliza hotuba ya Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (hayupo pichani) wakati wa tarfija ya mwaka mpya aliyowaandalia wenza wa mabalozi wa nchi za nje waliopo hapa Tanzania tarehe 10.1.2015. unnamed5F Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mama Anna Mkapa wakati wa tafrija ya mwaka mpya aliyoiandaa huko ikulu tarehe 10.1.2015 kwa ajili ya wenza wa mabalozi wa nje hapa nchini. unnamed6FMke wa Rais Mama Salma Kikwete akipongezwa kwa hotuba yake na Mama Celine Mpango, Mke wa Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hapa nchini. Mama Mpango ni kiongozi wa wenza wa mabalozi wa nje waliopo hapa Tanzania. unnamed7F Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akijumuika na wenza wa mabalozi na wageni waalikwa kupiga picha ya kumbukumbu. unnamed8F Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na na baadhi ya wenza wa mabalozi wa nje waliopo hapa Tanzania wakati wa tafrija ya mwaka mpya aliyowaandalia huko Ikulu tarehe 10.1.2015. unnamed9FMke wa Makamu wa Rais Mama Zakhia Bilal akijadiana jambo na Kiongozi wa wenza wa mabalozi waliopo hapa nchini Mama Celine Mpango wakati wa tafrija ya mwaka mpya.

DK.SHEIN AONGOZA SHEREHE ZA KILELE CHA MATEMBEZI YA UMOJA WA UVCCM.

unnamed1DRais wa Zanzibar na Mwenyekiti  wa  Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar akikagua gwaride la Chipukizi wa UVCCM wakati alipofika katika viwanja vya Mnazi Mmoja leo Mjini Zanzinar  kupokea matembezi ya Umoja wa UVCCM yenye lengo la kuwaenzi Viongozi na kuadhimisha miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar,[Picha na Ikulu.] unnamed2DVijana wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM wakiwa wamebeba Bendera na Picha za Viongozi wakati wa kilele cha matembezi  ya Umoja wa UVCCM yenye lengo la kuwaenzi Viongozi na kuadhimisha miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyopokelewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti  wa  Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar  leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja Mjini Unguja ,[Picha na Ikulu.] unnamed3DVijana wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM wakiwa katika  matembezi  ya Umoja wa UVCCM yenye lengo la kuwaenzi Viongozi na kuadhimisha miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyopokelewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti  wa  Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibarleo katika viwanja vya Mnazi Mmoja Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] unnamed4DVijana wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM wa Mkoa wa Kaskazini Unguja wakiwa katika  matembezi  ya Umoja wa UVCCM yenye lengo la kuwaenzi Viongozi na kuadhimisha miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyopokelewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti  wa  Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar leo ambapo kilele chake  katika viwanja vya Mnazi Mmoja Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] unnamed5DRais wa Zanzibar na Mwenyekiti  wa  Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar akipokea picha za Viongozi kutoka kwa kiongozi wa Matembezi ya UVCCM Daudi Ismail Juma Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) kupitia UVCCM wakati wa kilele cha Matembezi ya kuwaenzi Viongozi na kuadhimisha miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] unnamed6DRais wa Zanzibar na Mwenyekiti  wa  Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar akimkabidhi Picha ya Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Mwenyekiti wa UVCCM Sadifa Juma Khamis baada ya kuyapokea matembezi ya Vijana wa UVCCM yaliyofikia kilele chake leo katika viwanja wa Mnazi Mmjoa Mjini Unguja katika kuadhimisha miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,[Picha na Ikulu.] unnamed7DRais wa Zanzibar na Mwenyekiti  wa  Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar akipokea  Bendera kutoka kwa Kiongozi wa Matembezi ya UVCCM Daudi Ismail Juma Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC)kupitia UVCCM wakati wa kilele cha Matembezi ya kuwaenzi Viongozi na kuadhimisha miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] unnamed8DVijana wa Chipukizi wakipita kwa gwaride la mwendo wa haraka mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti  wa  Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibarwakati wa kilele cha matembezi ya Umoja wa UVCCM yenye lengo la kuwaenzi Viongozi na kuadhimisha miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar leo katika viwanja vya Mnazi mmoja mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] unnamed9DViongozi wa Chama cha Mapinduzi wakiwepo wa UVCCM wakisimama wakati Makamo Mwenyekti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipokea matembezi ya Vijana wa Umoja wa UVCCM yaliyofikia kilele chake leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Mjini Unguja ikiwa ni kuadhimisha miaka 51 ya mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,[Picha na Ikulu.] unnamed10D Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Makamo Mwenyekti wa CCM Zanzibar akitoa hutuba yake wakati wa Kilele cha   matembezi ya Vijana wa Umoja wa UVCCM yaliyofikia  leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Mjini Unguja ikiwa ni kuadhimisha miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar (kushoto) Mwenyekiti wa UVCCM Sadifa Juma Khamis,[Picha na Ikulu.] unnamed11DBaadhi ya Vijana wa UVCCM wakimasikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Makamo Mwenyekti wa CCM Zanzibar alipokuwa akitoa hutuba yake wakati wa Kilele cha   matembezi ya Vijana wa Umoja wa UVCCM yaliyofikia  leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Mjini Unguja ikiwa ni kuadhimisha miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar (kushoto) Mwenyekiti wa UVCCM Sadifa Juma Khamis,[Picha na Ikulu.] unnamed12DRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Makamo Mwenyekti wa CCM Zanzibar akimkabidhi Cheti   Makamo Mwenyekiti wa Chipukizi Taifa Pili Hassan Suluhu   wakati wa  matembezi ya Vijana wa Umoja wa UVCCM yaliyofikia kilele chake leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Mjini Unguja ikiwa ni kuadhimisha miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar (kushoto) Mwenyekiti wa UVCCM Sadifa Juma Khamis,[Picha na Ikulu.] unnamed13D///// Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Makamo Mwenyekti wa CCM Zanzibar akimkabidhi Cheti Mke wa Makamo wa Pili wa Rais Mama Asha Suleiman kwa niaba ya Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idii kwa mchango wake mkubwa kufanikisha  matembezi ya Vijana wa Umoja wa UVCCM yaliyofikia kilele chake leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Mjini Unguja ikiwa ni kuadhimisha miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar (kushoto) Mwenyekiti wa UVCCM Sadifa Juma Khamis,[Picha na Ikulu.]
  unnamed14D 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Makamo Mwenyekti wa CCM Zanzibar akipokea matembezi ya Vijana wa Umoja wa UVCCM yaliyofikia kilele chake leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Mjini Unguja ikiwa ni kuadhimisha miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar (kushoto) Mwenyekiti wa UVCCM Sadifa Juma Khamis,[Picha na Ikulu.]

MBUNGE WA MBEYA MJINI JOSEPH MBILINYI APATA AJALI KITONGA MKOANI IRINGA


unnamed1kPicha zikionyesha matukio mbalimbali ya tukio la ajali ya gari iliyohusisha gari la  Mbunge wa jimbo la Mbeya mjini Mh. Joseph Mbilinyi Mr II iliyotokea leo mchana  kwenye mlima wa Kitonga akiwa safarini kutoka Mbeya. hata hivyo katika ajali hiyo watu wote wamenusulika kama wanavyoonekana kwenye picha wa pili kutoka kulia ni Mh. Joseph Mbilinyi Mbunge wa Mbeya mjini. unnamed2k unnamed3k unnamed4k

MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR MAALIM SEIF SHARIF HAMAD AFUNGUA CHUMBA CHA WAGONJWA MAHTUTI (ICU) SPITALI KUU MNAZI MMOJA.

unnamed1c
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akifungua pazia kuashiria ufunguzi wa wodi mpya ya wagonjwa mahututi (ICU) katika Hospitali Kuu ya Mnazimmoja ikiwa ni miongoni mwa maadhimisho ya miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar. (Picha zote na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar). unnamed2cSehemu ya vitanda vya wodi mpya ya wagonjwa mahututi (ICU) katika Hospitali Kuu ya Mnazimmoja. (Picha zote na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).
unnamed3cMakamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad wa tatu kutoka (kushoto) akionyeshwa kifaa maalum cha kusaidia wagonjwa  mahututi wanapolazwa katika wodi hiyo. (Picha zote na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar). unnamed4cWaziri wa Afya Rashid Seif akitoa taarifa juu ya wodi mpya ya wagonjwa mahututi kabla ya kumkaribisha Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kuzungumza na walikwa katika hafla hiyo. unnamed5cMakamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na wafanyakazi na wageni waalikwa katika ufunguzi wa wodi mpya ya ICU katika Hospitali  Kuu ya Mnazimmoja Mjini Zanzibar. unnamed6c Baadhi ya Wafanyakazi wa sekta ya Afya wakimsikiliza Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad wakati wa ufunguzi wa wodi ya wagonjwa mahututi (ICU). Hafla hiyo imefanya Hopitali Kuu ya Mnazimmoja Mjini  Zanzibar.  unnamed7cMaalim Seif Sharif Hamad akiagana na Mkurugenzi wa Hospitali Kuu ya Mnazimmoja Dkt. Jamala baada ya ufunguzi wa wodi ya wagonjwa mahututi (ICU).(Picha zote na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).
………………………………………………………………………….
Na Miza Kona na Abdulla Ali –Maelezo Zanzibar  
arif Hamad amewataka wauguzi kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake wabadilike kifikra na mawazo katika kutekeleza majukumu yao.
Hayo ameyaeleza katika Hospitali kuu ya Mnazi Mmoja Wilaya ya Mjini Unguja wakati wa Ufunguzi wa Wodi mpya ya Wagonjwa Mahututi (ICU) ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha miaka 51 ya sherehe ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Amesema wauguzi wana dhamana kubwa ya kuokoa maisha ya watu hivyo wanajukumu la kuhakikisha wanatoa huduma iliyo bora na ya uhakika.
Maalim  Seif amesema wauguzi wa wagonjwa mahututi (ICU) wana haki ya kupata mafunzo ili waweze kutoa huduma hiyo kwa ufanisi wa hali ya juu ili kufikia lengo lililokusudiwa.
“Wafanyakazi kuwa wapole, wenye kutumia lugha nzuri kwa wagonjwa, kuwa wastahamilivu na waliotayari katika kutoa huduma zao”, amesema Maalim Seif.   
Amewataka wafanyakazi wa ICU kuwa wawazi katika kutoa taarifa zinazohusu maendeleo ya wagonjwa pale inapohitajika ili kuondosha usumbufu kwa ndugu na jamaa wanapotaka kupata taarifa hizo.
Aidha amewataka wananchi kufuata taratibu zilizowekwa ili kuepusha usumbufu na matatizo zaidi kwa wagonjwa wa sehemu hiyo.
Maalim Seif amewataka wananchi kutumia vyema huduma hiyo muhimu ili iweze kudumu na kupunguza gharama za usafirishaji wa wagonjwa hao kufuata huduma nje ya nchi.
Mapema Waziri wa Afya Seif Rashid Suleiman amesema huduma ya ICU ni muhimu kwa ajili ya kuokoa maisha ya watu na ni lazima ipate zana za uchunguzi za uhakika ili kuweza kufanya matibabu ya uhakika na usahihi.
Amefahamisha kuwa Wizara imeandaa mpango maalum wa kuratibu dawa zinazotumika nchini kupitia Bohari Kuu ya dawa na Mfamasia mkuu wa serikali kuwacha kuagiza dawa zisizotumika ili kupunguza gharama na hasara.
Nae Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dr. Mohamed Saleh Jidawi amesema Wodi ya ICU ina vifaa vya kutosha na huduma zote zinapatikana bila ya usumbufu katika wodi hiyo.
Wodi hiyo imegharimu zaidi ya Dola millioni moja hadi kukamilika kwake ambayo ina vitanda nane na inajitosheleza kwa huduma zote zinazohitajika kwa wagonjwa.