Mchoro wa mkia wa ndege ukionyesha kifaa cha kutunza kumbukumbu za ndege 'black box'.
Kikosi cha uokoaji kikikusanya baadhi ya mabaki ya ndege ya AirAsia.
Majeneza ya baadhi ya miili iliyoopolewa kutoka bahari ya Java.
MKIA wa Ndege ya AirAsia QZ8501 iliyopotea na watu 162 Desemba 28, mwaka jana umepatikana leo katika Bahari ya Java, Indonesia.
Eneo
 la mkia ndipo kifaa cha kutunza kumbukumbu za ndege 'black box' 
kinapatikana na upatakianaji wake utasaidia wachunguzi kubaini chanzo 
cha ndege hiyo kupotea na kisha kuanguka baharini.
Ndege
 hiyo ilikuwa ikitokea Jiji la Surabaya nchini Indonesia kuelekea 
Singaporea. Mpaka sasa miili 40 imeopolewa kutoka baharini katika eneo 
ambalo ndege hiyo ilianguka.





No comments:
Post a Comment