Naibu
 Waziri wa Ardhi Makaazi Maji na Nishati Haji Mwadini Makame akifungua 
kitambaa kuashiria Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Kituo cha Polisi mbweni 
nje ya mji wa Zanzibar ikiwa ni Shamra shamra za kutimia miaka 51 ya 
Mapinduzi ya Zanzibar. 
-Vijana
 wadogo kutoka katika kituo cha Nyerere Shaolin Group wakionyesha 
umahiri wa kuweza kupambana na uhalifu katika sherehe za Uwekaji wa jiwe
 la Msingi la Kituo cha Polisi mbweni nje ya mji wa Zanzibar ikiwa ni 
Shamra shamra za kutimia miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar. 
Kamishna
 wa Polisi Zanzibar Hamdani Omar akitoa maelezo kuhusiana na Uwekaji wa 
Jiwe la Msingi la Kituo cha Polisi mbweni nje ya mji wa Zanzibar ikiwa 
ni Shamra shamra za kutimia miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar. 
-Katibu
 Mkuu Wizara ya mambo yandani Mbaraka Abdullwakili akitoa hotuba na 
kumkaribisha mgeni rasmi katika Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Kituo cha 
Polisi mbweni nje ya mji wa Zanzibar ikiwa ni Shamra shamra za kutimia 
miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar. 
-Naibu
 Waziri wa Ardhi Makaazi Maji na Nishati Haji Mwadini Makame akitoa 
hotuba katika Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Kituo cha Polisi mbweni nje 
ya mji wa Zanzibar ikiwa ni Shamra shamra za kutimia miaka 51 ya 
Mapinduzi ya Zanzibar.kushoto yake ni Katibu Mkuu Wizara ya mambo 
yandani Mbaraka Abdullwakili na kulia ni Kamishna wa Polisi Zanzibar 
Hamdani Omar. 
Naibu
 Waziri wa Ardhi Makaazi Maji na Nishati Haji Mwadini Makame katikati 
akiwa katika Picha ya pamoja na Viongozi wa Jeshi la Polisi katika 
Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Kituo cha Polisi mbweni nje ya mji wa 
Zanzibar ikiwa ni Shamra shamra za kutimia miaka 51 ya Mapinduzi ya 
Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.
…………………………………………………….
Na Ali Issa Maelezo-Zanzibar. 5/1215 
Katika kufanikisha kuwafichua na  kuwakamata wahalifu wa 
vitendo viovu  vya ujambazi na ubakaji kunahitaji ushirikiano mkubwa 
kati ya Jeshi la Polisi na wananchi wanaoishi katika maeneo yao. 
Hayo yamesemwa leo huko Mbweni nje kidogo ya mji wa Zanzibar 
na Naibu Waziri wa Aridhi, Makazi, Maji na Nishati Haji Mwadini Makame 
wakati wa uzinduzi wa kituo cha Polisi kijijini hapo. 
Amesema Jeshi la Polisi liko tayari kufanya kazi na raia 
wema  katika maeneo yao kwa kuwafichua wahalifu na kuwatia hatiani kwani
 wananchi ndio wanaoishi katika maeneo yanayofanyiwa uhalifu na kuwepo 
uwezekano mkubwa wa kufanikisha kazi zao.  
“Wananchi  shirikianeni kuwafichua  wanaofanya vitendo vya 
uhalifu,  ujambazi, uvutaji wa bangi na uuzaji wa madawa ya kulevya ili 
kazi ya  jeshi la polisi  ya kuwatia hatiani iwe rahisi”, alisema Haji 
Mwadini.
Aidha alisema kuwa kujengwa kituo cha Polisi katika eneo hilo
 la Mbweni ni faraja kubwa kwa jamii inayoishi hapo kwani lengo kuu ni 
kuwepo ulizi na usalama wa raia na mali zao hivyo alitaka kituo hicho 
kutumike kwa maengo yaliyokusudiwa.  
Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Hamdani Omar Makame 
akimkaribisha mgeni rasmi katika hafla hiyo, alisema kuwa kituo hicho 
kimejengwa kwa msaada wa mdau mzalendo ili kuwanusuru wananchi wanaoishi
 maeneo hayo na vitendo viovu vya ujambazi na uhalifu. 
Aliwaomba wananchi wanaoishi wa hapo  kukitumia kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi  kuanzisha ulizi shirikishi. 
Nae Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Mbaraka Abdul 
Wakili alisema kuwa Jeshi la Polisi limekuwa na changamoto nyingi za 
kupambana na vitendo vya ujambazi, hata hivyo wameweza kufanikiwa 
kuwadhibiti majaambazi. 
Alisema  kujengwa kwa kituo hicho ni mfululizo wa kujenga 
vituo vyengine kwa daraja A na C katika maeneo ya Pongwe, Mbuyutende na 
Jozani kwa Unguja. 
Ameongeza kuwa wamekuwa wakijenga vituo  pembezoni mwa fukwe 
za Bahari ili  kwanusuru watalii na wananchi  wa maeneo hayo kwa kuwapa 
ulizi  wa uhakika. 
Uzinduzi wa kituo cha Polisi Mbweni ni moja ya shamrashamra 
za maadhimisho ya  miaka 51 ya Mapinduzi matukufu  ya Zanzibar ya 
1964.   
No comments:
Post a Comment