Rais wa 
Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein 
akisalimiana na Waziri wa Afya Rashid Seif Suleiman pamoja na Viongozi 
wengine alipofika katika Hospitali ya Mnanzi Mmoja leo kufungua jengo 
jipya ya upasuaji wa Ubongo na Uti wa Mgongo (Neurosurgical Unit) ikiwa 
ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya 
Zanzibar,[Picha na Ikulu.]
Rais wa 
Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein 
akisalimiana na  Mkurugenzi Mkuu wa    Hospitali ya Mnanzi Mmoja Dk.Jamala Adam Taibu,alipofika  
 kufungua jengo jipya ya upasuaji wa Ubongo  na Uti wa Mgongo leo 
(Neurosurgical Unit) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka 51 ya 
Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,[Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akikata utepe kufungua jengo jipya ya upasuaji wa Ubongo na Uti wa Mgongo (Neurosurgical Unit) katika Hospitali ya Mnanzi Mmoja leo (kushoto) Waziri wa Afya Rashid Seif Suleiman na Prof,Dk. Mahmoud Quresh Mwakili wa   taasisi ya ND kutoka Spein  sherehe hizo  ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,[Picha na Ikulu.]
Rais wa 
Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa 
pili kulia) akipata maelezo kutoka kwa Dk.Mohamed Ali Haji (ustadh) wa 
sehemu ya upasuaji wa Ubongo na Uti wa Mgongo (Neurosurgical Unit) katika
 Hospitali ya Mnanzi Mmoja wakati Rais alipowatembelea wagonjwa mbali 
mbali waliokwisha fanyiwa matibu na Kituo hicho baada ya kulifungua 
jengo hilo leo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,[Picha na Ikulu.]
Rais wa 
Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa 
pilikushoto) na Makamo wa Kwanza wa Rais maalim Seif Sharif Hamad 
wakipata maelezo kutoka kwa Prof,Dk. Mahmoud Quresh Mwakilishi  wa   taasisi ya ND kutoka Spain  wakati alipotembelea mashine za upasuaji baada ya kulifungua jengo jipya ya upasuaji wa Ubongo na Uti wa Mgongo (Neurosurgical Unit) katika Hospitali ya Mnanzi Mmoja leo (kulia)  Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali Dk.Jamala Adam Taibu pia  sherehe hizo  ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,[Picha na Ikulu.]
Wanafunzi wa Chuo cha Sayansi ya Afya wakiwa mbele ya jengo la jipya ya upasuaji wa Ubongo na Uti wa Mgongo (Neurosurgical Unit) katika Hospitali ya Mnanzi Mmoja baada ya kufunguliwa rasmi leo na Rais wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein likiwa la horofa mbili na uwezo wa vitanda 30 pamoja na vyumba (2)viwili vya upasuaji,[Picha na Ikulu.]
…………………………………………………………………………………
Na Miza Kona    –    Maelezo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa 
Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohammed Shein amekemea tabia ya baadhi 
viongozi wa Taasisi  kuwazuia wafanyakazi wake kujiendeleza kielimu kwa 
lengo la kuongeza ujuzi na kuleta ufanisi.
Hayo ameyasema  Hospitali kuu ya 
Mnazi Mmoja katika ufunguzi wa Jengo la Upasuaji Vichwa maji na Uti wa 
Mgongo ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za maadhimisho ya  miaka 51 
ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Amesema tabia hiyo haifai kwani 
inarejesha nyuma maendeleo ya wafanyakazi na kuanzisha majungu, fitna 
 na uhasama katika taasisi  kati ya wafanyakazi wa kawaida na viongozi 
wao.
Amefahamisha kuwa taaluma ndiyo 
inayopelekea ufanisi bora wa kazi na  kuleta mabadiliko kwa   kutoa 
huduma bora  na uhakika na kujenga taifa lililo imara.
“Mabadiliko hayaji   bila ya kuwa 
na taaluma  hasa katika sekta ya Afya hivyo viongozi  waruhusuni 
wafanyakzi wenu kupata elimu ili waweze kufanyakazi kwa ufanisi”, 
alieleza Dkt. Shein.
Amesema lengo la  Serikali ni 
kuipa hadhi Hospitali ya Mnazi Mmoja kuwa ya rufaa kwa lengo la 
kuimarisha huduma bora lakini  kutokana upungufu wa vitendea kazi 
mabadiliko hayo yanakuja hatua kwa  hatua.
Dkt. Shein ameeleza lengo la  
Serikali ni kutoa huduma bora za afya kwa wananchi kwa kutumia 
 wataalamu wenye elimu na vifaa  vya  uhakika kadiri ya uwezo uliopo ili
 kuimarisha afya za wananchi.
Aidha Dkt Shein amesema jitihada 
kubwa zinahitajika katika kuandaa mipango madhubuti itakayosimamia 
kuendeleza kitengo cha  upasuaji wa ubongo na uti wa mgongo kwa kutafuta
 wataalamu na madaktari bingwa watakaoendesha matibabu hayo.
Amesema kitengo  cha huduma ya 
upasuaji wa ubongo na uti wa mgongo ni cha pekee kwa Afrika Mashariki na
 Kati ambacho kitasaidia kupnguza gharama za usafirishaji wa wagonjwa wa
 matatizo hayo  nje ya nchi.
Amesisitiza madaktari kuwafanyia 
wagonjwa uchunguzi wa kina kabla ya kuwapa  matibabu ili waweze kutoa 
huduma ya uhakika na  kujiepusha kubahatisha.
Aidha ameutaka uongozi wa 
Hospitali ya Mnazi Mmoja kukamilisha sheria na kuweka taratibu ili 
Hospitali hiyo iweze kujiendesha na kusimamia kazi bila kutegemea 
 Serikali kuu“Nijukumu la uongozi wa Hospitali 
hii kuandaa mipango mizuri  itakayoweza kuiimarisha  ili lengo  la 
kujiendesha  liweze kufanikiwa”. Alisitiza Rais wa Zanzibar.
Mapema akimkaribisha Mgeni rasmi, 
Waziri wa Afya Rashid Seif Suleiman alisema kupatikana kwa miundombinu 
katika kitengo hicho ni kuleta maendeleo katika sekta hiyo na ameeleza 
kitatoa huduma ya uhakika  Jengo hilo lenye vyumba viwili 
vya upasuaji, wodi nne za kulaza wagonjwa na chumba cha mikutano 
 limejengwa kwa msaada wa Shirika moja la Hispania  na Serikali ya 
Mapinduzi ya Zanzibar  na limegharimu zaidi ya shilingi Mill 600 ambapo 
asilimia 60 zimetolewa na wafadhili.






No comments:
Post a Comment