Na Mwamvua Mwinyi,Bwilingu.
WANAFUNZI
 wa shule ya msingi Maluwi,Mtambani,kitongoji cha Mdaula,kata ya 
Bwilingu,jimbo la Chalinze wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani,wanakabiliwa 
na kero ya ukosefu wa vyoo suala linalowasababishia kwenda kujisaidia 
maporini.
Wakati
 huo huo walimu na wanafunzi wa shule hiyo wanakabiliwa na changamoto ya
 ukosefu wa maji na kupelekea kufuata maji mtoni ambako maji yake sio 
salama kutokana,nyakati za mvua kusomba vinyesi na uchafu mbalimbali 
unaoingia mtoni humo.
Akizungumzia
 kero hiyo ,juzi,shuleni hapo,mwalimu mkuu wa shule ya Maluwi,Shabani 
Makuka alisema changamoto hizo sio za wanafunzi pekee bali hata walimu 
wanashida ya vyoo kutokana na sasa wanatumia choo kilichojengwa kwa 
nyasi.
“Shule
 hii kijumla na wakazi wa Mtambani pia inakumbwa na kero ya ukosefu wa 
huduma za kiafya hali inayosababishia kufuata huduma za kiafya Chalinze 
ambako umbali wake ni km zaidi ya 15 kutoka Mtambani,na kwa wale 
wanaoshindwa kwenda Chalinze uamua kumeza panadol za kununua bila 
ushauri wa daktari”alisema Mwalimu mkuu huyo.
Aidha
 Makuka alisema zipo changamoto nyingine ambazo ni pamoja na uhaba wa 
madarasa,madawati na utoro mkubwa unaofanywa na wanafunzi hasa walio 
jamii ya wafugaji ambao utoroka na kwenda kuchunga mifugo nyakati za 
masomo.
Hata
 hivyo Makuka alisema zipo hatua walizozichukua tangu ahamie kwenye 
shule hiyo mwaka 2013 ambapo aliwaomba amjirani kuwa wakisaidia 
wanafunzi hao kujistili pale inapobidi hasa kwa watoto wakike ambao 
wamepevuka.
Pia walichangisha wananchi na kupata kiasi cha sh.1,200,000 na halmashauri ilitenga fedha na kuwapatia  mil 2.5 jumla mil 3.7 ambazo wanatarajia kujenga choo kitakachosaidia kupunguza tatizo la ukosefu wa choo shule hapo.
Changamoto
 hizo zilifikishwa kwa mbunge mwenye dhamana ya kusimamia kero za 
wananchi jimboni chalinze Ridhiwani Kikwete ambae alisema kitendo cha 
kujisaidia maporini ni hatari kwa wanafunzi.
Ridhiwani
 alisema atachukua hatua za haraka kuangalia namna ya kutatua kero 
zilizopo shuleni hapo kwa kushirikiana na kamati ya shule na halmashauri
 ya wilaya .
Shule ya msingi Maluwi  imejengwa miaka 10 iliyopita,ina jumla ya wanafunzi 203,upungufu wa madawati 35 yaliyopo 45. 

No comments:
Post a Comment