Kaimu
 Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam 
(DAWASA) Didas Mwilawi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Fedha akisalimiana na
 Mwenyekiti wa wa Kamati ya Ufundi ya Bodi ya DAWASA Christine Kilindu 
alipowasili eneo zinapojengwa ofisi za mradi wa bomba kuu la maji kutoka
 Ruvu Juu zilizopo Kibaha.
Wajumbe
 wa Kamati ya Ufundi ya Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es
 salaam (DAWASA) wakiwa wameanza ziara yao ya siku moja katika mikoa ya 
Dar es salaam na Pwani kukagua na kujionea hatua iliyofikiwa katika 
mradi wa ujenzi wa miundo mbinu ya maji kutoka Ruvu Chini na Ruvu Juu 
ili kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji kwa wananchi katika mikoa 
hiyo.
 Meneja wa Mradi wa upanuzi wa mtambo wa Ruvu Juu Pintu Dutta kwa 
kampuni ya VA TECH WABAG kutoka India akifafanua jambo kwa Wajumbe wa 
Kamati ya Ufundi ya Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es 
salaam (DAWASA) walipotembelea huo eneo la upanuzi wa mtambo wa Ruvu Juu
 wakati wa ziara yao ya siku moja katika mikoa ya Dar es salaam na Pwani
 kukagua na kujionea hatua iliyofikiwa katika mradi wa ujenzi wa miundo 
mbinu ya maji kutoka Ruvu Chini na Ruvu Juu ili kuboresha huduma ya 
upatikanaji wa maji kwa wananchi katika mikoa hiyo.
.
 Wajumbe wa Kamati ya Ufundi ya Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji 
Taka Dar es salaam (DAWASA) wakiangalia maungio ya mradi wa bomba jipya 
kutoka mtambo wa Ruvu Chini yaliyopo eneo la Mpiji wilaya ya Bagamoyo 
mkoa wa Pwani
.Wajumbe
 wa Kamati ya Ufundi ya Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es
 salaam (DAWASA) kukagua mabomba yaliyohifadhiwa eneo la Kibaha 
Mwendapole wakati wa ziara yao ya siku moja katika mikoa ya Dar es 
salaam na Pwani kukagua na kujionea hatua iliyofikiwa katika mradi wa 
ujenzi wa miundo mbinu ya maji kutoka Ruvu Chini na Ruvu Juu ili 
kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji kwa wananchi katika mikoa hiyo. 
Wajumbe
 wa Kamati ya Ufundi ya Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es
 salaam (DAWASA) wakitembelea sehemu unapofanyika upanuzi wa mtambo wa 
Ruvu Juu wakati wa ziara yao ya siku moja katika mikoa ya Dar es salaam 
na Pwani kukagua na kujionea hatua iliyofikiwa katika mradi wa ujenzi wa
 miundo mbinu ya maji kutoka Ruvu Chini na Ruvu Juu ili kuboresha huduma
 ya upatikanaji wa maji kwa wananchi katika mikoa hiyo.
Sehemu ya mtambo wa Ruvu Juu kabla ya upanuzi. 
Moja
 ya hatua ya kusafisha maji katika mtambo wa Ruvu Juu kabla ya 
kusafirishwa tayari kwa matumizi kwa wakazi wa mikoa ya Dar es salaasm 
na Pwani 
(Picha zote na Eleuteri Mangi- MAELEZO)
……………………………………………………………………………….
Na Eleuteri Mangi- MAELEZO
Wajumbe wa Kamati ya Ufundi ya Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na 
Maji Taka Dar es salaam (DAWASA) wamefanya ziara ya siku moja katika 
mikoa ya Dar es salaam na Pwani kukagua na kujionea hatua iliyofikiwa 
katika mradi wa ujenzi wa miundo mbinu ya maji kutoka Ruvu Chini na Ruvu
 Juu ili kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji kwa wananchi katika 
mikoa hiyo.
Ziara ya wajumbe hao wa kamati Ufundi ilianza kwa kukagua kazi 
ya ukarabati wa kituo yalipo matangi ya maji eneo la Chuo Kiukuu cha Dar
 es salaam, maungio ya mradi wa bomba jipya yaliyopo eneo la Mpiji, 
ujenzi wa ofisi ya mradi wa bomba kuu la maji kutoka Ruvu Juu zilizopo 
Kibaha, kukagua mabomba yaliyohifadhiwa eneo la Kibaha Mwendapole na 
upanuzi wa mtambo wa Ruvu Juu Mladizi na Ruvu darajani. 
Akifanya majumuisho ya ziara hiyo Mwenyekiti wa wa Kamati ya 
Ufundi ya Bodi ya DAWASA Christine Kilindu amesema kuwa wajumbe 
wameridhishwa na kasi ya ujenzi wa miundo mbimu hiyo ambapo matarajio 
mradi huo utakamilika kwa wakati kama ilivyopangwa mwishoni mwa mwaka 
huu.
Mwenyekiti huyo alisisitiza kuwa wananchi wa mikoa ya Dar es 
salaam na Pwani watarajie kupata huduma ya maji iliyo bora mara miradi 
ya Ruvu Juu Chini itakapokamilika.
Aidha, Christine amewaasa wananchi wa maeneo yanapopita mabomba 
wa miradi hiyo kuyatunza vizuri kuanzia wakati huu yalipohifadhiwa na 
yatakapokuwa yameanza kutumika ili yawanufaishe wananchi wote wa mikoa 
hiyo.
Naye Kaimu Mkurugenzi DAWASA Romanus Mwang’ingo alisema kuwa 
pamoja na kuboresha huduma kwa maeneo yaliyo pembezoni mwa barabara ya 
Morogoro yaani Kimara, Mbezi, Kiluvya, Kibaha, Visiga, Mlandizi na 
Kibamba, utekelezaji huo pia utawanufaisha wakazi wa Ubungo, Vingunguti,
 Kimara, Tabata na Kinyerezi ambao nao wanahudumiwa na mtambo unaotoa 
maji kutoka Ruvu Juu.
Mradi wa upanuzi wa mtambo wa Ruvu Chini unalenga kuongeza 
uzalishaji maji na kuwahudumia wakazi wa maeneo ya uwekezaji (EPZ), 
Chasimba, Buma, Zinga, Kerege, Mpiji, Bunju, Wazo, Salasala, Madale, 
Kinzudi, Mbezi Juu, Goba, Kawe, Makongo, Mwenge, Msasani, Mikocheni, 
Mlalakua, Masaki, Sinza, kijitonyama, Manzese, Konondoni, Magomeni, 
Kigogo, Vingunguti, Buguruni, Kariakoo na Ilala. 
Kazi hiyo ya maboresho inafanyika chini ya mpango maalumu wa 
kuboresha huduma ya upatikanaji wa Maji Safi na Maji Taka jijini Dar es 
salaam na maeneo mengine yanayohudumiwa na DAWASA unaohususha ujenzi wa 
miradi mipya na pamoja na kukarabati miundombinu iliyopo.

No comments:
Post a Comment