TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, January 9, 2015

HAFLA YA KUWAKARIBISHA NA KUWAPONGEZA VIONGOZI WAPYA WA TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA YAFANYIKA

unnamed1Mwenyekiti mteule wa THBUB Mhe. Bahame Tom Nyanduga (aliyekaa
katikati), akiwa katika picha ya pamoja na timu yake. Kushoto kwake
ni: Makamu Mwenyekiti wa Tume, Mhe. Iddi Ramadhani Mapuri na Mhe.
Kamishna Rehema Msabila Ntimizi. Na kulia kwake ni: Mhe. Kamishna
Kevin Mandopi na Mhe. Kamishna Salma Ali Hassan. Waliosimama kutoka
kushoto ni: Mhe. Kamishna Mohamed Khamis Hamad, Mhe. Kamishna Ali
Hassan Rajab na Katibu Mtendaji wa Tume, Bibi Mary Massay.
unnamed2Viongozi wateule wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa
Sekretarieti ya Tume.
unnamed3Mwenyekiti Mtaafu, Mhe. Amiri Manento na Katibu Mtendaji, Bibi Mary
Massay wakimpongeza Mwenyekiti mteule wa Tume, Mhe. Bahame Tom
Nyanduga.
unnamed4Katibu Mtendaji wa Tume, Bibi Mary Massay akiongea katika hafla hiyo
kuwapongeza na kuwakaribisha viongozi wateule.
 
unnamed5Mwenyekiti mstaafu wa Tume, Mhe. Amiri Manento akitoa neno wakati wa
hafla fupi ya kuwapongeza na kuwakaribisha viongozi wateule.
unnamed6Mwenyekiti mteule wa THBUB, Mhe. Bahame Tom Mukirya Nyanduga akiongea wakati wa hafla hiyo. unnamed7Baadhi ya viongozi wateule wakifuatilia kwa makini nasaha zilizokuwa zikitolewa. unnamed8Mhe. Manento (kushoto) na Mhe. Nyanduga wakibadilishana mawazo. unnamed9Kamishna mteule, Mhe. Dk. Kevin Mandopi (kulia), Mkurugenzi wa Utawala
Bora, Bibi Fatuma Muya na Kaimu Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma na Mafunzo, Bw. Alexander Sales Hassan wakifurahia jambo mara baada ya kumalizika kwa hafla hiyo.
………………………………………………………………………………..
JANUARI 8 mwaka huu, Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Bibi Mary Massay aliandaa hafla fupi kwa ajili ya kuwapongeza na kuwakaribisha katika ofisi za Tume Mwenyekiti mteule wa Tume, Makamu Mwenyekiti na Makamishna wapya. Viongozi hao wapya walikula viapo vyao mbele ya Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Ikulu jijini Dar es Salaam mchana wa siku hiyo. Nao ni: Mhe. Bahame Tom Mukirya Nyanduga (Mwenyeketi), Mhe. Iddi Ramadhani Mapuri (Makamu Mwenyekiti) na Mhe. Mohamed Khamis Hamad (Kamishna) Wengine ni: Wahe. Makamishna Kevin Mandopi, Rehema Msabila Ntimizi na Salma Ali Hassan. Katika hafla hiyo viongozi hao wapya walipata fursa ya kufahamiana na wajumbe wa Sekretarieti ya Tume na pia Mwenyekiti Mstaafu wa Tume,Mhe. Amiri Manento. Akiongea katika hafla hiyo, Mhe. Manento alisema kuwa amefurahi Tume kupata viongozi wapya na hususan kumpata Mwenyekiti mwenye uzoefu mkubwa katika masuala ya haki za binadamu. Aidha, aliwaasa viongozi hao na wajumbe wa Sekretarieti ya Tume kutambua mamlaka (mandate) yao na kuyazingatia, kutojichanganya na siasa na kujitahidi wawezavyo kuitetea na kuiendeleza Tume. “CHRAGG is your mother, protect her at all cost,” alisema, akimaanisha kuwa pale mtu alipo au panapompatia riziki ndipo pake, hivyo ni budi apatetee na kupaendeleza. Kwa upande wake Mwenyekiti mteule, Mhe. Bahame Tom Nyanduga alisema kuwa wanatambua kuwa jukumu lililo mbele yao ni kubwa na kwamba watakumbana na changamoto nyingi lakini anaamini kuwa kwa neema za Mwenyezi Mungu watakabiliana nazo. Alisema ili kuepuka lawama watahakikisha kuwa wanazingatia kiapo chao,ambacho ni moja ya misingi muhimu. “Naamini tutatenda kazi zetu kwa uhuru, bidii, haki, uaminifu, na bila upendeleo wala woga…kwa kufanya hivyo tutakuwa tumeongeza thamani kwenye haki za watu wetu na hivyo kuleta amani nchini. Chini ni picha za baadhi ya matukio katika hafla hiyo iliyofanyika ukumbi wa mahakama, makao makuu ya ofisi za Tume jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment