IMEELEZWA kuwa kitu ambacho 
kimewapa wapinzani nafasi ya kushika viti mbalimbali vya  madaraka hapa 
nchini ni kutokana na makundi makundi ambayo yamo ndani ya chama cha 
mapinduzi(CCM)
Hataivyo makundi hayo wakati mwingine husababisha hata kuyumba kwa chama hicho ambacho kina nguvu kubwa sana hapa nchini.
“napenda kusema kuwa makundi ndani ya chama sio kitu 
kizuri hata kidogo na makundi haya haya ndiyo yaliyosababisha Nasari 
kuchukua hili jimbo ila tumemuazima tu mwakani lazima tuhakikishe kuwa 
tunalirudisha”alisema Bulembo.
Naye kamanda wa vijana Wilaya hiyo ya Meru John Palangyo alisema pamoja na kuwa tayari ameshasimikwa rasmi kuwa kamanda wa vijana wa Wilaya hiyo atafanya michakato mbalimbali ya kuweza kutatua kero za vijana.

No comments:
Post a Comment